back page

MAZISHI YAKE BIBI MAASUMU.

next page

 

Kutokana na mapenzi mazito waliyokuwa nayo wanawake wa kishia waliokuwa Qom juu ya bibi Maasumah walijitolea kwa mapenzi makubwa na moyo mkunjufu kuuosha mwili mtukufu wa bibi maasumah na kisha wakaukafini na sasa ulifika wakati wa mazishi.

Wakati wa mazishi walionelea ni vema azikwe na kiongozi mwadilifu na mwenye utukufu fulani huyo haswa ndiye auzike mwili mtukufu mahala palipostahili tofauti kabisa na yale maeneo yaliyokuwa yanazikwa watu wengine na hilo alilikusudia kutoakana na mapenzi mazito waliyokuwa nayo juu ya bibi maasumah hawakupenda kabisa azikwe katika makaburi ya pamoja na yaliyozikwa watu wengine.

Na ni yule yule Mussa bin Khazraj ambaye kutokana na nafasi aliyokuwa nayo aliweza kumtengea ardhi kubwa katika sehemu iliyojulikana kwa jina la “Babilon” iliyokuwa pembezoni mwa mto Qom. Mahali ilipo haram tukufu kwa hivi sasa.

Kila kitu kilikuwa ni tayari lakini jambo moja ni kwamba ni nani haswa ambaye angeshughulika na kuuzika mwili mtukufu wa bibi maasumah?

Tendo hilo lilipelekea maelfu ya watu waliokuwa pale kuanza kujadili kuhusu nani hasa anayefaa na kustahiki kuuzika mwili wa bibi maasumah.

Baada ya mjadala wa muda waliafikiana kwa pamoja kwamba wamwite sheikh mkubwa na wakuaminika aliyekuwa anakaa maeneo hayo shekhe huyo alijulikana kwa jina la “KAADIR” hivyo walimtuma mtu kumwita sheikh huyo haraka iwezekanavyo lakini kwa bahati mbaya mtu huyo hakumkuta lakini nyumbani kwake, na alipokuwa akirejea toka nyumbani kwa sheikh Kaadir alikuatana na watu wawili waliokuwa wamepanda vipando walitokea pembezoni mwa mto Qom. Na huku wakielekea sehemu ya maziko na walipofika ulipokuwa mwili mtukufu waliuswalia swala ya jeneza na kisha wakaanza kuuzika mwili mtukufu wa bibi maasumah.

 Na kwa mshangao wa watu wengi pindi watu hao walipomaliza kuuzika mwili mtukufu wa bibi maasumah walipanda vipando vyao na kutokomea kwa haraka.

Yalimalizika maziko kwa kila aina ya heshima na taadhima toka kwa mashia waliokuwa wamejaa majonzi na masikitiko na kuanzia kipindi hicho ndipo mji wa Qom ulipoanza kujulikana kama kiota cha familia ya Muhammad rehema na amani za mwenyezi Mungui ziwe juu yake na ahli zake.

Na baada ya muda Mussa bin Khazraj aliamua kuitoa sehemu hiyo aliyozikiwa bibi Fatuma wakfu kutokana na heshima aliyokuwa amempa bibi huyo maasumah na kwa kuwa sehemu hiyo alizikwa kiumbe kitukufu na ili pia iwe ni sehemu ya kuzikiwa mashia wa Ally pembezoni mwa kaburi lake tukufu.

index