back page

KABURI TUKUFU LA BIBI FATUMA MAASUMU (A.S).

next page

Kutokana na mapenzi mazito waliyokuwa nayo watu wa Qom juu ya bibi maasumah waliijenga vema shemu aliyozikwa na kuipa heshima zinazotakikana na miaka hamsini baadaye alipatili umuhimu zaidi bibi Zainabu mtoto wa Imamu Jawaad (a.s) kwa kujenga haram ya mwanzo kabisa kisha wakawa wanalikarabati jengo la mahala hapo patukufu wapenzi wa Ahlulbaiti na hadi lilipofikia hapo lilipo kwa hivi sasa.

Na baada ya kupita muda mrefu tangu azikwe bibi maasumah pembezoni mwa mahala hapo palizikwa pia idadi kubwa ya watoto wa maimamu ambao walipazidishia heshima kubwa sana sehemu hiyo na katika historia haramu ya bibi maasumah ni sehemu inayotoa nuru yenye ladha kwa mashia na ni sababu pekee ya kheri nyingi zilizo katika mji wa Qom.

Na ni wahitaji wangapi ambao wamefanikiwa katika mahitaji yao?  Na ni wagonjwa wangapi walioomba shifaa na wakapona kwa kutokana na karama za Ahalulbayt?  Na siku ya malipo ni wangapi kwa uwezo wa mwenyezi mungu wataepukana na adhabu kutokana na ziara zao katika kaburi la bibi maasume wakati walipokuwa duniani?  “Ee Faatuma tuombee pepo…”

Na imepokelewa kwa Imamu Swaadiki (a.s) anasema:- “Hakika bibi maasumah atawaingiza mashia wote peponi kutokana na uombezi wake kwao”

Na katika zama hizi za mwisho ni maulamaa wangapi wanaolilea kaburi hilo la maasumah na kufanya tawasul kwake? 

Na ni maulamaa wengi sana waliopita walikuwa katika hali kama hiyo na miongoni mwao ni Imamu Khomeini (q.s) na mafanikio yote yaliyopatikana ni kutokana na ziara zake kwa bibi maasumah na ilifungua mwangaza na nuru ya ajabu kwa Imamu na katika hiyo haram tukufu ndiyo sehemu pekee ambayo Imamu alianzia harakati zake za ukombozi katika Iran.

Na katika zama hizi haramu ya bibi maasumah imekuwa kama kito cha dhamani sana katikati ya mji wa Qom na kila kunapokucha wanakuja watu kutoka katika kila kona ya Irani na dunia kufanya ziara katika kaburi hilo la bibi maasumah. Na wakidhihirisha mapenzi yao ya dhati kwa bibi maasumah na Ahalulbayt pia.

index