back

DIBAJI

next page

 

Kama vile yanavyobadilika yaliyomo ulimwenguni, vile vile maumbile ya binadamu hupatwa na mabadiliko. Tofauti zipatikanazo baina ya binadamu na binadamu mwingine husababisha tofauti  pia  katika  tabia na nyenendo, kwa mfano katika unyenyekevu, kiburi, usahaulifu, kumbukumba nzuri, hisia ya kutaka hifadha, n.k.

Kwa hivyo, ikiwa katika jamii baadhi ya itikadi, desturi na sheria, hazina misingi thabiti, na ikiwa watu wanaosimamia jamii hii sio waamimifu, bila shaka zitapatwa na mabadiliko na ulegevu, na hata mwishowe kutoweka kabisa. Hili ni jambo la hakika lililothibiti kwa njia ya uchunguzi na ujuzi.

Ili kuepuka hatari hii na kuuhifadhi uislamu –
(dini tukufu ya milele) – Mtume Mtukufu (s.a.w.a.) aliwaachia maswahaba wake maandiko matukufu yenye mfumo mzima wa maisha pamoja na viongozi waaminifu, ili kuwaongoza katika njia iliyonyooka. Aliwausia waislamu kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Quran tukufu) na Ahlul bait (kizazi chake kitukufu) na kuwasihi kutoviacha kamwe vitu hivi viwili. Huu wasia wake mtukufu umenakiliwa na wapokezi wa hadithi wa kisunni na wa kishia. Ulamaa wengi wa madhehebu tofauti tofauti wameelezea ya kwamba hii ni hadithi ya Mtume Mtukufu (s.awa) iliyo sahihi.

Mtume Mtukufu (s.awa.) amesema ya kwamba:

(اني تارك فيكم ما ان تمسكتم به لن تضلّوا بعدي احدهما اعظم من الآخر كتاب الله حبل ممدود من السماء الى الارض و عترتي اهل بيتي و لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فانظروا كيف تخلفوني فيهما)[1]

“Hakika mimi ninaacha kati yenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, kimoja ni kitukufu kuliko cha pili navyo ni kitabu cha Mwenyezi Mungu (ambacho ni) kamba iliyonyooshwa toka binguni hadi ardhini na kizazi changu, (ambacho ni) Ahlu baiti wangu na wala havitatengana kamwe hadi vitakapo nikuta kwenye hodhi (ya kauthar). Basi angalieni vile mtakavyo vitendea baada yangu. (Sunanut Tirmidhi hadithi ya 3788.)


 

[1] - سنن الترمذي، حديث 3788.

 

 

index