back page

KUMFAHAMU MWENYEZI MUNGU KUPITIA MAUMBILE NA DALILI.

next page

 

( )

 

Je kuna shaka juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, muu-mbaji wa mbingu na ardhi (Qurani).

( , . . , ).                                                                             Vipi itatolewa dalili ya kuthibitisha  kuwepo kwako ewe Allah kwa kitu ambacho kuwepo kwake kuna kuhitaji wewe?

Je kuna kitu kilicho dhahiri zaidi yako, hadi kiwe ni chenye kukudhihirisha wewe, niwakati gani umefichika hadi uhitajie dalili ya kuthibitisha kuwepo kwako. Na ni wakati gani ulikuwa mbali hadi athari zako zikawa ndizo zenye kutufikisha kwako Hussen (a.s).

     Ni ajabu iliyoje vipi ana asiwa Mwenyezi Mungu au vipi mpingaji anapinga kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, wakati ambapo kila chenye kutikisika na kila kilicho tulia, kinashu-hudiwa na Mwenyezi Mungu na katika kila kitu kuna dalili ijulishayo ya kuwa yeye ni mmoja. (Malenga wa zamani).

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHMA MWENYE    KUREHEMU.     

 

Sifa zote njema ni za mola wa viumbe na rehma na amani ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad (s.a.w) na kizazi chake kitukufu na kilicho twahirika (Kilicho safi).

Tangu walipopatikana viumbe wa mwanzo juu ya ardhi, wanadamu walishughulishwa na fikra, walimfikiria muumba wa uhai na mtoaji wa uhai katika ulimwengu huu mpana, na mazungumzo ya watu hao yaliyo husiana na uungu katika zama hizo za zamani yakijadili suala hilo kulingana na uwezo mdogo wa kufahamu na ufahamu wenye mipaka, na ufinyu wa kiakili na kielimu walio kuwa nao.

Kisha kutokana na kupanuka kwa akili na kukua kwa mawazo ya mwanadamu mazungumzo yakapanuka hadi kufikia kwenye upeo wake katika zama za falsafa, wakati fikra ya falsafa ilipo cheza duru kubwa katika uwanja huu na ikaingia kila nyanja, na ikaiwekea imani misingi madhubuti na vizingiti thabiti na kanuni ambazo hazinakishiwi (hazijadiliwi), misingi ambayo ilitumika kuzibatilisha shaka za wajinga na shubha za wapingaji.

Na elimu ilipo panuka hasa katika zama zetu hizi za mwisho, walio kuwa na elimu hiyo walifanya majaribio mengi kuitumia elimu hiyo kuipiga vita dini na kuivuruga (kuipotosha) itikadi, wakatoa madai ya kuwa elimu inapinga kuwepo kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, na inapinga kanuni ya akili isemayo  kuwa ni lazima (ni dharura) kuwepo muumba wa kila kiumbe na msababishaji wa kila kilichopo, kisha wakakinasibisha kila kitu katika ulimwengu ya kuwa kimetokana na kukua kwa madda  (movement of matter) na kutokana na ghafla (accident), au kuwa ulimwengu ulianza bila kupangiliwa.

Na wakati huo ( katika kipindi hicho) zikaenea shubha na shaka nyingi, na zikaenea kauli tofauti na dhana mbalimbali, na zikaenea kelele zisemazo ya kuwa madda ndio ya tangu na tangu na itadumu milele.

Na jamii ya kiislamu ikapambana na zama hizi ngumu, zama ambazo zilizitia misukusuko fikra na kuwachukua watu wengi ambao itikadi zao zilisimama juu ya msingi wa kuwafuata walio tangulia, itikadi ambazo hazikusimama juu ya msingi wa dalili au kukinaika kwa kutumia dalili.

Wakati ambapo sisi tulikuwa tukiamini ya kuwa haiwezekani uislamu ukapingana na elimu na akili kamwe.

Kwa sababu tunaamini kuwa dini ya kiislamu imesimama juu ya misingi ya akili na elimu, inatulazimu kufanya utafiti juu ya maudhui ya uungu kufuatana na elimu ya kisasa, elimu ambayo waliikusudia wale wenye shaka kuitumia kuharibu na kubomoa itikadi ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa ufupi ni kuwa matokeo ya utafiti uliofanywa ni kuwa, elimu hii kwa lugha yake maalum na mfumo wake ulio wazi, na kwa nadharia zake za kisasa na ugunduzi wake wa kina, imetuzidishia imani ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, na imetupatia dalili na ushahidi ambao hawakuwa nao watafiti na waandishi  walio tangulia.

Na kwamba elimu hii imebatilisha kwa uwazi kabisa madai mengine ya wasemao ya kuwa madda ndio ya tangu na tangu na athari ya harakati zake na maendeleo yake katika kuumba na kuvifanya vitu viwepo, na ilibatilisha madai ya wale wajitege-mezao juu ya sudfa, yaani accident, kutokea kitu kwa ghafla, katika kudhihiri kwa uhai na viumbe katika ulimwengu huu ulio mkubwa.

Na ili kitabu hiki kikusanye na kielezee pande zote za maudhui haya, utafiti wangu umeanza kwa kutoa muhtasari wa dalili za kimaumbile yaliyo salama na dalili za kifalsafa na ushahidi wa elimu ya akida.

Kisha nikatoa uchambuzi kiasi wa mfumo wa Quran tukufu jinsi inavyo utolea ushahidi uhakika huu, nao ni mfumo wa pekee na wa aina yake kati ya mifumo ya kutoa ushahidi au dalili, kwa kukusanya kwake mfumo wa kuizungumzia akili na wenye kuzifanya hisia ziwe ni zenye kuelewa, na kwa kujitegemeza juu ya hisia na athari za nje ya maumbile tunayo yashuhudia.

Kisha dalili za elimu hii ya kisasa zimechukua sehemu ya mwisho katika mwendo huu (safari ) wa kiroho ulio mpana.

Na kila ninalo litarajia kutokana na utafiti huu ni kupata thawabu na malipo, na ninatarajia uwe na manufaa na uwe ni muongozo kwa wasomaji na Mwenyezi Mungu ndie muwafiki-shaji.

Na ninamshukuru Allah alietuongoza kwa haya kwani hatukuwa ni wenye kuongoka kama si uongozi wake.

Ewe mola wetu hakika sisi tulimsikia mnadi (muitaji) akiitia watu kwenye Imani ya kuwa muaminini mola wenu tukaamini.

Ewe mola wetu tusamehe madhambi yetu na utufutie makosa yetu na utufishe pamoja na watu wema.

 

 

         Mohammad Hassan Aalu Yaasin,

                IRAQ.  Baghdad.  Kadhimiyya.

 

 

Utafiti uhusianao na kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, muumba na muendeshaji wa ulimwengu, na dalili za kuwepo kwa Mungu huyu muumba, ni utafiti wa tangu, yaani ni utafiti ulio anza muda mrefu sana hata kama itatofautiana miundo yake kutokana na muda mrefu kupita, na hata kama itapishana mifumo yake, na zikabadilika dalili zake na ushahidi wake.

Na mwanadamu tangu alipokuwa ni mtu mwenye kufahamu na kuhisi ameumbwa kuwa ni mtu mwenye kupenda kuelewa mambo hata yale yaliyo nyuma ya sitara, na ameumbwa na hali ya kupenda kufahamu chanzo cha vitu na malengo yake na kufahamu uhakika wa kila kitu, mwanzo wake ni upi? Na vipi kimekuwa? Na mwisho wake ni upi?Au wapi kitaishia kitu hicho?

Na kutokana na athari za maumbile hayo aliyo umbwa nayo ya kupenda kufahamu ukweli na uhakika wa vitu, mwanadamu huyo ameweza  kuufahamu ulimwengu na hakuacha kutafiti katika siri zake na kuzama katika kina chake kilicho kirefu kwa kiasi cha akili yake na ufahamu wake katika kila mzunguko kati ya mizunguko ya tamaduni mbalimbali zilizo pita katika historia. Na utafiti kuhusu kuwepo kwa mwanzishaji wa ulimwengu na alie ufanya ulimwengu uwepo, huo ulikua ndio utafiti wa mwanzo kufanyika katika siri za ulimwengu, utafiti  ambao ulijaribu kuufahamu ulimwengu na kufanya uchunguzi kuhusu ulimwengu kulingana na nyenzo alizo kuwa nazo, au alizo kuwa akizimiliki zimuwezeshazo kufahamu na kufikiria.

Kutokana na kuwa kufahamu kwa mwanadamu uhakika wa vitu kumeanza tangu alipokuja duniani, kukiwa na mipaka basi kufahamu kwake hakukuvuka mzunguko wa maisha yake mepesi na yaliyo finyu. Kisha kutokana na karne kadhaa kupita kukapanuka maisha yake kufuatana na kupanuka kwake katika maarifa, hakuna ajabu yoyote ikiwa tutaona maudhui ya itikadi kuhusiana na Mwenyezi Mungu muumba na msababishaji wa ulimwengu yakipanuka na kupiga hatua katika kupanuka kwake kulingana na ukuaji wa akili ya mwanadamu  na fikira zake katika historia ya kukua kwake hapo kabla na hata hivi sasa.

Na ndio sababu tunaona  ya kuwa wanadamu tangu zama za mwanzo za kuwepo kwao, kuna watu walio kuwa wakiabudu wanyama au nyota au baadhi ya vitu visivyo na hisia, na wakiitakidi ya kuwa vitu hivyo ni mola wao ahuishae na afishae mwenye kuumba na kutoa riziki mwenye kutoa na mwenye kuzuia, na hawakutosheka na kuviabudu na kuvinyenyekea tu au kukubali uungu wa vitu hivyo isipokuwa walipiga magoti chini ya miguu yao wakitoa sadaka na wakivichinjia wanyama ili viwaletee kheri na viwaepushe na shari.

Waliona jua ya kuwa ndilo linalo tengeneza uhai na likitoa joto na kuvifanya viumbe hai viwe ni vyenye kukua, bali waliona ya kuwa hapatakuwa na uhai bila kuwepo kwa jua, wakadhani ya kuwa ndio mwenyezi mungu.

Na waliuona mwezi ukiwaangazia katika kiza cha usiku wate-mbeao usiku wakiwa wamepotea njia katikati ya majangwa yaliyo makubwa wakadhani ya kuwa ndiyo Mwenyezi Mungu.

Na waliziona nyota zikitoa mwanga wake kutokea kwenye mapango yake ya mbali zikiwa kama jambo gumu na lenye kutatiza nakuifanya akili itahayari na kushikwa na mshangao wakazichukulia ya kuwa ni mwenyezi mungu.

Mwisho wakawaona baadhi ya wanyama wakimpatia chakula au vinywaji au mavazi au wakiwa na mambo yanayo staajabisha kama ushujaa na nguvu, kiwiliwili kikubwa vikawapelekea vitu hivyo kuwaabudu wanyama hao kwa msingi wa kuwa ni Mwenyezi Mungu.

 

Mambo yote haya yanatujulisha juu ya ufinyu wa mwanadamu katika fikra zake na akili yake kwa wakati huo, kama yanavyo tujulisha juu ya ufahamu wa maumbile yake yaliyo salama yanayo ona dharura ya kuwepo kwa Mungu alie ufanya ulimwengu huu uwepo baada ya kutokuwepo.

Kisha kutokana na mwongozo wa Mitume na mwongozo wa vitabu vya Allah, mtizamo wake juu ya vitu hivi ukawa ukibadili -ka na kupanuka na hisia zake pia kufahamu kwake kukapanuka, mwishowe kutokana na ufahamu wake uliokuwa ukitafiti ukamfahamu Mola wake muumba na alievifanya vitu vyote viwepo ambae aliumba mbingu saba tabaka juu ya tabaka huwezi kuona tofauti katika uumbaji wa Mwenyezi mungu mwingi wa rehma, hebu rudisha macho (angalia tena), je unaona kasoro yoyote? Kisha rudisha macho yako kwa mara ya pili yatarudia macho yako hali ya kuwa yamehasirika na  yakiwa yamechoka.

Hakika maumbile ni chanzo muhimu cha mwanadamu katika njia ya kutaka kumfahamu mola wake na kumuamini, na maumbile hayo yamemfanya mwanadamu au ufahamu wake wa ndani uitwao Alla-shuur (Usio na hisia) kuitakidi kuwepo kwa muumba wa ulimwengu huu, alieumba  viumbe vyote na alie viumba kwa mara ya mwanzo baada ya kutokuwepo, na kila kiumbe akakiwekea nidhamu yake na kanuni yake ili kiweze kutekeleza majukumu  yake na malengo yake ambayo kwa ajili yake kimeumbwa, akakiwekea nidhamu na kanuni zilizo madhu-buti na zinazofanya kazi kwa mpangilio na nidhamu thabiti isiyo badilika wala kugeuka.

Na wakati walipofanya utafiti walimu wa kifaransa kuhusiana na maisha ya mbilikimo katikati ya afrika na katika visiwa vya Andiana na kisiwa cha  Molncces na sehemu nyingine za Filipin, walifikia kwenye natija ifuatayo, nayo ni kuwa kabila la mbilikimo walikuwa mfano bora wa mabadiliko ya tangu tunayoweza kuyafikia katika maendeleo ya kijinsia ya wanadamu, na kwamba wao katika utangulizi wanawapita makabila ya kusini mashariki mwa Asia.

Na mtafiti huyu bwana Shamt na watafiti wengine hawaku-pata athari yoyote katika itikadi ya watu hao inayo ashiria ya kuwa waliabudu maumbile au roho fulani.

 Ama imani zao za uchawi zilikuwa ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na imani za  makabila yaliyo kuwa jirani nao na yaliyo kuwa yamewatangulia kimaendeleo na kiutamaduni, ama itikadi yao ya kipekee ilikuwa ni ibada ya kitu kitukufu kilichopo nacho ni Muumba na Bwana wa ulimwengu.

Na tunaweza kusema kwa mara nyingine ya kuwa kugunduliwa zama za makabila haya na kugunduliwa kwa itikadi zao, hakika ulikuwa ni ugunduzi hatari katika historia ya dini, kwani ulitoa ripoti ya kielimu iliyo simama juu ya misingi imara, isiyo na shaka juu ya mahusiano kati ya maumbile na kumpwe-kesha Mwenyezi Mungu[1].

Na amesema mwanafikra wa kiskotlandi aitwae Lanj:Kila mwanaadamu amebeba ndani ya nafsi yake fikra ya sababu na msababishwaji na kwamba fikra hii inatosha kutengeneza itikadi ya kuwa kuna Mungu muumba wa ulimwengu.

Hakika mwanadamu aliufahamu ukweli huu kwa maumbile yake ya kibinadamu na dalili ya maumbile haya ni nyepesi kama maumbile yake yaliyo wazi, yenye kueleweka, kwani maumbile haya yanaamini ya kwamba kila athari inajulisha kuwepo kwa mwenye kuathiri, na kila kilichopo kinajulisha juu ya kuwepo aliekifanya kiwepo, na kwamba kinyesi cha ngamia kinajulisha kuwepo kwa ngamia, na athari za nyayo zinajulisha kupita kwa mtu katika sehemu hiyo, je mbingu zenye nyota na ardhi yenye njia pana havijulishi kuwepo kwa Mwenyezi Mungu alie mpole na mwenye habari zote za ulimwengu?

 

Na kuna mfano uoneshao jinsi maumbile yalivyo mpelekea mwanadamu kumuamini au kumuitakidi Mwenyezi Mungu unasimuliwa kwenye kisa hiki kifuatacho:

Siku moja asubuhi mmoja kati ya walahidi (wapingao kuwepo kwa Mwenyezi Mungu) alihudhuria kwenye kikao cha kidini kati ya vikao vilivyo kuwa vikifanyika Baghdaad Iraq, akitaka kufanya mazungumzo na yeyote anaepinga il-haad yake, yaani kukataa kwake kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, mwenye kikao akamtuma mjumbe akamuitie mmoja kati ya wanazuoni wa akida ili asimamie jukumu hili, yule mjumbe akafika hadi nyumbani kwa yule aalim wa akida na akamfahamisha tukio lenyewe, yule bwana akamuomba  mwenye kikao amjulishe ya kuwa yeye yuko njiani anakuja.

Baada ya kufika mjumbe watu wakabakia kwenye kikao wakisubiri, na walisubiri kwa muda mrefu kiasi cha kukata tamaa na kutaka kutawanyika, ghafla yule mwana zuoni akaingia na kutoa salamu huku akimgeukia mwenye kikao na akimtaka samahani kutokana na kuchelewa kwani hakutarajia kama atachelewa na akatoa sababu ya kuwa hakuchelewa muda wote huo kwa kutembea taratibu au kwa ajili ya mapumziko bali alipokuwa njiani kuelekea kwenye kikao hicho aliona jambo la ajabu, jambo ambalo lilizimiliki hisia zake zote na hakuweza kujielewa na wala kukumbuka ahadi yake ya kikao isipokuwa baada ya kupita muda  mrefu ndipo akaja haraka haraka kwenye kikao.

Na alipoulizwa kuhusiana na jambo hilo la ajabu lililo chukua akili yake akasema:Nilipofika ukingoni mwa mto Dijla nikiwa njiani kuja hapa nimeuona mti mkubwa ukiangukia kando ya mto wenyewe bila kuwepo alie uangusha, kisha nikauona ukijikata vipande vipande tena vyenye kufanana na vilivyoshikana na kupangiliwa kisha nikaviona vipande hivyo vikiungana na kushikamana kuwa mtumbwi, kisha ndani yake ikajiweka lami na misumari ikaingia kwenye bolti zake ukawa ni mtumbwi mzuri wenye kupendeza, baadae nikauona mtumbwi huo umesimama ukingoni mwa mto wenyewe, ghafla watu wakaanza kupanda na mtumbwi ukiwa ukingoni ukaanza kuwavusha bila kuwa na kafi la kuvushia wala nahodha hadi ukawafikisha ngambo ya pili, pia wakapanda watu upande ule wa pili na kuwavusha hadi upande wa mwanzo, hili ndilo jambo la ajabu nililoliona na sababu ya kuchelewa kwangu.

Na yule bwana hakumaliza maneno yake mara yule mpingaji wa kuwepo kwa Mungu akaanza kucheka kicheko cha maskhara na kejeli na akasema:Ninasikitika sana kupoteza muda wangu kwa kumsubiri mtu huyu ambae sijawahi kuona katika maisha yangu mtu mjinga na mpumbavu kama yeye. Je inakubalika akilini ya kuwa mti ujiangushe na ujikate ujiunganishe na ukaungana na ujipake lami kisha uwe ni mtumbwi ukihamisha watu kutoka upande hadi upande mwingine bila kuwepo mtu wa kufanya hayo?Yule mwanazuoni akamgeukia na kusema:

Ikiwa kujitengeneza mtumbwi wenyewe ni jambo lisilo wezekana kiakili na mwenye kusema hivyo huonekana kuwa ni mjinga na mpumbavu wa kupita kiasi, vipi inawezekana kuwepo kwa ardhi na mbingu na sayari na viumbe vilivyo hai bila kuwepo muumbaji? Je mimi ndio mpumbavu sana au wewe?

Yule mpingaji wa kuwepo kwa Mungu akanyamaza huku akiinamisha kichwa na kufikiria na hakuwa na jambo la kufanya ispokuwa ni kukiri makosa yake na kughafilika kwake.

Na hivi ndivyo maumbile ya mwanadamu yamuonyeshavyo dalili ya kuitakidi kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Na kwa utaratibu huu ulio mbali na ushahidi wa kifalsafa uliofichika na isitilahi zake na mifumo yake iliyofungika.

 

Ama falsafa ilikuwa na mfano maalum katika kutoa ushahidi na dalili, na wanafalsafa katika maudhui haya wanayo mizunguko kadha wa kadha ambapo katika mizunguko hiyo walikomea kwenye dalili kadha za kiakili na kimantiki zithibitishazo itikadi na kuzidisha imani na kubatilisha shubha.

Na dalili ya wazi kabisa kati ya dalili hizo ni kauli yao isemayo:Kitu kilichopo ikiwa kuwepo kwake ni wajibu (yaani ni lazima kuwepo kwake) hilo ndilo litakiwalo, la sivyo, kikiwa si wajibu kitalazimika kuhitajia kingine cha wajibu kwani mzunguko wa vyenye kuhitajia kuwepo usio na mwisho (dauru), na silsila na kufuatana kusiko na mwisho (tasalsuli) ni muhali na batili.

Maana ya maneno haya ni kuwa:

Kwa kawaida kila kitu kilichopo ikiwa niwajibul-wujuud, yaani ni lazima kuwepo kwake hilo ndilo tunalo dai, na ndilo sahihi na kikiwa ni (mumkinul-wujuud) yaani kinawezekana kuwepo au kutokuwepo, kwa kawaida kitahitajia muwekaji wake au msababishaji wake na huyo msababishaji ikiwa ni waajibul-wujuud ni lazima kuwepo kwake hilo ndilo tunalo dai na akiwa ni mumkinul-wujuud, yaani yawezekana kuwepo au kutokuwepo atahitajia msababishaji vilevile, akiwa ni (wajibul-wujuud) hivyo ndivyo itakiwavyo kudaiwa na akiwa ni mumkinul-wujuud pia italazimika kuwepo tasalsuli, yaani kufuatana kwa vyenye kuhi-taji msababishaji kusiko na mwisho na tasalsul ni batili, yaani kufuatana kusiko na mwisho ni batili.

Kwa ufafanuzi zaidi wamesema:Hakuna shaka juu ya kuwepo kwa huyo aliopo, na huyo aliopo ikiwa ni waajibul-wujuud kidhati yaani ni lazima kuwepo kwake na kuwepo kwake kunatokana na dhati yake, yaani kuwepo ni dhati yake kama ambavyo joto la moto ni dhati ya moto, kwa maana ya kuwa huwezi kutenganisha kati ya joto la moto na moto wenyewe, unapo patikana moto joto nalo hupatikana, tutakuwa tumefikia dai letu na ikiwa huyo aliepo katika dhati yake ni mwenye uwezekano wa kuwepo au kutokuwepo, atahitajia msababishaji wa kuwepo kwake na huyo msababishaji ikiwa ni waajibul wujuud kwa dhaati yake yaani hahitajii msababishaji kwa maana ya kuwa kuwepo kwake kunatokana na yeye mwenyewe litakuwa limepatikana litakiwalo tunalo lidai vilevile, na ikiwa kwa dhati yake ni mumkinul-wujuud atahitaji msababishaji wake, na huyo msababishaji akiwa yeye mwenyewe ndio athari yake italazimika kuwepo kwa dauru (yaani mzunguko) nao ni muhali kwa sababu wakati huo itakuwa kila mmoja ni sababu ya kupatikana kwa mwengine, wakati ambapo inalazimika au inawajibika kutangulia kuwepo kwa muathiri kabla ya kuwepo kwa athari au kuwepo kwa msababishaji kabla ya kuwepo kwa sababu[2].

Na akiwa huyo msababishaji ni kitu kingine yaani si athari yake kwa maana ya kuwa ni vitu viwili tofauti itakuwa kama ifuatavyo:
1: Ima imalizikie kuwa aliepo ni wajibul-wujuud (yaani ni lazima kuwepo kwake) kwa  dhati yake

2: Ima kuwe na tasal-sul isiyo na mwisho . La kwanza ndilo tunalo dai, na la pili ni batili.

Na kwa kuwa kila kitu mumkini, yaani kile kiwezekanacho kuwepo au kuto kuwepo, ni lazima kiwe na msababishaji wake, msabababishaji huyo ima:

i)                    Awe ni yeye mwenyewe.

ii)                  Au ni kitu kilicho ingia ndani yake.

iii)                Au ni kitu kilicho nje yake.

 

Nadharia ya kwanza ni batili, kwa sababu msababishaji ni lazima aitangulie athari yake katika kuwepo yaani akitangulie alicho kisababisha, na kitu kujitangulia chenyewe ni jambo lisilo kubalika kiakili.

Nadharia ya pili ni muhali vilevile (yaani haiwezekani) kwa sababu msababishaji wa kitu huwa ni msababishaji wa kila sehemu ndani ya kitu kile . Lau kama kungekuwa na sehemu ndani ya kitu kile ambayo ndio iliyo sababisha kuwepo kwa kitu chenyewe italazimu kuwa msababishaji alijisababisha mwenyewe na  kukisababisha kile kitu ambacho yumo ndani yake, na yote hayo ni muhali.

Ama nadharia ya kwanza ni batili kwa sababu ya kutokubalika kiakili kitu kujitangulia chenyewe, na ya pili ni kwa sababu kutapatikana dauru (mzunguko), yaani cha kwanza kimetokana na cha pili  na cha pili kimetokana na cha kwanza na mzunguko ni batili.

Na baada ya kuonekana ubatili wa nadharia mbili za mwanzo inabakia nadharia ya tatu kuwa ndio sahihi nayo ni kuwa msababishaji wa kile kitu ni kitu kingine kilicho nje yake na kitu hicho si miongoni mwa vitu vilivyo mumkini, yaani yawezekana kuwepo au kutokuwepo.

Na wala hakiwi ni mumkini kwa dhati yake na ikiwa kitakuwa mumkini kwa dhati yake  basi kitakuwa miongoni mwa vitu vilivyo mumkini, kwa hivyo basi ni lazima kiwe ni kitu kilicho nje yake, na hilo ndilo tunalotaka kulithibitisha.

Na makusudio ya ushahidi huu kwa ibara iliyo wazi ni kuwa:

Kwa kuzingatia ya kuwa ulimwengu unamsababishaji wa kuwepo kwake bila shaka yoyote, kwani haiwezekani kitu ambacho hakikuwepo kikajifanya chenyewe kiwepo, na huyo alie kifanya kiwepo alikuwepo bila ya shaka yeyote kwa sababu haiwezekani ulimwengu kuwepo, na kuwepo kwake hakujatokana na chochote, yaani umetokana na msababishaji asie kuwepo.

Basi msababishaji huyu je atakuwa ni waajibul-wujuud au hapana?

Na ikiwa huyo msababishaji ni lazima kuwepo wakati huo litakuwa limethibiti litakiwalo, na kama hakuwa lazima kuwepo (yaani hakuwa waajibul-wujuud) itamlazimu awe na msababi-shaji wake aliemfanya awepo, na msababishaji huyo akiwa  ni waajibul wujud hivyo utakuwa umepatikana muradi vilevile na kama hakuwa wajibul-wujuud itamlazimu vilevile awe na msababishaji.

Na mwisho kabisa tutaishia kukubali kuwepo kwa muumba ambae ni waajibul-wujuud (alielazima kuwepo kwake) na ndie chimbuko la kuwepo kwa vitu vyote na yeye ndie alievifanya vitu hivyo na ulimwengu viwepo na kama hatakuwepo waajibul- wujuud italazimika kuwepo moja kati ya hali mbili:

 

1:Tasalsul (kufuatana). Maana yake ni kuwa itamlazimu kila aliekuwepo au kila kilichopo kiwe na msababishaji, na huyu msababishaji itamlazimu nae awe na msababishaji wake mwingi-ne vilevile atahitaji awe na msababishaji alie mfanya awepo na hali itaendelea hivyo hivyo bila kuwa na mwisho na akili imethibitisha ya kuwa silsila kama hii isiyo na mwisho ni batili kwa sababu haitufikishi  kwenye natija .

2:Dauru (mzunguko) maana yake ni kuwa huyu alie vifanya vitu viwepo au msababishaji aliumba kitu nacho ndicho kiitwacho Athari na kitu hicho ndicho kinachomfanya msababishaji awepo na hali hii ubatili wake uko wazi kwani kitu hicho kitakuwa kimetokana na nafsi, yaani kimejifanya chenyewe kiwepo.

Na kama ilivyo thibiti ya kuwa Tasalsul na Dauru vyote viwili ni batili kama tulivyo elezea hapo mwanzo, na hapo itakuwa imethibiti ya kuwa ni lazima kukubali na kukiri kuwepo muumba alie vifanya vitu vyote viwepo au msababisha wa vitu vyote ambae ni waajibul-wujuud yaani ni lazima kuwepo kwake kwa dhati yake, nae ni Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ama wanazuoni wa akida wao walitumia njia zingine katika kutoa ushahidi juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na walijitegemeza katika utoaji wa ushahidi juu ya mfumo wa kiakili ulio huru, wakiwa mbali na riwaya na hata kuwafuata walio tangulia kufanya  Takliid na miongoni mwa dalili zao ni kauli isemayo:

Hakika vitu vyenye miili na vitu vingine vilivyo mfano wa hivyo ni vitu vilivyo zuka yaani havikuwapo kisha vikapatikana, na dalili ya kuzuka kwake ni kusifika kwake na maana zenye kubadilika au nikusifiwa kwake na hali ya mabadiliko, na chochote chenye kusifiwa na hali ya kugeukageuka kimezuka, na ikithibiti kuzuka kwake basi kipime kitu hicho na matendo yetu kwani kila kitendo kina mtendaji  kutokana na hali hii kina msababishaji wake.

Na miongoni mwa vitu hivyo ni ulimwengu, umezuka na umekuwepo baada ya kutokuwepo, kwa sababu katika ulimwe-ngu wote kuna athari ya ujenzi kama vile urefu na ufipi, ukubwa na udogo, kuzidi na kupungua, na mabadiliko ya kutoka hali fulani kuingia hali nyingine na kupishana kwa usiku na mchana.

Na Mwenyezi Mungu ndie muumba wa hayo, na ndie muanzilishi na aliekipa kila kitu umbile na sura, na ndie alie kianzisha kila kitu kwa mara ya mwanzo, kwa sababu kutengenezwa kitu ni lazima kuwe na mtengenezaji, na kitabu ni lazima kiwe na muandishi na ujenzi ni lazima kuwepo na mjenzi.

Na kwa muhtasari ni kuwa tunafaidika kutokana na maneno haya na dalili hizi na mengineyo yaliyo kuwa mfano wa haya ambayo hatuna nafasi ya kuyataja ya kuwa kutokana na ukweli kuwa ulimwengu na vyote vilivyomo kama wanyama na viumbe vilivyo hai na visivyo hai na viumbe vya juu na chini ni vitu vilivyo zuka yaani vimetanguliwa na kutokuwepo, na vimekuwepo baada ya kuwa havikuwepo, na kutokana na ukweli kuwa athari za kuwepo ziko wazi kwenye vitu hivyo kama urefu na ufupi kuzidi na kupungua na kubadilika kutoka hali fulani hadi hali nyingine na kupishana kwa usiku na mchana na mfano wa hayo, miongoni mwa athari nyingi ambazo ni dalili zionyeshazo ya kuwa ni vitu vilivyo zuka, vimekuwepo baada ya kuwa havikuwepo.

Na kutokana na ukweli kuwa kugeuka na kubadilika kusiko tengana na viumbe vilivyomo ulimwenguni, mabadiliko hayo yote yanafanana kwa uwazi kabisa na mabadiliko na mageuko yasiyotengana na vitendo vyetu na harakati zetu, kama ambavyo vitendo vyetu maalum- kama tunavyojuwa na kuhisi- havijifanyi vyenyewe bali sisi wenyewe ndio tufanyao vitendo hivyo, kiasi kwamba sisi ndio tunao kula na kunywa, na kutikisika pia, kuandika na kusoma na matendo mengine mfano wa haya kati ya matendo yetu ya kila siku na mengine, kutokana na haya tunafahamu ya kuwa ulimwengu huu pamoja na viumbe vilivyomo na mfano wa hivyo ni lazima kuwepo muanzilishaji wake ambae ndie alie vipa sura vitu hivyo, nae ni Mwenyezi Mungu au (Allah) alie mtukufu na mtakasifu. Kwa sababu kutengeneza kunahitaji mtengenezaji, na kitabu kinahitaji muandishi, na ujenzi unahitaji mjenzi.

Na hivi sasa tunarudi kwenye Qurani tukufu ili tuzisome dalili zilizomo na tuweze kuzifahamu dalili ilizo kuja nazo Quran na ushahidi mbalimbali juu ya ukweli huu wa milele.

Na Quran ilitilia umuhimu jambo hili na kuzirudia rudia dalili na ushahidi juu ya jambo hili kwa kutumia maneno na mifumo tofauti zaidi ya kitabu chochote kilicho teremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, si hivyo tu bali hatuoni ndani ya vitabu hivyo kama yale tuyaonayo ndani ya Qurani katika dalili na ushahidi wake na hatuoni dalili zinazo zindua akili zilizo ganda na zimkataazo Mwenyezi Mungu.

Na huwenda sababu ya kuto onekana dalili hizo ni kwamba Taurati haikuletwa kwa ajili ya kuwakinaisha wapingao kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na wenye shaka, kwa sababu ilikuwa ikiwazungumzia watu walio kwisha muamini  Mungu wa Israili, na hawakuwa na shaka juu ya kuwepo kwake. Kwa hiyo hima yake yote ilielekezwa kuwatahadharisha watu hao kutokana na ghadhabu za Mwenyezi Mungu na mwisho wa mwenye kumuamini Mungu mwingine  asiye yeye na ilikuwa  ikiwaku-mbusha ahadi zake ikiwa watasahau au watazembea katika kutekeleza majukumu yao.

Na vilevile injili haikuwa na mvutano kati yake na kati ya madhehebu za kiisraili juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu bali tofauti zao ziliuelekea unafiki wa viongozi na makuhani na kuitumia kwao dini  na alama zake katika kujitajirisha na kuchuma mali na kujitafutia vyeo na ufakhari.

Lakini ulipo dhihiri Uislamu na ikateremka Quran watu walikuwa kwenye tofauti kubwa juu ya suala hili, kwani kulikuwa na wanao kataa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (walahidi) na washirikina na walikuwepo wafuasi wa Taurati na Injili na kila kundi lilikuwa na rai yake maalum kuhusiana na Mola na njia ya kumuabudu, kwa hivyo  Qurani  ilikuwa ni lazima ielekeze hima yake upande huu na itilie umuhimu kwa kiasi kikubwa, kwani waliokuwa wakihutubiwa na wito wa kiislamu walikuwa wakihitajia sana kupewa dalili za kuwakinaisha juu ya jambo hili na kuwaongoza kwenye njia ya kweli.

Kisha kutokana na ukweli kuwa Uislamu ni dini ya mwisho na Qurani ni Kitabu cha mwisho na kutokana na ukweli kuwa ilikwisha kadiriwa na Mwenyezi Mungu kuwa dini hii na kitabu hiki viwe ni vyenye kuendelea katika kuyapangilia maisha ya watu kiitikadi na kidunia hadi siku ya kiama, ilikuwa ni lazima juu ya Qurani kutilia mkazo na umuhimu upande huu, kwa kuweka dalili thabiti  juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, na ilikuwa ni lazima kuwatanabahisha wapingaji wa kuwepo kwa muumba wa ulimwengu na athari zake zilizo kubwa na madhubuti zinazo julisha kuwepo kwake na kuwa ni mkamilifu, alie takasika na ilikuwa ni lazima kuziba njia ili zisiingie shubha zinazo weza kujitokeza kwa kutumia dalili za kiakili  na ushahidi wa athari zilizopo. Kwa hivyo basi aya zote zinazo husiana na maudhui haya, ziliielekea akili ya mwanadamu zikiizinduwa kutoka usingizini mwake na katika kughafilika kwake kwa upole na zikaipeleka hadi kwenye malengo kwa mwendo wa utaratibu, na zikamuongoza kwenye njia ya sawa kwa upole na kwa njia nyepesi, na zikamuwekea mbele yake ushahidi wa viumbe na athari za utengenezaji au uumbaji kwa uwazi kabisa, na zikamtanabahisha juu ya umadhubuti wa ulimwengu na uhakika wake kwa kutumia hekima na kwa upole, na zikamfikisha kwenye natija ya utafiti huu kwa hali ya utulivu na kukinai na kwa kupata yakini juu ya natija ile.

 

                    Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi na kupishana kwa usiku na mchana na katika majahazi yapitayo baharini kwa ajili ya manufaa ya watu na katika vitu alivyo viteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni au mawinguni kuwa maji na kwa maji hayo akaihuisha ardhi baada ya kuwa ilikuwa imekufa na akatawanya katika ardhi hiyo aina tofauti ya wanyama, na kubadilisha pepo, na mawingu yaliyo tandazwa kati ya mbingu na ardhi kuna dalili ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye akili (Ufahamu).

  ) (

 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kupishana kwa usiku na mchana kuna dalili kwa wale wenye akili.

Hakika aya nyingi tukufu zilielekea juu ya kutoa ushahidi wa kuwepo kwa mwenyezi Mungu kwa njia ya mazingatio au kuyazingatia na kuyadadisi maumbile ya mwanadamu na mambo yaliyomo kwenye umbile la mwanadamu mambo ambayo ni magumu kugunduliwa kwake na mambo ambayo hayawezekani kuwepo bila kuwepo mwenye uwezo mkubwa wa kufanya yawepo au bila utashi madhubuti wa muumba.

.Suratul-waakia :58) (

Je, mmeyaona maji ya uzazi mnayo yatoneza, je ni nyinyi ndio  myaumbayo  au sisi ndio tunao yaumba?                                                    

)           (.                                             

 

Basi na angalie mwanadamu ameumbwa kutokana na nini, ameumbwa kutokana na maji yatokayo kwa kuchupa, yatokayo katikati ya mifupa ya mgongo wa mwanamume na kifua cha       mwanamke.                                                                                             

 )   .(      

                                                                                                                     Je wameumbwa pasipo kitu ama wao ndio walio jiumba                                         )   (.

 

   Suratu ruum : 20 .     Na miongoni mwa ishara na dalili zake ni kukuumbeni nyinyi kutokana na udongo kisha mkawa ni viumbe     wenye kuenea kwa  kuzaliana.                                                                                              

Suratu-Annahl 78 .Na Mwenyezi Mungu amekutoeni kwenye matumbo ya mama zenu mkiwa hamjui chochote na akakujaalieni masikio na macho na nyoyo.

Basi ni maajabu yapi yaliyomo ndani ya maumbile ya mwanadamu na ni ushahidi upi uliopo katika maumbile ya mwanadamu juu ya kuwepo kwa Mwenyezi  Mungu?

Elimu ya kisasa inasema:Hakika mwanadamu katika asili yake anatengenezeka kutokana na seli (mbegu au chembe moja ya uhai) na Seli hii ya uhai hujifunika kwa ukuta au uzio mwembamba usio hai, huuwekea mipaka ya umbo na umbile lake, kisha huzungukwa, ndani ya uzio huo au ukuta huo na kifuniko kilicho hai kilicho laini na chembamba sana, na kifuniko hicho ndicho kitoacho ruhusa ya kuingia kwa chembechembe kwenye seli au kutoka kwa chembechembe katika seli hiyo.

Baada ya hayo tunaingia katika uwanja ambao hujikusanya humo bilioni kwa mabilioni za chembechembe za kemikali za aina tofauti. Isipokuwa ni kwamba chembe chembee hizi zina kiwango maalumu katika ulimwengu wake na zinamipaka maaluum. Kuna ambazo ni chache na ndogo hazizidi chembe mbili za atomu, kama chembe chembe chumvi ya chakula, au chembe tatu za atomu au tano au kumi au mia moja au elfu moja, hadi kufikia kwenye chembe chembe ambazo kilamoja imeundika kutokana na maelfu na maelfu ya chembe chembe (Kama chembe chembe za protini na chembe  za urithi).

Na katika uwanja huu maelfu ya chembe chembe hufanya kazi kati kati ya maji ili kujenga aina fulani ya chembe na kuziharibu zingine kulingana na hali ya uhai wake utakavyo, kana kwamba katika uwanja huu ulio madhubuti kuna kiwanda cha kemikali za uhai ambapo hufanyika kazi ndani yake kwa kasi sana na utaalamu wa hali ya juu ambapo mwanadamu hawezi au anashindwa kufikia kiwango hicho, kwa hivyo basi sisi hadi hivi sasa hatujaweza na hatuwezi kuunda chembechembe za protini iliyo saizi ya kati ambapo chembe moja yenyewe ndani ya seli (mbegu ya uhai) haikai katika kutengenezwa kwake zaidi ya sekunde kadhaa.

Na katika uwanja huu haifanywi kazi ya kutengeneza protine tu bali kuna kazi nyingi na tofauti za kikemia zifanywazo kwa umakini na utaalamu na kwa nidhamu makini na chini ya uangalizi mkali kutoka kwenye idara ya ulinzi ya mbegu ya uzazi (seli) au umbile lake linalo ilinda, nayo ni idara ya ulinzi ya kikemia, iliyo undwa na chembechembe zenye uwezo mkubwa iliyo shujaa.

Na katika kiini cha chembe ndogo za mbegu ya uzazi (kiiniseli) au katika idara yake (mlinzi wake ailindae) hupanga na kuweka michoro ya mambo ya msingi.

Vilevile seli imekusanya chembe mbili ambazo ni zenye thamani zaidi kuliko chochote katika uhai na chembe zilizo ngumu na kufungika zaidi.

Ya kwanza ni Asidi (Acid) nayo inajina refu la kikemia (kifupi chake ni D.N.A) Asidi Kiini dioksiribo (Deoxyribo-nucliecacid).

Na Asidi nyingine jina lake kwa ufupi ni (R.N.A). Ribonucliec acid (Asidi kiini ribo). Hakika D.N.A inafanana na R.N.A. katika kila kitu isipokuwa tofauti yake ni kidogo sana katika R.N.A.

Na miongoni mwa mabadiliko hayo ya kikemia au siasa ya kikemia ni kuweko na mwenye utawala wa mambo yote katika ulimwengu wa seli kwa mfano chembe chembe za urithi.

D.N.A ndizo mabwana wakubwa katika ulimwengu wake na (R.N.A) ni yenye daraja ya chini yake. Na tukio kubwa kabisa katika uhai wa seli ni njia ambazo hutumika kuzidisha (D.N.A) ambae ndie mwenye udhibiti kamili, chembe chembe zake na kuumba au kutengeneza kutokana na chembe chembe hizo umbile (sura) iliyo sawa na asili kutokana na chembechembe hizo, na sura hii au umbile hili huendelea hivyo hivyo katika kiwiliwili hicho cha mwanadamu kwa mamilioni ya miaka bila kubadilika na hivyo hivyo huendelea kuwepo ndani ya punda na hata chura.

Na kwa ajili hii akapatikana chura katika ulimwengu, kwa hivyo basi kila kiumbe kimekwisha wekewa michoro yake na kimekwisha kadiriwa na kuwekewa kiwango maalumu kwenye chembechembe za D.N.A.

Na anachukua jukumu (D.N.A) la kumtuma mjumbe wake ambae ni (R.N.A) ili akatengeneze chembechembe zingine zilizo na uwezo wa juu na zilizo shujaa, zenye uwezo wa kuzidhibiti  chembe chembe zilizo chini yake kiuwezo, na hizi nazo zinakuwa na uangalizi juu ya chembechembe zilizo duni yake au chini kiuwezo, na hizi nazo zinakuwa na uangalizi juu ya chembe-chembe zingine zilizo chini yake zaidi, hadi kufikia kwenye mkusanyiko mkubwa wa chembe chembe ambazo huingia kwenye msongamano na mvutano.

Na mbegu moja (Seli) hii iliyo shujaa na yenye uwezo mkubwa na ambayo ndio mwanadamu ameumbwa kutokana nayo, ndiyo inayo ifanya au inayo itengeneza mifupa iliyo migumu na mifupa laini kiasi, kama makwato na nyama iliyo laini, na ni hiyo inayo vifanya vitu vingine au chembe zingine ziwe ni zenye kuvutika kama kamasi, na zenye kutiririka kama damu.

Na mwishowe humtengeneza mwanadamu aliekamilika katika viungo vyake vyote na sehemu zake za nje na za ndani na kutokana nayo kumepatikana mtu mrefu na mfupi, mweupe na mweusi kwa usawa. Mbegu hii ina maana ya kuwa ni uhai wa ajabu uliofungika, elimu imeweza kugundua muundo wake na imeweza kuzipima harakati zake na kuichambua mada yake na njia ya kujigawa kwake. Ama siri ya uhai iliyomo ndani mwake ni ile ambayo elimu na wanazuoni wamekiri kwake na kukubali ya kuwa kuna Mwenyezi Mungu, kwa maana kwamba wameshindwa kutokana na elimu yao kusema lolote, bali ni kugunduwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ndio unao dhihiri kwenye siri hiyo.

Na mtoto huyu mchanga alie ndani ya tumbo la mama yake vipi anapata chakula na ni vipi anapumua na ni vipi anazikidhi haja zake na anaweza kuvishughulisha viungo vyake, na ni vipi kimeweza kuangaliwa kitovu ambacho ndicho kiunganishi kati yake na mama yake ili aweze kula chakula kupitia humo na aweze kufikia malengo yake, kitovu ambacho hakikurefushwa kiasi kwamba kikawa ni sababu ya chakula kuchachuka ndani yake kabla ya kumfikia mtoto, au kufanywa kifupi kiasi kwamba kitapeleka chakula kwa mtoto katika hali ya msukumo, msukumo ambao huenda ungesababisha maudhi kwa moto?

Nayo mimba inapo pevuka  na kufikia hali ya kujifungua, sehemu za siri za kike hutoa minyeso (umajimaji kama kimiminiko) mengi yenye malengo tofauti, kuna zinazo saidia juu ya kukunjamana mfuko wa uzazi na kujikusanya kwake na kuna zinazo rahisisha kuteleza kwa mtoto anapotoka tumboni na kuna zinazo fanya kazi ya kumsaidia atoke kwa njia ya kawaida katika kuzaliwa kwake.

Na kwa kuzingatia ya kuwa chuchu ni kiungo ambacho mwishoni mwa ujauzito, na mama anapo jifungua hutoa umaji-maji wenye rangi nyeupe uliyo mili kwenye njano, na miongoni mwa maajabu ya uumbaji ni kuwa umajimaji huu ni chembe za kemikali zenye kuyayuka ambazo humkinga mtoto kutokana na kuambukizwa na magonjwa.

Na katika siku ya pili baada ya kuzaliwa mtoto, huanza kutengenezeka maziwa safi na katika upangiliaji wa huyo apangae (M.Mungu) kuwa chuchu hutoa siku hadi siku kiwango zaidi cha maziwa. Si hivyo tu bali muundo wa maziwa hubadilika vilevile kulingana na vitu vitumikavyo kutengeneza maziwa na huzingatia zaidi vitamini zake. Na maziwa hayo hukaribia kuwa kama maji yakiwa na kiwango kidogo cha sukari mwanzoni, kisha huongezwa vitamini zake na kiwango cha sukari na mafuta kila muda unavyozidi kupita.

Na kila akuavyo mtoto huanza kuchomoza meno ili kumuandaa mtoto kwa ajili ya kula chakula, na kuota kwa meno tu huzingatiwa ya kuwa ni moja kati ya dalili za kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.

Meno hayo hutofautiana kwani kuna makato nayo huwa katikati ya kinywa na huwa karibu na sehemu ya mbele ya mdomo ili yafanye kazi ya kukata chakula, na pembezoni mwake kuna chonge yafanyayo kazi ya kukichambua chakula, kisha kuna magego madogo na makubwa kila upande nayo hufanya kazi ya kusaga chakula.

Wataalamu wamejaribu kwa bidii zao zote kutengeneza meno na wakajaribu kutafuta njia na mbinu ya kuyabadilisha meno ili watengeneze meno yaliyo tofauti na aliyo nayo mwanadamu na yaliyo bora, mwishowe walikiri kuwepo uwezo wa Muumba, na kukiri kwao kulitokana na kuthibitisha kwao ya kuwa nidhamu iliyo bora na iliyo kamili ambayo kuna uwezekano wa meno yakawa katika nidhamu hiyo ni nidhamu ya kawaida ya kimaumbile, kwa hivyo wakatengeneza aina ya meno yanayo fanana na meno ya kawaida, ya kimaumbile ya mwanadamu.

Na mtoto anapo achishwa ziwa na akaanza kula chakula huzidi kuonekana alama za kuwepo kwa Mwenyezi Mungu zaidi na zaidi kwa kuona vitu mbalimbali vilivyo umbwa kwa umakini na vinavyo mpatia mwanadamu usalama wa maisha yake, kwa mfano utaona mdomoni mwa mwanadamu matundu yaliyo ungana na pua kwa sehemu ya ndani, na tundu kwa ajili ya kupumua lililopo mwanzoni mwa mrija wa hewa na kolomeo lililopo mwanzoni mwa kituo cha kusaga chakula, na elimu inasema:

Hakika chembe chembe yoyote ya vumbi, ikipotea njia na ikafika kwenye chanzo cha kupumulia au ikaingia kwenye koromeo, njia ya kupumulia, ni lazima chembe chembe hiyo itafukuzwa na kitendo cha kukohoa ni majaribio ya kuondoa vumbi lililo ingia kwenye koromeo.

Sasa ni vipi chakula huingia kwenye tundu na kituo cha kusaga chakula, na kisiingii kwenye tundu la koromeo, wakati ambapo matundu hayo mawili yameungana, huku tukifahamu ya kuwa chembe yeyote ya vumbi seuze chakula na kinywaji vikiingia katika kituo cha hewa hupelekea kifo?

Naam, koo husukumwa juu wakati wa kumeza chakula na kuziba kwa kiungo kiitwacho kimeonjia ya kupumua mpaka kiingie chakula mahali pake, na haijawahi kutokea kimeo kikakosea katika kazi yake pamoja na kuwa hufanya kazi hii ya kupangilia upitaji wa chakula katika sehemu hii na kati ya mirija mara kadha kwa kila siku.

Na hufanyika kazi ya kumengenya (kuvunja) chakula yaani kukitoa katika hali yake ya kawaida ya ugumu na kukiweka kwenye hali nyengine ambapo huwa ni maji maji ambapo huwa ni rahisi kufyonzwa, na hufanyika kazi hii kwa umakini usio na mfano na hiyo ni dalili bora kabisa juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Na kila akilacho mwanadamu miongoni mwa vyakula vigumu na vikavu au vyakula vya majimaji, vichungu na vitamu, vizito na vyepesi vichachu na vilivyo poa na vyenye fukuto na baridi, vyote husagwa kwa mara moja na kwa njia moja, na vyakula hivi ambavyo huvila mwanadamu pamoja na kuwa ni vyakula tofauti, mwili wa mwanadamu huvipokea na kuviweka sehemu yake iliyopangiwa ili  tezi zivimwagilie minyeso  yake ya kusahilisha  kusaga (kumengenya) chakula kwa kiwango kilicho kadiriwa ambacho lau kitapungua kiwango hiki kwa kiasi kidogo hakutakuwa na uwezekano wa kusagwa chakula, na lau kitazidi kiasi kidogo mwili ungeungua, na kisha tonge la chakula liingiapo mdomoni huanza hatua ya kwanza, nayo ni kutafunwa  kwa chakula, na kazi hiyo hufanyika kwa kukichanganya chakula na mate ambayo hutolewa na tezimate.

Na mate hayo huwa ni mwanzo wa hatua za kusagwa chakula kwani mate hayo huwa yamekusanya kemikali maalum, nayo husaidia kushusha kiwango cha joto la chakula ikiwa chakula kitakuwa ni cha moto na huvunja makali ya ubaridi wake ikiwa chakula kimeganda kwa baridi, kama ambavyo ni kiungo cha msingi katika kuweka kiwango cha wastani cha uchachu na kupungua athari za mchanganyiko wa uchachu, na baada ya hapo tonge la chakula huteremka  likiwa limechanganyika na udenda hadi kwenye koromeo kwa kuanzia kwenye koromeo kisha kikahamia kwenye utumbo ambao hutoa asidi klorifriki (Choridric acid) kwa kiwango maalum kilicho andaliwa kwa makini, na kufikia kiwango chake kutoka nne hadi tano katika elfu, na lau ingezidi asidi hii kiwango chake hata kama ni kwa kiwango kidogo tu, mfumo wa utumbo unge ungua kiukamilifu. Na baada ya hapo hufuatia utoaji wa minyeso katika sehemu tofauti za mfumo mkubwa wa kusaga chakula. Hutoka minyesi ya matumbo, na minyesi ya nyonga na minyesi (kimengenya) vya kongosho na zinginezo. Na vimengenya vyote hivi huwa vinawiana na hali ya chakula kinacho fikiwa navyo.

Na elimu inasema ya kuwa vimengenya (umajimaji) hivi vinavyotolewa na utumbo mdogo  pamoja na matumbo na vilevile uteute (mfano wa kamasi) ambao husitiri kuta zake ni katika viungo msingi katika kupambana na vijiumbe maradhi (vijidudu vya magonjwa). Minyesi husimamisha ufanyaji kazi wake, nao uteute huwa ni kizuizi kati yake na kati ya tishu za tabaka nyembamba kiasi kwamba huzuia kusonga mbele kwake na huifunga mikono yake hadi kuvitupa nje (vijiumbe maradhi) pamoja na mabaki mengine ya chakula.

Na hazikujulikana kazi za sehemu ziitwazo tezi viziwi ila miaka michache iliyo pita nazo ni sehemu zitengenezazo kemikali ndogo ambazo huupa mwili chembe za dharura chembe ambazo hufikia kiwango chake cha nguvu ambapo sehemu moja yake ni sehemu katika bilioni zingine, lau kama itaingiwa na kasoro ingesababisha athari katika maumbile ya mwanadamu. Nazo zimepangwa kiasi kwamba kila tezi inakuwa ni kiungo cha kukamilisha kazi ya tezi nyingine na kasoro yoyote inayo weza kutokea katika ufanyaji kazi wa tezi moja, ikiendelea kwa muda fulani yaweza kufikia uhatari mkubwa.

Na miongoni mwa maajabu ni taarifa ya kielimu isemayo ya kuwa, utumbo mwepesi ambao urefu wake hufikia mita sita na nusu unakazi mbili za msingi:

Kazi ya kwanza ni kuchanganya chakula na minyesi (vimeng-enya) kiukamilifu kiasi  kwamba usagaji uwe ni wa jumla.

Na kazi yapili ni kukiweka chakula kilicho sagwa kwenye eneo kubwa la utumbo iwezekanavyo ili  ufyonze kiwango kikubwa cha chakula kadiri iwezekanavyo. Kisha baadae hufuatia hatua ya kusagwa chakula kwenye utumbo mgumu ambao kuzikamua chembe za mwisho za chakula kilicho sagwa ili kisitoke kwenye mwili isipokuwa mabaki yasiyo na faida kwa mwanadamu.

Na katika kiwiliwili cha mwanadamu pamoja na chembe chembe za kemikali zilizomo ambazo ni ngumu na za aina tofauti kuna vijiumbe maradhi na seli zazi na bacteria. Wataalamu wanasema:

Ikizidi idadi moja wapo kati ya vijidudu hivi kati ya idadi iliyo kadiriwa au ikapungua kazi ya kijidudu moja wapo au vijidudu vyenyewe vikatofautiana idadi ya kila aina iliyo  pangwa, kunge-pelekea kutofautiana huko kuangamia kwa mwanadamu.

Na viumbe hivi hai hutoa minyesi na hivyo hivyo hufanya kazi ya kukigeuza chakula kutoka kwenye hali ya ugumu na kukifanya kiwe laini na chepesi, na chenye madhara hukifanya kiwe chenye manufaa. Na ili kufahamu maumbile ya viumbe hivi, yatosha kufahamu ya kuwa wataalamu wameweza kufahamu idadi ya viumbe (vijidudu) vilivyomo kwenye tumbo kiasi cha laki moja kwenye upana wa sentimita moja mraba.

Na mwili hufunikwa na sitara madhubuti na ya ajabu, nayo ni ngozi. Pamoja na kuwa ngozi hiyo inavitundu (vinyweleo) ambavyo hutoa maji nje ya kiwiliwili, kwani vitundu hivyo huwa havifyonzi maji na kuyaingiza ndani kamwe. Na kutokana na kuwa ngozi ndio ambayo hushambuliwa na vijiumbe maradhi na vijidudu vitembeavyo angani utakuta kwamba ngozi hiyo imepewa uwezo wa kutoa minyesi ya kupambana na vijidudu hivyo na kuviangamiza.

     Ama ikiwa vijidudu vya nje vitashinda na kuvuka na kuizidi nguvu ngozi, hapo huanza vita kali kati ya vijidudu ambavyo hulinda mwili na vijidudu vya magonjwa vilivyo ingia, na huweka ngome kali kumzuwia adui yake alie kuja kufanya mashambulizi na hapo ima vijidudu vya kulinda mwili vimshinde adui yake na kumfukuzia nje ya mwili, au ni kushindwa na kuuwawa kundi hili. Kisha huja kundi jingine na jingine na jingine, hadi kufikia ushindi. Na vikundi hivi ni seli za damu ambazo idadi yake hufikia kiasi cha bilioni elfu thalathini nazo ni kati ya seli nyekundu na seli nyeupe.

       Basi utakapo ona juu ya ngozi kijipele chekundu chenye usaha,  fahamu ya kuwa usaha wake ni kundi lililo zidiwa nguvu limekufa wakati likitekeleza wajibu wake, na wekundu ni seli za damu zilizo kuwa zikipigana na adui yake.

      Na tukitaka kufanya uchunguzi kidogo kuhusiana na ngozi ili tufahamu umuhimu wake na nafasi yake na maajabu ya maumbile yake, basi suala la kwanza linalo staajabisha ni kuwa ngozi ndicho kiungo kikubwa zaidi katika mwili wa mwanadamu na upana wake kwa kiwango cha kati ni  inchi elfu tatu za mraba (karibu mita mbili za mraba) na katika kila inchi moja  mraba hutawanyika tezi nyingi, karibu mia, zitoazo mafuta na mamia ya tezi jasho ya nuroni (nerve cells), na futi kadha za nywele (malaika) za damu na ma milioni ya seli nyingine.

         Na vyovyote itakavyo semwa kuhusiana na ulaini wa ngozi na kuwa sawa sawa kwa sehemu yake ya juu. Ukweli ni kuwa ngozi haiko sawa na vile tuionavyo. Lau kama tutaiangalia kwa kutumia darubini (microscope) ambapo huikuza kwa mara kadhaa ili ionekane ngozi kama kijimlima kidogo kilicho inuka nyuma ya kilima kingine, na kati ya vilima hivi kuna jigawa matundu madogo madogo kana kwamba ni visima .

       Matundu ambayo hutoa mafuta juu ya mwili ili kuilainisha ngozi na mengine hutoa jasho na huwa kama kiyoyozi pindi joto linapo zidi, na huchomoza kwenye matundu haya malaika kama mashina ya mimea. Na kwenye sehemu ya juu ya ngozi kwa kutumia darubini, utaweza kuona vinavyopelekea kulika kwa ngozi kwa wepesi.

        Na sababu hizi za kupelekea kulika kwa ngozi tunazifahamu katika ulimwengu wetu huu uonekanao kutokana na yatokeayo kwenye milima, majabali, miamba na pembezoni mwa bahari kwa mmomonyoko upatikanao kutokana na zama kupita. Na ukitaka kufahamu zaidi ni kutokana na msuguano na chembe chembe za hewa na maji au mchanga ubebwao kwenye upepo au kwa sababu ya kutofautiana kiwango cha joto  hewani.

        Na vilevile ngozi yetu hulika kutokana na msuguano utokeao kati ya mwili (ngozi) na mavazi tuyavaayo, au kutokana na kunyoa nywele au kuchana au kuosha au kujikuna au kujisugua vyovyote msuguano huo utakavyo kuwa aina yake, nguvu zake au udhaifu wake.

      Na natija yake ni kuwa sisi tutaona kuanguka kwa ngozi yetu ikiwa kama magamba mepesi na ni vigumu kuyaona kwa macho yetu  ya kawaida, lakini lau tutafanya utafiti kwa kutumia vyombo vya kukuza vitu vidogo, kama darubini, tungeziona kuwa ni vijidudu (seli) ambavyo vimekufa na kuacha nafasi yake iliyokuwa vikiilinda na havitarudi tena. Na ngozi nayo hukosa ma milioni ya seli kama hizi kila siku. Na lau kama ingekuwa kukosekana kwa vijidudu hivi hakuna badala, basi mwanadamu angekuwa akionekana kama alie chunika ngozi. Kwa hivyo basi kutokana na upungufu upatikanao wa seli hizi ni lazima kuwe na seli nyingine zinazo chukua nafasi ya hizi zilizo kufa na kutoweka, na tabaka la ngozi la mwisho ni lazima lifanye kazi ya kuandaa seli kama hizi na halitosheki na idadi hiyo maadamu kiumbe bado kina uhai.

      Tabaka hili limeenea na kuufunika mwili wote kwa kiwamba chepesi, laini sana, nacho ni tabaka moja la tishu (kundi za seli za aina moja) ambazo bado ni vijana na kamwe hazizeeki na kamwe haziachi kujigawa, na mishipa midogo ya damu chini yake wakati wote huzipa chakula ili ziandae kwa kila siku mamilioni ya seli mpya na kuzitoa nje ya mwili.

      Na miongoni mwa vitu ambavyo haitakiwi kuvisahau wakati tukizungumzia mwili wa binadamu, ni kuwa sehemu moja ya sikio lake ni mfumo ulio kama mtiririko wa karibuni pinde elfu nne zilizo madhubuti na ngumu zilizo pangwa kwa nidhamu ya juu kupita kiasi, katika ukubwa na umbile lake.

       Na twaweza kusema ya kuwa pinde hizi zinafanana na chombo cha muziki kilicho andaliwa kwa makusudi kabisa kwa ajili ya kuvuta na kuhamisha vitu ivisikiavyo na kuvifikisha kwenye ubongo kwa utaratibu maalumu, kila inapo toka sauti au mvumo, iwe ni ngurumo za radi au mchakarisho wa majani.

      Na hivyo hivyo tunakuta katika yale tuliyo yaelezea hapo kabla na mengineyo maajabu ya kiwiliwili au viungo vya mwanadamu katika masikio yake macho yake puwa yake, ulimi wake, mifupa yake na mishipa yake na tezi za mwilini mwake na mifupa yake na mzunguuko wake wa damu na figo zake mbili zenyekushangaza na zenye kutuonyesha maelfu ya dalili ya kwamba nidhamu hii makini iliyopo kwenye kiwiliwili hiki haikutengenezwa bila sababu, kipuuzi, na haikupatikana kwa ghafla bila kuwepo mpangaji na haikutokea kutokana na msogeo na mageuko na mabadiliko ya madda (revolution of matter) iliyo pofu na kiziwi na isiyokuwa na mpango wa malengo maalum.

      Na vizuri kumalizia mazungumzo haya kwa kukiangalia kiungo cha ajabu zaidi kilicho gunduliwa na elimu ya kisasa ndani ya mwili wa mwanadamu nacho ni kromosomu (Chromo-some).

Kromosomu ni nyuzi nyuzi nyembamba zilizofunikwa na kiini seli kwa utandio mwembamba unao zitenganisha na viungo vingine vilivyopo pembezoni mwake, kana kwamba zina jiweka kando na kutotekeleza jukumu lake la msingi ambalo zimepatikana kwa ajili yake.

      Lakini utandio huu hauzuwii kufanya kazi ya usaidizi na maandalizi kutoka kwenye chembe chembe za kemikali nyingine-zo ambazo huisukuma kwake sitoplazimu (cytoplasm) zilizoko pembezoni mwake, ili kuzitumia kujenga chembechembe, na vilevile ili vitengeneze chembechembe zingine ambazo huhitajika katika kazi ya uhai.

       Na kromosomu zimeundwa kutokana na chembechembe ziitwazo D.N.A au kwa jina geni genes za urithi, ambazo zinakurithisha urefu wako na ufupi wako, na rangi ya nywele zako na macho yako na kiwiliwili chako, na zaidi ya hayo ubinadamu wako.

       Kisha ndizo ambazo hushikana (huungana) na kuumba farasi kutokana na farasi na kumfanya kima amzae kima nazo ndizo zinazo wafanya viumbe wawe ni wenye sura moja, na viumbe viwe ni vyenye kufanana na walio watangulia kwa mamilioni ya miaka.

      Huwezi kumuona mwanaadamu akimzaa punda, wala punda kumzaa kima na miti badala ya kutoa maua haitoi ndege. Sifa hizo zote ziko kwenye (D.N.A). Ama njia ya kutengeneza vichembechembe hivi ni njia ya aina pekee tena mzuri kwani zimeundwa kwa umbo mfano wa ngazi ya kuzunguka zunguka, kama skyubu (au tundu la konokono).

     Zote zinatokana na chembe za atomi ngumu, huikusanya mara moja na kuwa sukari maalumu iitwayo ribosi (ribose) wataalamu hadi leo hawaja fahamu vipi hujiunda na hutokea wapi, na sukari hii inaungana na vichembechembe vya fosfati (phosphate).

      Ngazi hii ya kuzunguka zunguka huanza kujizunguka zunguka kwa kinyume mara milioni kumi mzunguko ambao humalizika kwa kuundwa kitu mfano wa mkanda au kamba zisizo sokotwa. Na elimu bado haijaweza kufahamu hadi hivi sasa siri ya nguvu au uwezo ambao huzifanya zijizunguke na kujifungua kutokana na miviringo yake. Kwa uwezo wa Muweza wa yote Mwenyezimungu, ngazi hii inauwezo wa kujipasua mara mbili (nusu yake) kwa urefu kana kwamba imepasuliwa na msumeno, na vile mamilioni ya daraja za ngazi hujipasua nusu nusu.

       Na baada ya hapo huanza tukio kubwa kabisa la kuumba vichembechembe, na hujisukuma kupitia kwenye ukuta wa kiini na kuingia ndani vichembechembe au mawe ya ujenzi, nazo ni sukari na fosfati ademini, thiamini, gowamini na sitosini na zote hizo isipokuwa fosfati huundwa na kutengenezwa kwa njia ya ajabu.

Kisha hutiririka na kuzunguka pembeni mwa nusu ya ngazi au tabaka, na kila chembe hizi zilizo ndogo hufahamu sehemu yake na pembe yake ambayo hutakiwa kukaa. Baadhi yake huukamilisha mzunguko wa ngazi au tabaka na zingine huchukua sehemu ya nusu, yaani upande wa pili ambao ni mpya. Kazi ya upande wa pili inapo kamilika, hujiunda upande mwengine mpya katika kila nusu na hapo huanza kazi (ya sukari na fosfati) ili kutuundia ngazi mbili zilizo kamili au chembechembe mbili kubwa, kisha huanza kazi ya kuunda mzunguko wa mara milioni kumi mpya katika kila ngazi, ili kujizunguushia kama uzi ulio sokotwa na baada ya hapo, hufuatia kazi ya kuunda mzunguko mwingine wa mara milioni kumi vilevile kwa muelekeo kinyume na ule wa mwanzo, ili kujifungua na ili iweze kujigawa kwa mara nyingine, na kutokana na kazi hii huzaa vichembechembe vipya, na hivyo hivyo hupokezana.

Vichembechembe (vya D.N.A.) si makhsusi kwa ajili ya mwa-nadam tu, bali zimo katika kila kiumbe hai kama vijiumbe maradhi hadi wadudu na hata tembo na nyoka.

Na hizo ni chembechembe za msingi ambazo huingia kwenye mpangilio na uundaji wa chembe chembe za uhai, uchambuzi wa kikemia umethibitisha ya kuwa misingi iliyo jengwa na kufanywa na jeni, hazitofautiani katika upangiliaji wa viungo vyake katika viumbe vyote vilivyo hai, kwa hivyo basi ni kwa nini viumbe tuvionavyo, hivi leo vikatofautiana katika sura na maumbile yake?

            Baadhi ya wataalamu wanaamini ya kuwa, siri ya tofauti hii hurejea kwenye kiwango cha jeni (vichembechembe)D.N.A-ambazo hutengeneza gameti (mbegu za uzazi) na nidhamu za misingi minne tuliyo itaja hapo kabla katika muundo wake kwenye ngazi ndefu ya kuzungukazunguka pamoja na hayo hakuna yeyote alie toa taarifa ya kuridhisha na kukinaisha.

     Kuna wataalamu walio wengi ambao walijitolea wakati wao katika uchunguzi ili kulifumbua fumbo la maishaWaliandika vitabu na kutunga na wakafanya utafiti na mara nyingi wame kuwa wakitumia maneno yafuatayo katika kutoa sababu (huenda) au tunadhani na hadi leo bado wanatoa matamshi kama hayo kwa sababu siri ya uhai bado haifumbuliwi na kutoa pazia lake. Hakika kwenye kiini (nucleus), kromosomu (chromosome), nazo kromosomu hutengenezwa kutokana na jeni au chembechembe za urithi, na chembechembe za urithi hukaa chini ya mkondo wake chembe chembe D.N.A, nazo chembechembe D.N.A hutenge-nezwa na chembechembe ndogo, na chembechembe ndogo hutengenezwa na atomu, kwa hivyo ni jengo ndani ya jengo jingine.

Aya nyingine zilizo nyingi zilielekea kwenye kutoa ushahidi juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa kuelezea maumbile ya wanyama na maajabu na nidhamu iliyomo ndani ya wanyama hao, nidhamu ambayo ni muhali kupatikana kwake kimzaha na ghafla bila kupangwa na kwa matarajio kamwe.

ی            

 

Suratu Nuru 45 Na Mwenyezi Mungu ameuumba kila mnyama kutokana na maji, katika wanyama hao kunawate-mbeleao matumbo yao na kuna watembeleao miguu miwili na kuna watembeleao miguu mine Mwenyezi Mungu huumba atakayo.

                         

                                            (    )

Suratu faatir 28.Na miongoni mwa watu na wanyama wanaotambaa na  wanyama wengine rangi zao ni mbalimbali

                          ( )

Na hakuna mnyama yeyote atembeaye juu ya ardhi wala ndege wenye kupaa kwa mbawa mbili isipokuwa ni umma kama nyinyi (kama mfano wenu).Suratul Al-an-aam:38.

               .( )       Suratul   Mulk :19 :Je hawaangalii ndege wapaao juu yao hali ya kuwa ni wenye kuzichanua mbawa zao na kuzikunja, hakuna awazuiae kudondoka isipokuwa ni Mwenyezi Mungu mwenye rehema.

) . . . (.

Suratu-An nahl: 5-6  .Na wanyama amewaumba kwa ajili yenu, katika wanyama hao hupata vitu vya kuwatiya joto na manufaa mengine na wengine mnawala. Na katika wanyama hao kunamapambo wakati muwarudishapo kutoka malishoni na hukubebeeni mizigo hadi kwenye miji ambayo hamkuwa ni wenye kufika, isipokuwa baada ya taabu kubwa. Hakika mola wenu ni mpole sana na Mwenye huruma nyingi.

Na farasi na nyumbu na punda amewaumba ili muwapande na ni mapambo na anaumba msivyo vijua.

Wanazuoni wanakadiriya ya kuwa aina za wanyama hapa duniani ni zaidi ya aina milioni mbili. Na sehemu wanazoishi wanyama hawa ni za aina tofauti, kuna wanao ishi nchi kavu (bara), na kuna waishio baharini na pia bara au baharini kuna sehemu tofauti pia ya kuishi wanyama tofauti, na wanyama hawa wanatofautiana maumbile yao, tofauti ambayo ni kubwa, kwani kila aina moja wapo ina maumbile na viungo vinavyo wiana na mazingira wanayo ishi, na chakula wanacho kula. Na mdomo ndio sehemu ya mwanzo ya kulia chakula.

Nao mdomo ni kiungo cha kwanza cha kusagia chakula umetengenezwa kimakini na kwa utaalamu mkubwa, na hiyo ina julisha ukubwa na utukufu wa Muumbaji na Mtengenezaji wake, kwa mfano wanyama wakali kama simba, mbwa mwitu na wanyama wengine walio mfano wa hawa, waishio majangwani na mwituni na hawana chakula kingine tofauti na kile kiwindo chao wakipatacho kutokana na wanyama wengine, katika kuwinda kwao ni lazima wamshambulie ndio wapate chakula, na wanyama hawa wamepewa meno maalumu yaliyo makali na yenye kukata, na kutokana na kuwa katika mawindo yao huhitajia kutumia misuli yake, utakuta kuwa miguu yao ina misuli yenye nguvu na misuli hii imepewa silaha ya kucha zilizo kali sana  nao utumbo wake ukapewa asidi (vimengenya) na vifaa vingine vya kusaidia kumengenya na kusagia nyama na chakula.

Na miongoni mwa wanyama hao kuna aina ya wanyama wale ambao mwanadamu hufanya kazi ya kuwaandalia chakula, na kuishi kwao hutegemea mimea au miti fulani na nyasi na wanyama hawa viungo vyao vya kulia chakula vimetengenezwa kulingana na mazingira wanayo ishi na vyakula wanavyo kula kwa mfano utakuta kiasi fulani midomo yao ni mipana, na haina meno magumu wala magego magumu na badala yake wamepewa meno ambayo ni maalumu kwa kuvunja na kukata, kwa hivyo hula majani na mimea kwa haraka, na huyameza haraka kwa mara moja.

Na wanyama hawa wametengenezewa viungo vya ajabu sana vya kulia chakula kwa mfano chakula wakilacho huteremka hadi kwenye tumbo cheno (sehemu ya mwanzo ya tumbo katika wanyama wanaocheua) pindi wanapomaliza kazi zao na wakaketi kwa ajili ya mapumziko, chakula kile hutoka kwenye tumbo;cheno na kuhamia sehemu nyingine kisha hurudi mdomo-ni kwa ajili ya kusagwa kwa mara ya pili na baada ya hapo huingia kwenye sehemu ya tatu na ya nne.

Na kazi yote hiyo ndefu imeandaliwa kwa ajili ya faida ya wanyama, na elimu inasema: Hakika kazi ya kula na kucheua chakula ni ya lazima na itoayo uhai, kwa sababu nyasi ni katika mimea ambayo ni migumu kusagika kutokana na kuwa na nyuzinyuzi (selluloses) juu yake ambazo hufunika chembe chembe zote za mmea, kwa hivyo basi kusagwa kwake kunahitaji mnyama apate muda mrefu. Lau kama asingekuwa ni mwenye kucheua na tumbo lake lisingekuwa na mahala maalumu pa kuweka chakula muda mrefu ungepotea katika malisho takriban siku nzima bila mnyama yule kupata majani ya kumtosheleza na kumshibisha, na ingekuwa juhudi zake zote ni kuchukua chakula na kutafuna.

Kwa hivyo basi kazi yake ya kula na kukiweka chakula kisha kukirudisha baada ya kuwa kimepata uchachu wa kutosha, kazi hiyo ndiyo inayo kifanya chakula hicho kiwe ni chenye manufaa na chenye kutoa faida.

Ama viungo vya kusagia chakula vya ndege vinatofautiana sana na viungo vya aina ya wanyama tulio wataja, kwani ndege wana mdomo mrefu na mgumu usio na meno ulio undwa kwa mfupa, nao ni mdomo mrefu autumiao kulia chakula badala ya kuwa na mdomo kama wa wanyama wengine na usio na meno, na ndege humeza chakula chake bila kutafuna.

Na midomo ya ndege nayo hutofautiana kutokana na tofauti ya chakula wakilacho, kwa mfano ndege wenye kujeruhi wana midomo migumu iliyo pinda tena mikali kwa ajili ya kuchana nyama wakati ambapo bata na bata mzingo wana midomo mipana iliyo panuka kama kijiko au upawa unao wiana na utafutaji wa chakula kwenye udongo au tope au kwenye maji. Na pembezoni mwa midomo yao kuna vipande vidogo, vimedidimia kama meno ambavyo hudonoa donoa punje ardhini, midomo yao ni mifupi iliyo tengenezwa kwa namna ambayo itaweza kutekeleza au kufikia lengo lake.

Na upande mwingine ambao tunaweza tukaona katika sehemu hizo uumbaji na upangiliaji mkubwa na makini katika maumbile ya viumbe ni yale tuyaonayo kwenye miguu ya wanyama.Wanyama ambao ni wenye kukimbia au kubeba, tunaona ya kuwa miguu yao ni yenye nguvu imetengenezwa hivyo ili imsaidie kukimbia kwa kasi, kama ambavyo kila mguu huwa na kwato ngumu ambazo huuhami mguu na chochote kinacho weza kuudhuru kutokana na kukimbia sana au kutokana na njia mbaya.

Ama ngombe na nyati, miguu yao ni mifupi na yenye nguvu yenye kwato ngumu zenye kupasuliwa katikati, ili zimsaidie kutembea kwenye ardhi laini ya kilimo, wakati ambapo miguu ya ngamia ina kwato zenye kupasuliwa katikati na chini yake kuna ngozi laini na ndefu, huitwa Fumbo, ili kuuzuia unyayo usizame kwenye mchanga, na juu ya miguu yake vilevile kuna maungio ya ngozi ngumu humhami na kumkinga asiweze kuumia kutokana na kokoto na changarawe na michanga wakati anapotaka kukaa au kulala.

Na nyayo za ndege hutofautiana vile vile kutokana na tofauti ya maumbile yake. Kwa mfano ndege ambae hula nyama tuna- kuta kuwa miguu yao ina makucha magumu na makali, na yenye kupinda kidogo na ndiyo yanayo msaidia kushika na kuwinda, kama mwewe na kipanga, ama ndege ambao hula nafaka kama kuku na njiwa miguu yao ina makucha yaliyo tengenezwa yanayo faa kwa ajili ya kufukua na kuparura ardhi. Na ndege ambao hulazimika kupata chakula chao kwa kukitafuta kwenye maji, mikono yao au miguu yao imefunikwa na ngozi ambayo hutumia kama kafi katika kuogelea kwao.

 Na miongoni mwa maajabu ya viumbe vya Mwenyezi mungu ni yale tuyaonayo kwa chura.Hakika ulimi wake ni mrefu zaidi ukilinganisha na ndimi za viumbe wengine walio hai, kiasi kwamba urefu wake ni nusu ya urefu wake, na umeandaliwa na kupewa ute ulio kama gundi ili aweze kuwinda nzi, yeye husimama hadi wamkaribie nzi na wanapo mkaribia hurusha na kuurefusha ulimi wake ili wagandie hapo nzi kadhaa ambao ndio chakula cha msingi cha chura.

Na la ajabu zaidi ni kuwa, kutokana na kuwa chura hana shingo ambayo ingemuwezesha kuzungusha kichwa chake na kuweza kuona vitu vilivyopo pembezoni mwake utakuta amepewa macho yaliyo tokeza mbele yenye kuzunguuka pande zote. Na miongoni mwa maajabu yanayo sisitizwa na elimu ya kisasa ni kuwa wanyama wengi wenye kunyonyesha wanahisia kali za kunusa na zenye nguvu, na hisia zao za kuona ni dhaifu, tofauti na ndege, wanahisia za kuona ambazo ni kali sana  na hisia za kunusa ni dhaifu, na haikuwa hivyo isipokuwa ni kwa sababu wanyama hupata chakula chao na kukifikia chakula ambacho wakati wote huwa ardhini kwa kutumia hisia ya kunusa, wakati ambapo ndege hutumia hisia yake ya kuona iliyo kali na akiwa juu angani ili aweze kuona chakula chake na huku akiwa juu kabisa.

Ama chazo (konokono) wa kawaida ana macho mengi sana yenye kufanana na macho yetu na macho hayo humwekua mwekua kutokana na kuwa na virudisha nuru mfano wa vioo vidogo vingi visivyo hesabika. Inasemekana ya kuwa virudisha nuru hivyo humsaidia kuona vitu pande zote kuanzia kulia hadi juu.

Virudisha nuru hivi havimo kwenye macho ya mwanadamu. Je amepewa konokono virudisha nuru hivyo (vioo) kwa sababu hana uwezo wa kiakili kama mwanadamu! Na kutokana na kuwa idadi ya macho katika wanyama ni kati ya mawili na zaidi, na yote ni yenye kutofautiana, je maumbile yalikuwa katika kiwango kama hiki  kikubwa cha ujuzi katika vitu vionekanavyo?!

Naye Samaki anahisia ya ajabu hisia ambayo humkinga asigongane na mawe na vizuizi katika giza la bahari. Na wataa-lamu baada ya kuyafanyia uchunguzi maumbile haya walitoa riporti isemayo  kwamba waliona ndani ya mwili wa samaki msitari mrefu kwenye mbavu zake msitari huu anapo angaliwa na darubini (chombo cha kukuza vitu) huonekana kuwa ni viungo vingi vilivyo kusanyika na vidogo vidogo na vyenye hisia ya hali ya juu sana, huhisi kama kuna kizuwizi au kuna mawe na hufahamu hivyo kutokana na mbano wa maji kutokana na kugongana na kizuizi, na samaki hugeuza njia yake.

Ama popo hakika mambo yake yaliwashangaza wataalamu, yeye anapo paa au kuruka kwenye kiza cha usiku hagongani na nyumba au miti au kitu  chochote kilichoko njiani mwake. Mtaalamu mmoja wa Italy alifanya uchunguzi kufahamu uwezo huu wa popo, akatundika kwenye chumba kamba nyingi sana, na katika kila kamba akafunga kengele ndogo ili ikiguswa tu ile kamba kengele inagonga, kisha akamuweka popo mmoja na kufunga chumba, yule popo akaanza kuruka mule chumbani na kuzunguka kila upande na hakuna kengele yoyote iliyo lia, na maana yake ni kuwa popo pamoja na kuruka kwake haku-gongana na kamba yoyote kati ya kamba zilizo tundikwa chumbani humo. Kutokana na kazi hii yule mtaalamu na wenzake wakagundua ya kuwa mnyama huyu anaporuka hutumia mitetemo (vibrations) ya sauti hewani ambayo kurudi kwake inapogongana na kitu chochote kilicho mbele yake na kumfanya kukihisi na kukiepuka.Waligundua pia kwamba njia zake za kufahamu na kuhisia kwake kuwepo kwa kizuwizi ni njia ileile ya rada (radar).

Ama ngamia yeye vilevile amejaa dalili za utukufu wa Mwenyezi Mungu kwa namna ambayo inatufahamisha au inatupa ufahamu kamili wa yale aliyotuelekezea Mwenyezi Mungu kwa kusema:

Suratul-ghaashiya:17  

         Je hawamuangalii ngamia vipi ameumbwa?

Kutokana na kuwa sehemu anazofanyia kazi mnyama huyu na kuishi ni jangwani, ameumbwa na uwezo wa kuweka akiba ya chakula au maji kwa muda mrefu katika nundu yake ili aweze kupambana na njaa jangwani na kiu yake, kama amabavyo aliumbiwa -kwa malengo hayo- makope marefu ambayo yamezunguka macho yake na kope ambazo hufanana na nyavu zinazoyahami macho yake yasipatwe na chembechembe za mchanga wakati unapo vuma upepo mkali wa mchanga, na wakati huohuo anaweza kuona kupitia wavu huo wala halazimiki kufunga macho yake kama tufanyavyo wakati linapo enea vumbi.

 

Na vilevile miguu yake yenye kwato laini inayostahili kutembelea kwenye michanga bila kudidimia, na pua yake ambayo anauwezo wakati wa kuifungua kwake kuzuwia kuingia kwa michanga kutokana na upepo mkali, na midomo yake ya juu ambayo imeumbwa ikiwa imepasuliwa ili imsaidie kula mimea ya jangwani ambayo mara nyingi huwa ina miba.

Ama sisimizi anazo dalili nyingi za kuwepo Mwenyezi Mungu, mdudu huyo amepewa fahamu na subira na hisia, ambazo mtu yoyote hawezi kuelewa kiwango chake wakati akimuona umbile lake na mwili wake mdogo.

Na huenda mji wa sisimizi ni mji ulio bara zaidi na ambao unastahili kufanyiwa uchunguzi na utafiti kwani ndani yake kuna utaalamu ulio makini na usaidizanaji wa ajabu, na nidhamu iliyo pangwa vizuri kwa umaridadi wa hali ya juu na ufahamu wa kitaalam.

Na katika baadhi ya aina ya sisimizi wafanyakazi huleta punje ndogondogo kwa ajili ya kuwalisha wengine wakati wa kipindi cha masika. Nao sisimizi huanzisha sehemu ya kuweka akiba ya chakula ijulikanayo kama ghala la kusaga na sehemu hiyo sisimizi ambao wamepewa midomo mikubwa yenye uwezo wa kusaga, hufanya kazi ya kuandaa chakula kwenye mamlaka yao na hii huwa ndio kazi pekee ya sisimizi hawa.

Na kuna aina ya sisimizi wengine ambao tabia za maumbile yao huwapa msukumo  wa kutengeneza viota vya chakula, viota ambavyo twaweza kuviita Bustani ya viota, na huwinda aina fulani ya wadudu na mabuu kutokana na wadudu hawa sisimizi huchukua minyesi aina fulani yenye kufanana na asali ili iwe ndio chakula chao.

Vile vile  huliteka kundi fulani katika hawa wadudu na kuwa-fanya watumwa. Na baadhi ya sisimizi wakati wanapo tengeneza viota vyao huyakatakata majani ya miti kwa ukubwa utakikanao, na wakati huo huo baadhi ya wafanyakazi  wa sisimizi huyaweka majani pembezoni katika sehemu yake, wakiwatumikisha watoto wao kuyafuma majani hayo.

Sasa ni vipi zitaweza chembe chembe atomi ya madda ambazo ndizo ziundazo sisimizi kama wanavyo dai, kumpa uwezo sisimizi wa kufanya kazi kama hii iliyo ngumu na inayo hitaji utaalamu wa hali ya juu?!

Na wanyama nao baada ya haya au kabla ya haya wanayo lugha ya kuwasiliana na kuzungumza , na Qurani tukufu wakati ilipoteremka iliwazindua watu kahusu ukweli huu, kama ilivyo elezwa kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Katika aya hii, kisa cha Nabii  Sulaimani alipopita mahala ambapo kulikuwa na sisimizi, walipo muona wakaambizana, anaelezea hadi walipo fika kwenye bonde la sisimizi, sisimizi mmoja akasema:Enyi sisimizi ingieni majumbani mwenu ili Sulaimani na jeshi lake wasikupondeni hali ya kuwa hawahisi (kuwepo kwenu). Kisha elimu baada ya kuteremka aya hii kwa karne kadhaa, ikaja na kuthibitisha ukweli huu kwa kuona na kwa uchunguzi uliofanywa.

Lugha ya kila mnyama kati ya wanyama wenye kuzaliana inatofautiana na lugha ya mnyama mwingine. Kwa mfano kuku ni ndege, (mnyama) ambae ana maingiliano sana na mwana damu, wakati mwingine hutoa sauti maalumu iliyo tofauti, na baada ya sauti hiyo utaona vifaranga vyake vikimkimbilia na kuanza kudonoa punje, kisha hutoa sauti nyingine maalumu, na ghafla utaviona vifaranga vikikimbilia kwenye kiota wakati uleule.

Naye nyuki anapopata shamba lenye maua mara hurudi haraka kwenye mzinga na huwa hajafika katikati mara utaona akitaharuki kwa njia maalumu na ghafla nyuki wengine humki-mbilia na kumfuata nyuma yake hadi kuwafikisha kwenye shamba la maua.

Mtaalamu mmoja anasema kwamba yeye alifanya majaribio kwa sisimizi, kwani alimuona sisimizi mmoja ametoka kwenye shimo lake akiwa peke yake.Yule bwana akamchukua nzi na kumchomeka kwenye kizibo cha chupa (cork), kwa kipini kidogo na akamuweka kwenye njia ya sisimizi. Baada tu ya yule sisimizi kumfikia nzi yule alianza kumtoa kwa mdomo wake na miguu yake kwa muda wa zaidi ya dakika ishirini, baada ya kuwa na yakini kuwa hawezi, akarudi kwenye shimo lake, na baada ya sekunde kadha akatoka  yule sisimizi akiwa amewatangulia sisimizi wengine wengi kati ya jamii na ndugu zake hadi akawafikisha pale nzi alipo, wakampanda nzi yule na wakaanza kumchanachana, na wakarudi sisimizi kwenye shimo lao na kila mmoja akiwa amebeba sehemu fulani ya yule nzi.

Yule sisimizi wa mwanzo alikuwa amerudi kwa rafiki zake na hakuwa amebeba chochote, basi aliweza vipi kuwafahamisha sisimizi wengine ya kuwa amepata chakula kinacho faa kama hakuwajulisha kwa kutumia lugha maalumu?

Watafiti wanasema ya kuwa tembo wanapo kuwa kundi, tembo wa kike huwa haachi hata sekunde moja kutoa mlio wakati wote anapo kuwa akitembea kwenye kundi, na wanapo tawanyika na kila mmoja akaanza kutembea peke yake sauti hukatika.

Na sauti za kunguru zina tofautiana. Na kuna sauti ijulishayo kuwepo kwa hatari nae huitoa sauti hiyo kuwatahadharisha wenzake juu ya kuwepo kwa hatari wakati ambapo akiwa na furaha hutoa sauti nyingine ambayo hukaribiana na kicheko.

Na lugha hawanazo tu aina ya wanyama tulio wataja hapo kabla, bali kila aina moja wapo ya aina ya wadudu wana lugha maalumu vilevile kwa mfano, buibui  huzitumia nyuzi zake kama nyezo za kuzungumza na wenzake, dume husimama pembeni mwa wavu na kuuvuta, ghafla utamuona jike anatoka ilikumpo-kea au atamjibu kwa kuvuta uzi ule kwa njia tofauti na ile ya mwanzo, kana kwamba wanajibizana kwa njia ya simu maalumu.

Na tukirudi na kumwangalia kuku ili tujifunze katika dunia yake ushahidi wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu tuweze kuona maajabu mengi, na inatosha kati ya maajabu hayo kufahamu ukweli huu ufuatao. Mtaalamu wa kiamerika alifikiria njia ya kuzalisha vifaranga vya kuku kwa mayai yasiyo laliwa na kutotolewa na kuku, na akafanya hivyo kwa kuliweka yai kwenye joto kama lile lipatikanalo kwa kulaliwa na kuku. Akayakusanya mayai na kuyaweka kwenye chombo cha kutotolea, na mkulima mmoja akamnasihi ayageuze mayai yale kutoka kipindi hadi kipingi kingine, kwani alimuona kuku akifanya hivyo.Yule mtaalamu alimcheka na kumjulisha kuwa kuku huyageuza mayai ili upande ulio kuwa chini nao upate joto la kuku, ama yeye aliweka joto na kuyaeneza mayai yote kwa kifaa cha kutotolea na joto likaenea kwenye sehemu zote za mayai. Na mtaalamu huyu akaendelea na kazi hadi ulipo fika wakati wa kutotoa muda ukavuka bila yai lolote kutotolewa, na akarudia majaribio yake kwa kufuata maelekezo ya yule mkulima, akawa akiyageuza mayai hadi ulipofika muda wake na vifaranga vikatoka (vika-totolewa).

Na sababu  ya kielimu ya kuyageuza mayai ni kuwa kifaranga kinapo kuwa kimeumbwa kwenye yai chembechembe za chakula, hutuwama sehemu ya chini ya kifaranga kwa hiyo likibakia yai bila kutikiswa huchanikachanika mifuko yake na kutokana na sababu hiyo, utaona kuwa kuku haligeuzi yai siku ya kwanza na ya mwisho. Je kuku anaweza kufahamu siri hizi kama si kupewa kufahamishwa kwa njia fulani ambazo mwanaadamu ameshindwa kuzielewa.

 Na kutokana na muongozo huu pekee nyoka wa majini hutembea na kuhama kutoka sehemu kwenda sehemu ya mbali, uhamaji wa ajabu na wenye kushangaza na unao takiwa kuangaliwa kwa makini, kwani viumbe hivi vya ajabu vinapo kuwa vimekuwa na kukamilika maumbile yake, huhamia sehemu tofauti za mabwawa na mito wakikusudia kwenda kwenye kina cha mbali na kirefu kusini mwa barmuda, na anapofika huko hutotoa na kufariki. Ama watoto wake ambao hawana nyenzo yoyote ya kuwafahamisha chochote, tofauti na sehemu ile waliopo, wao hurudi alikotokea mama yao na kupata njia ya kuwafikisha ukingoni mwa bahari alikotokea mama yao, na baada ya hapo huhamia kwenye mto wowote au bwawa dogo, baada ya kuwa amepambana na mawimbi makali ya ukingoni mwa bahari. Na wakati anapo kamilika ukuaji wake kuna kanuni iliyofichika ambayo humpa msukumo wa kurudi sehemu alipo zaliwa baada ya kukamilisha safari zote. Sasa ni kipi chanzo (kitu) ambacho humuelekea kufanya au kuyaelewa hayo? Haijatokea kamwe kuvuliwa nyoka wa majini wa amerika kwenye maji ya ulaya, au nyoka wa ulaya kuvuliwa kwenye maji ya Amerika!

Na jambo la kushangaza na kufanyiwa utafiti, ni kuwa ukuwaji wa nyoka wa majini wa ulaya ni wa taratibu kuliko wengine, ni kati ya mwaka na zaidi, na imekuwa hivyo kutokana na mwendo mrefu autumiao katika kusafiri.

Je kwa fikra zako unaona ya kuwa chembe za madda zisizokuwa na akili zilizo ungana katika mwili wa nyoka huyu wa majini, zilikuwa na hisia za kuuelekeza ufahamu wa ndani au nguvu za utashi wa kufanya yote hayo?

Na ufahamu huu (il-haam) pekee ndio unaomfanya ndege anae wachukua vifaranga vyake kutoka  kwenye viota vyake vilivyo zeeka, nao wanapokuwa  wakubwa hutengeneza viota vingine kama vile bila kuwepo tofauti yoyote.

Na vilevile kutokana na ufahamu huu pekee ndio huwafanya baadhi ya wanyama kubadilisha sehemu ya mwili wake iliyoji-tenga na kuweka sehemu nyingine. Kama kaa wa baharini ambae anapokosa kucha zake hufahamu ya kuwa sehemu moja wapo ya mwili wake imepotea, na kufanya haraka ya kuweka badala kwa kuzifanyisha kazi chembe chembe za urithi, na kazi hiyo inapo timia chembe za urithi husimama kufanya kazi, kwani zinafa-hamu kwa kupitia njia fulani ya kuwa wakati wa mapumziko umewadia.

Na hivyo hivyo hufanyika kwenye mdudu aitwae kathirul-arijul wa majini yeye anapojigawa sehemu mbili, anaweza kujitengeneza upya kupitia moja kati ya sehemu hizi mbili. Na pia ukimkata kichwa funza, hutengeneza kichwa kingine haraka sana badala ya kile kilicho katwa.

Na sisi tunaweza kuzifanyisha kazi seli ili kuponya jeraha, lakini ni vipi madaktari watafahamu kuzifanyisha kazi seli hizo ili zitengeneze mkono mwingine, au nyama au mfupa au kucha au sehemu nyingine yoyote?!

Ama ulimwengu wa wadudu, ikiwa utafanya mazingatio na uchunguzi, utaona maajabu mengi na makubwa, na huenda uchunguzi mdogo wa kutaka kufahamu tabia za wadudu tu unatutosheleza kutokana na maelezo mapana na marefu. Hakika mdudu aitwae kipepeo, huchagua majani ya kabichi kwa ajili ya kutagia na hali ya kuwa yeye hali majani ya mmea huu wala hauhitajii, bali kinacho mfanya afanye hivyo, ni ujuzi wake wa ndani wa kitabia na kimaumbile, kwani anafahamu ya kuwa mayai yatapasuka na kutatoka vijidudu vidogo vidogo ambavyo havina chakula viwezavyo kula isipokuwa majani ya kabichi, kwa hivyo ni lazima atage mdudu huyu kwenye majani ya kabichi ili watoto wapate chakula baada ya kutotolewa.

Na pamoja na hayo mdudu huyu hajui masuala haya kwa kutumia akili yenye kujua na kupambanua mambo.

Na dondola huwinda wadudu na kuwaweka kwenye shimo ardhini kama aina fulani ya nyama iliyo hifadhiwa kisha hutaga juu yake yai moja, kisha huliweka kwenye kiota na baada ya hapo huanza kutafuta vijiwe vidogovidogo, na anapo vipata huvibeba na kuzibia mlango wa kiota chake. Na hufanya hivyo ili vitakapo totolewa vifaranga vyake viweze kukuta chakula chao kime-kwisha andaliwa.

Na mbu ambae hutaga juu ya maji, kila yai huliweka mifuko miwili ya hewa inayo lifanya yai lielee juu ya maji. Je mbu anafahamu kanuni ya archimids?

Na mdudu aitwae kaadhifatul-kanabil, mdudu ambae anapo kutana na mnyama mkali, hutulia na kulala mbele ya mnyama huyo bila ya woga wala wasiwasi, na mnyama yule anapofungua mdomo wake ili kumla mdudu huyo, wakati huohuo hukifinya kifuko kilichomo tumboni mwake na kuchanganya kemikali fulani ambayo ni mchanganyiko wa vitu vitatu ikiwa imeundwa kwa hydroquinin na  oxid hydrogen na enzelon maalum, na kutokana na mchanganyiko wa vitu hivi vitatu, hupatikana gesi kali yenye kuuma (kuwasha) na yenye harufu mbaya na huitoa gesi hiyo kujihami na mnyama yule, na huyo mnyama anaposikia harufu ile hukimbia kutokana na woga.

Je mdudu huyu alipata diploma ya kemia katika chuo kikuu cha Cambridge?

  Na wadudu ambao huweka nyavu kutokana na hariri kwa ajili ya kuwinda. Na kimulimuli ambao hutoa mwanga usiku ili kuwavuta mbu na kuwala, na wadudu wa majini ambao huogelea majini kwa miguu yao iliyo kama kafi na kupaa angani kwa miguu yao iliyo kama mbawa. Na vipepeo ambao mbawa zao huwa zimefunikwa na gamba ambalo sehemu yake moja imetengenezwa kutokana na vipande vya mifupa  myepesi sana kutokana na madda laini sana na hupitisha mwanga na kugeuka kuwa rangi nzuri ya bluu.

Na lau kama kutatokea mabadiliko kidogo sana kiwango cha chembe kati ya maelfu ya chembe chembe katika ncha moja, ya unene wa gamba la ubawa wa kipepeo, mwanga ule ungebadilika au kutoweka kabisa. Na kwa muhtasari ni kuwa:

Hakika kwenye ulimwengu wa wanyama kuna maajabu mengi na yote hayo ni ushahidi juu ya maumbile na utengenezaji na uumbaji ulio makini, uumbaji ambao hatuwezi kuuelezea kiukamilifu kwenye kurasa hizi chache, na uumbaji huo ni wa Mwenyezi Mungu ambae kila kitu alikiumba katika hali ya umakini, na Mwenyezi Mungu ameepukana na yale wayasemayo wapingaji wa kuwepo kwake.

Na kuna aya nyingi zingine ambazo hutoa ushahidi juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na kuwa yeye ndie muumbaji wa viumbe, kwa kutumia njia ya kuhimiza kufikiria na kuzingatia yaliyomo kwenye ulimwengu wa mimea, na kuteremsha maji kutoka mawinguni na maajabu ya sayari na mbingu na ardhi, kiasi kwamba vitu hivi haiwezekani kuwepo kwake na kuwa na kanuni kama hizi zisizo badilika bila kuwepo alie viweka na akavipangia kanuni, yaani haiwezekani vikajiweka vyenyewe na kujiwekea kanuni  kama hizi tuzionazo!

)  (.

Suratul waaqia: 63-65 Je mnaiona mimea  mnayoipanda, haya mazao myalimayo, je nyinyi ndio myalimayo au sisi ndio tunao iotesha? Tungelitaka tungeliifanya mapepe (haizai).     
) (                    Suratul-waaqia:71-72 Je mmeuona huo moto muuwashao, je nyinyi ndio mlio umba mti wake au sisi ndio tumeuumba?                                       )    (

 Suratul -An- aam 99.

 Nayeye ndie ambae ameteremsha maji kutoka mawinguni na kutokana na maji hayo tukaiotesha mimea ya kila kitu. Kisha tunapelekea kuchipua majani ya kijani katika mimea hiyo, tukatoa ndani yake punje zilizoganda. Na katika mitende vinatoka katika makola yake vishada vyenye kuinama vimeka-ribia kufika chini kwa vilivyo tia, hata vimekuwa vizito  na anakuotesheeni mabustani ya zabibu na zaituni na makoma-manga yenye kufanana na yasiyo fanana, angalieni matunda yake pindi yanapo toa matunda, kuiva kwake, hakika katika yote hayo kuna dalili kwa watu wenye kuamini.      

) (.  Surat-twaha 53.

Mwenyezi Mungu ndiye alikufanyieni ardhi iwe tandiko na akakuwekeeni njia ndani ya ardhi hiyo, na akakuteremshieni maji kutoka mawinguni na kutokana na maji hayo tukaotesha namna ya mimea mbalimbali .                                                              

 ) ֡   .(                         
Ama yule alie umba mbigu na ardhi na akakuteremshieni maji kutoka mawinguni na kutokana na maji hayo akakuotesheeni mimea kwenye mabustani yenye kuvutia nyinyi  hamna uwezo  wa kuiotesha miti  yake.                                                                              
                                                                               Mimeya ni ulimwengu unaojitegemea, na wataalamu wa mimea bado wanaendelea na kazi ya kuifanyia utafiti, na kila wanavyo fanya utafiti ndivyo wanavyo zidi kugundua mambo mapya ambayo walikuwa hawayajui. Na aina ya mimea inakaribia kuwa nusu milioni, na mimea hiyo inatofautiana katika maumbile na jinsi ya kuzaliwa na umri inayoishi na mengineyo.                           

 Na kuna baadhi ya mimeya ambayo huishi kwa muda wa masiku kadhaa, na kuna mingine huishi kwa muda wa miaka miwili, na mingine huishi zaidi ya umri wa mwanadamu kwa mamia ya miaka. Na mimea yote humea kupitia mbegu  ambazo huwa zimekusanya mazingira maalumu ya uhai ndani yake, na mbegu hizo huhifadhi kiini cha uhai wake, na kwa muda mrefu, na wakati inapoota au kumea ni lazima ipate maji ya kutosha na joto linalo stahili kwani kila aina ya mbegu humea kwenye kiwango maalumu cha joto kama ambavyo huwa vilevile ni muhimu kwa mmea kwa sababu ni kiumbe kilicho hai kinachoishi na kupumua.

   Na mbegu inapo ota na kutoa mmea ulio hai wenye mizizi midogomidogo huanza mmea huo kujipatia chakula kilicho wekwa akiba ndani ya mbegu hadi mmea wake urefuke, na baada ya hapo hutambaa mizizi yake kwenye ardhi ili kujipatia chakula, na mfano wa mmea ni sawa na mtoto mdogo tumboni mwa mama yake na hata wanyama wengine, hupata chakula wakiwa ma-tumboni mwa mama zao, baada ya kuzaliwa chakula chao huwa ni maziwa, kisha hujitegemea na kujitafutia chakula wenyewe. Je kuna alieupa mmea uhai  tofauti na Mwenyezi Mungu?

Ama tumbo la chakula la mmea kwanza kabisa hutegemea mizizi. Na mizizi ndio sehemu ya kwanza ya mmea ya kujipatia chakula, na mimea yenyewe hutofautiana kwa kiasi kikubwa kulingana na mahitajio ya mmea, kuna mizizi ambayo ndio vizingiti vya mmea, na kuna mizizi ya chakula na kuna mingine midogomidogo ya hewa na ya kupumulia, na kutofautiana kwa maumbile na tofauti zingine zimeumbwa ili ziwiane na uwezekano wa mmea kufikia mahitajio yake ya chakula.

Na mizizi hukua na kutoa mizizi mingine midogomidogo ambayo hufyonza lishe yake ya ardhini na kuhamia lishe ile iliyo fyonzwa sehemu ya juu, na kwa njia hizi mmea huweza kujipatia chakula na kukua, na kukua kwa mmea kunahitajia mwanga na maji na vitu vingine ambavyo ni dharura kama kaboni (carbon) na oksijeni (oxygen) na pia fosforasi (phosphorus) na sulfuri (sulphur) na nyingine nyingi.

Na mmea hupumua kupitia majani yake ambayo ndiyo mapafu yake ya kuchukua hewa ya oxygen na kutoa hewa ya carbon dioxide na mfano wake ni kama mwanadamu na mnyama, na kupumua kwa mmea hufuatana na kuzidi kiwango cha joto, na kupumua huko hufanyika usiku na mchana, isipokuwa ni kwamba tija ya kazi hii huwa haionekani wakati wa mchana, kutokana na ufanyaji kazi wa carbon ambayo mmea huifanya kwa kasi zaidi kuliko kazi ya kupumua, na hapo hutoka oxygen na kufyonza hewa ya carbon dioxide.

Na utafiti umetufahamisha ya kuwa ufanyaji kazi wa carbon, unajitosheleza kuiangamiza hewa ya carbon dioxide iliyomo ulimwenguni. Lau kama mimea ingetegemea carbon dioxide hiyo tu, lakini Muumba Mtukufu amevifanya baadhi ya viumbe vilivyo hai vitoe hewa hii ya carbon dioxide wakati wa kupumua kwake, kama ambavyo vitu vilivyo vifu katika hali ya kutawanyika viungo vyake huitoa hewa hii vilevile, na hivyo hivyo katika baadhi ya kazi nyingine hupatikana.

Na suala la kuangamiza hewa hiyo na kuzalisha au kutenge-neza mada  hii, haikuachiwa huru kiasi kwamba inaweza kuzidi au kupungua, bali hekima ya Muumba iliamua kiwango cha carbon dioxide angani daima kiwe kutoka chembe tatu hadi nne katika kila chembe chembe elfu kumi za hewa. Na kwamba kiwango hiki ni lazima kiwe thabiti kwa wakati wote ambao ulimwengu utazidi kuwepo, na haijawahi kutokea kamwe pamoja na kutofautiana kazi za kuangamiza na kazi ya kuzalisha hewa hii kukuta  kiwango hiki kimetofautiana.

Na badhi ya wataalamu wanasema, hakika oxygen  lau ingekuwa angani kwa kiwango cha asilimia 50% kwa mfano au zaidi, badala ya asilimia, 21% vitu vyote vyenye uwezekano wa kuunguwa katika ulimwengu, vingekuwa na hatari ya kushika moto kwa kiwango cha kuwa cheche za umeme zinapo kutana na mti ni lazima uwake moto na mapori yote kuungua hadi yangefikia hali ya kutaka kulipuka.

Na lau kama kiwango cha oxygen katika hewa kingeshuka hadi asilimia kumi (10%) au chini yake, labda maisha yange jiendesha yenyewe kwa zama zote, au kwa muda wote, lakini katika hali hii kungekuwa na kiwango kidogo sana ambacho hutumika kwenye makazi ya watu ya kimaendeleo aliyo yazowea mwanaadamu - kama moto kwa mfano- umeweza kupatikana kwa ajili yake.

Ama maji nayo ni miongoni mwa vitu vya dharura ambavyo haiwezekani kamwe kutoyahitajia kwa viumbe vingine vilivyo hai (na kutokana na maji tumekifanya kila kitu kilicho hai), kwa hiyo maji ni chanzo cha msingi kati ya vyanzo vya uhai, na Quran tukufu imehimiza juu ya kufanya mazingatio katika kinywaji hiki adhimu na katika udharura wake na umuhimu wake, bali imewataka watu wafahamu ya kuwa kupatikana kwa maji na kuyaandaa kwake juu ya ardhi, ni dalili ya kuwepo muumba aliyeumba, alievifanya viumbe vyote viwepo.

) (.Suratul-waaqia 68-70

Je mmeyaona maji myanywayo? Je nyinyi ndio mlio yatere-msha kutoka mawinguni au sisi ndio tulio yateremsha? Lau tungetaka tunge yafanya kuwa ya chumvi (makali) basi mbona hamshukuru?

                                            

Suratur-rum 24.Na miongoni mwa ishara zake, ni kuwa anakuonyesheni umeme kwa ajili ya kukuogopesheni na kukutieni matamanio. Na uteremshaji maji kutoka mawinguni na kwayo huifanya ardhi iwe hai baada ya kuwa imekufa.

Na wataalamu wanasema:

Hakika bahari ndio msingi wa maji matamu na chanzo chake, na maji ya bahari yenye chumvi, viumbe walio hai wa ardhini hawawezi kuyatumia na hayafai kuwa ndio yenye kuulinda uhai wa viumbe, kutokana na sababu hiyo Mwenyezi Mungu aliwaandalia waja wake na viumbe vyake vingine matone matone kupitia mvua, na ikawa mvua ndio iyahamishayo maji ya bahari kuyatoa kwenye hali yake ya kwanza ya kuwa na chumvi na kuyafanya yawe matamu na mapya.

Na hivyo hivyo Mwenyezi Mungu akayateremsha maji kutoka mawinguni, na kutokana na maji hayo akaifanya ardhi iliyo kuwa imekufa iwe hai, na akatawanya kwenye ardhi kila aina ya wanyama, na kama angetaka angeyafanya kuwa machu-ngu yenye chumvi kama yalivyo kuwa mwanzo, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu alietukuka. Pamoja na kufahamu ya kuwa chumvi ni lazima katika maji ya bahari kama ambavyo maji matamu ni ya dharura kwetu, na hiyo ni kwa sababu bahari japo kuwa ni yenye kina kirefu sana na ni pana kwa kiwango kikubwa, lakini ni yenye kusimama (kutuwama). Pamoja na hayo bahari inamipaka maalumu na maji yake yametuwama na yenye kusimama, lau kama yasingekuwa ya chumvi yange haribika harufu yake na kuchafuka kutokana na kupita miaka na miaka.

Na maji nayo, baada ya hayo tuliyo yasema na kabla yake, yana sifa nyingine zenye umuhimu mkubwa na ambazo ikiwa mwanadamu ataziangalia zote kwa ujumla ataziona zikimjulisha juu ya uumbaji wa makini na upangiliaji madhubuti. Na maji nayo yamefunika robo tatu ya ardhi, nayo kutokana na hali hiyo yanatoa taathira kubwa sana katika anga lililopo na katika kiwango cha joto.

Na lau kama maji yangekosa baadhi ya sifa zake, kungeone-kana mabadiliko juu ya ardhi katika kiwango cha joto ambacho kingepelekea kutokea kwa mabalaa au maangamizi. Na maji yanacho kiwango cha juu cha kuyayuka, na hubakia yakiwa ni yenye kubadilika na kuwa mvuke kwa muda mrefu, na yanajoto la kiwango kikubwa na cha juu zaidi, na kutokana na hali hiyo, maji husaidia kubakia kwa kiwango cha joto juu ya ardhi kwa kiwango kilicho thabiti na huilinda ardhi kutokana na mabadi-liko makali, na lau yasingekuwepo yote hayo kustahiki kwa ardhi kuwa sehemu ya kuishi kungepungua kwa kiwango kikubwa na starehe na uchangamfu wa mwanadamu juu ya ardhi ungepungua kwa kiwango kikubwa.

Na maji nayo yana sifa nyingine ya aina ya pekee, na yote hayo yanatujulisha ya kwamba Muumbaji wa ulimwengu huu aliuumba na kuunda kwa mpangilio wenye kuwaletea mazuri yenye kuwafaa viumbe wake.

Na maji ndio kitu pekee kinacho julikana kwa kupunguza uzito wake wakati yanapo ganda na kuwa barafu, na sifa hii ina umuhimu mkubwa katika maisha, kwani kutokana na sifa hii barafu huelea juu ya maji wakati wa baridi kali, badala ya kuzama kwenye bahari kubwa na mabwawa na mito, na kwa sura ya taratibu hugeuka  na kuwa ni donge gumu ambalo hakuna uwezekano wa kulitoa na kuliyayusha .

Na ile barafu ieleayo juu ya bahari huwa kama tabaka lililo jitenga lenye kuyahifadhi maji yaliyopo chini yake katika kiwango maalumu cha joto kinacho yazuia kuganda, na kutokana na hali hiyo samaki na viumbe vingine kati ya wanyama wa majini hubakia wakiwa hai, na wakati wa kipupwe kinapofika, barafu ile huyeyuka haraka sana.

Na tunaweza kuziashiria sifa nyingine nyingi za maji tena za ajabu, kwa mfano ni hali ya kutiririka kwake juu ya ardhi ambayo husaidia kukua kwa mimea kutokana na chembechembe za chakula inazo zihamisha kutoka kwenye udongo na kuzipeleka kwenye mimea, na maji ni kitu maarufu sana kati ya vitu vyenye kutiririka, kwani ni yenye kuyeyuka haraka zaidi, na kutokana na hali hiyo maji yana dauru kubwa sana katika kazi ya uhai ndani ya miili yetu yakiwa na sifa ya kuwa ni kitu muhimu na cha msingi katika muundo wa damu, na maji yana msukumo wa mvuke wa hali ya juu sana katika kiwango cha joto, pamoja na hayo maji hubakia ni yenye sifa ya utiririkaji kwa muda wote huu wa uhai.

Na bahari nazo ni miongoni mwa dalili kubwa za Mwenyezi Mungu, na ndani ya bahari kuna aina nyingi za viumbe vilivyo hai zaidi ya vile vilivyopo nchi kavu, na viumbe hivi hutofautiana sana, ukianzia na wanyama wadogo wadogo ambao hupatikana kwenye mita moja ya mraba yenye maelfu ya wanyama hao na kwa kumalizia na samaki wakubwa (nyangumi) waliopewa meno makali na nguvu kupita kiasi, ambazo kwa kuzitumia wanauwezo wa kuyahujumu majahazi na hata kuyaharibu na Mwenyezi Mungu mtukufu amesema kweli pale alipo sema:

) (Surat-Annahl 14 .

Na yeye Mwenyezi Mungu ndie ambae ameitiisha bahari ili humo mule nyama mpya (mzuri) mtoe humo mapambo myavaayo, na utayaona majahazi yakipasuwa humo na ili mtafute fadhila zake na mpate kushukuru.

      Lau tutarudi na kufanya mazingatio kuhusiana na mbingu hii ya bluu iliyotuzunguuka na tukaviangalia vyote vinavyo elea humo kama sayari na nyota na vile vimetavyo juu yake kama nyota, jua na mwezi, lau tutafanya mazingatio na kufikiria kuhusu mambo haya tungeshikwa na bumbuwazi na mwishowe macho yangerudi yakiwa yameshikwa na mshangao  na kuchoka na kwa sababu hii tunaikuta Qurani ikituhimiza kuvizingatia vitu hivi ili tuweze kufikia kwenye faida  ya milele na kubwa, nayo ni kuwa maajabu yote hayo hayawezekani kupatikana kwa ghafla bila kupangiliwa au matarajio yaliyokuwa yakifikiriwa, au kuto-kana na mada isiyo ona.

             .( )              Je hawaangalii ufalme wa mbingu na ardhi na vitu mbalimbali alivyo viumba Mwenyezi Mungu. Suuratul Aaraaf 185.

) (.Suratu-Yunusu

Sema (ewe Mohammad) angalieni maajabu ya vitu vilivyomo mbinguni na ardhini.  

                 .(   )                                                                                                 

Suratul-Qaf: 6.           

   Je hawakuiangalia mbingu  iliyopo juu yao vipi tumeijenga na vipi tulivyo ipamba na kuwa haina nyufa?

                  .Suratur-raad:2. (      )    Mwenyezi Mungu ndie ambae alie iinua mbingu kwa nguzo msizo ziona.

                   Suratu-dhaariyaat :47. (   )          Na mbingu tumeijenga kwa nguvu na uwezo wetu, na sisi ni wenye uwezo wa kuipanua.                                           

                Suratu-fatiri:13    Mwenyezi Mungu ndie alie litiisha jua na mwezi na kila kimoja kinatembea kwa muda maalumu, ulio kadiriwa.

Hakika nyota zote kwa ujumla takribani ni kati ya bilioni mia moja. Na kati ya hizo zipo ambazo kuna uwezekano wa kuziona kwa macho ya kawaida, na kunazingine hazionekani hadi tutumie vifaa maalumu vikuzavyo vitu, na kuna zingine ambazo mtaala-mu mwenye ujuzi huhisi kuwepo kwa nyota hizo lakini hana uwezo wa kuziona, hizi zote zimejaa kwenye sayari isiyo eleweka ambayo iko mbali na hakuna matarajio yoyote ya kusogeleana kati ya sehemu ya mvuto (magnetism) wa nyota fulani na sehemu ya mvuto wa nyota nyingine, isipokuwa kama ambavyo hutarajiwa kugongana merikebu kwenye bahari nyeupe ya kati (mediterranean sea) na kati ya merikebu nyingine kwenye bahari ya pacific, zenye kutembea kuelekea sehemu moja kwa kasi moja.

      Na elimu inasema ya kuwa kasi ya mwanga ni maili  186 elfu kwa sekunde moja, na miongoni mwa nyota kuna zitumazo mwanga wake na kutufikia kwa haraka sana, na kuna zingine hutufikia kwa miezi kadha na kuna zingine mwanga wake hutufikia baada ya miaka kadhaa ya jua, sasa upana wa ulimwengu ni wa kiasi gani na unaukubwa upi?

      Je yote hayo yametokea ghafla bila malengo wala  kupangi-liwa? Na je yote haya hayahitaji muumba? Na je madda isiyoona na kuelewa inaweza kuvifanya vitu vyote hivi viwepo na kujipanga katika nidhamu kama hii iliyo makini?  

  ( )     Suratu Luqman:11.Hivi ni viumbe vya Mwenyezi Mungu basi nionyesheni wale wasiokuwa yeye walicho kiumba. Bali madha-limu wako kwenye upotevu wa wazi kabisa.

    Ardhi imeumbwa na vyote vilivyomo ndani yake vinasema ya kuwa adhi hiyo inawiana na uhai.

     Na ardhi ni yenye kujizunguka na kwa kufanya hivyo kunapatikana kufuatana kwa usiku na mchana. Na inazunguuka pembezoni mwa jua na kutokana na hali hiyo kuna patikana misimu, misimu ambayo mzunguko wake hupelekea kuzidi kwa masaha yanayo faa kuishi ndani yake, na inazidisha kupatikana kwa tofauti ya aina ya mimea.

      Na mzunguko huu unafanywa kwa mahesabu madhubuti hayazidi wala kupungua kwani kuzidi kwake au kupungua kwake kutoka kwenye hali iliyopo kwa hivi sasa kutayafanya maisha au uhai usiwepo tena.

      Na ardhi imezungukwa na utando wa gesi nyingi na za lazima katika maisha, na hujitawanya pembezoni mwake kwa urefu unao zidi maili 500, utando huu uzito wake ni wa kiwango kikubwa kiasi kwamba huzuwia mamilioni ya vimondo vyenye kuuwa kila siku visitufikie, na vyenye mwendo wa haraka sana, takriban maili 30 kwa sekunde moja. Utando huu wa anga ambao umeizu-nguuka ardhi, huhifadhi kiwango cha joto lake kwenye mipaka inayofaa kwa ajili ya maisha, na huchukua mvuke wa maji kutoka kwenye mikondo fulani na kuupeleka sehemu za mbali ndani ya mabara, kiasi kwamba mvuke huo unaweza kujikusanya na kuwa ni mvua iihuishayo ardhi baada ya kufa. Na mvua ni chanzo cha maji matamu na kama si kuwepo kwa mvua ardhi ingekuwa kavu isiyo kuwa na athari yoyote kwa ajili ya uhai wa mimea.

     Na maji yana sifa ya pekee na muhimu sana, hufanya kazi ya kuyalinda maisha kwenye mikondo na maziwa au mabwawa na kwenye mito, na hasa kwenye sehemu ambazo msimu wake wa masika huwa ni wa baridi kali na mrefu.

Maji hufyonza kiwango kikubwa sana cha oxygen wakati kiwango cha joto kinapo kuwa kimepungua. Na barafu iliyo jikusanya kwenye mabwawa na mito huelea juu ya ardhi kutokana na wepesi wake na kwakufanya hivyo huandaa mazingira na nafasi nzuri ya uhai wa viumbe ambavyo huishi kwenye maji kwenye sehemu za baridi -kama tulivyo eleza hapo kabla- na wakati maji yanayo ganda, kiasi kikubwa cha joto hutoweka, kitu ambacho husaidia kuyalinda maisha ya viumbe hai ambavyo huishi kwenye bahari.

     Ama ardhi kavu ni mazingira thabiti kwa ajili ya maisha ya viumbe wengi, mchanga una chembechembe ambazo hufyonzwa na mimea na kuichukua na kuzigeuza kuwa aina tofauti ya chakula ambacho mwanadaamu na wanyama hukihitajia, na juu ya ardhi hupatikana madini mengi, vitu ambavyo vimeandaa mazingira na njia ya kuwepo utamaduni na maendeleo.

      Na lau kama ardhi, kipenyo chake (diameter) kingekuwa ni robo ya kipenyo chake cha hivi sasa, ingeshindikana kuhifadhiwa kwa tando mbili, utando wa anga na wa maji, vitu ambavyo vimeifunika ardhi, na kiwango cha joto ndani ya ardhi kingekuwa kikubwa kiasi cha kuweza kuuwa.

Ama lau kama kipenyo chake kingekuwa ni zaidi ya kipenyo chake cha hivi sasa uso wa ardhi (surface) ungepanuka na mvuto (gravity) wake wa vitu ungekuwa zaidi kuliko ulivyo hivi sasa, na hivyohivyo umbali wa utando wake wa hewa, ungeshuka na msukumo wa anga ungezidi kutoka kilomita moja hadi kilomita mbili kwenye senti mita  mraba na yote hayo yangeathiri kwa kiwango kikubwa sana katika maisha ya ardhini, upana wa sehemu za baridi ungeongezeka kwa kiasi kikubwa, na upana wa ardhi inayofaa kwa maisha ya watu ungepungua vilevile kwa kiasi kikubwa, na kwa hali hiyo watu wangetengana na kuishi sehemu za mbali kiasi kwamba kusinge kuwa na uwezekano wa kuwasiliana kati yao.

Na lau kama unene wa utando wa ardhi ungezidi kwa kiasi cha hatua kadhaa ingefyonzwa hewa ya carbon dioxide na oxygen na mimea haingewezekana kuwepo.

Na lau ardhi ingeondelewa kwenye umbali uliopo hivi sasa kati yake na jua, na kuwekwa chini zaidi, kiwango cha joto inacho kipokea kutoka kwenye jua kingepungua hadi kufikia robo ya kiwango chake  ikipatacho kwa hivi sasa, na mzunguuko wa ardhi pembezoni mwa jua ungekuwa ukichukua muda mrefu sana na kufuatia hali hiyo msimu wa masika ungeongezeka, na viumbe hai  vinge ganda juu ya ardhi.

Na kama umbali uliopo kati ya ardhi na jua ungepungua hadi kufikia nusu ya umbali ulivyo hivi sasa, joto ilipatalo ardhi lingefikia mara nne zaidi ya kiwango cha leo. Na kasi yake ya kulizunguka jua ingeongezeka na isinge wezekana kuishi juu ya ardhi. Na hata kupinda kwa ardhi ambako kuna kadiriwa kuwa kwa kiwango cha pembe 23 (degrees) kumekuwa hivyo kwa sababu maalumu zilizo pelekea kuwe na kupinda kama huko, kwani lau kama ardhi isinge kuwa ni yenye kupinda pande zake mbili za mzunguko zingekuwa katika hali ya giza kwa wakati wote, na mvuke wa maji utokeao kwenye bahari kubwa ungekuwa ukielekea kusini na kaskazini ukikusanya njiani mwake mabara ya barafu.

Na kwa hali hiyo ardhi kwa ukubwa wake na umbali wake na jua na kasi yake ya kuzunguuka imekuwa ikimuandalia mwanadamu sababu za uhai. Je yote haya yamekuwepo kibahati tu bila mpangilio?

Ama udongo hakika ni ulimwengu utowao maajabu mengi, na huenda la ajabu zaidi ni yale mahusiano yenye maingiliano na ambayo ni mengi ambayo haiwezekani yawe yamepatikana bila uumbaji makini na utengenezaji madhubuti. Hebu tuangalie udongo ili tuone vipi hupatikana kutokana na vitendaji kazi (mmomonyoko au soil erosion) ambavyo huidhihirisha ardhi katika asili yake.

Matokeo ya ufanyaji kazi wa mmomonyoko huu yamegawanywa sehemu kadhaa:

Kuna tabaka la nyuma na lililo la chini, na juu yake huwa kuna anga lingine lifuatialo, kisha hufuatia juu yake tabaka la udongo. Na matabaka yote yaliyo tangulia hutokana na kazi ya kutenganisha na kuvunjavunja ambayo husababishwa na utendaji kazi wa ardhi ambao huifanya ardhi ionekane kwenye umbile lake la asili.

Na udongo una umuhimu maalamu kwetu kwani ni chanzo cha chakula kilicho cha msingi ambacho mmea hukipata pale unapo anza kukua, kama ambavyo udongo ni dharura kwa kuuzatiti mmea juu ya ardhi. Na mawe ya moto yanapo pitiwa na kazi ya kupasuliwa au kuvunjwa vunjwa (kumomonyoka) misingi yake kutoweka taratibu, misingi iwezayo kuyayuka kwenye maji kama calcium na magnesium na potasium na hubakia oxidesilicone na aluminium na madini ya chuma yakiwa ndio mengi zaidi kwenye udongo, na kutokana na kazi hii huwa hakipungui kiwango kikubwa cha madini ya phospharus wakati ambapo hufatia kwa kawaida kuongezeka kwa kiwango cha nitrogen.

Na kutokana na kuathirika na vitendakazi vya kuvunja na kuchanganyika kwa aina tofauti za silica (silika) husababisha kupatikana kwa udongo mgumu (clay) na miongoni mwa sifa kubwa za udongo huu mgumu ni kuwa kwake na uwezo wa kubadilisha nguvu ya umeme ya hasi, kwa sifa hii inauwezesha kuhifadhi misingi yenye uwezo wa kuyayuka na ambayo niya lazima katika ukuaji wa mmea.

Ama kuhusu nitrogen, yatosha kufahamu ya kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya msingi vya umeme huu ambao watu wengi hudhania ya kuwa si kitu zaidi ya moja wapo kati ya nyenzo za kuangamiza, lakini utoaji wa nguvu ya umeme kutokana na umeme (radi) hupelekea kupatikana kwa oxide nitrogen ambayo huteremka na mvua au barafu na kuingiza kwenye udongo na mmea kufaidika nayo.

Na kiwango cha nitrogen ambacho udongo hukipata kwa njia hii inayokaribia ratili tano za ekari kwa nutroni (neutron) moja kila mwaka. Nayo inatosha  na ratli thelathini za neutron  sodium, na kiwango hiki kinatosha kuufanya mmea uweze kukua.

Na imegunduliwa ya kuwa kiwango cha nitrogen ambacho huwekwa na umeme, huwa kwenye nchi zilizochini ya jua (tropical lands) zaidi kuliko nchi ambazo hali yake ya hewa huwa ni ya wastani na yenye maji maji. Nazo  nchi hizi kiwango chake kinazidi kiwango ambacho huwa kwenye nchi kavu za jangwani.

Kutokana na hayo tunaona ya kuwa nitrogen hutawanywa kwenye sehemu mbalimbali za kijografia kwa aina tofauti kufata-na na mahitajio ya kila sehemu mbali mbali za kijografia, na kufatana na mahitajio ya kila sehemu ya kiungo hiki muhimu. Sasa ni nani ambae aliyapangilia yote haya?!

Kisha maajabu haya ambayo yamejaa kwenye ulimwengu kama ugawaji tofauti na mzunguko wa maji katika maumbile na mzunguko wa carbondioxide ulimwenguni, na kazi ya ajabu ya uzalishaji, na kazi ya kutengeza mwanga, yenye umuhimu mku-bwa katika kuhifadhi nguvu ya jua na kutokana na umuhimu wake mkubwa katika maisha ya viumbe hai. Na vilevile nidhamu hii iliyopo ulimwenguni, na mahusiano ya sababu na visaba-bishwa na ukamilifu na makubaliano, na usawa, vitu ambavyo hupangika na kuweka nidhamu ya viumbe vingine vyote na kuendelea athari zake kutoka kipindi, hadi zama nyingine. Je maajabu haya yamekuwepo kwa ghafla, kibahati, na bila ya mpangilio?!

Na vilevile chembechembe ndogo zisizopasuka hazina umbile  maalumu na kati yake hakuna nafasi wala faragha.Viumbe ambavyo (chembechembe) vimetoa mamilioni ya sayari na nyota nyingine nyingi zenye maumbile (sura) maalumu na umri maalumu na zenye kufuata kanuni thabiti, je zimepatikana ghafla bila kupangwa?

Na kuna elementi hizi za kemikali zilizo maarufu (chemical elements) ambazo idadi yake imefikia mia na zaidi, je mwana-damu amezifanyia uchunguzi na akafahamu aina ya chembe zenye kufanana na zenye kutofautiana? Kuna zenye rangi na zisizo na rangi, na baadhi yake ni gesi ambayo ni vigumu kuigeuza na kuifanya iwe ni yenye kutiririka kama maji au kuifanya iwe ngumu, na zingine ni zenye kutiririka, nyingine ni nyepesi na nyingine ni nzito, na baadhi ni zenye maungano mazuri  na nyingine ni zenye maungano mabaya na baadhi ni zenye sumaku (magnetic) na nyingine si zenye sumaku, nyingine ni changamfu na nyingine ni laini (dhaifu) na nyingine zinakuwa ni acid na zingine zinakuwa ni misingi, zingine zina umri mrefu, na zingine ni zenye kuishi muda mchache tu pamoja na yote hayo hakika chembe chembe hizo zote zinafanya kazi chini ya kanuni moja, nayo ni kanuni ya mzunguko.

Katika tofauti iliyopo kati ya chembe chembe za elementi fulani na chembe chembe za elementi nyingine, inatokana na tofauti ya idadi ya protons na neutrons ambazo zimo kwenye kiini chake (nucleus), na tofauti inarudi vilevile kwenye idadi na njia zinazopangilia electrons ambazo ziko nje ya kiini chake na kwa msingi huo, mamilioni ya aina za madda tofauti, ziwe ni elementi au msombo (compounds) huundika kutokana na chembe chembe za umeme ambazo hazina maumbile bali ni sura au aina fulani ya nishati (Energy).

Na madda kwa kuwa imeundwa kutokana na mjumuiko wa chembe chembe za  atom zenyewe, na electrons na neutrons ambazo ndizo ziundazo chembechembe za atom na nguvu ya umeme na nishati, madda yenyewe hufanya kazi kwa kufuata kanuni maalum kiasi kwamba inatosha kujua idadi ndogo ya chembe chembe za aina ya elementi, ili kuigundua ile madda na kufahamu sifa zake.

Je vyote hivyo vimetimia kwa ghafla bila upangiliaji? Na je kanuni za ulimwengu zimepatikana kutokana na kugongana kwa madda kusiko na mpangilio? Hakika sisi baada ya kuamini -kwa yakini kabisa- ya kuwa ulimwengu huu na vyote vilivyomo ndani yake vipo kweli kama tuvionavyo mbele yetu, na kuwa kuwepo kwenye wakati maalumu tangu zama zake za kale na kwamba haiwezekani kitu kisicho kuwepo kikawa ni sababu ya kuwepo kwa ulimwengu, bali ni lazima awepo alie ufanya kuwepo aliye uumba baada ya kuwa haukuwepo. Sasa ni nani huyo alie ufanya ulimwengu kuwepo? Ni madda au Mwenyezi Mungu.

Na kwanza kabisa tunauliza: Hiyo madda imepatikana vipi na ni nani alie ifanya iwepo? Na watu wanao amini madda (materialists) wanasema katika kujibu swali hili: Hakika madda ni ya tangu na tangu, ipo tangu zama za kale haihitaji kuumbwa wala muumbaji. Na kupinga uzushi na madai hayo imekuwa ni jambo jepesi kwa kutumia nyenzo ya elimu kwani elimu imethibitisha na imethibiti kwenye elimu kwa uwazi kabisa ya kuwa ulimwengu huu hauwezekani ukawa ni watangu na tangu, kwani kuna uhamaji wa joto wenye kuendelea kwenye vitu vya moto kwenda kwenye vitu vya baridi, na haiwezekani kutokea kinyume cha hivyo kwa nguvu ya kitu chenyewe, kiasi kwamba joto lihame kutoka kwenye vitu vya baridi na kuhamia kwenye vitu vya moto, na maana ya hayo ni kuwa ulimwengu unaelekea kwenye kiwango kinacho lingana joto lake katika viumbe (vitu) vyote, na nguvu (energy) zake zitakwisha, na siku hiyo hapata-kuwa na utendaji kazi wa kikemikali au kimaumbile.

Na hakutabaki athari zozote za uhai katika ulimwengu huu na kutokana na kuwa maisha (uhai) bado yapo na kwa kuzingatia ya kuwa utendaji kazi wa kikemikali na kimaumbile zinaendelea na zinapita kwenye njia zake za kawaida, tuna weza kufaidika ya kuwa ulimwengu huu haiwezekani ukawa ni wa tangu na tangu laa sivyo nguvu zake zinge angamia tangu zamani, na ufanyaji kazi wote kwenye ulimwengu unge simama tangu zamani.

Na katika zama zetu hizi hutumika njia kadha tofauti kukadiria umri wa ardhi kwa vyombo au njia zinazotofautiana katika umakini wake, lakini natija ya njia hizi inakaribiana kwa kiasi kikubwa, nazo zina ashiria ya kuwa ulimwengu ulianza tangu miaka bilioni tano iliyopita, kwa msingi huo ulimwengu huu si watangu, kwani kama ungekuwa ni wa tangu kusingebakia ndani yake chembechembe yoyote ya mnururisho (radiation) na rai hii inakubaliana na kanuni ya pili kati ya kanuni dinamika za kalori (Dynamic law of calorie).

Ama rai isemayo ya kuwa ulimwengu ni wa mzunguko, yaani ulimwengu hujikunja kisha hujitanua kisha hurudi tena kujikunja kwa mara nyingine, ni rai ambayo wataalamu bado hawaja pata dalili ya usahihi wake, na haiwezekani kuchukuliwa kama dalili ya kielimu na kanuni za Dinamika za kalori (joto) na dalili za kinajimu (astronomy) na za kijiolojia (geology) zinaunga mkono neno lisemalo: Hakika Mwenyezi Mungu mwanzo aliumba mbingu na ardhi.

Hakika jua liwakalo na nyota zenye kumetameta na ardhi iliyo jawa na aina tofauti ya viumbe hai ni dalili ya wazi ya kujulisha kuwa asili ya ulimwengu au msingi wa ulimwengu una mahusiano na zama zilizo anza kwenye sekunde maalumu. Kwa hivyo basi kutokea kwa ulimwengu ni tukio miongoni mwa matukio.

Na elimu ya kemia inatujulisha ya kuwa baadhi ya vitu vilivyopo, vina muelekeo wa kutoweka au kuisha kwa haraka sana vingine kwa kasi ndogo na kwa msingi huo madda si ya kubakia milele na ina maana ya kuwa, madda si ya tangu na tangu, kwa maana ya kwamba ina mwanzo. Na ushahidi wa kikemia na elimu zingine unaonyesha kuwa mwanzo wa madda haukuwa wa polepole wala wa taratibu, bali ilipatikana kwa njiya ya ghafla, na elimu zinaweza kutueleza muda ambao madda hiyo ilipoanza. Kwa msingi huo katika ulimwengu huu wa madda, yaani wenye maumbile yenye kuonekana, ni lazima uwe umeumbwa, nao tangu ulipo umbwa unafanya kazi kwa kufuata kanuni hizo hakuna nafasi ya kutokea kitu au kuumbwa kitu kwa njia ya ghafla bila kupangiliwa.

Na tangu miaka mia moja iliyopita mtaalamu wa urusi aitwae Mandaliof alizipanga elementi za kemikali kufuatana na kuzidi kwa uzani atomu (atomic weight) katika mpango wa mzunguko. Na akagundua ya kuwa elementi ambazo hujikusanya sehemu moja huunda kiumbe kimoja chenye sifa zenye kufanana. Basi je haya yote twaweza kusema ya kuwa yametokea ghafla bila kupangwa (By chance)?

Hakika ugunduzi wa Mandaliof hauitwi kwa jina la ughafla wa mzunguko (revolution by chance) lakini huitwa kanuni ya mzunguko (law of revolution). Na je yawezekana tukaitafsiri ile hali waliyo isifu wataalamu na waliyo igundua ya utendanaji (reaction) wa elementi A pamoja na elementi B na kutotengana kwake A na elementi C ya kuwa kumetokea kwa msingi wa ghafla bila kupangwa?

Haiwezekani kamwe. Hakika wao waliitafsiri hali hii kwa msingi wa kuwa kuna aina fulani ya muelekeo na mvuto kati ya chembe za elementi A na za B, lakini muelekeo huu na mvuto huu haupatikani kati ya chembe za elementi A na chembe za elementi C. Na wataalamu wameweza kufahamu vile vile ya kuwa kasi ya utendaji kati ya chembe za madini ya chumvi na maji kwa mfano, huzidi kila inavyo zidi uzani atomu wakati ambapo elementi za halojen (halogen) hufuata mfumo unao pingana na mfumo wa kwanza kiukamilifu na hakuna yeyote anae fahamu sababu ya tofauti hiyo.

Pamoja na hayo hakuna yeyote alie sema ya kuwa imetokea hivyo kwa ghafla, au kudhania ya kuwa huenda mfumo huu ukawa sawa baada ya mwezi au miezi miwili au ukawa sawa kufuatia kutofautiana muda na sehemu au kumjia kwenye fikra zake za kuwa atom hizi huenda hazitendani (react) kwa njia ileile au kwa njia ya kinyume au kwa njia isiyo pangiliwa.

Na ugunduzi wa mpangilio wa chembe za atomu umethibiti-sha ya kuwa utendaji wa kemikali tuuonao na sifa zake tuzionazo zinarejea kwenye msingi wa kuwepo kanuni maalumu, na sio kuwa mpangilio huo umetokea ghafla na umesababishwa na kitu kisicho ona wala kuelewa.

Ili tuchukue fikra ya wazi kuhusiana na udogo wa atomu ni lazima tuone au tufikirie ya kuwa lau kama zitapangwa chembe milioni kumi kati ya chembe za hydrogen kwenye mstari mmoja usingefikia urefu wake milimeter moja.

Na wakati ukiwa na kiu na ukanywa lita moja ya maji, kwa hakika maji yale uyanywayo yamekusanya idadi kadhaa ya chembechembe za atom zinazo lingana na punje ya mchanga ufunikao ardhi yote pamoja na bahari zake. Na pamoja na udogo huu hakika atom ni ulimwengu wenye kujitosheleza, imeundika kutokana na vijiwe vilivyo vidogo sana, yaani vijiwe vilivyo vidogo kuliko hata hiyo atomu yenyewe.

Hakika atomu imeundwa kutokana na kiini (nucleus), imejengwa kutokana na vijiwe vidogo sana baadhi yake ni proton (protons) na nyingine ni nutroni (neutrons) nazo electroni (electrons) huzunguka pembezoni mwake kwa masafa ya mbali kiasi.

Na ndani ya jengo hili lililo makini na zuri wataalamu wamegundua viumbe vingine vidogo vidogo ambavyo hadi sasa idadi yake imefika aina thelathini, na miongoni mwazo ndizo tulizotaja, yaani protoni na nutroni na pia elektroni.

Na wataalamu wemeukadiria mzunguko wa elektroni pembezoni mwa kiini chake kuwa mara milioni elfu saba kwa sekunde moja. Na kati ya baadhi ya chembechembe za atom, kuna hali ya mapenzi na kuelewana na mvuto na mahusiano, na kati ya chembe chembe zingine kuna hali ya kuchukiana na kutowiana, na kitu kinacho zikusanya kati ya chembe chembe za atomu au kuzitenganisha ni kanuni ya atomu yenyewe au kanuni ya electroni za nje, na ni nzuri zaidi na makini zaidi kuliko kanuni ya ndoa na talaka iliyopo kati ya wanaadamu.

Hakika chumvi ya chakula tuilayo, asili yake ni chembe-chembe mbili zilizo jikusanya, na kama zisingejikusanya katika sehemu moja kila chembe ingekuwa ni mbaya na yenye kuuwa na zenye kuviharibu viumbe hai, kwa mfano kroridi (chloride) ni gesi ambayo mwanadamu akiivuta au kiumbe hai chochote kita kufa. Nayo sodium ni elementi laini lau itaguswa na maji itatoa moshi mkubwa na moto mkubwa na ingeweza kuviunguza viumbe hai ambavyo hubebwa  ndani yake.

Lakini kukutana kwa chembe chembe za sumu na chembe chembe zenye kuunguza na kukusanyika kwazo kumezigeuza chembechembe hizi kuwa chumvi isiyo unguza wala kuifanya kuwa sumu. Na hivyo ndivyo ilivyo kwenye chembe chembe tatu za maji zilizo ungana. Na ikiwa sheria ya kiislamu imemruhusu mwanamume kuoa mke mmoja, wawili, watatu au wanne, basi hivyo hivyo hali hiyo iko kwenye kanuni ya mahusiano ya chembe chembe za atom.

Kwa mfano chloride huungana na sodium katika kisehemu fulani ili kutupatia chumvi ya chakula na huoni muungano wa chembe chembe moja nayo ni oxygen huungana na chembe mbili za hydrogeni ili ziweze kutupatia maji. Nayo nitrogen huungana na chembe chembe tatu za hydrogen ili kutupatia amonia (ammonia).

Na carbon huungana na chembe chembe nne za hydrogen ili kutoa gesi ya methani (methan gas). Na hapa kuna baadhi ya elementi ambazo chembe chembe zake huishi peke yake bila ya mwenza kwa wakati wote, na miongoni mwa chembe chembe hizo ni gesi ya neon na raon.

Na tukihama, hali ya kuwa tunazungumzia mahusiano ya chembe chembe za atom kutokana na ulimwengu wa atom na kwenda kwenye ulimwengu wa chembe chembe zingine kwani kukadiriwa idadi ya aina za chembe chembe zipatikanazo kutokana na maungano kati ya chembe za elementi zilizomo kwenye ardhi yetu, ni jambo lisilowezekana kufahamika kwa mtu.Yatosha kuthibitisha hilo kwa kuchukua kamusi ya lugha ili tuweze kuona idadi ya maneno ambayo yanatokana na herufi ishirini na nane ambazo ndizo zinazo unda lugha ya kiarabu, na kisha tuweze kufahamu ni kiasi gani cha chembe chembe elementi karibu miamoja zinaweza kuzitoa. Kiukweli kabisa ni idadi kubwa sana, ni mamilioni na mamilioni ya chembe chembe hizo.

 Mfano juu ya hayo tuliyo yasema ni kuwa muungano wa chembe chembe za carbon na oxygen na hydrogen tu, hututolea zaidi ya miundo milioni moja ya kemikali, kila moja ina nidhamu yake maalumu katika kuzipanga chembe chembe zake.

Na badhi ya wataalamu wanakadiria ya kuwa aina ya protini (proteins) zilizomo kwenye mwili wa mwanadamu na za aina tofauti hizo peke ni zaidi ya aina laki moja na zaidi, ikiwa si milioni moja. Na protini hapo haitengenezwi isipokuwa na carbon na hydrogen na oxygen na nitrogen na huenda ikiwa na phosphorus au sulphur, na huenda isiwe nayo.

Na hivyo inaonekana wazi kwetu chembe chembe za uhai na hivyohivyo huzunguka na kutembea na kuungana na kutengana. Na mzunguko pia muungano na utengano vyote hivyo hufanyika kwa mahesabu yenye kujulikana na hatua zilizo pangwa, katika mwendo huo hakuna fujo bali ni mwendo unao fuata kanuni, bali kila hali inafuata kanuni na nidhamu inayo hukumu sehemu hiyo.

Je mtu mwenye akili na mwenye kufikiria anaweza kuitakidi ya kuwa mada isiyo na akili na hekima imejiumba kwa ghafla bila kupangwa?Au madda hiyo ndio ilio weka nidhamu hii na kanuni hizo kisha ikazifanya zifanye kazi ndani yake (madda)? Hapana shaka ya kuwa jawabu litakuwa ni la kukataa, bali ni kuwa madda inapo geuka na kuwa nguvu au nguvu kugeuka na kuwa madda, hakika yote hayo yanafanyika kufuatia kanuni maalumu, na madda nayo iliyotengenezwa hufanya kazi kufuatia kanuni ambazo zinafuatwa na madda  maarufu iliyokuwa imetengenezwa kabla ya kupatikana hii madda.

Na ikiwa ulimwengu huu wa madda umeshindwa kujiumba au kujiwekea kanuni ambazo hufanya kazi chini yake, ni lazima uumbaji wa ulimwengu uwe umefanywa kwa uwezo wa huyo aliepo ambae si madda.

Na utafiti wa joto umeunga mkono rai hizi na umetusaidia kupambanua kati ya nguvu nyepesi na nguvu zisizo nyepesi na imegundulika ya kuwa wakati yanapo tokea mabadiliko ya joto, sehemu fulani ya nguvu nyepesi hugeuka na kuwa nguvu isiyo nyepesi, na kuwa hakuna uwezekano wa mabadiliko haya yakaenda kwenye maumbile kwa njia ya kinyume, na hii ndio kanuni ya pili kati ya kanuni za dinamic za joto.

Na kutokana na kuwa madda imetokea na si ya tangu kama tulivyo sema ni lazima iwe na alie ifanya iwepo, kwa sababu kitu chochote hakiwezekani kuwepo bila muwekaji au hakiwezi kujiweka, bali jambo hilo ni muhali kiakili.

Kwa hivyo hakika Mwenyezi Mungu ndie muumbaji wa madda na ndie aliefanya iwepo bila ya shaka yoyote. Lau tukisimama kidogo na kukifikiria kitu kiitwacho maendeleo au ukuaji wa madda, na tukafikiria juu ya uwezekano wa maendeleo haya au kukua huku kwa njia ya ghafla (Kibahati), tutakuta ya kuwa ghafla, kama sababu ya kuumba na kuvifanya viumbe hai viwepo na vitu vingine, kamwe haiwezekani akili ikakubali kitu hiki au kujengea juu ya kitu hiki ya kuwa ndio sababu ya kupatikana viumbe.

Mtaalamu wa maumbile Dr Von Plotshe anasema:

Siwezi kufikiriia ya kuwa bahati peke yake inaweza ikatutafsiria kudhihiri kwa electrons na protons za mwanzo au atoms za mwanzo au asidi amino (amino acid) ya mwanzo au protoplasm za mwanzo au mbegu ya mwanzo au akili ya mwanzo yaani kiumbe cha mwanzo.

Hakika mimi nina itikadi katika kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa kuwepo kwake kuliko takasika ndio tafsiri ya kimantiki na ya pekee kwa kila kinacho tuzunguka miongoni mwa maumbile ya ulimwengu huu. Na utafiti wa kinadharia kuhusu ghafla na matarajio uliofanyika hapo kabla katika njia ya mahesabu, una maendeleo kwa kiasi kikubwa hadi kufikia kuwa na uwezo wa kutabiri kutokea baadhi ya matukio ambayo tunadai ya kuwa hutokea kwa  ghafla, na matukio ambayo hatuwezi kuyatafsiri yalivyo kwa njia nyingine, na kwa fadhila ya utafiti huo tumekuwa na uwezo wa kupambanua kati ya vitu vinavyoweza kutokea kwa njia ya ghafla  na visivyo wezekana kutokea kwa njia hii. Hebu na tuangalie kwa hivi sasa ghafla (accident) inaweza kuchukua nafasi gani katika kusababisha uhai wa viumbe?

Protini ni miongoni mwa misombo (compounds) muhimu katika seli zilizo hai. Nazo zinaundwa kutokana na elementi tano, nazo ni carbon, hydrogen, nitrogen, oxygen na sulfur. Na idadi ya chembe chembe za atom zinazo unda protini moja ni  atomu elfu arobaini (40 elfu). Na kutokana na kuwa idadi ya elementi za kemikali katika maumbile imevuka mia moja, nazo zikiwa zimegawanywa hovyo bila mpango basi matarajio ya kukusanyika elementi hizi tano ili kuunda chembe chembe moja kati ya chembe chembe za protini yanawezekana kwa kufanyia hesabu ili kufahamu kiwango cha madda ambayo inapaswa kuchanganywa kwa muda wote, ili kuunda chembe chembe hii.

Kisha ili kuelewa kiasi cha muda ambao hutumika hadi kutokea mkusanyiko wa viungo vya chembe moja, mtaalamu mmoja wa mahesabu aitwae Charles Yuujin wa Uswizi, alifanya mahesabu ya vitendakazi hivi vyote akagundua ya kuwa fursa haijileti kwa njia ya ghafla (kibahati) ili kuunda chembe chembe ya protini moja isipokuwa kwa kadiri (asilimia) moja katika kumi (1/10) ikigawanywa yenyewe mara 160, na hiyo ni namba ambayo haiwezekani kutajwa au kuielezea kwa maneno. Na inapaswa kiwango cha madda ambacho hupelekea kutokea ushirikiano huo kwa njia ya ghafla kiasi kwamba huzalisha chembe moja kiwe zaidi ya upana wa ulimwengu huu kwa mara mamilioni  kadhaa na inabidi kuundwa kwa chembe chembe hii juu ya ardhi pekee yake kwa njia ya ghafla kwa ma bilioni ya miaka yasiyo hesabika, aliyo kadiria mtaalamu huyu wa Uswizi (tulie mtaja hapo kabla) kuwa ni namba kumi kuipiga kwa kumi mara 243 katika miaka (yaani 10x10x10x10).

    Na kama tutaacha kuzizungumzia chembe chembe zote hizo na tukaizungumzia chembe chembe iitwayo hymoglobin ambayo hutia rangi nyekundu kwenye damu na ni chembe chembe ambayo wataalamu wanasema ya kuwa ni katika aina ya protini zenye  mpangilio mwepesi zaidi, tutaikuta imekusanya chembe chembe zaidi ya 600 za carbon zilizo ungana kwa chembe zaidi ya miamoja za hydrogen na chembe chembe zingine za nitrogen zaidi ya miambili na zingine kama hizohizo za oxygen. Na mwili wa binadamu umekusanya trilioni 25 za chembe chembe za damu, yaani ukiweka namba 25 na ukaongeza sifuri kumi na nane.

Na mtaalamu wa kemikali aitwae Dr Poeler amesema: Mwanadamu anapo ifanyisha kazi kanuni ya ghafla ili kutaka kuelewa kiwango cha matarajio ya kutokea kwa hali fulani kati ya hali za kimaumbile kwa mfano kuundika kwa chembe moja kati ya chembe chembe za protini kutokana na chembe ziundazo protini, tutakuta kuwa umri wa ardhi unao kadiriwa kuwa ni karibu miaka bilioni tatu au zaidi ya muda huu, hauzingatiwi kuwa ni muda utoshao wa kutoa maumbile haya na kutengeneza chembe chembe hizi kwa njia ya ghafla (kibahati).

Pamoja na yote hayo protini si kitu kingine bali ni chembe chembe za kemikali zisizo na uhai, na haziingiliwi na uhai isipokuwa pale zinapo ingiliwa na ile siri ya ajabu ambayo hatufahamu uhakika wake. Hakika chembe za msingi ambazo huingia na kujenga chembe chembe zingine za viungo ni hydrogen na oxygen na carbon pamoja na kiasi kidogo cha nitrogen pamoja na chembe nyingine. Na ni lazima zikusanyike mamilioni ya chembe chembe hizi ili ziweze kuunda kiumbe kidogo kilicho hai.

Na tukiziangalia aina nyingine ambazo ni zenye umbile kubwa na yenye kutatanisha zaidi, matarajio ya kuundika kwa chembe chembe zake kwa msingi wa ghafla hupungua hadi kufikia kiwango ambacho akili haikifikirii  bali haikubali kuwepo kwa ghafla wala tafsiri ya kuwepo vitu kupitia njia hiyo.

Ili kufafanua hayo anasema professor Chrissy Morrison raisi wa chuo cha elimu za sayansi huko New York, ya kuwa:Tujaalie ya kuwa una mfuko wenye vipande mia moja vya mawe, vipande tisini na tisa ni vyeusi na kimoja ni cheupe, sasa tikisa mfuko na uchukue kipande kimoja, hakika bahati ya kuchukuwa kipande kimoja cheupe ni asilimia moja kwa mia. Na hivi sasa kirushe kipande hicho kwenye mfuko na uanze tena kama ulivyofanya mwanzo, hakika bahati ya kuchukua kipande cheupe bado ni asili mia moja kwa mia, isopokuwa ni kwamba kukivuta kipande cheupe kwa mara mbili mfululizo ni sawa na asilimia moja kwa elfu kumi. Hebu jaribu kwa mara ya tatu, hakika muda wa kuvuta kipande hicho cheupe kwa mara tatu mfululizo ni asilimia mara mia moja katika elfu kumi, yaani asilimia moja katika milioni moja. Kisha jaribu kwa mara nyingine au mara mbili namba zitakuwa za kisayari.

Hakika makusudio yangu katika kuichambua accident (ghafla) ni kumbainishia msomaji kwa njia ya kielimu iliyo wazi hiyo mipaka iliyofinyu ambayo kupitia mipaka hiyo maisha yanawezekana kupatikana juu ya ardhi. Na ninakusudia kuthibitisha dalili za kweli ya kuwa vitu vyote vinavyo sababisha maisha ya kweli kupatikana ni vitu ambavyo vinawezekana kupatikana kwenye sayari moja kwa wakati mmoja kwa ghafla.

Hakika tukiangalia kwa mazingatio kwenye ulimwengu wa madda kuanzia chembe chembe za atom zilizo ndogo kupita kiasi hadi kufikia kwenye sayari zilizo kubwa kabisa, tutakuta kwamba kila kitu hufuata kanuni ya hesabu maalumu na zilizo dhibitiwa.

Hata electrons hazihami kutoka sehemu moja ya kuzungukia (orbit) na kuhamia sehemu nyingine kwenye mzunguko (orbit) wa kiini (nucleus) isipokuwa itakapo toa au kuchukua nguvu fulani, nguvu inayolingana na kiasi cha uhamaji wake kana kwamba ni msafiri asiye weza kusafiri au asiyeweza kuthibitisha safari yake isipokuwa baada ya kulipa thamani ya tiketi.

Na kuzaliwa kwa nyota na kufa kwake kuna kanuni na sababu maalum. Na mwendo wa sayari kwenye mzunguko wa mvuto (gravity) wake, una kiwango maalumu. Na kugeuka kwa madda kuwa nguvu na kugeuka umbile la jua kuwa mwanga kuna kiwango maalum. Na kuhama kwa mwanga kuna kasi maalumu na mawimbi yote ya sauti yana urefu na harakati na yana kasi maalumu. Kama ambavyo kila aina ya madini yana spektra (spectrum), nuru iliyogeuzwa kwa koo kuwa rangi mbali mbali, na yana misitari ya mfyonyaji wa nuru (lines of absorption) iliyo tofauti ambayo hutambuliwa kwenye chombo cha uchambuzi na ugunduzi wa madini (Spectrograph).

Na kila madini hulainika na kunyooka kwa kiwango maalumu na hujikunja kwa kiwango maalumu kwa joto na kwa baridi. Na kila aina ya madini yana unene na uzito atomu na sifa maalumu. Bwana Anestine ametuthibitishia ya kuwa kuna mahusiano kati ya uzito wa mwili (mass of the body) na kasi yake, na kati ya wakati na nidhamu ya harakati ndani ya mkusanyiko wa vyenye harakati, na kati ya muda na sehemu. Kama ambavyo umeme huzalishwa kwa kanuni maalumu.

Na mitetemeko ya ardhi ambayo huonekana kuwa ni aina fulani ya tukio lisilo pangiliwa, ni nidhamu nyingine na kanuni na mpangilio ambao tetemeko hutokea kwa nidhamu hiyo kwa hivyo basi ulimwengu wote unakuwa kama ratiba ya kanuni madhubuti  zilizo pangwa kwa makini, na zilizo wazi, zisizo na udanganyifu wala hadaa.

Hakika ukubwa wa ardhi na umbali kati yake na jua, na kiwango cha joto la jua na mionzi yake ipelekeayo kuishi kwa viumbe, na urefu wa funiko (anga) la ardhi na kiasi cha maji, na kiwango cha nitrogen, na kudhihiri kwa binadamu na kubakia akiwa hai, vyote hivyo vinatujulisha kuwepo kwa nidhamu na kuwa vitu vyote viko kwenye mpango maalumu na makusudio maalumu na kuepukana na kutokuwa na mpangilio na fujo kama ambavyo vinatujulisha kufuatana na kanuni ya kimahesabu isiyo tetereka ya kuwa hapakuwa na uwezekano wa kutokea yote hayo kwa ghafla kwa wakati mmoja kwenye sayari moja mara moja katika mara bilioni moja.

Na wale wasemao ya kuwa vitu vimetokea  kutokana na madda (materialist) wamepiga mfano juu ya madai yao na wakasema:Lau kama litachukuliwa sanduku la herufi za alifabeti kisha zikakusanywa na kupangwa kwa mara moja na zaidi na mara maelfu kadhaa na kwa mamilioni kadhaa kwa muda mrefu sana kwa miaka wala karne bali muda usio kuwa na mwisho, hakuna kizuizi kuwa huo ukusanyaji au upangiliaji huo wa herufi kwa mara kadhaa ukatoa kasida ya mashairi yaliyo pangwa katika nidhamu maalumu, na hakuna aliefanya kazi ya kuzipanga herufi hizi na kukubaliana herufi zake zikawa kwenye sura hii isipo kuwa ni ghafla moja inayo tokea katika mamilioni ya mamilioni ya ghafla (bahati). Na hali ndivyo ilivyo kwenye huu ulimwengu wa madda katika mitikisiko yake ya aina tofauti inayotokea kwenye ghafla zote zinazo wezekana kwenye akili, hakuna kizuwizi kwenye akili kutokana na madai yao ya accident (ghafla) ikatoa nidhamu kama hii na kuweza kuunda ulimwengu kama huu wenye viumbe visivyo na uhai na vyenye uhai.

Na kwa ajili ya kuichambua kauli yao hii turudi kwenye mfano walio utoa tutapata mambo yafuatayo:

1: Kupatikana kwa herufi zinazo wiana kiasi kwamba zinaweza kuunda shairi, kiasi kwamba haipungui hata herufi moja au kuzidi.

2: Kuwepo kwa nguvu fulani ifanyayo kazi ya kuzipanga na kuzijumuisha.

3: Kuendelea kwa nguvu ile katika kuzikusanya bila kusima-ma katikati.

4: Kuwepo kwa ufahamu kamili kwenye nguvu hiyo ambayo husimamisha kazi na kuzipanga herufi baada ya kumaliza na kuwa ni kasida ya mashahiri.

Na kila moja kati ya mambo haya manne hakuna mazungu-mzo, bali kuna dalili ya ubatili wa madai hayo.

Ama kuhusu jambo la kwanza tujiulize, ni vipi zimepatikana herufi tulizo ziashiria ili kufanya kazi ya kuzikusanya? Na vipi madda ilijigawa kwenye sehemu za aina tofauti ambapo kukusanyika kwake kumetoa natija kama hii? Kisha vipi aina hizi tofauti zilikuwa na uwezo wa kuungana na kuwa katika mfumo wenye kueleweka?

Ama jambo la pili vilevile tujiulize:

Kwa kutegemea msingi huu wa kuwepo kwa nguvu inayo simamia kazi ya kuzikusanya herufi na kuzipangilia, je inakuba-lika kiakili ya kuwa nguvu hii ifanyayo kazi hii chanzo chake ni herufi zenyewe kiasi kwamba zilikusanyika na kujipanga?

Ama jambo la tatu vile vile tujiulize kwa kutegemea msingi huu wa kuwepo kwa nguvu katika herufi, vipi nguvu hii inaweza kuendelea na kazi ya kukusanya herufi hizo kwa muda wote na isiweze kusimama katikati ya kazi hiyo? Na je inaufahamu utakiwao ambao huifanya au huipa msukumo wa kuendelea na kazi kwa kuhisi umuhimu wake?

Ama jambo la nne ni lazima tujiulize vilevile vipi tunajaalia ya kwamba kufikia hali ya kukusanya na kuzipanga herufi hadi kuwa kasida, inailazimu kusimama  mwisho wa kasida hiyo? Na ni kwanini nguvu hiyo isiendelee na kazi ya kukusanya na kuzipanga baada ya kufikia  mwisho wa kasida ya mashairi ili iingiwe na kasoro au kutoweka nidhamu kabla haijapangika kasida mara ya pili na ya tatu na ya nne? Na ni nguvu ipi iliyo zizuia harakati hizi kwenye kiwango hiki zisiendele kukusanya?

( ǡ )            Suratul-faatir : 41.  

Hakika Mwenyezi Mungu huizuia mbingu na ardhi zisiondoke, na ikiwa zitaondoka hakuna awezae kuzizuwia isipokuwa yeye.

Hakika mazungumzo haya yanatufahamisha kwa wazi kabisa kwamba jambo lililo jaaliwa kuwa ndio msingi wa shubha hii si la kimantiki wala akili haikubaliani na usahihi wake, na kwamba yote hayo waliyo yachukulia kama misingi ya kutegemewa mwishowe kwenye nukta moja na kuonyesha ulazima wa kuwepo nguvu ya milele yenye akili ndio ambayo iliufanya ulimwengu uwepo na iliyofanya nguvu ziwepo zenye kuyaendesha na kupa-ngilia kazi zake bila ya kuwepo fujo au kuyumba au ghafla.

Na kwa ajili ya kuweka wazi ubatili wa accident (ghafla) tunasema:Hakika kudhihiri kwa uhai kwenye madda iliyo kiziwi, kunailazimu akili kushika moja kati ya mambo mawili na hakuna la  tatu yake.

1: Ima uhai uwe ni kitu kimoja wapo kati ya vitu maalumu vya madda usio jitenga na madda na wala haihitaji muumba mwenye utashi.

2: Au madda ni miongoni mwa viumbe vya Muumba mwenye kupanga  na mwenye utashi.

Tukisema ya kuwa uhai ni katika vitu maalumu vya madda itatulazimu kusema ya kuwa madda ni ya tangu na ni ya milele isiyo na mwanzo wala mwisho, na kwamba ilikuwepo tangu na tangu ikiwa na sifa zake zote, na kwamba sifa zake ni lazima ziwe nayo hazitengani nayo kamwe, sawa iwe sehemu hii katika ulimwengu au sehemu nyingine.

Kwa hivyo basi, hakuna maana ya kudhihiri uhai kwenye sayari fulani na usidhihiri uhai kwenye sayari fulani au kwenye muda fulani na usidhiri kwenye muda mwingine. Na hakuna maana ya kubakia sifa za uhai zote bila ya kufanya kazi wala athari, kwa mamilioni na mamilioni ya miaka, kisha baada ya hapo ukadhihiri kwenye muda unaodhaniwa kuwa ni maelfu au malaki ya miaka. Ni kwanini ulichelewa kudhihiri huo uhai kwa muda wote huo, muda ambao haiwezekani kuuhesabu wala kuuwekea mipaka pamoja na kuwa sifa zake zilikuwepo tangu na tangu??

Na ikiwa uhai ni wa tangu, kwanini miongoni mwa sifa za madda ambayo ni ya tangu na tangu -kufuatana na misingi waliyo ijaalia- sasa kwa nini ikaja ghafla kisha ikabakia milele? Na ilikuwa wapi hiyo madda katika zama hizo za mbali hadi ikadhihiri ghafla bila kuwa na malengo wala utashi?

Na kwa kuyazingatia haya ni lazima tuishie kukubali jambo la pili, nalo ni kuwa kudhihiri uhai kwenye madda iliyo kiziwi ilitokana na uumbaji wa muumba wa tangu na tangu mwenye utashi mwenye kufahamu alitakalo, na akauchagulia muda autakao na sehemu aitakayo, akauumba ulimwengu huu na vyote vilivyomo katika muda alio uchagua na sehemu iliyo chaguliwa na kuteuliwa kutokana na hekima zake.

Katika maudhui yetu hayo kumebakia suali moja ambalo ni lazima kulitoa kabla hatuja malizia mazungumzo yetu, nalo ni kuwa maisha au uhai ulianza vipi juu ya ardhi? Je yawezekana ikawa chanzo chake ni jua?

Na ili kulijibu  suali hili ni lazima kwanza tujiulize. Uhai ni nini? Je ni kitu chenye ukubwa au umbile na kipimo au uzito maalumu? Au ni mchanganyiko kati ya hiki na kile?

Uhai ni athari inayodhihiri kwenye seli zilizo hai ambazo ni chembe chembe ndogo ambazo hazionekani isipokuwa kwa kutumia vyombo vya kukuza vitu. Basi chembe chembe hiyo hufanya kazi na kuchukua angani chembe chembe za carbon dioxide wakati linapo kuwepo jua, na huchukua chembe chembe za hydrogen kwenye maji na kwa kufanya hivyo ndiyo hutengeza msombo (mchanganyiko) wa kemikali ambao ndio chakula cha seli, ambacho huifanya ikue na kujigawa.

Na wataalamu wamejaribu kwa mara kadhaa kuunda chembe chembe za protoplasm zilizo hai kwa kutumia nyenzo tofauti na katika sehemu na hali tofauti, wakashindwa na kuzidisha imani juu ya kuwepo kwa muumba wa seli hizi za uhai, na wakakiri ya kuwa viumbe hawa hawana uwezo wa kujiumba.

Seli hii ya uhai ambayo ndio msingi wa uhai, huongezeka au kuzaliana na kusababisha kupatikana viumbe vingine vingi, sasa chembe chembe ya kwanza ya uhai iliumbwa au ilipatikana kutokana na ghafla (accident)?

Ziliwekwa nadharia nyingi sana ili kutafsiri jinsi uhai ulivyo anza kwenye ulimwengu wa viumbe visivyo na uhai, baadhi ya waandishi wakasema ya kuwa uhai umetokana na progyn au kutokana na virus au kutokana na kukusanyika chembe chembe za protein kubwa. Na huenda baadhi ya watu wakadhania ya kuwa nadharia hizi zimeziba ufa ambao hutenganisha kati ya ulimwengu wa viumbe hai na ulimwengu wa viumbe visivyo hai.

Lakini ukweli ambao yapaswa tuukubali ni kuwa juhudi zote zilizo tolewa au zilizo fanywa ili kufikia kwenye madda iliyo hai kutoka kwenye ile isiyo hai, zimeshindwa kwa kiwango kikubwa na pamoja na hayo mwenye kukataa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu hawezi kutoa dalili moja kwa moja  kwa mwanazuoni mwenye kufahamu mambo ya kuwa kukusanyika kwa baadhi ya atomu  na baadhi ya chembe chembe kwa njia ya ghafla kuna-weza kukapelekea kudhihiri kwa uhai na kuuhifadhi na kuuelekeza kwa sura au picha tulio iona kwenye seli za uhai, kwani kila seli moja kati ya seli za uhai ni ngumu sana kiasi kwamba ni vigumu kwetu kuifahamu, na kwa hakika mamilioni ya seli za uhai zilizopo juu ya ardhi zinaleta ushahidi wa kuwepo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, ushahidi ambao umesimama juu ya msingi wa fikra mantiki na uwazi wa kiakili.

Hakika tafsiri ya kielimu ya uhai ya kuwa ni ufanyakazi wa kemikali ni tafsiri isiyotosheleza, kwani kiwiliwili kilicho kufa kinazo chembe chembe hizo hizo za kemikali ambazo zimo kwenye kiwiliwili kilicho hai, na mchanga nao una kiwango hicho hicho cha chembe chembe za irons na shaba (copper) na carbon.

Na kauli isemayo kwamba mapenzi ya kijinsia hupewa msukumo na homoni ya testosteroni (testosterone hormone) haitupi tafsiri ya mapenzi ya kijinsia kwani sisi tutasema:Ni kitu gani kilicho tengeneza hizo testeroni kwenye kiwiliwili?

Kwa mfano mtaalamu wa mimea alipo sema ya kwamba harakati ya mmea uitwao mmea wa Alizeti (Sunflower) kulielekea jua hupangwa na homoni oksini (Oxine hormone), hatutaweza kukubali ya kuwa tatizo limetatuliwa, bali tutauliza:Ni yupi au ni nguvu ipi iliyo tengeneza chembe chembe hizi zitoazo msukumo na ambazo hudhibiti kiwango chake katika mfumo wa mmea?

Muundo wa kemikali wa seli  za uhai hautuonyeshi kwa uwazi siri ya uhai wake, kwa sababu uhai sio kitu kilicho pangiliwa tu na chenye umbo kama nyumba au kiwanda, bali ni kitu kilicho pangiliwa na kilicho hai, ndani yake kuna uwezo wa kujirudi chenyewe (kuzaana), na kuna maumbile ya muongozo yanayo uongoza ndani kwa ndani nayo ni maumbile yaliyo wekwa kwenye mfumo wake, huzitengeneza kuwa mpya zilizo haribika na hutoa zingine badala ya zile zilizopotea.

Na hivi ndivyo lilivyo fumbo linalotakiwa kutatuliwa, lililo-fichika kwenye uchuguzi huu mfupi kuhusu kuongezeka (kuzaana) kwa madda, na sio katika kuundika kwa madda yenyewe, yaani imejengeka kutokana na nini.

Na elimu ya kisasa inaona ya kuwa ardhi yetu hii ilikuwa ni kipande cha jua kilicho jitenga na jua, na bila shaka wakati wa kujitenga kwake kilikuwa na kiwango cha joto kama jua kwa hivi sasa pamoja na kupita mamilion ya miaka, ambayo hufanya kazi ya kupunguza joto lake. Na kwa hivyo kiwango chake cha joto kinakuwa ni nyuzi joto (centigrade) elfu sita, na ndani yake kiwango ni nyuzi joto milioni arobaini.

Na kutokana na kupoa kwa gesi iliyo jitenga na jua ili kujitengeneza ardhi kwa njia ya taratibu likaundika ardhi, na yakatengenezeka maji ambayo kila yanapo gusana na anga la ardhi lenye kiwango cha juu  cha joto, huelekea juu angani katika umbile la mvuke wenye kiwango kisichoweza kufikiriwa, na kukutana na anga lenye baridi kati ya ardhi na jua na kurudi ardhini katika umbile la kimbunga (tufani) kiangamizacho.

Na kutokana na ufafanua wa yote yaliyo tangulia tunarudi hivi sasa kwenye swali letu la msingi katika  maudhui yetu.

Huyo aliepo au alie kuwepo wa mwanzo ambae hakutangu-liwa na uhai, alitokea wapi? Na ametokana na nini? Wakati ambapo kabla yake hapakuwa na uhai? Je ametokana na kutoku-wepo (kisichokuwepo)? Je amejiumba kutokana na madda iliyo kufa?! Ni vipi alie hai ajiumbe kutokana na kitu kilicho kufa na atokee kuwepo kutokana na kuto kuwepo?

Maswali haya hayana majibu na hakuna mbinu ya kielimu juu ya maswali haya isipokuwa ni kujaalia fikra fulani za kubahatisha na dhana fulani. Mmoja anajaalia kuwa hicho kiumbe cha kwanza kilidondoka kutoka mbinguni kikiwa kime-fungwa kwenye vimondo kikitokea kwenye sayari za mbali zenye wakazi.

Na jawabu hili linatupelekea kwenye swali lilelile la mwanzo, viumbe hivyo vya mwanzo vilianza vipi kwenye sayari hizo za mbali? Na mtaalamu mwingine anasema, uhai umejiunda kuto-kana na madda iliyo kufa na hiyo ni natija ya mpangilio wa aina ya pekee uliopo kwenye chembe chembe zake.

Na ushahidi wake juu ya hayo ni kuwa madda iliyo hai imeundika kutokana na elementi zilezile zilizomo kwenye vitu vilivyo kufa tuvionavyo pembezoni mwetu kwenye mawe, maji na udongo. Chembe chembe (elementi) zilezile, kama carbon na hydrogen na oxygen na nitrogen. Kwa mara nyingine ziliundwa tena kwa kiwango na mfumo na mahusiano ya aina ya pekee ili itoe asidi amino (amino acid) na protini na wanga (starch) na sukari, vitu tuvionavyo kwenye viumbe hai.

Bwana huyu hatosheki na nadharia za kujaalia, bali anatoa majaribio yenye kuvutia sana kwa kuweka humo cheche za umeme na mnururisho kiuka urujuani (ultra-violet radiation) kwenye mchanganyiko wa gesi ya Noshadra na Carbon dioxide na methane gas na mvuke wa maji, kisha anakusanya matokeo ya ushirikiano (reaction), anakuta kuna athari za asidi amino.

Na Asidi amino hufahamika kuwa ni tofali la msingi ambalo kutokana nalo kimetengenezwa kiumbe hai. Kwa hivyo basi kuto-kana na mchanganyiko wa asidi kwa njia moja au nyingine kunatokea aina fulani au aina nyingine za protini. Nazo hizi zina uwezekano wa kuungana na kuchanganyika kwa mara milioni na milioni ya njia kama ambavyo herufi au alfabeti zinavyo ungana katika lugha moja na kuweza kutoa ibara na maana zisizo na kikomo.

Na proteni zizaliwazo mara zote ni chembe chembe zenye hisia kali kutokana na baridi, joto, mwanga na umeme hutengana na kuungana ikiwa zitakutana na athari ndogo itokayo nje, kwa hivyo asidi inamiliki sifa ya dharura ya uhai kwenye umbile lake, nayo ni kuathiriwa na mazingira na kuathirika kutokana na vitu vinavyo iathiri.

Na tangu mamilioni ya miaka iliyopita kulikuwa na mazingi-ra juu ya ardhi yanayo faa kujikariri kwa mfano wa majaribio kama haya na kuweza kuunda vitu kama hivi vya aina ya pekee vilivyo itwa asidi amino na zilikuwa zikiyayuka majini pale tu zinapo undwa na kuungana na zingine ili kuunda mamilioni ya makisio ya chembe za protini.

Na asidi hizi zilikuwa ni lazima zikutane kwa mara moja, kwenye mfumo wa aina yake uliomaarufu kwa jina la (D.N.A) dioxyribonucleic Acid (Asidi kiinidioksiribo) ile chembe ambayo huunda virusi kutokana nayo. Huo ni mkusanyiko wa mambo yanayo jaaliwa (assumptions) na kila jambo moja hushika shingo ya mwenziwe.

Hakika wataalamu hawa wanasema ya kuwa kanuni ya ghafla inatuunga mkono. Kwa mfano nyani akae kwenye typewriter huku akiibonyeza kwa muda mrefu usio na mwisho ni lazima aandike kwa mara moja shairi la Shake spear, je si mbele yake kuna nafasi isiyo na mwisho na muda usio na mwisho.

Hakika kila wanacho kitafuta ni kuwa chembe chembe hizi za asidimino ziungane kwenye umbile la kipekee, walilo liita (D.N.A). Nayo madda ya kipekee, itasimamia kazi yake yenyewe na kuongezeka kwa kutumia vyombo vyake maalumu huku ikiweka mbegu za uhai za mwanzo.

Tulikubali na kuamini kwa misingi ya mjadala na makisio ya kuwa chembe chembe za mchanga na maji ziliungana kwa ghafla bila kupangiliwa na kibahati na mfumo wa Asidi za mwanzo (D.N.A), kisha asidi ikaanza kuzaana kwa njia zake, ili itengeneze kutokana nayo yenyewe mamilioni ya viumbe mfano wake. Hakika yote haya sio uhai tuonao. Kwa hivyo ni lazima turudi na tujaalie ya kuwa viungo vya asidi hii vilirudi tena na kuungana kwa ghafla na kibahati bila kupangwa ili kuunda protini. Kisha protini kwa ghafla na bila kupangwa ilijiunda kwenye sura au umbo la seli ya uhai.

Kisha hapo hapo tunarudi na kusema:

Seli moja ya uhai ilijichagulia kighafla na bila kupangwa, umbile la mmea na seli nyingine ilijichagulia kighafla na kibahati umbo au mwelekeo wa kuwa mnyama.

Kisha tuna kwea mti wa uhai hatua kwa hatua, na maana ya funguo hizi za uchawi ni kuwa kila tunapotatizwa na kitu fulani kwenye ufumbuzi wake husema:

Hakika kitu hiki kimetokea kwa ghaflaJe haya yanakubalika akilini ya kwamba ndege na samaki wahamao miji yao na kwenda umbali wa ma elfu ya maili kwa kuvuka majangwa  na mabahari, hurudi miji yao kwa ghafla na bahati?

Kuendelea kupungua kwa joto, maji kutuwana na kutengene-zeka mabahari kisha milima. Hata kama tutasema ya kuwa nadharia hii ni ya kweli na sahihi ioneshayo jinsi ardhi ilivyo patikana, sisi bado tunafikiria katika suala la seli za uhai ambazo huenda ikasemekana ya kuwa ziliteremka pamoja na ardhi kutoka kwenye jua. Vipi seli hizi za uhai zinaweza kuishi kwenye kiwango cha joto kisicho pungua nyuzi joto elfu sita chini ya mia (centigrade), vyovyote itakavyo kuwa imefunikwa seli hii, na vyovyote itakavyo jitengenezea vitu vya kuikinga na kuihifadhi.

Hakika kiwango cha joto cha mwanadamu, na binadamu huyo ndie anayechukuliwa kuwa ni kiumbe hai wa daraja la juu, hakizidi 37% (kwa mia), isipokuwa kwenye hali ya ugonjwa huzidi kidogo kwenye arobaini. Na ikiwa maji yanakuwa mvuke kwenye kiwango cha nyuzi joto mia moja, hakika nyuzi joto elfu moja inatosha kukifanya kila kitu vyovyote kitakavyo kuwa kigumu, kikose ugumu wake na kuwa gesi. Sasa ni vipi hali yetu itakuwa kwenye joto lililo fikia kiwango cha elfu sita?

Na kwa msingi huu hakika elimu na akili vina kubaliana juu ya kuwa ni muhali kuanza kwa uhai kutokana na seli ya uhai iliyo toka kwenye jua, na ni lazima kila kiumbe hai kiwe kime umbwa juu ya ardhi baada ya kuumbwa ardhi. Na ni uzuri ulioje wa maneno ayatangazayo mtaalamu huyu maarufu aitwaye Gostof Buniy, pindi aliposema:

Eti tuunde madda iliyo hai!! Vipi linawezekana hilo wakati tunapofikiria ni sifa ngapi zilizo kusanyika kwenye chembe chembe za urithi na mustakbali usio fahamika (uliofungika) hupatikana kwenye kipande cha protoplasm iliyo hai? Na kwa kutumia ghafla kifaranga huvunjia yai katika sehemu  iliyo dhaifu, ili kiweze kutoka kwenye yai lake.

Na kwa ghafla jeraha hujikusanya na kujiunga bila kuwepo tabibu wa majeraha. Kwa ghafla mmea wa alizeti (sunflower) hufahamu ya kuwa jua ndio chanzo cha uhai wake na kulifuata. Na kwa ghafla miti ya jangwani hujitengenezea mbegu zenye mbawa ili ziweze kupaa jangwani hadi kufikia kwenye mazingira yenye kumea na ya maji maji na mvua iliyo nzuri.

Na kwa ghafla virusi viligundua njia yake yenye kutatiza katika kuishinda nguvu seli ya uhai na kuweza kuiba uhai wake ikiwa ndani yake na kuiangamiza. Kwa ghafla mmea uligundua chembe ya chlorophyl na kuitumia kuzalisha nguvu (nishati) ya uhai wake.

Kwa ghafla, kibahati, mbu alitengeneza mifuko yenye kuelea kwa kila yai ili yaweze kuelea juu ya maji na yasiangamie. Na sisimizi ambae hupiga sindano ya sumu kwenye mishipa ya fahamu ya wadudu ili aipoze kisha humkokota ili kumhifadhi kwenye kiota chake akiwa ni chakula cha akiba kwa ajili ya watoto, je kisa chote hiki hufanyika kwa ghafla?

Na nyuki alieweka jamii na nidhamu na akafanya kazi ya ujenzi na akaonyesha utaalamu wake katika kazi ya kemikali yenye kutatanisha ya kuibadilisha mbochi (nector) kuwa asali na ua likawa nta (beeswax), je huyafanya yote haya kwa ghafla? Na wadudu hawa waitwao mchwa (termites) ambao waligundua kanuni ya mwanzo ya kupoza hewa na kuitekeleza kwenye jamii yao nidhamu iliyo madhubuti na makini, kwa tabaka zote je walifikia kwenye mambo hayo kwa njia ya ghafla?

Na wadudu wenye rangi ambao waligundua misingi ya kifani na njia za kufanya vitimbi kujificha. Na wadudu waitwao kaadhi-fatul kanabil ambao huzalisha gesi ya sumu na kuitawanya, je yote haya yamefanyika kwa ghafla na bila kupangwa?

Ikiwa sisi tuta amini na kukubali ya kuwa uhai umeanza kwa njia ya ghafla! Vipi tutaweza kukubali ya kuwa matukio yote haya yamefanyika kwa ghafla ?

Ikiwa tutasema maneno kama haya na kukubali, huo utakuwa ni ujahili na utovu wa  elimu. Na fikra ya madda ilijikuta kwenye taabu mbele ya utovu huu wa elimu, ikaanza kujiokoa kutokana na neno ghafla ili kuweka dhana (assumption) nyengine wakase-ma: Hakika uhai wote huu wenye kushangaza na wa aina tofauti umeanzia kwenye hali ya dharura kama ile hali ambayo hukupa msukumo wa kula chakula wakati unaposhikwa na njaa, kisha dharura hiyo ikafungika (ikatatanisha) kutokana na kufungika kwa mazingira na mahitajio na kukatokea aina zote hizi za uhai.

Huu ni mchezo wa maneno tu. Sehemu ya neno ghafla wameweka neno dharura ikafungika (kutatanisha). Nayo kati-ka nadhariya yao ni kuwa dharura hujifunga yenyewe na hukua yenyewe kwa njia ya ghafla. Vipi itakuwa hivyo? Vipi tukio litaweza kukua na kuwa kisa chenye kutungwa bila kuwepo akili iliyo kitunga?

Na ni nani alie simamisha asili hiyo ya dharura? Na vipi itaweza kupatikana dharura kutokana na kutokuwepo dharura? Hakika hayo ni kujiuwa na kujimaliza kwa ajili ya kujiepusha na ukweli wa kimaumbile ulio wazi ambao hauhitaji kufikiria na unao jionyesha wenyewe na kuthibitisha ya kuwa kuna muumba na mpangaji au muendeshaji wa vitu vyote.

Kwa nini kuwepo upingaji huu na inadi (ukaidi)? Na ni kwa nini tuna kitafuta kitu kisicho wezekana ili kujiepusha na ukweli ulio wazi ambao maumbile huyapigia kelele (kunadi) na usio hitaji nguvu za kufikiria ndani mwetu? Na ikiwa tutakanusha uwazi huu ni kitu gani katika akili zetu kitabakia ilihali akili yetu yote imejengeka kwenye nidhamu ya kimantiki yenye kubeba mambo ya kiujuzi (intuitive) yaingiayo akilini ghafla bila kuhitaji kufikiria sana wala kudadisi.

Na yote hayo hayatakuwa na maana bali ni kuzibomoa akili zetu na faida zake wakati ambapo tunadai ya kuwa sisi ni watu wenye akili na wenye elimu, tunatumia na kuongozwa na elimu kwenye kila kitu.

Mtaalamu mmoja wa fizikia (physics) Dr Konjidan anasema:

Hakika vitu vyote vilivyomo ulimwenguni vinashuhudia kuwepo kwa Mwenyezi Mungu alie takasika na vinatujulisha uwezo wake na utukufu wake. Na sisi wataalamu tuna simama na kufanya uchambuzi wa maumbile ya ulimwengu huu na kuya soma, hata kwa kutumia njia za kutoa dalili, hakika sisi hakuna tukifanyacho zaidi ya kuvifanyia uchunguzi vitu vilivyo tengene-zwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Huyo ndie Mwenyezi Mungu ambae hatuwezi kumfikia kwa nyenzo za kielimu zenye asili ya madda (material), lakini sisi tukionacho ni alama zake katika nafsi zetu na katika kila chembe chembe kati ya chembe chembe za ulimwengu huu.

Na elimu hizi si jambo lingine bali ni utafiti wa viumbe vya Mwenyezi Mungu na athari za uwezo wake.                                                                                                  

) (.

        Huyo ni Mola wenu hapana Mola wa kweli isipokuwa yeye, Muumba wa kila kitu basi muabuduni.

) ȡ ޡ (.

Yeye ndie ambae alilifanya jua litoe mwanga na mwezi utoe nuru na akaukadiria mwezi vituo ili muweze kufahamu idadi ya miaka na kuhesabu. Mwenyezi Mungu hakuyaumba hayo isipo-kuwa kwa haki, ana zipambanua aya zake kwa watu wenye kujua.

) ֡ ѡ (.

Ibrahim:32-34.Mwenyezi Mungu ndie ambae aliumba mbingu na ardhi na akateremsha maji kutoka mawinguni, na kwa maji hayo akakutoleeni matunda ikiwa ni riziki yenu, na akakutii-shieni mito na akakutiishieni jua na mwezi vyenye kutembea, na akakutiishieni usiku na mchana, na akakupeni kila mlicho muomba.

) ѡ (.Al-aaraf:54

Fahamuni, kuumba ni kwake tu Mwenyezi Mungu, amri zote ni zake (Mwenyezi Mungu) Mola wa walimwengu wote.

                               

***


 

[1] Nash-atud din:196-197 (mwanzo wa dini)

[2] Mfano: A ndie msababishaji wa B na B ni msababishaji wa A.

 

index