back page

UADILIFU WA MWENYEZI MUNGU

next page

 

 

KATI YA KULAZIMISHWA NA KHIYARI.

 

  

Kwa jina la mwenyezi mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.

 

) ( 

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na kutenda wema.

 

) (

Na Mola wako si mwenye kuwadhulumu waja.

 

) (.

 

 

UTANGULIZI

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.

Ninamshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema zake, na rehma na amani ziwe juu ya mtume wake wa mwisho na watu wa nyumbani kwake walio wasafi na walio twahirika hoja wa Mwenyezi Mungu na Mawali wake.

Uadilifu wa Mwenyezi Mungu kwa wenye kumuamini Mwenyezi Mungu mtukufu ni jambo la badaha (intuitive) ambalo halihitaji kuwaza sana, na haliingiliwi na shaka wala halikaribiwi na shubha ya aina yoyote.

Na dini zote za mbinguni na maamuzi yote ya akili salama na mantiki ya kielimu vinakubali hivyo kwa ukamilifu na vinakiri ukweli huo bila  matatizo yoyote.

Na kwa sababu hii, uadilifu wa Mwenyezi Mungu haukuwa- kwa maana yake  ni maudhui mepesi- ni jambo gumu miongoni mwa mambo magumu ya kifikra na yaliyo fungika, maudhui ambayo yanahitaji kuwekewa utafiti maalumu, yakiwa peke yake, kwa maana ya kuwa ni muhali kuyatolea ushahidi na kutoa dalili zake na kuyachambua yaliyo semwa na yasemwayo kuhusu huo uadilifu kama vile shubha na shaka.

Bali huenda ikachukuliwa utafiti katika jambo hili ni upuuzi kwa kiwango kikubwa, kwani kufanya hivyo ni mfano wa mazu-ngumzo kuhusiana na kulifafanua jambo lililowazi na kuyatolea dalili mambo yaliyo kubalika na yasiyo na shaka.

Lakini masuali ya kiakili yaliyo wazi na ya badaha pengine huzungukwa na mambo maalumu yaliyo changanywa ya pembeni na kuongezewa matawi ya pembeni ambayo ni magumu na yaliyo fungika, kisha ikawekewa kivuli au kizuwizi cha orodha ya tafsiri au maelezo ya ufafanuzi na taawili mbalimbali kwa hivyo usafi wake ukachafuliwa na kufifizwa ungaraji wake na kugeuka uwazi wake na kuwa ni jambo gumu, na uwazi wake kuwa ni jambo lisilo eleweka, na ikawa kugundua ukweli -katika hali kama hii- kunahitajia utafiti mkubwa na mazungumzo mengi kwa kuchukua baadhi na kuyapinga mengine, ili ukweli uliopotea uweze kudhihiri kwa uwazi, na kubainika ukweli usipatwe na kizuizi cha vumbi la pembeni, na matawi wala mafundisho yake yasifutike kwa misongamano mingi ya majadiliano yasiyo na matunda au natija na yalio marefu.

Wanazuoni wa elimu ya akida wamezungumza sana  kupita kiasi katika utafiti wao wa masala ya (Jabri na ikhtiyaar) kulazimishwa na kuwa na khiyari, na katika masala haya wakagawanyika pande mbili zenye kukabiliana -na huenda zikawa ni zenye kupingana- wakitupiana tuhma na wakibezana na kushambuliana kisha matokeo ya mijadala yao wakayabe-besha kwenye uadilifu wa Mwenyezi Mungu, maudhui ya Jabri na Ikhtiyaar yakawa ni kifungu kimojawapo kati ya vifungu vya Uadilifu na mlango moja wapo kati ya milango ya uadilifu.

Na wanazuoni wa elimu ya akida walipo zungumzia suala la Qadhaa na Qadar walirefusha vilevile na kuvuka mipaka kwenye mazungumzo yao, hadi kuleta tatizo katika masala haya yenye mikondo ya kifikra iliyo kabiliana na ambayo haiwezi kukutana vyovyote muda utakavyozidi kurefuka kisha wakaya-ongeza yote hayo kwenye maudhui ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu, wakayafanya kuwa kifungu kipya kwenye vifungu vya maudhui haya ya msingi.

Na matokeo ya kwanza yaliyofuatia baada ya mijadala yote hiyo, ni kuyageuza masala yote yaliyo ya wazi ya badaha kutoka kwenye hali yake ya mwanzo na kwenye ulimwengu wake ulio chomoza ulio wazi na kuyafanya kuwa ni maudhui yaliyo pinda na yenye kufungika hayawezi kufahamika isipokuwa kwa maelezo mengi ya ziada na mazungumzo (majibizano) na hata ufafanuzi wa nje.

Kisha miongoni mwa mambo yaliyo fuatia kutokana na masala haya kufanywa magumu (kufungwa), ni waislamu wengi kutofahamu maudhui haya, na vijana wengi kutia shaka kwenye masala ya Qadhaa na Qadar wale wenye kufahamu kidogo na kutia shaka hata kwenye matawi ya masuala haya ambayo ni rai zihusianazo na masala yaha na fikra mbali mbali. Na hapa ilikuwa ni lazima kwangu kutekeleza wajibu wa dini yangu wa kumtumikia msomaji mwisilamu kwa kufanya utafiti upande huu wa kifikra na wa msingi katika upande wa itikadi yetu ya kiislamu, huenda nikajaaliwa kwenye njia hii kutoa ufafanuzi unaoweka wazi makusudio ya maudhui haya na shubha kutoweka na kuondoa pazia kwenye ukweli uliofunikwa kwa fikra potovu na visa vya walio tangulia na dhana zilizopindishwa.

Na pamoja na kuwa masala haya ni miongoni mwa masala ya elimu ya akida yaliyo magumu zaidi kwenye maneno yake au istalahi zake, na yenye matawi au vifungu vingi zaidi vitokanavyo na kauli na nadharia mbalimbali na yenye kupanuka zaidi katika shubha na mambo yanayo dhaniwa, basi pamoja na  yote hayo, nimejaribu kutokana na juhudi na uwezo nilio nao kuyafanya mepesi maneno na maana na kuziweka wazi fikra, ili utafiti huu uwe kwenye kiwango chenye kufahamika kwa wote hasa kwa kizazi chetu kinacho jifunza na ili utafiti huu, uweze kuwafikia na kuwa mwepesi kwa wasomaji wote hasa watafutao ukweli na wapendao kuelewa.

Na matarajio yangu yote ni kuwa Mwenyezi Mungu anikuba-lie kazi yangu hii vizuri na aifanye ni chanzo (sababu) cha kunu-faika na kuongoka kwa watu, na ni nyenzo ya kupatia thawabu na malipo mema. Na nina mshukuru Mwenyezi Mungu alietuongoza kuyafahamu haya wala hatukuwa ni wenye kuongoka kama sio Mwenyezi Mungu kutuongoza.

 

 

Iraq-Kaadhimiya.

 

MOHAMMED HASSAN ALI YAASIN.

 

***

 

MWENYEZI MUNGU NI MUADILIFU.

 

Imani ya kweli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama ambavyo akili ilivyo tufahamisha na dalili zikatuongoza juu ya hilo, hiyo ni Imani ya moja kwa moja ya ile nguvu iumbayo ambayo iliufanya ulimwengu huu uwepo na vyote vilivyomo na waliomo, na nguvu hii ikauwekea ulimwengu nidhamu hii iliyo pangwa na mfumo madhubuti na kanuni zilizo thabiti ambazo maulama huziita kanuni hizo kwa jina la Sababu na wasababishwaji au Al-illatu wal-maalul (Cause and effects).

Hakika kuweka nidhamu kama hii ya ulimwengu yenye kushangaza na vyote vilivyomo kwenye kanuni zake na mpangilio wake ulio madhubuti uliohesabiwa kwa mahesabu ya juu kabisa na kukadiriwa kwa kiwango cha mwisho, na ustadi wa hali ya juu katika kazi zake na mfumo wake, na upangiliaji ambao ni wa  kiwango cha juu kabisa ulio sawa na thabiti na ulio jizatiti kama tulivyo elezea kwenye sehemu iliyo tangulia, hakika yote hayo yanatufahamisha kwa uwazi kabisa ya kwamba Muumba huyu ni Mwenye akili bila ya shaka yoyote, na ni mwenye hekima vilevile, na hufanya mambo kwa uteuzi wake bila shaka yoyote na ni mwenye uwezo moja kwa moja, na ni hai bila ya kutatizika, yaani kwa yakini na kiukweli kabisa. Bali amejikusanyia sifa zote nzuri na za ukamilifu usio na mipaka -kwa maana halisi ya maneno haya na kina chake- lakini sifa zake si sifa za ziada ambazo mtu akizisikia huenda akafahamu ndani ya akili yake -kutokana na matumizi ya sifa hizo yaliyo zoeleka hapa ardhini- bali ni sifa za dhati yake ambazo hazitengani naye na ambazo wanazuoni wa elimu ya akida huziita sifa hizo (ainudhati) yaani sifa yake ndie dhati yake.

Na kutokana na kuthibitika katika sehemu zake ya kuwa Mwenye mamlaka ya kuhukumu kimaumbile -kwa mapana yote ya kuhukumu- ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa kuzingatia kuwa yeye ni Mwenye uwezo wa kila kitu na afanyae lile alitakalo na ambae haulizwi kwa yale ayafanyayo na waja huulizwa[1] na yeye ndie Mwenye ufalme wa kila kitu[2], na ametakasika na maana yoyote ya kukosea na kuchanganyikiwa, na Mwenye nguvu ambae utawala wake hauna mipaka (hauwekewi miko na nguvu ya aina yoyote).

Na kutokana na ukweli kuwa imethibitika vilevile kwamba mamlaka ya kuhukumu kikanuni -kwa mapana ya mamlaka haya- ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu vilevile bila ya kuwa na mshirika au mwenye kumtatiza, hakika kuhukumu ni jukumu la Mwenyezi Mungu ame amuru ya kuwa msimwabudu yeyote isipokuwa yeyeSuratu Yusufu-40.

Na mwenye kuhukumu kinyume na aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu hao ndio makafiri .Suratul-Maaida-44.

Na kutokana na kuwa imethibiti kwa dalili za kunakiliwa (Quran na hadithi tukufu), na kutokana na yote yaliyopita ya kuwa kuna hesabu makini atakayo kumbana nayo mwanadamu siku ya marejeo baada ya kifo, na kupewa malipo mema mwenye kutii amri za Allah na kupewa daraja ya juu na neema yakiwa ni malipo ya utiifu wake, na kuadhibiwa mfanya maasi na kuweke-wa mambo mabaya na adhabu yakiwa ni malipo ya maasi yake.

Kutokana na kuthibiti yote hayo tunafikia kwenye natija ya lazima ambayo haina shaka kuichukua natija hiyo ni kukiri ya kuwa hakimu huyu ambaye mamlaka ya kutawala kimaumbile na kikanuni na ambaye inakusanyika kwake kazi ya kutoa thawabu na adhabu vimo mikononi mwake ni lazima awe ameepukana na sifa ya dhuluma na awe muadilifu kwa kiwango cha mwisho cha utakasifu na uadilifu ili mwanadamu aweze  kuchagua -kwa ridhaa yake na kwa makini na utulivu na kwa kusalim amri- njia ya utiifu na kujizuia na shahawa na kujikinga na matamanio ya nafsi na mapenzi yake kwa kiwango fulani, akiutegemea uadilifu wa hakimu kwenye hukumu zake na uadilifu wake katika kuku-bali ya kuwa atalipwa kwa hayo ayafanyayo.

Na kama si imani ya utakasifu wake kutokana na dhulma na ujeuri, mwanadamu asingepata kwenye nafsi yake kitu cha kumpa msukumo wa kupigana na matamanio ya nafsi, na kitu kimsukumacho kufanya mambo ya kheri, na kimsukumacho kutekeleza amri zote na kujiepusha na mambo mengine yaliyo zuiliwa na kuharamishwa. Na yatutosha kuona umuhimu wa uadilifu kiakida na kuwa ni nguzo moja wapo kati ya nguzo za dini na ni jambo la msingi lililotiliwa mkazo kwa ajili ya utiifu na kufuata amri, na yatosha kufahamu ubaya wa dhulma na kuwa ni chanzo cha fujo na mambo  mabaya na ufisadi. Yatosha Quran tukufu kuunga mkono hukumu ya akili kwa hayo iliyo yaona kuyathibitisha na ikawaamrisha watu kufanya uadilifu, na kuwakataza kufanya dhulma, na ikatumia mbinu na mifumo tofauti ya kuzungumza na kuhimiza na kuwatia hamasa ya kufanya hivyo.

Na miongoni mwa maneno yaliyo kuja kwenye Quran tukufu -yanayo husiana na uadilifu- ni kauli yake tukufu:

) ( Suratul-Annahl:90

Hakika Mwenyezi Mungu ana amrisha kutenda uadilifu na wema.

) (.Suratul-maaida:8

Fanyeni uadilifu kwani kufanya hivyo ndio kuwa karibu zaidi na uchamungu

) (.Suratu-Annisaa:58

Na pindi mkihukumu kati ya watu hukumuni kwa uadilifu.

) (Suratu-Shura:15

Na nimeamrishwa kufanya uadilifu kati yenu.

) .( Annahl:76

Je yeye analingana na yule mwenye kuamrisha uadilifu na akiwa kwenye njia iliyo nyooka?

) (Suratul-Anaam:115

Na limetimia neno la Mola wako kwa ukweli na uadilifu.

Na miongoni mwa yaliyo kuja kwenye Qurani tukufu katika kukataza dhulma na kuwatahadharisha watu na matokeo yake ni kauli zake tukufu:

) (.

Suratul-kahfi:87 .Ama mwenye kudhulumu tutamuadhi-bu.

) (. Suratu-Al-Imraan:57

Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhalimu.

) (. Suratul-Aaraaf:57

Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya madhalimu.

) (.Suratul-Shuaraa:227

Na wataelewa waliodhulumu ni marejeo gani watakayore-jea.

) (Suratu-Zukhruf:65

Olewao walio dhulumu kutokana na adhabu za siku iumizayo.

) (.Suratu-Annahl:118

Na hatukuwadhulumu lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

) (.Suratul-Huud:100

Na hatukuwadhulumu lakini walizidhulumu nafsi zao.

Na hivi ndivyo Quran ilivyo lieleza wazi suala la uadilifu na kulihimiza, na kuonyesha ubaya wa dhuluma na kuikataza, na ndivyo Quran ilivyokuwa ikiwapa msukumo waislamu zaidi na zaidi juu ya ulazima wa kuitakidi kwa uadilifu wa Mwenyezi Mungu mtukufu na kumtakasa na dhuluma.

Na ukweli ni kuwa kuamini uadilifu wa Mwenyezi Mungu alietukuka hakuhitajii dalili ya Quran au dalili ya matamshi, kwani akili peke yake inatujulisha hilo tena kwa dalili iliyo wazi, sana kwamba uzuri wa uadilifu na ubaya wa dhulma ni miongoni mwa mambo ya badaha kiakili (intuitive) ambayo hayahitajii dalili. Na lau kama mtu atakutii kiukamilifu na akatii amri zako zote kiukamilifu, kisha ukamlipa kwa maudhi au kumnyima malipo ya utiifu wake na utekelezaji wa amri zako, hakika akili ya mwanadamu awe muumini au kafiri haitaridhia kutoka kwako matendo hayo kamwe, bali itayaona hayo kuwa ni miongoni mwa mambo mabaya sana na ni sifa mbaya.

Na Mwenyezi Mungu -ambae ndie mwenye ukamilifu wote - hawezi kuwa na kiwango kidogo na cha chini kimwenendo kuliko mwanadamu wa kawaida katika matendo yake na hukumu zake. Ametakasika Mwenyezi Mungu kutokana na hayo utakasifu ulio mkubwa.

Na kwa ufafanuzi zaidi tunasema sisi tunaamini -kutokana na hukumu ya akili- kwa kufuata kanuni kubwa ya msingi ambayo muhtasari wake ni kuwa hakika Mwenyezi Mungu mtukufu hafanyi isipokuwa matendo mazuri, bali ni muhali kwake kufanya tendo lolote baya, kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu alietakasika anafahamu ubaya wa tendo hilo na hana sababu ya kumfanya (kumsukuma) afanye tendo baya.

Na kwamba mwanadamu anafanya tendo baya kwa msukumo wa kitu fulani kama mahitajio yake kwa kitu kile au kwa kutojua ubaya wake au kwa kuwepo maslahi yake binafsi kwa kufanya vile, hakika Mwenyezi Mungu alietakasika hatokifanya kitendo kama hicho, kwani yeye ni Mwenye kujitosheleza hakihitajii chochoote na ni mjuzi wa kila kitu.

Na vilevile sisi tunaamini -kutokana na asili iliyo tangulia na kwa kusalimu amri juu ya hukumu ya akili- ya kuwa Mwenyezi Mungu alietakasika hafanyi kitu isipo kuwa kwa malengo na faida .

 

) (.Suratul-Swaad:27

Na hatukuumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo kwa batili.

) (.Suratul-Addukhan:38

Na hatukuiumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo kwa mchezo.

) (.Suratu-Al-muuminuun:115

Je mnadhani ya kuwa tumekuumbeni bure?

Na neno bure lililotajwa katika aya maana yake ni kufanya kitu bila ya malengo, na kufanya kitu bila ya malengo ni kitendo kibaya ikiwa kitatendwa na mwenye hekima (wise reason) na kutenda matendo mabaya kama tulivyo tangulia kusema kwa Mwenyezi Mungu ni muhali.

Na hatukusudii kwa neno lengo-kama walivyo jaribu baadhi ya watu wachezeao matamshi kulitafsiri ili walipinge- ya kuwa hilo ni lengo ambalo maslahi yake humrejelea Mwenyezi Mungu kwa dhati yake na kwa maslahi binafsi, kwani Mwenyezi Mungu mtukufu hahitaji chochote na hana kitu tunacho weza kukitumia kama istilahi ya maslahi au manufaa yenye kumrudia yeye, bali tunakusudia kwa neno lengo lenye kurudi kwenye maslahi ya watu na lenye kuwiana pamoja na nidhamu ya ulimwengu.

Na kutokana na kuwa vitendo vya Mwenyezi Mungu vime-takasika na vimeepukana na kutokuwa na malengo, na michezo, ni lazima kwetu kuamini ya kuwa yeye Mwenyezi Mungu alietukuka hupenda utiifu wa viumbe na huchukia maasi yao.

) (.Suratul-Anfaal:7

Mwenyezi Mungu anataka kuithibitisha haki kwa maneno yake

) (.Suratu-Azzumar:7

Na Mwenyezi Mungu hairidhii kufru kwa waja wake.

) (.Suratu-Attawba:96

Hakika Mwenyezi Mungu hawaridhii watu waovu.

) (.Suratul-maaida:6

Mwenyezi Mungu anataka kukutwahirisheni (kukusafi-sheni) na kuzitimiza neema zake kwenu.

) (.Suratu-Annisaa:26

Mwenyezi Mungu anataka kukubainishieni na kukuongo-zeni kwenye njia za wale walio kuwa kabla yenu.

Na kukiri ukweli huu sio kwamba kunahitaji dalili ya matamshi, bali inatutosha katika suala hili ya kuwa yeye Mwenyezi Mungu alie tukuka amewaamuru watu kufanya utiifu na haifai kuamuru isipokuwa tu lile alitakalo na amekataza kufanya maasi  na haifai kukataza isipokuwa lile alichukialo bali haifai kiakili kuliamrisha asilo litaka na kulikataza asilo lichukia.

Lakini baadhi ya wanazuoni wa akida wakasema ya kuwa utiifu na uasi wote ufanywao na watu -bali watu wote- hakika si jambo jingine bali utiifu huo na uasi huo ni matendo ya Mwenyezi Mungu, na yamefanyika kwa utashi wake wa kidhati ambao ni mahsusi kwake.

Na dalili yao juu ya maneno hayo ni mambo mawili:

1: Hakika yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu lau kama angekuwa anataka utiifu kama tulivyo eleza ni lazima utashi wake uthibiti kwa hali yeyote ile,  hata kama mja atataka kukhalifu na kwenda kinyume, kwa sababu kufanyika kwa maasi kama alivyo-taka mja ni kinyume na utashi wa Mwenyezi Mungu, kwa maana ya kuwa utashi wa Mwenyezi Mungu umeshindwa nguvu na utashi mwingine na kuporomoka na hili haliwezekani na halikubaliki akilini,  kwa hivyo basi Mwenyezi Mungu Mtukufu hataki utiifu kwa wakati wote na hakuna kifanyikacho isipokuwa ni kile akitakacho.

Na jibu fupi juu ya shubha hii ni kama ifuatavyo:

Hakika Mwenyezi Mungu alie mtukufu bila shaka yoyote anataka utiifu, lakini hamlazimishi mja wake kuutenda, bali huipenda twaa au utiifu ufanywapo na mja kwa  khiyari yake Mwenyewe bila kulazimishwa na kwa kutaka kwake na kusalim amri kwake, na utekelezaji wa utiifu ule na jambo hilo hauwezi kuthibitika isipokuwa ni kutokana na utashi wa mtu mwenyewe peke yake, pasina kuwepo uhusiano wa utendaji huo na utashi wa Mwenyezi Mungu mtukufu.

2: Hakika alilolifahamu Mwenyezi Mungu kutokea kwake ni lazima litokee bila ya shaka, na kila alilolifahamu kuto tokea kwake ni lazima vilevile lisitokee, basi iwapo Mwenyezi Mungu atafahamu ya kuwa mwanadamu hatii amri fulani, ni muhali kwa huyu mwanadamu kuifanya, kwani yeye Mwenyezi Mungu atakuwa ni Mwenye kutaka jambo ambalo haliwezekani kutokea, na kutokana na ukweli kuwa elimu ya Mwenyezi Mungu imevizu-nguuka vitu vyote, yaani anavifahamu vitu vyote, ina maana ya kuwa vitendo vyote vya mja wa Mwenyezi Mungu vitatokea yaani vitafanyika kama Mwenyezi Mungu alivyo vifahamu, sawa waja wametaka kuvifanya au hawa kutaka, na kwamba katika mambo hayo hawana ikhtiyaari (hiyari) ya kufanya utiifu au uasi.

Na jawabu fupi juu ya pingamizi hili ni kuwa:

Hakika elimu ya Mwenyezi Mungu ina maana ya kwamba Mwenyezi Mungu hufunukiwa uhakika wa kitu au tukio fulani kiukamilifu na kuwa wazi kwake maumbile ya kitu  kile, kwa mfano tunakuta kwamba Mwenyezi Mungu hakutoa habari za ukafiri wa Abu Lahab na kwamba atakaa milele kwenye adhabu isipokuwa ni kueleza yaliyo dhihiri au aliyo yafahamu ya kuto kubali bwana huyo ujumbe wa Mwenyezi Mungu hadi mwisho wa umri wake, na haina maana ya kuwa elimu ya Mwenyezi Mungu ilikuwa ni sababu ya kuto amini Abu Lahab na kubaki kwake kwenye kufru na upotovu, hadi kufa kwake.

Na ili kukusogezea fikra hii kwenye akili tutatoa mfano wa kuliweka wazi jambo hilo kwa mfano wa kidunia na tunasema:

Hutokea daktari akamfanyia uchunguzi mgonjwa kutokana na maradhi fulani na kugundua ya kuwa ana ugonjwa, na baada ya kugundua ugonjwa wake akatoa habari ya kwamba mgonjwa huyo atakufa kutokana na kutokuwa na matarajio ya kupona mgonjwa huyo, na akatoa habari hizo kutokana na kufahamu kwake ukubwa wa maradhi yake, na huenda yule daktari akamueleza mtu mwingine wa pembeni hali aliyo nayo yule mgonjwa kama maumivu aliyo nayo mabadiliko yaliyomo mwilini mwake kabla ya kufa kwake, na alifanya hivyo kwa kuyafahamu mabadiliko na maendeleo ya ugonjwa na jinsi anavyo dhoofu kutokana na ugonjwa ule. Je kauli ya daktari na kufahamu kwake ndio sababu ya kifo cha mgonjwa, au kauli ile na kufahamu kule si jambo lingine bali ni katika kufunukiwa na kufahamu  hali halisi ilivyo ya mgonjwa, na kufunuka  uwazi wa jambo lile kwake.

Na jambo lililowazi ni kuwa aliyesema maneno hayo, jambo hilo lilimtatiza na kuchanganya kati ya elimu ya wafanyaji (wajenzi) na elimu ya wengine, kwani mfanyaji kama vile fundi au mtunzi au mshahiri ni lazima kwanza akifanyie maandalizi kitendo chake kwa kuyaangalia maudhui na kuchora ramani ya kazi na kuitekeleza kwenye akili yake na hapo uamuzi wa kiufundi au uandishi wa kitabu au utunzi wa qaswida, hufuatia baada ya kufanyika na kumalizika kwa kitu kile ambacho kilisababishwa na ujuzi wa kiakili uliotangulia.

Lakini kuyafahamu  matukio -kama vile ufahamu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu wa vitendo vya waja wake- ni tofauti na hayo tuliyo toka kuyaelezea na haiwi kuyafahamu matukio hayo ila tu kule kufunukiwa na kuyafahamu matukio hayo kama yatakavyo kuwa na hali itakavyo kuwa. Na katika kufahamu huku hakuna maana yoyote ya kuwa ni sababu ya kutokea matukio hayo.

Na hivyohivyo tunaelewa kwamba katika shubha hizi mbili, hakuna kitu kinacho weza kuthibiti na kubakia kwa ajili ya majadiliano na kutumia mantiki na kutoa dalili, na kwamba Mwenyezi Mungu hawalazimishi waja wake kutekeleza utashi wake kwa nguvu. Na elimu yake au kufahamu kwake kwa mambo sio sababu iwafanyayo watu (wanadamu) wafanye maasi au utiifu au imfanyayo fulani afanye maasi na mtu mwingine awe mtiifu.

       Mwenyezi Mungu anasema: (   )

hatapata mwanadamu isipokuwa aliyo yafanya[3], na kisha anasema :( )               

Hakika si jambo lingine, bali mtalipwa yale mliyo kuwa mkiyafanya. Na pia anasema:

                     

Mwenye kukufuru malipo ya kufuru yake yatakuwa juu yake na wenye kufanya matendo mema hufanya hivyo kwa ajili ya kuziandalia nafsi zao.

Na msomaji mtukufu atapata majibu na ubatilishaji zaidi wa shubha mbili hizi  na mengineyo kama hayo kwenye sehemu ifuatayo ya kitabu hiki.

 

***

 

 

 

KUTENZWA NGUVU NA UTEUZI (KHIYARI)

 

Mazungumzo kuhusiana na masala ya "Kutenzwa nguvu na kuwa na uteuzi (Khiyari)" ni mazungumzo marefu na mapana hayawezi kutosha kwenye kurasa kadhaa, na nafasi haitoshi kuweza kuyaelezea kwa upana wake.

Na pamoja na kwamba chanzo cha kisa cha (Al-jabri) kutenzwa nguvu ni suala la kisiasa na maudhui ambayo yalitumi-ka kutaka kusahihisha matendo ya watawala madhalimu walio-toka kwenye mafundisho ya dini na wakatengeneza nyudhuru zisizo na uteuzi na hiyari yao ili kuonyesha usahihi wa matendo yao yenye kupingana na hukumu za kiislamu. Hakika masala haya yalipiga hatua na kuendelea na kutoa matawi hadi yakawa ni masala ya msingi, na mlango muhimu kati ya milango ya itikadi.

Na ni suala gumu na lililo fungika kati ya masuala ya kifikra ya dini. Na msingi wa fikra ya (Al-jabri) kutenzwa nguvu au shubha yake ilikuwa ni rai walizo shikamana nazo baadhi ya waislamu ya kwamba matendo ya watu -watu wote- hayakufa-nyika na hayafanyiki kwa kutaka kwao tu na kwa khiyari au (uteuzi) wao, bali yametokea kwa kufanywa na Mwenyezi Mungu na utashi wake na mwandamu hana mahusiano yoyote na matendo hayo isipokuwa yeye ndie ayadhihirishae na mwana-damu ndio mahali pa kuthibitika matendo hayo. Na rai hii iliitwa kwa jina la Al-Jabri, yaani kutenzwa nguvu, kwani natija yake ni kuwa mwanadamu amelazimishwa (au ametenzwa nguvu) kufanya tendo zuri au kumuasi Mwenyezi Mungu, na amelazimi-shwa kufanya kazi hiyo atake asitake.

Na watu hawa wasemao au wafuatao rai hii ya Al-jabri ili kuyafanya yawe sawa waliyo yadai na kuyazua, walitegemea baadhi ya dhaahiri ya aya fulani za Quran ambazo huenda zikawa na maana hiyo kwa mbali, mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo:

 .( )Na hamtaki isipokuwa atake Mwenyezi Mungu. Na kauli isemayo: ( )

      Hayatatupata isipokuwa yale aliyotuandikia Mwenyezi Mungu. Na kauli isemayo:( )Yote hutoka kwa Mwenyezi Mungu                                              .

Hizi ni aya ambazo walidhania ya kuwa kutumia kwake matamko yakusanyayo vitu vyote na yenye mapana, yanakusanya na kuyahusu matendo mengine ya mwanadamu na kazi zake na matendo yake kwa  ujumla.

Na kikajitokeza kikundi kingine cha baadhi ya waislamu-ambao waliingiwa na hisia ya ubaya wa rai hiyo na ubatili wake- wao wakashikamana na rai isemayo kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya mwanadamu na Mola wake isipokuwa mahusiano ya uumbaji wa mwanzo. Na kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu alimuachia mwanadamu - baada ya kumuumba- uhuru wake wote na utashi wake, na akamuachia (kumtawalisha) kila kitu, na hakukubaki tena aina yoyote ya mahusiano au mawasiliano na Mwenyezi Mungu. Na msingi wa kinadharia wa fikra hii ulikuwa unatokana na nadharia waliyo shikamana nayo isemayo kuwa sababu yenye uwezo wa kukifanya kitu kiwepo - )contingency cause), inatosha kukifanya kitu kile kibakie, kiasi kwamba kubaki kwake hakuhitaji sababu tena yenye kuendelea pamoja nae, na hakihitaji isipokuwa ile sababu ya mwanzo iliyo kifanya kiwepo tu (contengency cause).

Wanazuoni wa elimu ya akida, shubha hii waliita kwa jina (Attafwiidh) yani ni Mwenyezi Mungu kumuachia na kumtege-mezea mambo yote mwanadamu moja kwa moja na hiyo ni natija ya kukatika uhusiano kati ya mwanadamu na mola wake.

Na ukweli ni kuwa rai ya katikati, kati ya rai hizi mbili ndio sahihi na Imam Swadia (a.s) alitoa ibara mzuri sana na iliyo bora na makini kuhusiana na masuala haya pale alipo sema maneno yake yaliyonakiliwa kutoka kwake na yaliyo mashuhuri:

Hakuna kutenzwa nguvu (kulazimishwa) wala kuachiliwa huru masuala haya ni kati kwa kati. Ufafanuzi wa hayo:

Hakika kila mwanadamu anafahamu kutokana  na maumbile yake mwenyewe ya kuwa anao uwezo wa kufanya mambo mengi, na kwamba anaweza kukifanya akitakacho na kukiacha akitaka-cho na sidhani ya kuwa katika watu kuna mwenye kutia shaka juu ya ubadaha na uwazi wa jambo hili na ufahamu huu, ambao ni miongoni mwa dalili za wazi juu ya utashi na uteuzi (khiari) kamili na uhuru usio na mipaka.

Na kwamba kila mwanadamu anafahamu vilevile kwa uwazi kabisa kwamba watu wote wenye akili timamu wanakubaliana juu ya kumsifu na kumpongeza mwenye kufanya matendo mazuri na kumkemea na kumbwatiza mwenye kufanya matendo mabaya, na hiyo ni dalili nyingine ionyeshayo kuwa mwanadamu anahiyari na uteuzi kamili katika vitendo vyake, kwani kama si mwana-damu kuwa na hiyari na uteuzi katika kufanya vitendo vyake isingekuwa sahihi kwa watu wenye akili kutumia maneno ya kusifu na kupongeza au kukemea na kubwatiza.

  Vilevile  kila mwanadamu anahisi- kwa kufahamu kwake mwenyewe- kwamba kitendo cha kushuka kutoka juu kwa kutumia ngazi ni tofauti sana na kitendo chake pindi anapo anguka kutoka juu angani hadi ardhini kwani anahisi kwamba kitendo chake cha mwanzo kilifanyika kwa hiari yake na cha pili alilazimika hakuwa na hiyari.

Na limethibiti -kwenye akili iliyo salama- jambo lisilo na shaka yoyote, kwamba muumba wa mambo yote haya na uwezo wote huu ndani ya mwanadamu hakujitenga na viumbe wake baada ya kuwaumba, na kwamba kubakia kwa viumbe na kuendelea kuwepo bado kunahitaji muumba kwa wakati wote, kwani muumba wa viumbe ukimlinganisha na viumbe wake si kama mjenzi ambae anajenga nyumba na kusimamisha kuta zake kisha nyumba ikawa haihitaji mjenzi wake na inaendeliea kuwepo hata kama mjenzi wake atakufa, au kama kitabu ambacho humuhitajia muandishi wake ili kipatikane kitabu hicho lakini kuendelea kuwepo na kubakia kwake ni chenye kujitosheleza yaani hakihitajii tena mwandishi wake.

Bali alieumba ulimwengu na vyote vilivyomo na waliomo ukimlinganisha na viumbe wake ni kama nguvu ya umeme na mwanga wa taa, kwani tunakuta kwamba taa haitoi mwanga ikiwa haikuungana na nguvu za umeme, na taa nayo itabaki ikihitaji nguvu za umeme kwa muda wote ili nayo iweze kubakia na iendelee kufanya kazi kwa wakati wote, na ikiwa nyaya zake zitaachana na sehemu itoayo nguvu ile ya umeme kwa kitambo kidogo tu  wakati uleule mwanga nao utatoweka.

Na hivyo ndivyo vitu vyote na viumbe vyote vimtegemeavyo muumba wake ili viendelee kuwepo kwa wakati wote na kwa kila sekunde kuanzia mwanzo wa kuwepo kwake na kubakia kwake, navyo huhitaji msaada wake kwa wakati wote.

Na kwa kufahamika hayo tuliyo yatanguliza inaonekana wazi ya kuwa matendo ya mwanadamu ni hali ya katikati kati ya Al-jabri na Attafwiidh kulazimishwa na kuachiliwa huru, yaani matendo yana nafasi kati ya pande hizo mbili, kwani kutumia uwezo wake kwenye kufanya kitendo chake au kuacha hata kama ni kwa hiyari yake, isipokuwa ni kwamba uwezo huu pamoja na vitu vingine unavyo vihitajia uwezo huu ili kuweza kupatikana, hupewa na Mwenyezi mungu mtukufu, kwa hiyo kitendo kwa upande mmoja kimetegemezwa kwa mwanadamu na kwa upande wa pili kimetegemezwa kwa Mwenyezi Mungu, na aya za Quran ambazo walizitumia kuzitolea dalili watu wa Aljabri zina muelekeo wa kubainisha kwamba uteuzi na hiyari au utashi wa mwanadamu katika kufanya vitendo vyake hauzuwii kuingia uwezo wa Mwenyezi Mungu na utawala wake, na haina maana kuwa mwanadamu amejitosheleza na Mwenyezi Mungu yaani hana haja ya uwezo wake na nguvu zake.

Mwalimu wetu Ayatu-llah Imam Khui alitoa mfano ili kufafanua maana ya kati kwa kati kwenye moja kati ya vikao vyake vya darsa zake alisema kama ifuatavyo: Lau kama mwanaadamu, mkono wake utapatwa na ugonjwa wa kupooza na akawa hana uwezo wa kuufanyisha kazi yeye mwenyewe, kisha baada ya kuonana na daktari, daktari akauwezesha mkono wake ufanye kazi, na hapo ni pale anapokiunganisha chombo cha umeme kwenye mkono wa mgonjwa, kiasi kwamba akawa ni mwenye uwezo wa kuufanyisha kazi mkono yeye mwenyewe pale anapo uunganisha na chombo kile, na mkono unarudi kwenye hali yake ya awali ikiwa atakizima chombo kile.

Kwa hivyo basi mkono unapo kuwa umeunganishwa na chombo cha umeme na kuwa na uwezo wa kuufanyisha kazi na ukaweza kufanya kazi zake za kawaida kwa wakati huo kazi ya mkono ina kuwa kati kwa kati, kwa maana kuwa mkono hautegemei nguvu za mwenye mkono moja kwa moja. Kwa sababu uwezo wake wa kufanya kazi unahitajia kuunganishwa na chombo cha umeme ambacho kina uwezo wa kuufanya ufanye kazi na hautegemei chombo cha umeme moja kwa moja au pekee, kwa sababu kufanya kazi hatakama kuna chombo cha umeme kunahitajia utashi wa yule mtu na uteuzi wake wa kufanya na kutofanya.

Na hivyo ndivyo mfano huu ulio tangulia unavyo tufafanulia jambo tunalo lizungumzia la masala ya Al-jabri na Attaf-wiidh. Kutokana na ukweli kuwa mwanadamu ni muhitaji wa vitu vya mwanzo vya msingi ili kumuwezesha kufanya kitendo fulani kama uhai na nguvu na mfano wa hayo na vitu hivyo hupewa na Mwenyezi Mungu mtukufu kwa wakati wote kwa maana hiyo hakuna Attafwiidh kuachiliwa huru au kuji-tegemea  katika mambo.

Na kutokana na ukweli kuwa halazimishwi kufanya na kuwa hafanyi chochote bila ya utashi au hiyari yake kwa hivyo basi hakuna Al-jabri kulazimishwa au kutenzwa nguvu.

Na kutokana na mazungumzo haya, hakuna kilicho bakia kwetu isipokuwa utashi au uteuzi au hiyari kamili katika kufanya na kuacha, bila kuwepo suala la kuachiwa huru kabisa wala shubha ya kulazimishwa.

Na kwa ajili ya kufaidika zaidi na kuyapambanua haya tuliyo yasema ya kuzibatilisha shubha na kuthibitisha madai yetu, tutatoa kama ifuatavyo, dalili kadhaa zihusianazo na utashi wa mwanadamu katika matendo yake, huku tukiyanukuu yaliyose-mwa katika kujibu dalili hizi na yale tuyasemayo katika kuyaba-tilisha majibu hayo:

 

1:TOFAUTI KATI YA KITENDO CHA HIYARI NA CHA           KULAZIMISHWA.

 

Tumeashiria hapo kabla dalili ya kuhisi kuwepo tofauti ya wazi kati ya kufanywa kitendo na mwanadamu kwa kukikusudia na kukipenda na kati ya kitendo akifanyacho bila kukusudia. Kwa mfano, kutetemeka kwa mkono na kutikisika, huenda ikawa ni kwa sababu ya maradhi ambapo mwanadamu hawezi kuidhibiti hali hiyo, bali akahisi kuwa hali hiyo iko nje ya uwezo wake na utashi wake. Na huenda ikawa kutetetemeka huko kumetokana na kutaka kwake kwa maana kuwa anaweza kuuzuwia na kuusimamisha pindi anapo taka.

Na hivi ndivyo ilivyo kwenye matendo kwa sura ya ujumla na katika kuhisi tofauti ya wazi kati ya matendo yatokeayo kwa hiyari na mengineyo.

Sasa ikiwa matendo yetu yote kama madai yao yalivyo-yameumbwa na Mwenyezi Mungu mtukufu na hakuna hiyari na utashi wa aina yoyote, basi ni kwanini tunahisi kuwepo kwa tofauti kubwa kati ya vitendo vifanyikavyo kwa hiyari na utashi wetu na kati ya vile ambavyo vinatokea bila hiyari yetu na hutokea kwa kulazimika?

Baadhi ya wanazuoni wa elimu ya akida wamejaribu kuleta falsafa zao (zilizo dhaifu) katika kubainisha tofauti kati ya aina mbili hizi za matendo, wakasema ya kuwa matendo ya kulazimi-shwa ni matendo ambayo hutokea au hufanywa na Mwenyezi Mungu pasina kuwepo uwezo wa mwanadamu au utashi wake katika kutokea kwa kitendo cha hiyari ambacho hufanywa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kikiwa kime ambatana na utashi wa mja wake.

Na ubatili wa kauli hii uko wazi kabisa:

Kwani uwezo ulio ashiriwa ukiwa ni kwa maana yake ya kilugha inayofahamika iliyo simama juu ya msingi kuwa:                                                                                                            Akitaka hufanya na kama hakutaka  hafanyi.     

Maana hiyo inakwenda kinyume na Jabri inayo daiwa, bali hiyo ni dalili juu ya tuyasemayo sisi ya utashi au uteuzi na hiyari. Na ikiwa ni kwa maana nyingine isiyopinga kulazimishwa basi huo si uwezo kamwe na wala haifai kuiita hivyo kamwe.

Ama utashi alio utaja huyu anayedai ujuzi wa falsafa ikiwa maana yake ni utashi (hiyari) katika matendo- kama ambavyo ni sahihi- hakika utashi huo haumo kwenye madai ya msemaji huyu, kwa sababu kitendo- kutokana na madai yake- hakifuati hiyari ya mja na utashi wake. Na ikiwa msemaji amekusudia katika neno utashi maana ya mapenzi ya kinafsi katika kutokea kwa kitendo fulani, hakika mapenzi haya, siyo ambayo hukifanya kitendo kiwe kama tuhisivyo kimaumbile, na ni mara nyingi mwanadamu akapenda kitu fulani lakini kisifanyike  kwa kupenda kwake tu, na kama mapenzi hayo hayakuwa ndio kitendo chenyewe -kama tulivyo sema-  basi tofauti waliyo iashiria kati ya vitendo vya hiyari na utashi na vitendo vya kulazimishwa inakuwa haina faida kamwe.

 

2: UWAZI WA QURAN TUKUFU KUHUSIANA NA    

                                UTASHI.

Huenda miongoni mwa dalili za wazi za utashi ambao tukombioni kuuthibitisha, ni usisitizaji wa Quran wa kuyanasibi-sha matendo kwa mwanadamu na kusema wazi kuhusu utashi wake ulio kamili, na kukitegemeza kitendo kwa mwanadamu moja kwa moja bila kuipelekea kwenye maana fulani au taawili fulani (tafsiri).

) (.Suratu-tuur:21           

Kila mtu atalipwa kwa kile alicho kichuma.

) (.Suratu-Annisaa:123

 Mwenye kufanya maovu atalipwa kwa (uovu) huo.

)   (.Suratul-Israai:7    

Ikiwa mtafanya mema mmejifanyia wenyewe nafsi zenu na mkifanya ubaya mmejifanyia nafsi zenu wenyewe.

) (.Suratul-kahfu:29

Mwenye kutaka na aamini na mwenye kutaka na akufuru.

) (

                                                                   .Suratu-Azzilzalah:7-8

Mwenye kufanya wema (hata) wa kiasi cha uzito wa mdudu chungu, atayaona malipo yake, na mwenye kufanya uovu (hata) wa kiasi cha mdudu chungu atayaona malipo yake.

) (.Suratu-fuswilat:17

Ama watu wa thamudu tuliwaongoza njia ya uongofu wakafuata njia ya upotovu na kuiacha ya uongovu.

) (Suratu-Attahrim:7

Hakika sijambo jingine ila ni kuwa mtalipwa kutokana na yale mliyo kuwa mkiyafanya.

) (.Suratu-Al-Imraan:195

Hakika mimi sipotezi amali (kazi) ya yeyote atendayo amali kati yenu.

Na aya nyengine nyingi mfano wa aya hizi tukufu na zote hizo ni dalili za wazi zinazo yahusisha matendo kwa mja na kwamba hufanyika kwa hiyari yake mwenyewe na kwamba hayafanyiki matendo hayo isipokuwa ni kwa utashi wake.

Na walitokea wengine wachache na kusema kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

) (. Suratu-Azzumar:64

Mwenyezi Mungu ndie muumba wa kila kitu iko wazi ikionyesha ya kuwa vitendo vyote vya waja navyo vimejumuishwa na neno Kila kitu vimeumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu  na sio katika ufanyaji wa mtu mwenyewe, na hayana maana nyingine maneno haya isipo kuwa ni ile maana ya Al-jabri kutenzwa nguvu kwenyewe , yaani kulazimishwa.

Na ukweli wa jambo hili ni kuwa aya hii haikuzungumzia kazi za watu na vitendo vyao, kwani aya hii iko kwenye malengo ya kuwajibu wale ambao wanaitakidi kuwepo waumba zaidi ya mmoja, kama vile muumba wa ardhi na muumba wa sayari na muumba wa watu na vinginevyo. Kwa hivyo basi majibu ya watu hao ilikuwa ni kuwaeleza ya kuwa Mwenyezi Mungu ndie muumba wa vitu vyote na havikuumbwa na muumbaji mwengine.

Ama kulihusisha neno Muumba na Mwenyezi Mungu mtukufu pekee sio dalili ya usahihi wa kujumlisha uumbaji wake kwa vitu vyote hata vitendo vya waja, kwani neno kuumba ndani ya Quran vile vile limenasibishwa kwa mwanadamu kama kauli hii ya Mwenyezi Mungu:

) (.[4]

Na pindi ulipo umba kutokana na udongo umbile mfano wa ndege kwa idhini yangu.

) (.[5]

Hakika mimi ninakuumbieni kutokana na udongo mfano wa ndege na ninapulizia ndani yake na anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

) (.[6] Na mnatengeneza uongo

)     (.[7]

 Ametakasika Mwenyezi Mungu mbora wa wenye kuumba                     ) (.[8]

Na mnamuacha mbora wa wenye kuumba 

 

Aya hizi zote ni dalili ya kwamba mwanaadamu ni muumba vilevile japo kuwa Mwenyezi Mungu ndie mbora wa wenye kuumba.

Ama kutoa dalili ya kwamba Mwenyezi Mungu ndie afanyae matendo ya watu kwa kutumia kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo:

) (.Suratu-swafaati:96

Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni na vile mvifanyavyoeti kwa kuwa aya imeeleza wazi kwamba matendo ayafanyayo mwanadamu au watu, ni matendo yaliyo umbwa na Mwenyezi Mungu mtukufu, kumepingwa kwa majibu yaliyo wazi, kwa sababu aya hii tukufu inaikamilisha aya iliyo tangulia, nayo ni kama ifuatavyo:

) (. Suratu-Aswafaati:95

Je mnaviabudu vile mvitengenezavyo?(Yaani masanamu) na jibu la swali hili ilikuwa ni aya tukufu isemayo:

( )Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni na vile mvifanyavyo.

Na kwa kukusanya kati ya aya mbili hizi inaonekana wazi kwamba makusudio ya aya hizi mbili ni kuwapinga wale ambao wana chonga masanamu kutokana na mawe au wanayatengeneza kutokana na tende -kwa mfano- kisha wakayaelekea na kuya-abudu na kuyatolea sadaka. Naye Mwenyezi Mungu alie takasika kwa kutumia aya hizi akawabainishia kuwa ndie alie waumba hao washirikina na akavitengeneza vile vitu wavitumiavyo kuchonga masanamu yao. Na aya hizi hazina mahusiano yoyote na matendo ya waja na kazi zao, na matendo yao mbalimbali wayafanyayo.

 

 

3: ADHABU NI DALILI YA UTASHI.

 

Hakika adhabu ya Mwenyezi Mungu imuelekeayo mfanya maasi - kama ilivyoelezwa kwenye Qurani tukufu- ni dalili ya wazi juu ya mwanadamu kuwa na hiyari na utashi kwenye matendo yake.

)      Suratu-Azzumar:65  

Ikiwa utamshirikisha Mwenyezi Mungu, matendo yako yataporomoka na utakuwa miongoni mwa watu wenye hasara.

) (.Suratul-Qasas:84

     Na hawatalipwa wale ambao walifanya maovu isipokuwa yale waliyo kuwa wakiyafanya.

) .(

                                                                                              Suratul Annur:24 .                                                                       

     Siku ambayo ndimi zao na mikono yao na miguu yao vitawatolea ushahidi juu ya yale waliyo kuwa wakiyafanya.

) (.Suratu-Assajda:14

Na onjeni adhabu ya milele kutokana na mliyokuwa mkiyafanya.

) (.Suratu-Azzumar:24

Na wakaambiwa madhalimu, onjeni malipo ya yale mliyo kuwa mkiyachuma.

) (.Suratu-nuur:63

Na wajihadhari wale ambao wanakhalifu amri zake.

) (.Suratu-sabaa:12

Na mwenye kwenda kinyume na amri zetu tutamuonjesha adhabu ya moto mkali.

 Ama Mwenyezi Mungu kuwa ndie ayawekae (kuyaumba) matendo kwa mja wake, kisha amuadhibu juu ya matendo yale, jambo hilo ni muhali bila ya shaka yoyote, kwani hiyo ni dhuluma ya wazi kabisa tunamtakasa Mwenyezi Mungu na dhuluma hiyo kama alivyo jitakasa nafsi yake:( ).

Na mola wako si mwenye kuwadhulumu waja.

  ( ) 

  Hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.

  ( ) Na mimi si mwenye kuwadhulumu waja.

  ( )                                                                          Na Mwenyezi Mungu hapendi dhuluma kwa walimwengu.

 ( )         .

 Na Mwenyezi Mungu si mwenye kutaka dhuluma kwa waja.      (   )      

 Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata kiasi cha tembe moja ya sisimizi.

( )                                                                         Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote.

 (   )                                                 

Na mola wako hamdhulumu yeyote.

 

Na baadhi ya wanazuoni waliobobea wa akida walijaribu kusahihisha maana ya kumnasibisha Mwenyezi Mungu na dhulu-ma, na wakasema  maneno ambayo muhtasari wake ni kama ufuatao:

Hakika dhuluma sio mbaya kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu dhuluma mbaya ambayo akili huichukia ni kumfanyia uadui mtu mwingine, sawa uadui huo uwe kwenye mwili wake au heshima yake au mali yake. Ama mtu kutumia anacho kimiliki, kufanya hivyo si vibaya, kutokana na uhuru kamili alio nao wa kufanya atakavyo kwenye vitu hivyo, bila ya kuwepo kizuizi au masharti, na miongoni mwa uhuru huo ni uhuru wa Mwenyezi Mungu kufanya atakavyo kwenye viumbe vyake, kwa kuzingatia kuwa yeye ndie muumba na mmiliki wa vitu hivyo, na kwa kuzingatia kuwa kila kilicho kwenye ulimwengu huu ni miliki yake na kinanyenyekea chini ya uwezo wake na utawala wake, kwa hivyo ana hiyari ya kufanya atakavyo, kama kumuadhibu amtakae hata kama ni muumini, na kumneemesha amtakae hata kama ni kafiri, kwa sababu wote au vyote hivyo ni milki yake na viko kwenye utawala wake.

)                                                        (

(Yeye Mwenyezi Mungu) haulizwi kuhusu yale ayafanyayo nao (waja) huulizwa. Na akili ya mwanadamu haina haki ya kujitwe-za hadi kwenye daraja ya Mwenyezi Mungu na kuvihukumu vitendo vyake kuwa ni vizuri au vibaya.

Shubha hii imepingwa vikali na kubatilishwa pande kadhaa:

Kwanza: Ni kwamba malengo ya utafiti huo sio kuweka au kubainisha hukumu ya akili juu ya Mwenyezi Mungu, bali ni kuweka wazi kinacho tarajiwa katika fadhila zake na upole wake kwenye matendo ya waja wake. Na hakika sisi tunakubali kiukamilifu kwamba kuamrishwa kutenda jambo ambalo ni muhali, au kuamrishwa kufanya jambo ambalo liko juu ya uwezo wa mwanadamu, na kumuingiza mfanya makosa au muovu peponi na mtu mwema motoni, hayo yako chini ya uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu. Kwa uwezo wake na utawala wake alie takasika anao uhuru wa kufanya hivyo na kuamuru kitendo kama hicho. Lakini sisi tunayakini kwamba yeye Mwenyezi Mungu hatofanya hivyo, kutokana na utukufu wake, fadhila yake na ukarimu wake, wala si kwamba hawezi kufanya hivyo kutokana na kuzembea au kushindwa.

Pili: Hakika kauli ya kwamba dhuluma si mbaya itampelekea mwanadamu kuacha kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu mtukufu, kutokana na kutokuwepo imani ya kuwa hukumu itolewayo ni sawa na sahihi na kwamba matokeo yaliyo patikana ni sawa na kuto kuwa  na uhakika na utulivu wa moyo kwamba Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na ahadi zake hata kama amesema: ( )

Hakika Mwenyezi Mungu hakhaalifu ahadi zake, kwani yote hayo yanategemea kauli ya ubaya wa dhuluma, uongo na kwenda kinyume na ahadi. Ama maudhui ya ubaya wa dhuluma yaki-toweka na kubatilika kama walivyo dai mabwana hao hakuta-kuwa na imani na matumaini na utulivu wa moyo wa kumfanya mwanadamu afanye utiifu kwa amri za Mwenyezi Mungu na kuyapinga matamanio yake na kupigana na nafsi iamrishayo maovu.

Tatu: Hakika maana ya dhuluma haifungiki tu na kitendo cha kumfanyia uadui au kumchokoza mtu mwengine, bali kila aina ya utokaji wa mja kwenye njia ya kati na mwelekeo wa aina yoyote wa utovu wa kiasi au kupitukia mipaka kwenye matendo, vile vile ni dhuluma, na kati ya hayo ni kama usikiavyo ya kuwa fulani amedhulumu nafsi yake, na hukusudiwa kuwa mtu yule ametoka na kuvuka ile hali ya kati, katika matendo yake kwenye kula au kuvaa au kutoa matumizi, pamoja na kuwa yote hayo ni milki yake, na ana uhuru wa moja kwa moja kuvitumia vitu hivyo kama atakavyo, lakini pamoja na kuwa ana uhuru huo akifanya hivyo atafahamika kuwa anafanya dhuluma kwa jinsi inavyo fahamika kwa watu wote (kwenye jamii zote).

Kwa mfano ikiwa mtu fulani atamuadhibu mnyama anae mmiliki pamoja na kuwa mnyama yule ni mtiifu kikamilifu na hamuudhi mwenye kummiliki, je kufanya hivyo itakuwa ni sawa kwa kutoa udhuru au sababu ya kuwa mnyama huyu ni milki yake au ni mali yake?

4: Dhuluma ni mbaya.

Lau kama mwanadamu asingekuwa ni mwenye uteuzi katika vitendo vyake na mwenye uwezo wa kufanya au kutofanya  au mwenye kukifanya kitendo kile kwa utashi na hiyari yake, Mwenyezi Mungu angekuwa ni dhalimu kuliko madhalimu wote, kwani kumuadhibu mfanya makosa ni jambo lisilo na shaka. Na kutokana na kuwa maasi -kama madai yasemayo- hayakufanyika kwa hiyari ya mwanadamu, kwa hiyo kumuadhibu mwanadamu huyo itakuwa ni aina mbaya sana ya dhuluma.

Na wale wenye kuamini Al-jabri walitoa majibu ya aina mbili kuhusu suala hili:

Kwanza: Hakika adhabu haitolewi kwa sababu ya kitendo bali hutolewa kutokana na kuchuma au aliyo ya chuma. Na sisi katika kuwajibu na kupinga hilo tunasema:

Hakika linalo fahamika katika maana ya kilugha na matumizi ya Qurani ya neno Ȼ (kuchuma) ni kitendo kilicho simama katika msingi wa uteuzi au utashi au hiyari ya mtu. Mwenyezi Mungu amesema:

] [Suratu-Annisaa:111

Na mwenye kuchuma dhambi hakika si jambo lingine (bali) anaichuma kwa ajili ya nafsi yake.

( ]

 Suratul-baqara:286 (Nafsi) faida  ya iliyo yachuma ni yake na (hasara ya) yale iliyo yachuma ni yake.

) (Suratul-maaida:38

Na mwizi wa kiume na mwizi wa kike ikateni mikono yao, ikiwa ni malipo ya yale waliyo yachuma.

) (Suratu-yuunusu:27

Na wale ambao wamechuma maovu malipo ya uovu ni mfano wake vilevile.

      ) (.am:120Suratul-An

Hakika wale ambao wanachuma (au wanafanya) madhambi watalipwa kwa yale waliyo kuwa wakiyachuma.

Na aya nyengine nyingi tukufu zinazo julisha ya kuwa kuchuma ni kitendo kifanyikacho kwa utashi na hiyari na kutii, na  miongoni mwa masharti yake ni kuwa na uwezo utokanao na mtu mwenyewe. Lakini wakati walipo fahamu watu hawa ubatili wa madai yao kwa ujumla wakadai kwamba, kuchuma kunako-pelekea kuadhibiwa ni kitendo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kikiwa kime ambatana na utashi wa mwanadamu ili kitendo kile kiweze kuthibitika nje.

Na tunawajibu kwa maneno haya:

Kwamba uambatano huo hauko kwenye uteuzi na utashi wa mtu kwa hivyo haifai kuadhibiwa kwa uambatano huo, kwa sababu mwanadamu kutokana na madai ya watu hawa hana isipokuwa utashi (mapenzi) wa kuthibitika kitendo kile, ama kufanyika kitendo chenyewe ni kuwa kimetoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na madai yao. Na uambatano ulitokea kati ya utashi na mja, na Mwenyezi Mungu kukifanya kitendo kile kiwepo vimethibitika kwa utashi wa Mwenyezi Mungu, na kwa kitendo chake na nguvu zake kwa kuzingatia kuwa yeye ndie mfanyaji hasa wa kitendo kile kulingana na madai yao, sasa ni vipi inasihi kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kumuadhibu mja kwa kitendo ambacho hakukifanya na kwa kuambatana tu bila kuwa na uteuzi au utashi kwenye kitendo kile.

Pili:Hakika dhuluma ya Mwenyezi Mungu mtukufu kwa waja wake sio mbaya kwani ni sehemu ya matumizi ya mmiliki wa kitu kilicho kwenye milki yake na utawala wake na tume-kwisha batilisha na kuipinga kauli hii na kueleza kwa uwazi makosa yaliyoko kwenye kauli hii na kwa sababu vitendo havina sifa za kidhati kiasi kwamba ikafaa kuvisifu kwa sifa ya uzuri au ubaya, bali uzuri na ubaya katika vitendo vya waja umetokana na sheria, basi kitendo kilicho kuwa ni kibaya, na kilicho amrishwa na sheria ndicho kiitwacho kizuri, na lau kama sheria itarudi kwenye kitendo ilichokikataza na kukiamrisha au ilicho kiamri-sha ikakikataza hapo ina maana kibaya kitageuka na kuwa kizuri na kizuri kuwa kibaya.

Na ikiwa uzuri wa matendo au ubaya wake hutokana au hutolewa kwenye sheria pasina kutolewa kwenye akili kutokana na madai yao, basi vitendo vya Mwenyezi Mungu mtukufu havitasifiwa na hali ya uzuri au ubaya, kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu yuko juu ya sheria au kukalifishwa chochote, na natija yake inakuwa kwamba yote ayafanyayo Mwenyezi Mungu -hata kama kutakuwa na dhulma kwenye matendo yale- ni mazuri na mema na kwamba akili haina uwezo wa kuhukumu ubaya wa kutotenda dhuluma kwa Mwenyezi Mungu alietakasika.

Na ni vizuri kwetu kabla ya kubainisha rai iliyo sahihi katika maudhui haya tuashirie na kuelezea kuwa ubaya na uzuri una maana tatu.

Maana ya kwanza:

Ni kuyatumia maneno uzuri na ubaya kwa maana ya ukamilifu na kasoro kwa mfano elimu ni nzuri na ujinga ni mbaya, na ushujaa na ukarimu ni vitu viwili vizuri, na kinyume chake ni woga na ubahili, na hivi viwili ni vibaya.

Na katika maana hii kuna tofauti kati ya wanafikra kwani ni miongoni mwa mambo ambayo yana aminiwa na yamethibitika katika matumizi ya watu na watu huyatumia.

Maana ya pili:

Kutumiwa neno uzuri au ubaya kwa maana ya mambo yaipendezayo nafsi na kupendwa na nafsi au yaichukizayo nafsi. Kwa mfano hii ni mandhari nzuri na hii ni sauti nzuri, kula chakula pindi unapokuwa na njaa ni jambo zuri na mengineyo, kama isemwavyo: Mandhari haya ni mabaya na sauti ya maumivu ni mbaya. Na maana hii haina mzozo kati ya pande mbili zenye kujadiliana, kwani maana hiyo imetokana na hisia za ndani ya nafsi ikiwa mbali na hukumu ya sheria na amri zake.

Maana ya tatu:

Ni kutumiwa neno uzuri au ubaya kwa kitendo kinachofaa kusifiwa au kukemewa na huwa ni sifa kwa maana hii katika vitendo vilivyo fanyika kwa hiyari, kiasi kwamba inakuwa uzuri ni ule ambao alie ufanya anastahili kusifiwa na kupewa malipo mema mbele ya watu wenye akili. Na ubaya ni ule ambao  mfanyaji wake anastahili adhabu mbele ya watu wote wenye akili.

Na maana hii ya tatu, ndio sehemu yenye mzozo. Wafuasi wa madhehebu ya Asharia, wao wamepinga kuwepo hukumu ya akili kwenye uzuri wa vitendo au ubaya wake, bali wamesema kilicho hukumiwa na sheria kuwa ni kizuri hicho ndicho kizuri, na kilicho hukumiwa na sheria kuwa ni kibaya hicho ndicho kibaya, na akili haina nafasi yoyote kwa yote hayo.

Na madhehebu ya Imamiyya (yaani Shia ithina-asharia), pamoja na madhehebu ya muutazila, wamepinga fikra hii na kusema:

Hakika matendo yana kima maalum kwenye akili ukiachilia mbali hukumu ya sheria, kuna matendo ambayo yenyewe ni mazuri katika dhati yeke, na kuna matendo ambayo ni mabaya kwa dhati yake, na kuna matendo ambayo hayana sifa moja wapo kati ya sifa hizi mbili, na sheria tukufu haiamuru isipo kuwa kilicho kizuri na haikatazi isipokuwa kilicho kibaya. Kwa mfano, ukweli wenyewe ni mzuri na kutokana na uzuri wake Mwenyezi Mungu ameamrisha kujipamba na ukweli, na haina maana kuwa umekuwa mzuri baada ya Mwenyezi Mungu kuuamrisha, na uongo wenyewe ni mbaya na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu amekataza kujipamba nao, na haina maana ya kuwa umekuwa mbaya baada ya kukatazwa.

Na dalili yetu juu ya haya ni kuwa hata wasio fuata na kufungika na sheria za dini -na aina zote za vikundi- huusifu ukweli kuwa ni mzuri na kuusifu uongo kuwa ni mbaya, bila ya kuwa hukumu ya sheria ina athari yoyote au kuwa ndiyo iliyo wafanya watoe sifa hii ya uzuri au ubaya.

Kutokana na dalili hii inaonekana wazi kuwa uzuri na ubaya ni mambo mawili ya kiakili kabla hayajawa ya kisheria, na kwamba uadilifu ni mzuri kabla ya kusifiwa na sheria, na dhuluma ni mbaya kwa sababu ni dhuluma, bila kuwepo mahu-siano yoyote na dalili ya kisheria na hukumu ya dini katika kulisifia hili ni zuri au lile ni baya.

Kwa hivyo basi, ni lazima Mwenyezi Mungu awe muadilifu kutokana na hukumu ya akili kwa sababu uadilifu ni mzuri, na ni muhali kuwa dhalimu, kutokana na hukumu ya akili vilevile kwani dhuluma ni mbaya.

Kwa maneno mafupi ni kuwa:

Hakika dalili zote za Quran na akili zinaeleza wazi kuwa mwanadamu ana hiyari na uteuzi kwenye vitendo vyake, na ana uhuru kamili katika mambo ayafanyayo halazimishwi wala kutenzwa nguvu, na kwamba shubha zote zilizo tolewa kuhusiana na Al-jabri (kulazimishwa au kutenzwa nguvu) hazina nguvu ya kusimama na kuthibiti mbele ya dalili zilizo wazi na dalili zikatazo mzizi wa fitina. Na Mwenyezi Mungu amesema kweli aliposema:

) ǡ ǡ ǡ

   (.

Na nina apa kwa nafsi na alie itengeneza kisha akaifahamisha uovu wake na uchamungu wake, hakika amefaulu mwenye kuitakasa, na amepata hasara mwenye kuitweza, mwenye kuishu-sha kutoka kwenye nafsi yake na usafi na kuipamba kwa madhambi. Suratu-Ashamsi:7-10.

 

***

 

QADHAA YA MUNGU NA MAKADIRIO YAKE

(ALQADHAA WAL QADAR)

 

Utafiti ufanywao kwenye masala ya Al-qadhaa wal-qadar, hukumu na makadirio yake, hata kama wanazuoni wa elimu ya akida watayapa anuani mahsusi ni sehemu isiyo jitenga, katika maudhui ya Al-jabri wal-Ikhtiyari (kutenzwa nguvu na uteuzi), na ni sehemu ikamilishayo maudhui hayo, kwa sababu -kinadha-riya- yamesimamia kwenye msingi uleule wa kifikra ambao masala mama (ya asili) tuliyo yaelezea yamesimama juu yake.

Na sisi hatutaki kwa uzungumzaji huu wa haraka kukusanya pande zote za maudhui haya, kwa sababu pande nyingi hazihitaji kurefushwa kusiko na faida, bali lengo tunalo likusudia hapo ni kuweka wazi maana ya kiislamu ya masala haya kama kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna tukufu za Mtume (s.w.a) vinavyo-tuonyesha ili tufahamu yanayo tupasa kuyaamini katika msingi huu muhimu kati ya misingi  ya dini, na hasa ukizingatia kuwa tunawaona watu wakiyabebesha masala ya Al-qadhaa wal-qadar hukumu ya Mungu na makadirio yake, mambo yao yote wayafanyayo kila siku, kama mabalaa na uovu na kheri na sharri na wema. Je yote hayo ni katika mambo ya kweli ya kuamini na ni katika fikra za uislamu?

Na tukiwa katika hali ya maandalizi kwa ajili ya kuweka wazi ufahamu wa kiislamu ulio salama kuhusu fikra hii, ni vizuri kuonyesha kwa ufupi maana ya maneno haya mawili kama yalivyo elezwa na kutolewa kwenye kamusi za lugha na kama yalivyo tumika ndani ya Quran tukufu, ili kutokana na ufahamu huu na kupitia njia hii ya kufamu maana yake tuweze kufahamu lengo la sheria kuhusu maneno haya katika matumizi yake kwenye dalili za kiislamu.

1: Maana ya kilugha:

Al-qadhaa: Ina maana ya kazi, na ina maana ya kutengeneza na kukadiria. Kwa mfano husemwa: 

Kwa maana kuwa amekitengeneza kitu na kukikadiria na kila kitu kilicho tengenezwa kwa makini na kutimizwa au kukamili-shwa au ametekeleza jambo fulani kama linavyo takiwa au kimewajibishwa au kueleweka au kutekelezwa, kimefanywa na kupasishwa  ina maana kitu hicho kimepatwa na Qadhaa. Na hutumika neno  kwa maana kuwa imehukumiwa. Na katika matumizi yake hutumika kwa maana ya kutoa hukumu ili kuondoa tofauti kati ya watu wawili.

Na neno Al-qadhaa, lina maana kutoa habari au kufikisha habari kama wasemavyo:

߻[9], Kwa maana kuwa tumemfikishia habari za jambo hilo.

       Ama neno Al-qadar ina maana ya kuhukumu.

"

2: Maana yake kwenye Qurani:

limetumika neno Al-qadhaa kwenye quran- kwa maana zifuatazo:

       A: Kuumba na kukifanya kitu kiwepo kama kauli ya Mwenyezi Mungu isemavyo: ( ) Suratu-fuswilat:12 Na akazitengeneza (kuziweka mbingu saba) kwa maana ya kuwa akaziumba na kuzifanya ziwepo.

      B: Hutumika kwa maana ya kuwajibisha na kuhukumu, kama

alivyo sema     kwenye kauli yake ( )  Suratul-Israai:23.Na Mola wako amehukumu ya kwamba msimuabudu yeyote isipokuwa yeye. Hapa limetumika kwa maana ya kuwajibisha na kuhukumu.

      C: Hutumika kwa maana ya kutoa habari kama kauli yake isemavyo:

( ) Suratul-Israai:4.

Na tuliwafahamisha (na kuwapa habari) wana wa Israil kwenye kitabu kwa maana ya kuwa tuliwajulisha na tukawapa habari.

Na limetumika neno Al-qadari kwenye Quran katika maana mbili zifatazo:

A: Limetumika kwa maana ya kuumba, na kupangilia, na kuweka nidhamu na kuweka utaratibu kama kauli isemavyo:

 Surat-Fuswilat:10 ( ).

Amekadiria ndani ya ardhi riziki za watu. Na kauli yake isemayo:

Surat Yaasin:39 ( ).

Na mwezi tumeukadiria kwenye vituo maalumu.

( ). Suratul-muzzammil:20 Anaukadiria usiku na mchana.

( )Suratul-furqaan:2Na akaumba kila kitu na akakikadiria, kwa kukiweka sehemu inayotakiwa.

B: Hutumika kwa maana ya kueleza wazi na kutoa habari kama kauli yake isemavyo:( ) Suratul Annaml:-57.Isipo kuwa mwanamke wake tuliwapa habari ya kuwa yeye atakuwa ni miongoni mwa wale wenye kuangamia. Kwa maana ya kuwa tuliwapa habari na kuwafahamisha wazi kuwa yeye ni miongoni mwa watakao angamia.

Na ikiwa maana ya kilugha imekuwa wazi kwenu sehemu ambazo Quran imeyatumia maneno hayo mawili, sasa imekuwa ni lazima kuyanasibisha au kuyahusisha matendo yetu na qadhaa na qadar, na uwe uhusiano huo unawiana na maana hizi na unakusudia maana hizi, wala usitoke na kuwa nje ya maana hizi. Tutakaposema kwamba kitendo chetu fulani kilifanyika kwa qadhaa ya Mwenyezi Mungu na qadari yake ni nini makusudio ya maneno hayo?

Hakika sisi hatuwezi kuyatafsiri maneno hayo kwa maana ya kuumba ambayo ni moja kati ya maana za maneno Al-qadhaa wal-qadarkutokana na tuliyo yaelezea mwanzo kwenye kifungu kilichopita kwamba vitendo vyetu hufanyika kwa hiyari yetu na utashi wetu na sisi ndio tuvifanyavyo, si kwa kuumbwa na Mwenyezi Mungu na kuvifanya viwepo.

Na maana hii ikibatilika kwa hukumu ya dalili, makusudio ya maneno haya mawili yatafungika, kwa maana fulani tu, kiasi kwamba itakuwa qadhaullah ina maana kuwajibisha kwake na kuhuku-mu kwake, na qadari yake kwa maana ya kubainisha na kujua kwake (elimu yake), na inakuwa maana ya maneno yetu tutakayo sema ya kwamba kimetokea au kimefanyika kitendo fulani kwa qadhaa ya Mwenyezi Mungu na qadari yake, ni kuwa kimefanyi-ka kwa kuwajibisha kwake na ubainishaji wake na kwa kukijua.

Na kwa msingi huu tunakuwa ni wajibu kuridhia qadhaa ya Mwenyezi Mungu na qadari yake kwa maana kuwa ni lazima kukubali na kusalim amri na kuamini na kukiri kwa lile alilo liwajibisha Mwenyezi Mungu kwetu na kutuwekea wazi amri na hukumu, na hayo ndio makusudio, na hakuna makusudio mengineyo.

Na dalili ya usahihi wa ufahamu huu, yanatutosha aliyo yasema Amirul-muuminiin Ali (a.s) katika jibu lake alilomjibu mtu wa sham alipokuwa akielekea Swifiin, kwa suali lake:je kwenda kwako Swifiin ilikuwa ni kwa qadhaa ya Mwenyezi Mungu na qadari yake?

Imam Ali (a.s) akamjibu:

Ndio, ewe sheikh, hampandi kilima wala kushuka kutoka kwenye jangwa isipokuwa ni kwa qadhaa na qadari kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Yule mtu wa Sham akasema:

Ninadhani taabu yangu inatoka kwa Mwenyezi Mungu ewe kiongozi wa waumini. Imam Ali (a.s) akasema:Nyamaza ewe sheikh, hakika Mwenyezi Mungu ameyafanya makubwa malipo yenu katika mwendo wenu huu hali ya kuwa nyinyi mnatembea, na katika makazi yenu hali ya kuwa mmetulia, na katika kutembea kwenu hali ya kuwa mnatembea na katika mambo yenu yote (myafanyayo) hamkuwa wenye kulazimishwa.[10] Kisha Imam akasema:

ϻ

Huenda wewe umedhania ya kuwa qadhaa ni lazima na qadari ni lazima iwe, lau kama ingekuwa hivyo malipo mema na adhabu vingebatilika na bishara na vitisho vingeporomoka, yaani zisingekuwa na maana.

Hakika Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waja wake kwa kuwahiyarisha (kawapa hiyari), na akawakataza kwa kuwataha-dharisha na akawakalifisha watu sheria zilizo nyepesi na hakuwakalifisha sheria zilizo nzito, na akatoa malipo mengi kwa kazi ndogo.[11]

Hakika sentensi hii ya kialawiy iliyosemwa na Ali (a.s) na yenye ufasaha iko wazi katika kuitolea dalili juu ya usahihi wa yale tuliyo yasema, kwani alisema wazi kuwa safari ya kuelekea Sham ilikuwa ni kwa kuwajibishwa na Mwenyezi Mungu mtukufu na ilikuwa ni kutokana na hukumu yake ikiwa na maana hukumu ya Mwenyezi Mungu ya kuwajibisha kuwapiga vita watu madhalimu, na kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu ameyafanya makubwa malipo ya wale wapiganaji kwa sababu wao walifanya hivyo kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na kwa kutii amri yake.

Amirul-muuminiin (a.s) amesema kwenye maneno yake katika kuwataja malaika:

[12]

Na miongoni mwao kuna waaminifu juu ya wahyi wake, na kuna wapishanao kwa mitume wake, na wajumbe waendao kwa mitume wake, na kuna wapishanao kwa qadhaa yake na amri zake.

Na qadhaa na amri hazikusudiwi isipokuwa yale mambo ya wajibu na hukumu mbalimbali ambazo hubebwa na malaika hadi kwa mitume na manabii ili wazifikishe kwa watu wao na kaumu zao.

Imam Swaadiq (a.s) katika kufafanua Imani ya Qadari anasema:

Watu katika suala la qadari wako mafungo matatu:

1: Kuna mtu anae dai ya kwamba mambo yote yametegeme-zwa kwake, hakika mtu huyu amemfanya Mwenyezi Mungu kuwa dhaifu kwenye utawala wake, na yeye ni mwenye kuangamia.

2: Na mtu wa pili ni yule mwenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha waja kufanya maasi na kuwakalifisha kufanya mambo wasio na uwezo nayo. Huyu amemdhulumu Mwenyezi Mungu kwenye hukumu zake nae ni mwenye kuanga-mia.

3: Na mtu wa tatu ni yule mwenye kudai ya kuwa Mwenyezi Mungu amewakalifisha waja mambo wawezayo kuyafanya na hakuwakalifisha kufanya mambo wasio na uwezo nayo yaani yaliyo juu ya uwezo wao, akifanya wema humshukuru na kumsifu Mwenyezi Mungu na akikosea humuomba Mwenyezi Mungu msamaha, na huyu ndie muislamu[13].

Na hivi ndivyo inavyo kuwa qadhaa ya Mwenyezi Mungu na qadari yake, kwa ibara nyingine ni amri zake na hukumu zake na mambo ya wajibu (taklifu) yaelekezwayo kwa waja na kuridhia kwetu uislamu na kukiri kwetu sheria  ni kuridhia qadhaa ya Mwenyezi Mungu na kukiri au kukubali qadari yake.

 

 

 

UONGOFU NA UPOTOVU.

 

Maneno yaliyo baki ni kuhusu masala ya Uongofu na upotovu, masala ambayo wanazuoni wameyahesabu kuwa ni katika vifungu vya masuala ya Al-jabri na ikhtiyaari na qadhaa na qadari. Zimekuja kwenye quran tukufu aya nyingi ambazo humpa hisia mtu kutokana na dhahiri ya aya hizo ya kuwa Mwenyezi Mungu mtukufu ndie ambae anawaongoza na kuwapoteza watu pasina mwanadamu kuwa na hiyari katika hayo.

     ( )                                                                Na humpoteza amtakae na kumuongoza amtakae 

    ( )             

    Na mwenye kupotezwa na Mwenyezi Mungu hana awezae kumuongoza. Basi ikiwa uongofu na upotovu hutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa nini anawaadhibu waliopotea juu ya upotovu wao nakuwapa malipo mema waumini juu ya uongofu wao, na yote mawili hayo ni katika vitendo vya Mwenyezi Mungu mtukufu na ni kwa utashi wake?

Ni vizuri kwetu kabla ya kujibu shubha hii tuonyeshe maana ya neno Al-huda na Adhwalaal kama yalivyo elezwa kwenye vitabu vya lugha na kama quran ilivyo yatumia kwenye aya zake, ili tufahamu malengo ya maneno hayo, bila kuchanganya au kutofahamika.

Asili ya neno Al-hidaya kwenye lugha ni kuongoza au kujulisha kwenye njia ya uongofu.[14] ޻ kwa maana amemjulisha na kumtambulisha njia. Na asemapo Nimemuelekeza njia na nyumba ina maana Nimemfahami-sha. Na Alhuda (uongofu) kinyume chake ni Adhwalaal (upotovu), nao ni muongozo na kujulisha.[15] Na husemwa: [16] ߻Kwa maana ya Nimekubainishia kama Mwenyezi Mungu alivyo sema:( ) Je haijawabainikia. Ama kauli yake isemayo:                                            

                                           ( )                                            

 Ambae kila kitu amekipa umbile lake linalo stahili kisha akakiongoza kwenye umbo ambalo kitanufaika nalo kisha akakiongoza kwenye maisha yake.[17] Nalo Al-hidaya katika maneno ya waarabu lina maana tawfiiq, amesema mshairi mmoja:

                                                  Anakusudia    kwenye kipande hiki cha shairi kuwa:

Mwenyezi Mungu akuafikishe (akujalie) kukidhi haja zangu[18]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

( ) kwa maana ya kuwaWaongozeni kwenye njia ya motoni. Yaani Waingizeni motoni kama  ambavyo mwanamke huongozwa kwenda kwa mumewe kwa maana ya kuwa anaingia kwa mumewe.[19] Na mwenye kuwatangulia watu na kuwajulisha njia huitwa haadin,[20]na Al-hidaya ni thawabu.[21]

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu                 : 

( )

Anawalipa Mola wao kwa imani zao yaani limetumika kwa maana anawapa thawabu. Na pia amesema:

        ( )                               

 Na Mwenyezi Mungu hawalipi mema watu madhalimu.

        ( )                                                                   Na Mwenyezi Mungu hawalipi mema watu walio makafiri.

        ( )              

Na Mwenyezi Mungu hawalipi mema watu waovu.

       ( )              

Hakika Mwenyezi Mungu hatavilipa wema vitimbi vya wafanya khiyana. Hapa limetumika kwa maana ya hawapi thawabu au hawalipi mema. Na vilevile kuna kauli yake nyingine isemayo:

                                          

Si juu yako kuongoka kwao lakini Mwenyezi Mungu humlipa wema mwenye kutaka.

Yaani si juu yako kuwalipa mema lakini Mwenyezi Mungu anamlipa wema mwenye kutaka. Na asili ya neno Adhwalaal ni maangamio kama kauli ya Mwenyezi Mungu isemavyo:

( ) yaani tukiangamia ardhini Na neno Adhwa-laal katika dini, ina maana kwenda kinyume na haki na Al-idhlaal huwa na maana kuwalingania watu kwenye upotofu na kuwavutia huko,  kama kauli yake isemayo:

       ( ) Na saamiriy akawapoteza. Na huwa lina maana pia ya kuwapeleka wafanya maasi motoni.[22]

Kwa hivyo basi, ukiangalia kwa makini katika maana hizi ambazo hutumika katika  tamko Al-huda na Adhwalaal, kunatufahamisha yafuatayo:

1: Hakika neno Al-idhlaal pengine hutumika kuashiria kwenye hali ya kwenda kinyume na haki na kulingania kwenye upotovu na kuwaitia watu huko. Na maana hii sio maana ambayo tunaweza kumuhusisha nayo Mwenyezi Mungu (kumsifu nayo)

       (     )                                                     

Suratul-Attawba 115. Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwapoteza watu baada ya kuwaongoza.

        Bali upotovu -kama Quran ilivyo eleza wazi- hautathibiti isipokuwa kwa kufanywa na mwanadamu na kwa hiyari yake mwenyewe. Mwenyezi Mungu amesema:

( ).Suratu-Annisaa:16.

Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu hakika amepotea upotovu ulio mbali na haki.( ). Suratu-Assabai 50. Sema ikiwa nitapotea hakika si jambo jingine bali ninapotea kwa kuidhuru nafsi yangu mwenyewe. 

        (     )

   Suratul-Israai:5.Mwenye kuongoka hakika huongoka kwa ajili yake mwenyewe na mwenye kupotoka hakika hupotoka juu ya nafsi yake.

         ( ).                                                          Suratul-Qalam:7.Hakika mola wako ndie mwenye kuwajua zaidi waliopotea kunako njia yake. Vilevile hutumika kwa maana ya kubatilisha na kuangamiza kama kauli yake isemayo:

          (   ).

     Suratul ghafir:74. Na hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu awaangamizavyo makafiri. Na kauli yake isemayo:

 

 

 

    

 

 [23]( )                                                                  Na mwenye kuangamizwa na Mwenyezi Mungu hana awezae kumlipa mema yaani mwenye kuangamizwa na Mwenyezi Mungu kati ya makafiri na madhalimu, hana awezae kumlipa wema. Na kauli yake isemayo:( )[24]

Na wale ambao wameuliwa kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, hayatabatilishwa matendo yao.

2: Hutumiwa neno Al-huda kwa maana kuongoza kwe-nye haki kama kauli yake isemayo:

        ( )[25]Sifa njema (Hi-midi) zote ni zake Mwenyezi Mungu ambae ametuongoza kwa hili,  na hatukuwa ni wenye kuongoka lau kama asingelituongoza Mwenyezi Mungu.

).                                                  [26](                              

Bali Mwenyezi Mungu ana kusimbulieni kwa kukuongozeni kwenye Imani. Na kauli yake isemayo:

( )                        

 Ama watu wa Thamud tuliwaongoza, wakafuata upofu (upotovu) na kuacha uongofu (waka ufadhilisha upofu juu ya uongofu)[27].

Kama ambavyo pia hutumika neno Al-hudaa kwa maana ya kutoa thawabu au malipo, kama kauli hii isemavyo:           

(    )         

Atawalipa mema na kuzifanya nzuri hali zao[28], kwa maana kuwa atawapa thawabu. Na kutokana na muhtasari huu wa maana ya neno Al-hudaa na Adhwalaal, tuna fikia kwenye natija ya maudhui yetu, nayo ni:

Hakika neno Al-idhlaal lililotumika kwa maana ya kuashi-ria hali iliyo kinyume na haki, ni muhali kwa Mwenyezi Mungu kwani yeye ndie muamrishaji wa haki, na haifai kiakili kuwa yeye aashirie au aamrishe kinyume na haki kamwe.

Na neno Al-hudaa lilitumika kwa maana ya kujulisha (kuonyesha au kuelekeza) kwenye njia ya haki, Mwenyezi Mungu amekwisha fanya hivyo na kuithibitisha maana hiyo kwa kutuma wajumbe (Mitume) na ma Nabii na akateremsha vitabu toka zama hadi zama nyingine.

Na hakuna maana inayo wiana na ukweli iliyo bakia kwetu isipokuwa kwa neno Al-idhlaal kwa maana ya maangamio katika adhabu na Al-hudaa kwa maana ya kutoa thawabu, na maana hizo mbili ndizo zinazo kuwa zimekusudiwa tu katika aya nyingi zilizo kaririwa matamshi yake katika Quran tukufu kama kauli yake tukufu:                                                         

Suratu-Annisaa:88       
je mnataka kumlipa mema alieangamizwa na Mwenyezi Mungu kwa adhabu? Yaani mnataka kumlipa thawabu alieangamizwa na Mwenyezi Mungu kwa adhabu? Na kama kauli yake isemayo                    

                                                                                           

     Suratul-Baqara:26.Kwayo (Quran), anawaangamiza wengi kwa adhabu na kuwalipa wengi thawabu yaani kwa (kupitia) Quran, ana waangamiza Mwenyezi Mungu watu wengi kwa kuikataa (kuiasi) kwao Qurani na kutotii kwao amri zake na makatazo yake, baada ya kuwaamrisha kuyafuata au kuzitii amri hizo. Na watu wengi ana wapa thawabu au malipo mema kwa utiifu wao na kusalimu amri kwao na kuikubali kwao Quran.

Na ikiwa lengo katika neno Al-hidaya sio kutoa thawabu, hatungefahamu kamwe maana yenye kukubalika ya maneno yaliyo kuja kwenye Qurani tukufu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu akimuelezea Mtume wake mtukufu:

   .Suratul-baqara:272 )     

                                            

Siyo juu yako kuwapa malipo lakini Mwenyezi Mungu humlipa mwenye kutaka (au amtakae). Na kauli nyingine isemayo:

) (.Suratul-qasas:56

Hakika wewe humpi malipo mema umtakae (umpendae) lakini Mwenyezi Mungu hulipa malipo mema mwenye kutaka au amtakae.

Lau kama neno Al-hidaya lingekuwa na maana ya kuongoza kwenye aya hizi mbili, aya hizi zingekuwa ni zenye kubomoa ujumbe wa Mtume (s.a.w) katika mojawapo kati ya jukumu muhimu sana la ujumbe wake, nao ni kujulisha na kuongoza na kuelekeza watu kwenye uislamu. Na kwa mfano huu tunaendelea na kuifuata nia hii katika kuzifahamu aya nyingine tukufu ambazo zimebeba neno Al-huda na Al-idhlaal, kiasi kwamba inatudhihi-rikia kusalimika kwa aya hizi na dalili hizi za Quran, kutokana na maana inayo pingana na hiyari kamili na utashi ulio huru utokao kwenye nafsi ya mwanadamu na mapenzi yake.

Na kutokana na hayo tunafahamu kwa uzuri zaidi maana ya kauli ya Mtume (s.a.w) alipo sema:

                 [ ]

Muovu ni yule aliekuwa muovu tumboni mwa mama yake na mwema ni yule alie kuwa mwema tumboni mwa mama yake).  

Haina maana kauli hii kwamba Mwenyezi Mungu amemu-umba akiwa amelazimishwa kufanya yatakayo mfanya awe muovu kama maasi na kufuata upotovu au yatakayo mfanya awe mwema kama kuwa mtiifu na kuongoka na kufuata njia ya sawa, bali lengo la maneno haya ni kama Imam Swadiq (a.s), alivyo sema akiweka wazi kwamba:

                                                                   Muovu ni yule ambae akiwa bado yuko tumboni mwa mama yake Mwenyezi Mungu alijuwa  kuwa yeye atafanya vitendo vya watu waovu, na mwema ni yule ambae akiwa  bado yuko tumboni mwa mama yake Mwenyezi Mungu alijua kuwa yeye atafanya vitendo vya watu wema.

Na hii ni katika hali ya mambo yote kuwa wazi na yenye kujulikana kwenye elimu ya Mwenyezi Mungu mtukufu kama tulivyo ashiria hapo nyuma, na hakuna maana yeyote hapo kati ya maana za kulazimishwa na kutenzwa nguvu.

) (.

Sema: Hii ndio njia yangu ninalingania kwenye njia ya Mwenyezi Mungu nikiwa na ufahamu kamili (busara) mimi na wanao nifuata, na Mwenyezi Mungu ametakasika, na mimi sio miongoni mwa wenye kumshirikisha.

Na maombi yetu ya mwisho ni kuwa  sifa (himidi) zote ni za Mwenyezi Mungu pekee Mola wa walimwengu.

 

***


 

[1] Quran.

[2] Quran.

[3] An-najm:39

[4] Suratul-maaida:110

[5] Suratu-Al-Imraan:49

[6] Suratu-Ankabuut:17

[7] Suratu-muuminuun:14

[8] Suratu-swafaati:125

[9] Lisanul-arab juzuu-15 Ukurasa 186-187

  Lisanul-arab juzuu 5    Ukurasa 74

[10] Tuhaful-uquul:Ukurasa 349-350

[11] Nahjul-balaagha juzuu 3/167

[12] Nahjul-balaagha khutuba ya kwanza 11/13 ukurasa131

[13] Tuhaful-ukuul ukurasa 334

[14] Attibiyaani juzuu ya 1 ukurasa 41

[15] Lisanul-arab juzu 15 ukurasa 355

[16] Lisanul-arab juzu 15 ukurasa 353/354

[17] Lisanul-arab juzu 15 ukurasa 355/354

[18] Tafsiru-Atwabari juzuu ya kwanza 1/72-73

[19] Tafsiru-Atwabari juzuu ya kwanza 1/72-73

[20] Majmaul-bayaan juzuu 1/27-28

[21] Majmaul-bayaan juzuu 1/27-28

[22] Attibyaan Juzuu 1/46

[23] Suratul Arraad :33

[24] Suratu-Mohammad:4

[25] Suratul-Aaraafu :43

[26] Suratul-hujraati:17

[27] Suratu-fuswilat:17

[28] Suratu-Mohammad:5

 

 

index