back page

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

next page

 

( ) (

 ) () 

 

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Jabir bin Abdullah Al-ansari anahadithia kutoka kwa Bibi Fatimatuz Zahra (a.s.) ya kwamba, Nilimsikia Fatima (a.s.)  akisema ya kwamba; Siku moja baba yangu (mpendwa) Mtume wa Allah, alinizuru nyumbani kwangu na kusema;

Amani ya Allah iwe juu yako, ewe Fatima Nami nikamjibu

 

  

 

Nawe pia amani ya Allah iwe juu yako.

Kisha akasema; (Mwanangu) ninahisi mwili wangu ni dhaifu

Nikamwambia; Allah Akulinde kutokana na udhaifu, ewe baba.

Akasema, Ewe Fatima, niletee ile shuka itokayo Yemen, na unifinikie, kwayo.

Basi nikamletea ile shuka ya Yemen na kumfunika kwayo.

Nilipokuwa nikimwangalia niliona kuwa uso wake unameremeta, kama mwezi katika usika wa (mwezi) kumi na tano


 

 


Baada ya muda mfupi mwanangu Hasan (a.s.) aliingia na kunisalimu : Amani ya Allah iwe juu yako, ewe mama (mpendwa) nami nikamjibu,  Amani ya Allah, pia, iwe juu yako ewe kiburudisho cha macho yangu! na tunda la moyo wangu!

Akasema, Ewe mama, hakika mimi ninapata harufu nzuri sana kutoka kwako, kana kwamba ni harufu ya baba yangu, Mtume wa Allah (Amani ya Mwenyezi iwe juu yake).

Nikamwambia, Naam, hakika babu yako yuko chini ya ile shuka.

Basi Hasan (a.s.) aliikaribia ile shuka, na kusema, Amani ya Allah, iwe juu yako, ewe babu!


 

ewe Mtume wa Allah. Je unaniruhusu kuingia chini ya shuka niwe pamoja nawe?

Naye akamjibu, Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe mwanangu!, ewe mwenye kuimiliki hodhi yangu (ya kauthar siku ya Qiyama) nimekuruhusu.

Basi akaingia chini ya shuka pamoja naye.

Baada ya muda mfupi kupita, naye mwanangu, Husein (a.s.) akaingia na kunitolea salamu. Amani ya Allah iwe juu yako, ewe mama (mpendwa)

Nami nikamjibu , Amani ya Allah pia, iwe juu yako, ewe mwanangu! Ewe kiburudisho cha macho yangu! Na tunda la moyo wangu!.

 

 

Akaniambia, Ewe mama! Hakika mimi ninapata harufu nzuri sana kutoka kwako, kana kwamba ni harufu ya babu yangu, Mtume wa Allah.

Nikamjibu, Naam, babu yako na ndugu yako wako chini ya ile shuka.

Basi, Husein akaikaribia ile shuka na kusema; Amani ya Allah, iwe juu yako ewe uliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu (kuwa Mtume wake). Je unaniruhusu kuingia chini ya shuka, niwe pamoja nanyi.

Akasema, Amani ya Allah, pia iwe juu yako ewe mwanangu! Ewe

 

 


 
 

muombezi wa umma wangu (mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Qiyama). Nimekuruhusu.

Basi akainga chini ya shuka, (akawa) pamoja nao.

Wakati huo huo, Abul-Hassan Ali bin Abi Talib (a.s.) akaingia na kutoa salamu, Amani ya Allah iwe juu yako ewe binti ya Mtume wa Allah!.

Nami nikamjibu, Amani ya Allah, pia, iwe juu yako, ewe babake Hasan! Ewe Kiongozi wa waumini!

Akasema Ewe Fatima, hakika ninaipata harufu nzuri sana kutoka kwako kana kwamba ni harufu ya ndugu yangu na binami yangu, Mtume wa Allah.


 


 

Nikamwanibia Naam, yuko pamoja na wanao chini ya ile shuka.

Basi, Ali akaikurubia ile shuka na kutoa salamu, Amani ya Allah iwe juu yako, ewe Mtume wa Allah,  je unaniruhusu niwe pamoja nanyi chini ya shuka?

Akamjibu, Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe ndugu na wasii wangu na khalifa wangu, na mbebaji wa bendera yangu, nimekuruhusu.

Basi Ali akaingia chini ya shuka, kisha mimi nami nikaikurubia ile shuka na kusema, Amani ya Allah iwe juu yako ewe baba (mpendwa), ewe Mtume


 

 

 

 

   

 


 

 

   wa Allah, Je unaniruhusu niwe pamoja nanyi chini ya shuka?.

   Akajibu, Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe binti yangu, na ewe kipande cha mwili wangu, nimekuruhusu.

   Basi nikaingi chini ya shuka.

   Tulipokuwa tumekusanyika sote chini ya shuka, babangu mpendwa, alizishika ncha mbili za ile shuka na kuuinua mkono wake wa kulia, akiulekeza binguni na kusema;

 Ewe Allah! Hawa ndio Ahlul bait wangu, wasiri


 

 

 
 

wangu na wasaidizi wangu. Mwili wao ni mwili wangu, damu yao ni damu yangu. Huniumiza kinachow- aumiza na hunihuzunisha kinacho wahuzunisha. Ninampiga vita kila ananyewapiga vita, na ninampa amani kila anayewatunuku amani.

Mimi ni adui kwa mwenye kuwafanyia uadui, na humpenda yule awapendaye. Hakika wao wametokana nami, nami nimetok- ana nao. Basi niteremshie amani yako, baraka zako, rehma zako, msamaha wako, na radhi yako, mimi pamoja na wao. Na uwaondolee uchafu na kuwataka sa kabisa kabisa.


 


 

 

Basi, Mwenyezi Mungu, Mshindi na Mtukufu Akasema Enyi malaika wangu! Enyi wakazi wa mbingu zangu! Hakika mimi sikuiumba mbingu madhubuti wala ardhi iliyotandaa, wala mwezi wenye nuru, wala jua lenye kuangaza, wala sayari yenye kuzunguka, wala bahari yenye mwendo wa mawimbi, wala dau lenye kuelea majini, ila tu kwa kuwapenda hawa watano, walioko chini ya shuka.

Hapa, malaika mkuu, Jibrail akasema, Ewe Mola

 

 

 
 

 wangu! Na ni nani walioko chini ya shuka?

Allah, Mshindi na Mtukufu akamwambia, Hao ni watu wa nyumba ya utume, na asili ya ujumbe.

Wao ni Fatima na babake na mumewe na wanawe.

Jibrail (a.s) akasema, Ewe Mola wangu! Je unaniruhusu kuteremka ardhini ili niwe wa sita pamoja nao?.

Allah Akamjibu na kusema, Naam nimekuruhusu.

Jibrail (a.s) akateremka ardhini na kusema, Amani


 

 
 

 ya Allah, iwe juu yako, ewe Mtume wa Allah. Mkuu wa wakuu Anakutolea salamu, na kukustahi na kukutukuza, na Anakujulisha ya kwamba Naapa kwa Ushindi na Utukufu wanga ya kwamba sikuiu- mba bingu madhubuti, wala ardhi iliyotandaa wala, mwezi wenye nuru, wala jua lenye kuzunguka, wala bahari yenye mawimbi wala dau lenye kuelea majini, ila tu kwa ajili yenyu na mapenzi yenyu.


 

 
 

 Na ameniruhusu kuingia pamoja nanyi. Basi, ewe Mtume wa Allah, unaniruhusu kuingia?

Mtume wa Allah (s.a.w.a.) akasema, Amani ya Allah, pia, iwe pamoja nawe, ewe mwaminifu juu ya wahyi (ujumbe) wa Allah, naam nimekuruhusu.

Basi Jibrail (a.s) naye akaingia nasi chini ya shuka na kumwambia babangu, (mpendwa). Hakika Allah amewateremshia wahyi, na kusema, Hakika Mwenyezi Mungu Anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya utume) na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa.

Ali (a.s.) akamwambia babangu

 
 

( )


 

(mpendwa) Ewe Mtume wa Allah! Hebu nijulishe, kikao chetu hiki chini ya shuka kina fadhila gani mbele ya Allah.

Mtume (s.a.w.a.) akamwambia, Naapa kwa Yule Aliyeniteua  kuwa Mtume, na kunipa ujumbe wenye kuokoa, ya kwamba, itaka- pokumbukwa habari yetu hii, katika hafla yoyote ya watu wa ardhini na ikawa ikati yao kuna shia wetu na wapenzi wetu, basi Allah atawateremshia rehma yake na malaika watawahudhuria na


 

 


 

 

kuwaombea msamaha hadi watakapotawanyika.

Ali (a.s.) akasema, Basi wallahi tumefuzu na (pia) shia wetu wamefuzu.

Kisha babangu, Mtume wa Allah (s.a.w.a.) akasema, Ewe Ali! Naapa kwa Yule Aliyeniteua kwa haki kuwa Mtume, na kunipa ujumbe wenye kuokoa, ya kwamba itakapotajwa habari yetu hii katika hafla yoyote ya watu  wa ardhini na ikawa kati yao kuna

 

 
 

shia wetu na wapenzi, na ikawa kati yao kuna mwenye huzuni, basi bila shaka Allah atamuondolea huzuni yake, na mwenye ghamu, Allah atamuondolea ghamu yake, na mwenye haja, Allah Atamtek- elezea haja yake.

Ali (a.s.) akasema, Basi, wallahi tumefuzu na tumebarikiwa na kadhalika shia wetu wamefuzu na kubarikiwa, humu duniani na huko akhera, naapa kwa Bwana wa Kaaba.

Ewe Allah mrehemu Muhammad na Aali zake Muhammad.