back page

AHLUL BAIT

next page

 

 

Ahlul bait kilugha kama ilivyo katika kamusi ya kiarabu ni jamii yote ya nyumba k.m. mke, mwana, binti na watumwa. Yaani wote wanao mtegemea mwenye nyumba. Wengine wamepanua zaidi maana yake ili kuwaingiza pia, jamaa wa karibu k.m. mama, baba, dada, kaka na watoto wake ami na shangazi (dada ya mama) pamoja na watoto wao. Lakini kulingana na Quran tukufu na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.a), hizi tafsiri mbili hazitumiki  kwa Ahlul bait wa Mtume (s.a.w.a).

Kulingana na hadithi za Mtume (s.a.w.a), ambazo zimenakiliwa na wapokezi wengi, Ahlul bait ni neno tukufu linalomaanisha watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume, ambao ni  Imam Ali (a.s.) Bibi Fatima(a.s.),  Imam Hasan (a.s.), na Imam Husein (a.s.). Hawa ndio wale watu watano watukufu (Ahlul kisaa, yaani watu wa shuka) ambao, hakuna shaka kuwa ndio Ahlul bait.

Kwa hivyo, Jamii nyingineyo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.a) haiingii katika maana, ya Ahlul bait. Hata Bibi Khadija (a.s.) mke wa Mtume Mtukufu (s.a.w.a). aliye heshimika sana, na aliye kuwa mama yake Fatima (a.s.), binti mpendwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.a.). Vile vile, Ibrahim mwanawe Mtukufu Mtume (s.a.w.a.), pamoja na cheo chake kitukufu, haingii katika Ahlul bait.

Bila shaka kulingana na ukweli wa hadithi nyingi ambazo zimekuwa zikinakiliwa na wapokezi wa hadithi mara kwa mara watu watano watukufu (Yaani watu wa shuka) na Maimamu tisa watukufu, ambao wanatokana na kizazi cha Imam Husein (a.s.) wanaingia katika Ahlul bait. Na kwa Ibara nyingine ni kuwa Ahlul bait ni kumi na wanne, katika idadi, na ndio wanaoitwa Maasumin kumi na wanne.

Kulingana na aya ya utakaso (Suratul Ahzab 33;33) Ahlul bait wana cheo kitukufu cha ucha Mungu na umaasumu (utakasifu), kwani hawakuwahi kutenda dhambi na wala hawatendi.

Katika hadithi ifwatayo, Mtukufu Mtume ameonyesha utukufu wa Ahlul bait juu ua maswahaba wake wote; na kwa maneno na vitendo vyake alifafanua maana ya aya ya utakaso. Alisema ya kwamba Mimi na Ahlul bait wangu tumetakaswa kutokakana na madhambi. Aliwatangazia watu haya akiwa msikitini. Kila alipokuwa akienda msikitini kwa sala ya alfajiri alikuwa akipita nyumbani kwa Imam Ali (a.s.) na Bibi Fatima (a.s.) na kusema;

(( ))

Amani ya Allah, rehma na baraka zake ziwashukieni, enyi Ahlul bait. (Wakati wa) swala (umewadia), Allah awarehemuni. Kisha alikuwa akifuatilizia kwa aya ya Quran, Mwenyezi Mungu Anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa. Kisha aliongeza, Mimi ni mwenye kumpiga vita kila anayekupigeni vita (na) mimi ni mwenye kumpa amani kila anayekupeni amani (Majmauz Zawaid, Juzu yaq, na Tafsirus Suyuti, Juzu ya 5).

Katika Sahihu Tirmidhi, Musnadu Ahmad, Musnadu Tialasi, Mustadrakus Sahihain, Asadul Ghaba na katika tafsiri za Tabari, Ibn kathir na Suyuti, Anas bin Malik Khazraji (aliyedai kuwa alibaki katika uswahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.a)  kwa muda wa miaka kumi. Alifariki huko basra akiwa na umri wa miaka tisiini) amenakiliwa akisema ya kwamba, Mtume Mtukufu (s.a.w.a) alikuwa akipita karibu na mlango wa Fatima Zahra (a.s.) kwa muda wa miezi sita akisema. Enyi watu wa nyumba! Wakati wa swala umewadia!!  kisha aliongeza kusema, Enyi watu wa nyumba!...

Hawa ndio Ahlul bait ambao Imam Shafii, mmoja kati ya maimamu wanne wa dhehebu la kisunni katika kuwasifu amesema. Enyi Ahlul bait wa Mtukufu Mtume (s.a.w.a), kuwapenda ni faradhi iliyofaradhishwa na Mwenyezi Mungu katika Quran tukufu. Kwa hakika yatosha kuwa fakhari kubwa kwenu kwamba asiye waswalia nyinyi (katika swala yake), basi

swala yake hubatilika!! (Almuhaddithul Qummi, Alkuna wal Alqab, Shablanji, Nurul Absar, ukurasa wa 104).

Vile vile Zamakhshari na Razi, katika tafsiri zao za Quran tukufu wameinakili hadithi ya Mtume Mtukufu (s.a.w.a.) ifwatayo;

Amesema (s.a.w.a.):

(( ...... .))

Anayekufa akiwapenda Aali (kizazi) zake Muhammad hufa shahidi. Tambueni kuwa, anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad hufa akiwa amesha samehewa (madhambi yake). Tambueni kuwa, anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad hufa (kifo cha) aliyetubia. Tambueni kuwa anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad, hufa akiwa muumini, aliyekamilika imani (yake) Tambueni kuwa anayekufa akiwachukia Aali zake Muhammad, hufa akiwa kafiri. Tambueni kuwa anayekufa akiwachukia Aali zake Muhammad hatoipata harufu ya pepo (Zamakhshari, Tafsirul Kash-shaf juzu ya 4, tafsiri ya sura Ash-shura, 42; 32, na Fakhrud Din Arrazi, Tafsirul Kabir, Juzu ya 26, Ukurasa wa 165 166).

Tutamalizia kwa misitari ya shairi moja la mwanashairi maarufu wa kiirani aitwaye Saadi.

 

 

()

 

 

 

 Ewe Saadi! Ikiwa watamani kupata furaha ya mapenzi na ukamilifu wa maisha usiokuwa na kikomo, basi yakutosha kumpenda Muhammad na Aali zake Muhammad.

Hakuna malipo bora na furaha zaidi ya humu duniani kuliko kuwapenda kidhati Ahlul bait na kuwafwata kwa vitendo.

 

 

index