back page

UTUME

next page

 

 

 

)   (.

Na hatuwatumi wajumbe (Mitume) isipokuwa ni wenye kutoa bishara na wenye kuonya, kwa hivyo basi Mwenye kuamini na akatenda mema (watu hao) hakuna khofu juu yao na wala hawata huzunika.

)    . (.

Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu kilicho teremshwa kwa mtume wake na Kitabu kilicho teremshwa kabla yake. Na mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake, na siku ya mwisho, hakika amepotea upotovu ulio mbali (na haki).Quran tukufu.

) (.

Na Mwenyezi Mungu aliwatumia Mitume mmoja baada ya mwingine ili wawakumbushe ahadi (agano) ya maumbile yake (iliyoko kwenye maumbile), na wawakumbushe neema zake zilizo sahaulika, na wawatolee hoja kwa kuwafikishia ujumbe, na wawafunulie mambo yaliyo fichwa akilini mwao (ili wazitumie ipasavyo).

Amirul-muuminin ALi bin Abi-twaalib (a.s).

 

 

 

 

 

         U T A N G U L I Z I

      

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.

 Sifa njema zote (Himidi)  ni za Mwenyezi Mungu pekee, mola wa walimwengu. Na rehema na amani ziwe juu ya mtume wake Muhammad (s.a.w), na kizazi chake chema na kilicho twahirika.

Hukumu ya mbinguni na ardhini inapokuwa ni ya Mwenyezi Mungu mtukufu -pekee- bila ya kuwa na mshirika au mwenye kugombea cheo hicho, kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipo kuwa yeye tu, Mfalme mtakasifu mwenye usalama, mtoaji wa amani, mwenye utawala wa kuyaendesha mambo yote, mtukufu, mwenye nguvu na ushindi na mwenye utukufu wote naYeye ni Mwenyezi Mungu muumba na mwenye kuvipa vitu maumbile, majina yote mazuri ni yake na Yeye ni Mwenyezi Mungu ambae hakuna apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye, Mjuzi wa mambo ya ghaibu (yasiyo onekana) na yaonekanayo, yeye ndie mwingi wa rehma mwenye kurehemu, basi hukumu inapokuwa ni ya Mwenyezi Mungu kwa undani huu na upana huu na kwa ushahidi wa dalili na maumbile, hakika jukumu la kwanza la hakimu huyu -kwa upole wake na ukarimu na kwa fadhila yake- ni lazima awawekee viumbe mambo ambayo yataufanya usalama na utulivu wao ubakie na mambo yenye kuzilinda haki zao na utukufu wao, na kuzitengeza (kuzitakasa) kabisa tabia zao na mwenendo wao. Kama ambavyo miongoni mwa majukumu yake ya mwanzo ili kukamilisha fadhila zake na neema zake na upole wake ni kuwafikishia viumbe wote kwa vizazi vyao vyote upambanuzi wa sheria zile na hukumu zile, ili manufaa  yake yaweze kuwafikia wote na hoja nayo iweze kutimia kwa viumbe wote.

Na -kwa ufupi- hii ndio mana ya Utume kwa maana yake ya ujumla. Na kutokana na akili ya mwanadamu kuwa ni yenye kupanuka na kuendelea -kila zama na karne zinavyo pita- na ikiwa kwenye maendeleo yenye kupanuka na mwendo wake wa haraka kuelekea kwenye kukomaa na kuzama na ufahamu ulioenea pande zote, sheria za mbinguni (takatifu) zilikuwa zikishuka taratibu kulingana na maendeleo ya akili na kupanuka kwake, kiasi kwamba katika kila zama na kwa kila kaumu sheria zile ziko katika kiwango kinachowiana na maslaha ya zama zile na watu wale na zenye kulingana na kiwango cha ukuaji wa fikra wa zama zile na watu wake, zikafikia kileleni (zile sheria) katika ujumbe wa kiislamu ambazo alizichagua Mwenyezi Mungu mtukufu ili ziwe ni sheria bora za mwanadamu katika zama za kukua kwake kiakili na kufikia kilele cha mwisho na katika zama za  maendeleo yake ya utamaduni wenye kushangaza na ulio mku-bwa.

Na haya -kwa ufupi- ndio maana ya utume kwa maana yake pana kiujumla.

Sehemu hii itaelezea suala la utume kwa maana yake ya ujumla wenye mahusiano na vitabu mbalimbali vingine vya mbinguni (vitukufu) na wale walio ufikisha au walio pewa jukumu la kuufikisha ujumbe huo kwa muda wote au zama zote, na kwa maana yake (maalum) yenye kuhusiana na ujumbe wa kiislamu na aliepewa jukumu la kuufikisha alie mtukufu (juu yake rehma na amani).

Huku tukizingatia wepesi katika kubainisha yote haya tutakayo yafafanua na uwazi wa sentensi na wa dalili.

Na huku nikiandika misitari hii ya mwisho  sitasahau kuele-zea kwamba, mimi katika kumtaja Mtume wetu Muhammad (s.a.w) sikuelezea historia ya maisha yake matukufu na sehemu fulani katika mwenendo wake mtukufu, kwa kuzingatia kuwa sehemu hizo ni pana na zinahitaji nafasi pana na ufafanuzi wa wazi na wenye kutosheleza, ufafanuzi ambao hautoshi kwenye kurasa zetu hizi finyu, nikiyategemeza yote haya kwenye kitabu changu kikubwa kiitwacho Fi-rihabi-rrasuul (s.a.w) ambacho ninatarajia kukikamilisha na kukisambaza katika muda mfupi iwezekanavyo insha allah.

Kwa hivyo basi msomaji mtukufu hatapata kwenye kitabu hiki isipokuwa mazungumzo kuhusiana na utume na katika mipaka mahsusi ya kielimu ya masala haya.

Na ninataraji msaada na msukumo wa Mwenyezi Mungu.

Ewe Mola wetu! Hakika sisi tumemsikia muitaji akiita (watu) kwenye Imani ya kwamba Muaminini Mola wenu tuka amini. (Ewe) Mola wetu! Tusamehe madhambi yetu na utufishe pamoja na watu wema. (Ewe) Mola wetu! Tupe ulichotuahidi kwa Mitume wako na usituache siku ya kiama (ya mwisho). Hakika wewe huendi kinyume na ahadi.

 

 

 

Na maombi yetu ya mwisho nikuwa tunasema sifa (himidi) zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu .

 

Kaadhimiya-Iraq.

 

 MOHAMMAD HASSAN  AALI-YASSIN.

 

 

***
 

UTUME

 

 

KWA MAANA YAKE YA UJUMLA.

 

Katika masomo yetu yaliyo pita tulimalizia kwa natija thabiti ambayo haina njia ya kulikimbia, bali ni lazima kukiri natija hiyo kutokana na hukumu ya dalili. Natija hii ni kuwa:

Hakika kuamini kuwepo kwa Muunba wa ulimwengu huu na vyote vilivyomo na waliomo ni suala lililo wazi na badaha (intuitive) kati ya mambo yaliyo wazi ya kiakili, kimantiki, na kimaumbile na hali halisi ilivyo, na kwamba yote yaliyo semwa kwa lengo la kutia shaka katika usahihi wa jambo hili la wazi na la badaha hayawezi kusimama kidete mbele ya mjadala na dalili, na kwamba madda kutokana na hali kuwa inafahamika jinsi ilivyotokea ni lazima iwe na chanzo chake kisicho kuwa na mwanzo nacho ni waajibul -wujuud alie wa lazima kuwepo na wadharura kuwepo kwake, na kwamba chanzo hicho cha mwanzo ni lazima kiwe na akili na chenye kufahamu na chenye hekima, na sifa hizo zote haziwezekani kuthibitika kwenye madda iliyo pofu na ambayo haina akili wala busara na iliyo bubu na isiyo na hekima.

Kisha tulikomea kwenye somo letu lililo tangulia pia kwenye natija nyingine ambayo muhtasari wake ni kama ufuatavyo:

Kwamba utawala wa kutoa hukumu katika maumbile- na nyanja zake zote- si wa mwingine, bali ni wa Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa kumzingatia kuwa yeye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu na afanyae alitakalo. Na yeye ndie mwenye ufalme wa kila kitu[1]Na haulizwi kwa lile alifanyalo nao waja huulizwa na ni mwenye kutakasika na makosa au kukosea, na ndie tajiri na mwenye kusifiwa (himidi).

Na haiwezekani kwetu sisi kuikubali nguvu yoyote kuwa ina utawala wa kutoa hukumu katika maumbile na kwamba nguvu hiyo ndio chimbuko la tawala zote isipokuwa itakapo jikusanyia sifa hizi, na sifa hizi haiwezekani kukusanyika kwa mwingine tofauti na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hukumu ya akili na kutokana na uwazi wa suala hili, na ubadaha wake.[2]

Na ikiwa utawala huu wa kutoa hukumu katika maumbile ni mahsusi tu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu -kama ilivyotangulia-ni lazima utawala wa kutoa hukumu katika ulimwengu wa kanuni- pamoja na tawala zake zote uwe ni wa Mwenyezi Mungu, vilevile bila kuwa na mshirika au mwenye kuzozana nae kwenye suala hilo, kwa sababu ya kutowezekana kutenganisha kati ya utawala huu wa kutoa hukumu na utawala wa kutoa hukumu katika maumbile tuliyo utaja hapo nyuma.

Kwa hivyo kutokana na yote hayo masala yanayo chukuliwa na kunyambuliwa humo ni kuwa:

Hakika Mwenyezi Mungu huyu mwenye akili na mwenye kufahamu na kuelewa na mwenye hekima alie mpweke katika utoaji wa hukumu katika maumbile na nyanja zake zote na katika utoaji hukumu katika ulimwengu kanuni na tawala zake zote, ni lazima awawekee viumbe nidhamu ambayo itadhihirisha utawala wake katika kutoa hukumu kwenye mambo ayatakayo au asiyo yataka, na hasa kwa kuzingatia kuwa yeye Mwenyezi Mungu ni mjuzi - ujuzi usio na mfano- wa matokeo na mwisho wa yatakayo- mfikia mwanadamu, kwenye makarne na makarne na kwenye malaki ya karne na zaidi ya hapo kutokana na idadi yenye kushangaza ambayo ni kubwa, na kutokana na kuwa watu ni wenye kupenda vitu tofauti na wenye hamu tofauti, wenye kutofautiana fikra na akili, kwa kiasi ambacho kwa wingi huu maisha hayawezi kuwa tulivu na thabiti na yenye kuendelea bila kuwepo nidhamu inayo wahukumu wote, na wote wawe ni wenye kuinyenyekea na kuitii, na kumuwekea kila kitu mtu na kila jamii haki zake na majukumu yake na kumpangia kila mwanadamu mfumo na mwenendo wake pamoja na nafsi yake na katika maisha yake ya kijamii, na kuwekwa chini yake utatuzi bora wa matatizo ya viumbe kwa muda wote wa karibu na wa mbali.

Na haya ndio wayapayo istilahi wanazuoni wa elimu ya akida Siri ya kutumwa Mitume na ambayo, ili kuweka maana wazi zaidi tunayoiita Lengo litakiwalo, nyuma ya utume.

Huwenda akawepo mwenye kujiuliza na kusema :Kwa nini Mwenyezi Mungu awawekee wanadamu nidhamu ya maisha yao na mfumo wa mwenendo wao, na asimuachie mwanadam uhuru wake kamili wa kuweka sheria na kutunga kanuni kwa kutegemea fikra zake na elimu yake na uzoefu anao upata, kwa kukosea na kupatia, kwa kufuta na kurekebisha na kuendelea kufanya marekebisho na mabadiliko, hadi aweze kufikia mwisho-we kuweka nidhamu bora na mfumo ulio mwema?

Na jawabu la suala hilo ni kama ifuatavyo:

Kwanza:

Hakika kuweka nidhamu na sheria ni haki ya chimbuko la tawala pekee bila kushirikiana na yeyote kwenye suala hilo. Na hayo ndio walio kubaliana wataalamu wa kanuni na siasa, katika ulimwengu wetu wa leo.

Na kutokana na tulivyo kuwa tukiitakidi -kama tulivyo tangulia kusema- ya kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu ndio chimbuko la tawala zote na kwamba yeye ndie hakimu katika ulimwengu wa maumbile na katika ulimwengu wa kanuni, ambae hakuna mwenye kumtatiza kwenye cheo hicho, ilikuwa ni lazima kusema ya kwamba yeye ndie mwenye haki ya kutoa kauli ya mwisho katika uwekaji wa kanuni na kuchagua nidhamu inayo faa.

) (

    Sema: Hakika muongozo wa Mwenyezi Mungu ndio muongozo   uliobora.                                                                                                  

Pili:

Hakika sisi tunaitakidi kwamba akili ya mwanadamu vyovyote itakavyo pewa uwezo wa kugundua na kuunda na udadisi wa ndani, haiwezi kuelewa maslahi ya siku za mbali ya matatizo ya mwanadamu mwenye kuadhibika, na utatuzi wake ulio sahihi isipokuwa ni baada ya taabu ya muda mrefu ambao amepitia majaribio mengi, na wenye makosa na ishtibaha nyingi, na huenda asiweze mwisho wa utatuzi - pamoja na yote hayo- kufikia utatuzi wa sawa na kwenye natija itakiwayo,Na hatukukiteremsha kwako kitabu isipokuwa (kwa lengo la kuwa) uwafafanulie lile ambalo wametofautiana kwalo.

 

Tatu:

Hakika kuwekwa kanuni na mwanadamu hakutaepukana na kutawaliwa na malengo ya kibinafsi na kuleta hali ya kutanguliza vyeo vikubwa na kuleta hisia za kibinafsi na za kitabaka kwa muwekaji wa nidhamu, vyovyote watakavyo kuwa na wakitokea kwenye tabaka lolote lile.

Na kutokana na haya ilikuwa ni lazima kuwaokoa wanadamu kutokana na adhabu ya kujikwaa au kutofuata muongozo, na ujinga na majaribio (au uzoefu) yenye makosa, awawekee kanuni (nidhamu) iliyopana, ambae anayaelewa mahitajio yao na ma-mbo yanayowafaa, na anafahamu matatizo yao ya leo na kesho na kutofautisha kati ya mambo yenye kuwanufaisha na kuwadhuru, na kuweka sawa kati ya kundi lingine, na tabaka fulani na tabaka lingine, au mtu na mwinginewe, na aina fulani ya watu na wasio kuwa wao, na nchi fulani na zisizo hizo.

Na hakuna katika ulimwengu huu alie kusanya sifa hizi isipokuwa Mwenyezi Mungu mtukufu. Na nidhamu zake na sheria au uwekaji wa sheria zake si jambo jingine bali ni zile risala tofauti tofauti ambazo zilibebwa na Mitume wake na manabii wake hadi ardhini ili kumfanya mwanadamu awe mja mwema na kumtoa kwenye kiza hadi kwenye mwangaza (wa uongofu).

Na hii ndio maana ya Lutfu (upole) na huruma ya Mwenyezi Mungu iliyo kusudiwa na wanazuoni wa elimu ya akida wakijitegemeza kwake wasemapo kuwa ni lazima watume Mitume na ni lazima waendelee kuwepo ardhini, maadamu maisha au uhai wa viumbe ungali bado upo.

Na baadhi ya watu walio julikana kwa jina dhehebu la

Al-barahima[3] walishikamana na kauli isemayo kuwa: Hakuna ulazima wa kuwepo au kutumwa ujumbe wa mbinguni yaani mitume wake, na wakayatolea dalili hayo kwa kudai kuwa ikiwa risala (ujumbe) wa Mwenyezi Mungu umeleta mambo yanayo kubaliana na kuafikiana na akili kwa hivyo basi akili itakuwa haihitajii ujumbe huo kwani imejitosheleza, na ikiwa amewataja pamoja na kauli yao hii  umeleta mambo yanayo tofautiana au kupingana na akili basi utakuwa ni wenye kupingwa na akili kabla ya kuletwa.

Na madai haya, ubatilifu wake uko wazi na ni yenye dalili dhaifu kwa sababu kila mwenye ujuzi wa sheria za mbinguni anafahamu ya kuwa sheria au ujumbe huo umekusanya mambo ambayo akili inayafahamu na yale akili isiyoyafahamu, ama mambo ambayo akili inayafahamu, sheria hii ilikuwa na jukumu la kuyatilia mkazo na kuyafanya yawe na ulazima, yaani kuwala-zimisha watu mambo hayo, na kufanya hivyo ilikuwa ni kuunga mkono cheo cha akili na ilikuwa ni kusema kupitia matendo, umuhimu wa akili katika ujenzi wa maisha.

Ama mambo ambayo akili haiyafahamu - na ambayo ni mengi zaidi- lengo lilikuwa ni kuwaongoza watu na kuwaelekeza kwenye kuchagua mambo yenye maslahi zaidi kwao kati ya masala au mambo wanayokutana nayo katika maisha, na ambayo ni magumu na mambo mengine asiyo yajua mwanadamu na matatizo yake mapya yatokeayo kila siku.

Na haya ambayo akili haiyafahamu ndiyo yaliyo itwa na kundi hili la Al-baraahimah mambo yenye kupingana na akili nayo ni ibara ambayo haikuzingatiwa vizuri kwani risala zote za mbinguni ndani yake hapa kuwa na jambo lolote linalopingana na akili kamwe, isipokuwa watu hawa wakizingatia kila jambo ambalo akili hailijui linapingana na akili na wakati huo (baada ya kuvunja kauli yao) jukumu la risala na ujumbe huu, linakuwa ni kuweka wazi mambo yasiyo julikana, na kuiweka huru akili.

) (.

 Hakika Mwenyezi Mungu aliwaneemesha waumini, pindi alipowatumia Mtume atokae miongoni mwao anasoma aya zake na anawatakasa na anawafundisha Kitabu  na hekima.

) (.

                 Ubainifu wa kila kitu na ni uongofu na rehema        

Hakika Mwenyezi Mungu aliwasifu mabalozi hawa watakati-fu kwa sifa ya viongozi (maimamu)( )Hakika mimi nimekufanya uwe kiongozi (Imamu) wa watu. Na amewasifu kwa sifa ya ukhalifa ( )hakika sisi tumekufanya uwe Khalifa katika ardhi. Na amewasifu kwa sifa ya wajumbe.

( ). Na amani iwe juu ya Mitume (wajumbe). 

(    )Wale ambao hufikisha ujumbe wa

Mwenyezi Mungu. Na kwa sifa ya unabii:

.(   )   Na Mwenyezi Mungu akawatuma manabii watoao bishara na waonyaji. Na hakuwasifu kwa sifa za utoaji hukumu si kwa maana yake ya kikanuni wala kisiasa hata kidogo, kwa sababu Mtume na Nabii sioMtoaji wa juu wa hukumu bali yeye ni naibu wa hakimu wa juu nae ni Mwenyezi mungu Mkufu.

Na pamoja na sifa nyingi tulizo ziashiria, Quran tukufu katika kumzungumzia Mtume Muhammad (s.a.w) ilikomea kwenye sifa mbili :

1- Arrasuul:

( )Ewe Mjumbe! Fikisha ulicho- teremshiwa kutoka kwa Mola wako.

Na sifa ya Annabiyu( ).

Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutosha. Katika Qurani tukufu katika matumizi yake imezirudia rudia sana sifa hizi mbili, je zote zina maana moja au kuna tofauti kati ya sifa mbili hizi?

Na ikiwa hayo hayana maana kwa Muhammad bin Abdillah (s.a.w) kwa sifa hizo mbili na yeye ni uthibitisho wa matamshi hayo mawili, basi tofauti - lau ikipatikana- athari yake itaonekana kwenye zama hizo zilizo tangulia, zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) kwenye zama za manabii na Mitume waliotangulia.

Na pamoja na mengi yaliyo semwa kuhusu tofauti ya maneno mawili hayo, na pamoja na kuwa masala haya na mielekeo mingi, hakika muelekeo bora zaidi tulio usoma kwenye maudhui haya ni kuwa Nabii ni mtu atowae habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu, bila ya kuwa na mtu wa kati, na hii imekusanya wote awe na sheria kama Mtume Muhammad (s.a.w) au asiwe na sheria kama Mtume Yahya (a.s).

Na kwamba ameitwa Nabii kwa sababu ametoa habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa lugha ya kiarabu. Na limetu-mika Faiil kwa maana ya Muf il.

 . .                                               Na Rasuul ni mwenye kutoa habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na mtu yeyote wa kati, na anasheria[4]

 Kwa hivyo inaonekana wazi kuwa Nabi na Rasul sifa zao zinalingana kwenye utoaji wa habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu, lakini Rasuli ana sifa khasa ambayo ni sifa ya kutumwa na sheria, ama Nabii, ni sifa ya yeyote mwenye kubeba sheria au mwenye kuisimamia baada ya kufa mbebaji wa sheria ile.

Na huu ndio muelekeo bora zaidi katika kutofautisha kati ya sifa mbili, na kutokana na haya wanazuoni wa akida walisema Hakika Rasuli Mjumbeni nabii (Mtume) na si kinyume chake (yaani si kila Nabii ni Rasuli).

Na kwa kuwa imebainika kutokana na yote yaliyo pita, usahihi wa kauli isemayo kuwa ni wajibu kuwepo Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa hukumu ya akili na kutokana na lutfu ya Mwenyezi Mungu na ulazima wa kusema kuwa yapasa kuwepo wawakilishi waaminifu kati ya Mwenyezi Mungu mtukufu na watu, kwa lengo la kufikisha majukumu (sheria zake) ilikuwa ni lazima kuwepo alama inayothibitisha ukweli wa mwenye kudai utume katika madai yake, kwa sababu uwakilishi huu wa Mwenyezi Mungu ni katika vyeo vikubwa ambavyo watu wengi hudai kuwa wanavyo na kuchanganyika ukweli na uongo. Na alama hii ni lazima iwe juu zaidi ya matendo ya kawaida ambayo mwenye kudai cheo hiki kwa uongo asiweze kutoa mfano wake. Kwa hivyo jambo hilo linafungika kwa kuleta Muujiza yaani jambo ambalo lina kiuka kanuni za kimaumbile.

Na neno Iijaaz kwa lugha ya kiarabu ni Kufanya mtu ashindwe. Husemwa:

  Nimemfanya Zaidi ashindwe.

Na katika istilahi:Ni yule mwenye kudai cheo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu, kuleta au kufanya jambo lenye kupitukia kanuni za maumbile na watu wakashindwa kufanya mfano wake ikiwa ni ushahidi wa ukweli wa madai yake.

Na inatubidi tusighafilike, kuwa sio katika muujiza kwa istilahi tuliyo taja, mambo ayatendayo mchawi au mtaalamu wa baadhi ya elimu za kinadharia zilizo ngumu na madhubuti, hata kama atafanya kitu ambacho watu wengine watashindwa kuleta mfano wake, kwa sababu elimu za kinadharia zina kanuni zenye kufahamika kwa wenye nazo, na ni lazima kwa kanuni hizo kumfikisha kwenye natija yake hata kama kutahitajika udadisi na ushupavu katika kuzitekeleza.

Na pengine mtu anaweza kudai cheo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu na akafanya mambo ambayo watu wengine wakashindwa kufanya mfano wake, kisha jambo lile likawa ni dalili ya uongo wa madai yake, kwa mfano mambo yahusishwayo na Musailamatul-Kadhaab, kuwa yeye alitema mate kwenye kisima chenye maji machache ili maji yake yaongezeke. Matokeo yake ni kuwa maji yote yali kauka kwenye kisima kile.

Na  kwamba aliupitisha mkono wake juu ya vichwa vya watoto wa kabila lake, matokeo yake yakawa kila mtoto aliegu-swa na mkono wa bwana yule kichwani nywele zote zilipukutika,  na kuwa vipara.

Kwa hivyo basi, ni lazima kwa kila Mtume awe na muujiza. Na muujiza huu ni lazima uwe sawa na madai ya Mtume huyo au mwenye kudai utume. Na kwa kufanya hivyo, yule mwenye muujiza huo anakuwa ndie Nabii atokae kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na mkweli.

      (    )                                                         Na haikuwa kwa Mtume (yeyote) kufanya dalili (muujiza) isipo kuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Na imekuwa sahihi kauli isemayo kuwa muujiza ni dalili ya ukweli wa Mwenye kudai utume na ni usahihi wa madai yake kwa sababu muujiza ukizingatiwa kuwa umefanyika na umesimama katika kupituka  kanuni za maumbile na mifumo yake yenye kueleweka hauwezi kufanywa na yeyote isipokuwa kwa kuweze-shwa na Mwenyezi Mungu.

( )                                                  Si mazungumzo (hadithi) yaliyo zuliwa lakini ni uthibitisho wa yale yaliyotangulia.

 Kwa hivyo muujiza uletwao na mwenye kudai utume unakuwa ni dalili juu ya ukweli wake kwa kuwa inadhihirisha kuridhia kwa Mwenyezi Mungu utume wake kiasi kwamba amemuwezesha kuleta muujiza huo. Na Mwenyezi Mungu ameashiria maana hii kwa kauli yake kwenye Kitabu chake kitukufu:

)   (

Lau kama (Mtume) angelizua juu yetu baadhi ya maneno  na kudai ya kuwa niya Mwenyezi Mungu, bila shaka tungemkamata kwa mkono wa kuume (uwezo wetu), kisha kwa hakika tunge-mkamata mshipa wake wa damu.

Na kauli yake isemayo:

) (.

Na Quran hii haikuwa ni yenye kuzuliwa na asiyekuwa Mwenyezi Mungu, lakini ni uthibitisho wa yule ambaye yuko mbele yake na ni uchambuzi wa kitabu kisicho na shaka kitoka-cho kwa Mola wa walimwengu.

) (

Ama wanasema ya kuwa hiyo Quran ameizua! Sema: Basi leteni sura moja mfano wake na ombeni usaidizi wa yeyote muwezae kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu ikiwa muwakweli.

 

***

 

MUHAMMAD (s.a.w) NI MWISHO WA MITUME.

 

Muhtasari wa kifungu au sehemu iliyo pita ulikuwa kwamba:

 

Utume ni jambo la dharura ambalo akili ya mwenye kumu-amini Mwenyezi Mungu imelihukumu na kulifanya kuwa ni suala muhimu linalo hitajiwa na wanadamu, na kwamba Mwenyezi Mungu -kwa upole wake na huruma yake- aliwatumia watu mitume na manabii na sheria na vitabu katika zama zote na watu wote, haikukomea kwa utaratibu huo kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.), akawa ndie bora wa mitume na mwisho wa manabii, na sheria yake ikawa ndio sheria ya mwisho na yenye kubakia kwa muda wote wa kubakia mbingu na ardhi.

Na huenda sifa muhimu ya kwanza tunayoweza kuisajili kwa Mtume huyu wa mwisho ni kuwa Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa bora juu ya mitume wengine kwa kuwa Mjumbe (Rasul) wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa manabii, na ujumbe wake ndio mkubwa na kuwa ni ujumbe wa kilimwengu kwa zama zote na sehemu zote, hauwahusu watu fulani tofauti na wengine, au sehemu fulani tu ya ardhi tofauti na nyingine, wala umma fulani tofauti na mwengine, wala zama fulani tofauti na zama nyingine.

    (   ) 

Na hatukukutuma isipokuwa ni kwa watu wote.

           ( ).

Na hatukukutuma isipokuwa uwe ni rehma kwa walimwengu.

           (   )

  Enyi watu! Hakika mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu nyote.

           ( )Ilinikuonyeni kwa hii (Quran) na yeyote itakaemfikia. ( )Enyi watu! Hakika si jambo jingine, ila ni kuwa mimi kwenu ni muonyaji wa wazi. Aya hizi tukufu zimetoa dalili za wazi kwa mambo yasiyo hitaji au kukubali mjadala au tafsiri, ya kwamba Muhammad (s.a.w) ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote, kwa wale walio kuwepo pindi alipotumwa na watakao kuwepo baada ya kupewa utume, na walio kuwa kwenye Bara arabu na walio kuwa nje ya sehemu hiyo (Bara la arabu).

Na hiyo ni sifa kubwa ya pekee, manabii walio tangulia hawa kupewa sifa hiyo, na wajumbe (ma Rasuli) wa mwanzo hawa kukirimiwa kwa sifa kama hiyo, kwani kila mmoja kati yao alitumwa kwa watu fulani maalumu na kundi fulani la wanadamu, na kwa muda maalumu, kama ambavyo Quran ilivyo eleza wazi kuhusu swala hilo. Amesema Mwenezi Mungu:

( ) Hakika Nuhu tulimtuma kwa watu wake. ( ) Na watu wa Thamud tuliwatumia ndugu yao Swaleh.

(  ) Na tulimtuma Mussa na dalili zetu (kwenda) kwa Firauni na wasaidizi wake.

( )

(Kumbuka) pindi Issa mwana wa Maryam alipo sema: Enyi wana wa Israil! Hakika mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu.

Na kutokana na hayo inatuwia wazi kuwa Nuhu alitumwa kwa watu wake, na Swaleh alitumwa kwa watu wa Thamud na Mussa alitumwa kwa Fir-auni na wasaidizi wake na Issa kwa wana wa Israili, na Muhammad pekee amejitenga kwa kutumwa kwake kwa watu wote.

Ama dalili na uthibitisho ya kwamba ujumbe wa mbinguni ulio utangulia uislamu ulikuwa ni kuwepo kwake kwa muda maalumu na zama zilizo pangwa na kuwekewa mipaka, unathibitika kwa kufutwa sheria za awali na sheria zilizo kuja baada yake, kiasi kwamba hukumu za mwanzo zinatoweka na mahala pake zina kaa sheria mpya, kwa kutokuwa mwanadamu na uwezo wa kukusanya kati ya aina mbili za sheria zenye hukumu nyingi zinazo tofautiana na kupingana maneno kadhaa kati ya maneno ya sheria zile.

Na hayo ndio tunayo julishwa na dalili ya kiakili na hali ya maumbile na hukumu ya badaha (uwazi wa mambo hayo).

Na mayahudi walijaribu ili kuifanya sheria ya ujumbe wao iwe ni yenye kuendelea na kubakia na kupinga fikra ya kufutwa kwa sheria, na kuwa jambo hilo haliwi[5] kwa kudai kuwa kusema hivyo ni sawa sawa na kusema kuwa Mwenyezi Mungu ni mjinga na kuwa hana hekima, na dalili ya shubha yao hii ilikuwa ni kwamba kuwekwa kwa sheria na Mwenyezi Mungu au hukumu ni lazima ifuatane na maslahi yapelekeayo kuwekwa kwa hukumu ile, kwani kuwekwa hukumu bila ya kuwepo maslahi yoyote ni aina moja wapo kati ya aina za mchezo (kufanya kitu bila lengo lolote), na hilo ni jambo linalo pingana na hekima ya Mwenye hekima yeyote.

Na kwa msingi huu kuifuta hukumu iliyothibiti na yenye maslahi inakuwa ni kinyume cha hekima, kwani katika kuifuta hukumu ile ni kuyafanya maslahi yale yawapite wanadamu, ila tu ikiwa muweka sheria baada ya kuiweka sheria ile atagundua ya kwamba ni hukumu isiyo na maslahi na akaifuta.

Na maana ya maneno haya ni kumnasibishia ujinga Mwenyezi Mungu kwa kuweka sheria ya kitu fulani aliyo kuwa akiitakidi kuwa inamaslahi kisha ikabainika tofauti na alivyo itakidi.

Na kutokana na matokeo ya kusema kuwa sheria inaweza kufutwa, ni kutokuwa na hekima mfutaji wa sheria au kuwa yeye haelewi lengo la hekima iliyoko kwenye sheria- na yote mawili hayo ni muhali kwa Mwenyezi Mungu- kwa hivyo kufutwa kwa sheria ni suala ambalo ni muhali kutokea.

Na jibu fupi la shubha hii ni kuwa:

Hakika hukumu za sheria zimetegemea na zimeambatana na maslahi, na maslahi mara nyingi hugeuka kwa kugeuka zama na huwa tofauti kwa kutofautiana zama za watu watungiwao sheria ile, huenda katika hukumu fulani kulikuwa na maslahi maalumu kwa watu fulani kwa muda maalumu akaweka sheria ile, kisha hukumu ile ikawa haina maslahi kwa watu wengine au kwenye zama zingine akaikataza na kuzuia matumizi ya sheria ile.

Pamoja na haya, ukiongezea kuwa akili ya mwanadamu iko kwenye hali ya kupanuka siku zote, na sheria za mbinguni -kama tunavyo fahamu- ilikuja polepole kulingana na ukuaji wa akili wa taratibu na kupanuka kwake, mfano wake ni kama ujuzi fulani tumpatiao mtoto kulingana na uweza wake wa ubongo na kiakili, kisha humuongezea ujuzi huo polepole hadi kufikia pale anapo komaa kiakili, na kumpatia nadharia na fikra zilizofungika na zilizo ngumu.

Na hali iko hivyo hivyo kwenye sheria za mbinguni zilizo letwa katika kila zama na kwa kila kaumu, ilikuja kulingana au ikiwa na maslahi ya zama zile na watu wale na ikija kulingana na kiwango cha ukomavu wa kifikra wa zama zile na watu wake, hadi kufikia kilele chake kwenye sheria ya kiislamu sheria ambayo Mwenyezi Mungu aliiteuwa iwe ndio sheria ya mwana-damu nae akiwa kwenye kilele cha maendeleo ya kiutamaduni na makuaji ya kiakili, na hayo hayana maana kuwa ni kutoelewa maslahi au kufunikwa jambo ambalo halikufahamika au kueleweka hapo kabla.

Kisha ni kuwa Taurat -yenyewe- imebeba ushahidi mwingi uthibitishao juu ya kutokea kwa ufutaji wa sheria, kama ilivyo-taja ruhusa ya kukusanya kati ya dada wawili (kuwaowa) kwenye sheria ya Adam na ruhusa hiyo ikaharamishwa kwenye sheria ya Mussa, na kama ruhusa ya kuchelewesha kutahiri hadi ukubwani katika sheria ya Nuhu na kuharamishwa hilo kwenye sheria ya Mussa, na mifano mingine mingi, mfano wa hiyo.

Kwa hivyo basi, haifai kusema kuwa ni muhali kufutwa sheria, na kauli hiyo haina dalili yeyote iitegemeayo, na kwamba waliyo yadai mayahudi katika suala hilo yamepingwa kwa ushahidi wa taurati baada ya ushahidi wa akili.

) (

Na mayahudi na wakristo hawata kuridhia hadi ufuate desturi zao (mila yao) sema: Hakika muongozo wa Mwenyezi Mungu ndio muongozo bora.

) (

Na mwenye kufuata dini isio ya kiislamu hatakubaliwa kamwe nae siku ya akhera atakuwa ni miongoni mwa watu wenye hasara.

Tumetangulia kusema kwamba dalili ya kuthibiti ukweli wa nabii yeyote katika madai yake ni kuleta au kufanya muujiza ambao viumbe wengine wanashindwa kuleta au kufanya mfano wake.

Mtume wetu Mtukufu (s.a.w) alikuwa na aina mbili za miujiza.

Wa kwanza ni: Quran tukufu.

Pili : Miujiza waliyo ishuhudia waislamu wa mwanzo ambao ni wengi sana, kisha habari zile zikanukuliwa kwa wingi sana na kuwa mutawatiri[6], na vikatungwa vitabu mbalimbali kuhusu suala hilo, na vitabu vikubwa vya hadithi vikajawa na riwaya hizo, na hadi leo bado husimuliwa na kupokelewa kwa hali hii na kunukuliwa  zikiwa mutawatiri pamoja na miaka kupita na zama kufuatana.

Na baadhi ya watunzi wajinga walijaribu kutia shaka kwenye miujiza hiyo, bali wengine walidai kuwa kwenye aya za Qurani kuna uthibitisho wenye kupinga miujiza yote ya Mtume Muhammad (s.a.w) isipokuwa Qurani, na kwamba Qurani ndio muujiza pekee alio kuja nao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) ili kuyathibitisha madai yake, na wakatoa dalili kuyathibitisha hayo kwa kauli ya Mwenyezi Mungu:

)                                (

Na hakuna kilichotuzuwia kuwatuma mitume kwa dalili (miuujiza) isipokuwa ni kuwa watu wa zamani (Waliotangulia) waliikadhibisha, kiasi kwamba walidai kuwa aya hii iko wazi kuwa Mtume (s.a.w) hakuja na dalili (Muujiza) zaidi ya Quran, na kwamba sababu ya kutoletwa miujiza hiyo ni kupingwa na watu wa mwanzo au kaumu zilizo tangulia kupinga na kukadhibi-sha dalili (miujiza) iliyo tumwa kwao.

Mwalimu wetu Ayatu llahi Imam Khui alijihusisha sana na kubatilisha shubha hii na kuonyesha aibu zake kwa kusema maneno ambayo muhtasari wake ni kuwa:[7]

Hakika makusudio ya miujiza ambayo aya tukufu imeyapi-nga na ambayo watu wa mwanzo waliyakadhibisha katika kaumu zilizo pita ni miujiza iliyopendekezwa na watu wale kwa Mitume wao.

Aya tukufu inatujulisha kuwa Mtume (s.a.w) hakuwajibu washirikina kwa kuleta miujiza  waliyo ipendekeza kwake, na haipingi kwamwe kuleta kwake au kutokea miujiza kwake, na lau kama upingaji wa wale wakadhibishao unafaa kuwa ni sababu ya kuzuwia kuletwa dalili au miujiza, upingaji huo ungekuwa kizuwizi cha kuletwa Quran vilevile, kwani hakuna sababu na dalili ya kuhusisha kizuwizi na baadhi ya miujiza bila ya kukihusisha na miujiza mengine na hasa kwa kuzingatia kuwa Quran ndio muujiza mkubwa kuliko miujiza waliyo kuja nayo mitume, na hili linatujulisha kwamba miujiza iliyozuiliwa ni aina fulani makhsusi, na sio miujiza yote kwa ujumla.

Pia ni kwamba, ukadhibishaji wa kaumu zilizo tangulia lau kama itasihi kuwa ni sababu ya kuzuwia kufanya kazi hekima ya Mwezi Mungu katika kuwatuma wajumbe kwa Miujiza, ingefaa pia kuwa ni sababu ya kuzuwia kutuma mitume, na ni jambo  lililo  wazi na badihi kuwa haya ni batili na yanayo kwenda kinyume na yanayotarajiwa vilevile.

Kwa hivyo imebainika kuwa utumwaji wa miujiza ulio zungumziwa ni mapendekezo ya watu. Na ni wazi kuwa wape-ndekezaji hupendekeza mambo yaliyo zaidi ya miujiza ambayo kwa kuletwa kwake hoja hutimia, na kiwango hiki cha dalili au miujiza si lazima kwa Mwenyezi Mungu kuileta toka mwanzo, wala si lazima kwake kuwajibu pale wanapo pendekeza kwa kutuma miujiza hiyo japokuwa hashindwi kufanya hivyo ikiwa maslahi yatakuwepo katika kufanya hilo.

Na juu ya msingi huu, mapendekezo ya watu huja na kuwa baada ya kutimizwa hoja kwao kwa kuleta muujiza au dalili inayo walazimu, na kuipinga dalili hiyo au muujiza huo, na ukadhibi-shaji wa kaumu zilizopita ulikuwa ni sababu ya kuzuwia kutu-mwa dalili au miujiza iliyopendekezwa, kwa sababu kukadhibisha na kupinga miujiza au dalili zilizopendekezwa hupelekea kuteremka adhabu kwa wakadhibishaji, na Mwenyezi Mungu amechukuwa dhamana ya kuondoa adhabu ya duniani kwenye umma huu kwa kumkirimu Mtume wake (s.a.w), na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:( )

Na Mwenyezi Mungu hakuwa ni mwenye kuwaadhibu na wewe uko miongoni mwao.

Ama kuhusu suala la kwamba kukadhibisha muujiza na dalili zilizo pendekezwa hupelekea kuteremka kwa adhabu juu ya wakadhibishaji, ni kwa kuwa dalili au muujiza wa Mwenyezi Mungu ukiwa umeletwa mwanzo kabla ya mapendekezo yao, unakuwa umeelekea na kujihusisha tu katika kuthibitisha utume wa yule nabii, na watu wakiukadhibisha matokeo yake ni kama matokeo ya kumkadhibisha mtume au nabii kwa kuadhibiwa siku ya mwisho.

Ama dalili na miujiza iliyo ombwa huweka wazi upinzani au inadi yayule alie ipendekeza na kuomba muujiza na upingaji wake kwani lau kama kweli angekuwa mtafutaji wa haki angeukubali na kuusadiki ule muujiza wa mwanzo kwani unatosheleza kuthibitisha linalo takiwa, na kwa kuwa maana ya kuomba kwake au kupendekeza kwake huku ni kwamba amejifunga (kuahidi) kumkubali yule nabii ikiwa atamjia na kumkubalia maombi yake au mapendekezo yake, na ikiwa ataikataa dalili na muujiza ule aliouomba baada ya kuwa umetokea, ana kuwa amemcheza shele nabii yule na haki ambayo yule nabii anailingania na kuwaitia watu.

 Kwa ufupi ni kuwa, hakuna dalili yoyote katika Qurani ya kupinga miujiza mingine isiyo kuwa Qurani, hata ingawa Qurani ndio muujiza mkubwa zaidi na wa milele wa Mtume (s.a.w) pamoja na kuwa na miujiza mingine iliyofanyika mikononi mwake.

Na upambanuzi wa kweli na sawa kati ya muujiza wa kweli na usio wa kweli, sio jambo jepesi na rahisi kwa kila mtu kama inavyo dhihiri kwa mara ya mwanzo bali hawawezi kutofautisha hilo isipokuwa wanazuoni wataalamu ambapo muujiza ule unakuwa katika kima cha kuelewa, kwa sababu wao ni wenye kufahamu zaidi na wenye kufahamu sifa zake maaulumu, nao ndio ambao wanaweza kutofautisha kati ya jambo wanaloshindwa watu kuleta au kufanya mfano wake na jambo ambalo wana uwezo nalo.

Kutokana na hayo tunakuta kuwa maulama walikuwa ndio wepesi zaidi kukubali muujiza ule. ( ) Hakika wamuogopao Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni.

Kwa sababu asie mwanazuoni hana uwezo wa kupambanua kati ya ukweli na uongo, na mlango wa shaka unabaki ukiwa umefunguliwa kwake maadamu bado atakuwa hajui misingi ya elimu ile, na maadamu bado atakuwa na matarajio na dhana kuwa mwenye kudai utume ametegemea misingi ya kielimu, na huenda misingi hii makhsusi, itakuwa  ni yenye kueleweka kwa watu mahsusi wenye ujuzi na utaalamu wa sanaa au ujuzi ule kwa hivyo akachelewa na kuwa mzito kuamini na kukubali. Na kwa sababu hii hekima ya Mwenyezi Mungu ilitaka kwamba kila muujiza wa kila mtume uwe ni wenye kufanana na elimu iliyo enea katika zama zake, na ambayo kuna watu wengi wenye kuitumia elimu ile na wenye ujuzi nayo katika watu wa zama zile, ili hiyo iwe ni sababu ya kuamini haraka na kukubali hukumu ya hoja ile, na kutokana na haya tunakuta kwamba wachawi katika zama za Nabii Mussa (a.s) ndio wali kuwa ni wepesi kuliko wengine katika kukubali kwa dalili na muujiza wa mtume wao, kwa sababu wao waliona kwamba aliyokuja nayo mtume wao yako kinyume au yako nje ya mipaka ya kielimu inayo julikana ya uchawi.

Na kutokana na ukweli  kuwa waarabu katika zama za kuteremka Qurani walikuwa wamefikia kileleni katika kutilia umuhimu kanuni za lugha na adabu zake na fani zake za ufasihi, ilikuwa ni lazima kutokana na hekima ya Mwenyezi Mungu, muujiza wa Mtume wa Uislamu (s.a.w) uwe sawa na hali hii iliyopo. Akaja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) kwa muujiza wa Qurani na lugha fasaha ili waarabu wote wafahamu kwamba haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyo safi, umepituka ufasaha wake wa hali ya juu uwezo wa mwanadamu na nguvu zake za kifikra na kiadabu (kifasaha).

   Pamoja na kuwepo miujiza mingineyo ya Mtume (s.a.w) kinyume cha Qurani na ambayo ni mingi kiasi cha kutoweza kuyataja kwenye kitabu hiki kidogo, lakini  Qurani ni muujiza mkubwa zaidi kati ya miujiza yote hiyo na yenye hoja madhubuti, kwa sababu muarabu asiejua elimu za maumbile na kanuni za ulimwengu anaweza kutia shaka kwenye miujiza ile na kuihusisha na sababu za kielimu ambazo hazijui zikiwa zimeta-nguliwa na uchawi ambao ndio sababu ya karibu zaidi kwenye akili yake ndogo lakini kutokana na kufahamu kwake fani mbalimbali za balagha na ufasaha na siri za maneno fasaha, hatii shaka juu ya  Quran kuwa muujiza na kwamba wanadamu hawana uwezo wa kuleta mfano wake.

Pamoja na kuwa ile miujiza mingine kubakia kwake ni kwa muda maalum, kwani haraka sana miujiza hiyo huwa ni habari au matukio yenye kusimuliwa tu na wapokezi wa riwaya, na ni mazungumzo yazungukayo vinywani mwa watu, na hapo hufu-nguliwa mlango wa kutia shaka na kuwa ni jambo la kukubaliwa au kupingwa.

Ama Quran ni yenye kubakia kwa muda wote ambao mbingu na ardhi zitabakia, na muujiza wake ni wenye kufanya kazi kwa kila kaumu na kila zama na uko wazi kwa kila mwenye macho mawili kwa karne zote na siku zote.

Na kila aliefikiwa na wito wa kiislamu, alifahamu ya kuwa Muhammad (s.a.w) ame waita watu wote na kaumu zote kwenye uislamu na kuwatolea hoja ya Qurani na kuwashinda kwa muujiza wake, na akawataka walete mfano wake hata kama wao kwa wao watasaidizana, kisha akashuka kidogo na akawataka walete sura kumi zilizo zuliwa mfano wa sura zilizomo ndani ya Qurani, kisha akawashinda kwa kuwataka wailete sura moja mfano wa zile za Qurani, lau kama waarabu wote pamoja na wanabalagha na wafasihi wange kuwa ni wenye uwezo wa kufanya hivyo, wangemjibu juu ya masuala haya na kuleta sura hizo na kuziangusha hoja zake kwa kuleta mfano wake, lakini wao walipo sikia Qurani wakakubali na kukiri suala hilo lililo tokea na kusalim amri kwenye muujiza wake, na wakafahamu ya kuwa wao hawawezi kuipinga, baadhi ya watu wakaamini na kutangaza uislamu wao, na wengine wakafanya kiburi na wakaendelea na upingaji na kuchagua njia ya vita na kutumia nguvu.

Na wanahistoria wanasimulia kwamba Waliid bin Mughira

Al-makhzumiy siku moja alipita kwenye msikiti mtukufu (nyumba ya Mwenyezi Mungu) akamsikia Mtume (s.a.w) akisoma Quran, akawa akimsikiliza kwa mbali kisha akenda kwa washiri-kina katika kaumu yake na miongoni mwa maneno aliyo wambia ni kuwa:

Hakika muda mchache uliopita nimesikia kutoka kwa Muhammad maneno ambayo si maneno ya binadamu, wala majini, na hakika maneno hayo ni matamu (mazuri) na yana-vutia, na kwamba juu yake kuna matunda na chini yake ni mazuri, na kwamba maneno hayo ni ya kiwango cha juu na hakuna maneno yawezayo kuwa juu yake. [8]Na Hisham binil Hakam anasimulia kwamba katika mwaka fulani wanafikra na wataalamu wa kanuni za lugha ambao ni wakubwa wanne wa zama zao walikusanyika kwenye msikiti mtukufu wa makka, nao niIbn Abil Awjaau, Abu Shaakir Addii Swaniy, Abdul-Malik Al-Baswarii na Ibnul-Muqaffaana watu hawa walikuwa ni wafuasi Dahriyya wenye kupinga kuwepo kwa Mwenyezi Mungu wakaingia katika mazungumzo ya hija na Mtume wa Uislamu, kisha wakakubaliana kuwa ni lazima wasimame kidete kuipinga Qurani ambayo ndio msingi wa dini hii, ili wauporomoshe muujiza wake kwa upinzani wao kwake na ushindani wao, na kila mmoja akachukua ahadi ya kuibatilisha robo ya Qurani, na waka weka siku ya kufanya kazi hiyo kuwa ni katika msimu ujao wa hijja, na pindi walipokutana katika muda maalumu kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu iliyo tukufu waka elezeana yale waliyo fanya.

Ibnu Abil-awjaau akawafahamisha kuwa yeye ameumaliza mwaka mzima akiifanyia utafiti na mazingatio jinsi ya kuipa muelekeo na kuigeuza kauli yake Mwenyezi Mungu.

( ) Yussuf:80.Basi walipokata tamaa naye walienda kando kunongona na hakuweza kutoa aya mfano wake, kama ambavyo Abdul-Maliki vilevile aliwafahamisha ya kuwa yeye ameumaliza mwaka wote akifikiria jinsi ya kushindana na kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

)                     (             Alhaji:74.Enyi watu!Umepigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale muwaombao badala ya Mwenyezi Mungu hawatoweza kumuumba nzi, hata kama watakusanyika na kusaidizana kwa jambo hilo. Na ikiwa nzi atawapokonya kitu, hawana uwezo wa kukirudisha amekuwa dhaifu kweli kweli huyu mtaka kurudisha na mtakiwa kupokonywa. Bwana yule hakuweza kuleta mfano wake, na hivyo hivyo alikuwa Abu-Shakiri kwenye aya isemayo :                                                             

)  :                                                                    (

Lau kama kungekuwa mbinguni na ardhini Miungu asie kuwa Mwenyezi Mungu, mbingu na ardhi zinge haribika. Kwani alishindwa kuleta aya inayo fanana na hii. Naye Ibnul-Muqaffa hakuwa ni mwenye bahati kuliko wenziwe. Nae aliumaliza mwaka wake huku akiwa ameshindwa kuipinga aya moja tu nayo ni:                                 

) (.Suratu Huud:44

Na ilisemwa: Ewe ardhi! Meza maji yako, na ewe mbingu zuwia kushusha mvua. Na maji yakatoweka na amri ikapitishwa (ya kuangamizwa makafiri) na Jahazi likasimama juu ya mlima juudiy, na ikasemwa: wameangamizwa mbali watu madhalimu.

Anasema Hisham, walipo kuwa katika hali hiyo (ya kuku-mbushana na kuelezea), ghafla akapita Jaafar bin Muhammad Assadiq (a.s) akawa angalia na akasema:

) ([9]

Sema hatakama watakusanyika watu na majini ili walete mfano wa Qurani hii, hawawezi kuleta mfano wake hata kama wao kwa wao watasaidizana. Na maadui wa uislamu pamoja na kuwa itikadi zao na fikra zao ni tofauti na falsafa zao na mifumo yao ni yenye kutofautiana, waliendeleza vita vyao dhidi ya muujiza huu wa Quran tukufu na kutia shaka kuwa ni muujiza na kwenye usahihi wa hukumu zake. Na maadui hawa -kwa karne zote hizo- walifanya, na bado hadi leo wanafanya mashambulizi ya kuweka fikra mbaya na kutia shaka, huku wakitoa nguvu zao zote na juhudi, ili kuyathibitisha malengo yao mabaya yasiyo kuwa na hesabu wala makadirio maalumu.

Na miongoni mwa shubha za mwanzo walizo zizua ni kurudia mara kwa mara kauli ya kuwepo kupingana kati ya aya za Quran, na hilo linapinga kuwa Qurani ni muujiza na linajulisha kwa dalili ya wazi kabisa - kulingana na madai yao- kuwa Quran imetengenezwa na binadamu na sio wahyi (ufunuo) utokao mbinguni.

Na madai hayo wakayatolea mfano wa aya zifuatazo:

) (.

Muujiza wako ni kuwa usiwasemeshe watu kwa muda wa siku tatu isipokuwa kutoa ishara. Eti kwamba inapingana na kauli ya Mwenyezi Mungu katika sehemu nyingine ya Qurani:

(   )Muujiza wako ni kuwa usiwase-meshe watu nyusiku tatu na hali wewe ni mzima. Kwani aya ya mwanzo imeweka muda wa siku tatu wakati ambapo aya ya pili imeeleza wazi na kupanga muda wa nyusiku tatu.

Katika kubatilisha shubha hii yatosha tuka ashiria kwamba tamko Al-yawmu katika lugha ya kiarabu hutamkwa na makusudio yake ya kiwa weupe wa mchana tu. Kama kauli ya Mwenyezi Mungu inavyo sema: ( ) Aliwapelekea huo (upepo) juu yao kwa masiku saba na michana minane na hutamkwa na kukusudiwa siku yote usiku na mchana wake kama kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

 ( ) Pumzikeni (stareheni) majumbani mwenu kwa muda wa siku tatu. Kama ambavyo tamko Allailupengine hutamkwa ukikusudiwa muda wa kuzama jua kama kauli ya mwenyezi Mungu isemayo: ( )Na ninaapa kwa usiku ufunikapo (vitu kwa giza lake). Na kauli isemayo:

       ( ) Masiku saba na michana minane. Na pengine hutamkwa kwa maana ya giza la usiku na weupe wa mchana, kama kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

       ( )O! Na (kumbukeni) tulipo muahidi Mussa (a.s) siku arobaini. Na kwa kuwa matumizi ya tamko allailu na annahaaru katika maana hizi mbili yanafaa na ni sahihi katika lugha, basi hakuna kupingana au tofauti ya maana katika aya hizi mbili, kwani matamko haya mawili yametumika kwa maana zote, weupe wa mchana na giza la usiku. Na katika aya hizi hakuna kitu kinacho leta shubha kama si kuelewa vibaya au kuwa na lengo baya kwao.

) (.

Kwa nini hawaifanyii mazingatio Qurani? Lau kama ingekuwa inatoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu wangekuta ndani yake khitilafu nyingi.

Na pamoja na kuwa Quran ni muujiza kwa mfano wake wa kibalagha wa kiwango cha juu kabisa, na ubainifu wake ulio fasaha ambao mwanadamu hawezi kuleta mfano wake na uwiano wake wenye kupendeza ulioepukana na aina yoyote ya kupishana au kupingana au kutofautiana, vile vile kunapande zingine za muujiza zilizo muhimu pia, na huenda upande uliodhahiri zaidi na wenye kushangaza na wenye kuthibitisha madai yetu ni aina ya maarifa ya ulimwengu yaliyo fichika aliyo yaweka Mwenyezi Mungu ndani ya muujiza huu, vitu ambavyo havitupi uwezekano wa kudhania kuwa Qurani hii imetoka kwa viumbe walio ishi kwenye zama zile, na hali ya kuwa hawakuwa na njia ya kuwawezesha kuyafahamu mambo haya.

Na pamoja na kukiri na kukubali kwetu kwamba Qurani tukufu ni kitabu cha dini na itikadi na sheria, na sio kitabu cha elimu ya sayari au kemikali au fizikia, lakini tunapo kipitia tunaona katika aya zake nyingi habari nyingi madhubuti na za kitaalamu kuhusu kanuni za ulimwengu na mambo ya kima-umbile, mambo ambayo haikuwezekana kuyafahamu katika zama zile isipokuwa kwa njia ya wahyi utokao kwa Mwenyezi Mungu.

Qurani ilitumia mfumo wa hekima sana katika kuelezea siri hizi, baadhi ya siri akazielezea wazi kwa mfumo mzuri ambao unafaa na aliziashiria zingine ambazo sehemu ambayo kulihitajia kuashiria tu kwa sababu baadhi ya mambo yale yalikuwa mazito sana kwa akili ya watu wa zama hizo kuyafahamu, kwa hivyo ilikuwa ni busara kuyatolea ishara itakayo wafanya watu wa zama zijazo wayafahamu pindi elimu itakapo panuka na ukweli kuwa wazi, na katika hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

) (

        Ambae amekufanyiyeni ardhi kuwa  tandiko. Kwani aya hii tukufu ina ashiria kuhusu mzunguko wa ardhi, ishara  ambayo haikufahamika isipokuwa baada ya kupita karne  nyingi. Na iliazima neno Al-mahdu ili kuelezea mtikisiko na harakati ya ardhi. Na Quran ili ashiria ukweli huo kwa ishara isiyojulikana na hakulielezea kwa uwazi, kwa sababu watu walikuwa na rai ya kuwa ardhi imetulia, na hili lilikuwa ni jambo la wazi na badaha ambalo halina mjadala wala majibizano, bali kauli ya kuwa ardhi inazunguka katika nadharia zao ni sawa na mambo ya kipuuzi na ambayo ni muhali kuwapo.

Na sisi tutatoa sehemu ifuatayo mifano ya ukweli wa mambo hayo ya kielimu yaliyo tajwa na Quran tukufu mara ikiyaeleza wazi, na mengine kuyatolea ishara, na tunamuachia mwenye kutaka ufafanuzi zaidi arejee kwenye vitabu maalumu vyenye kushughulikia maudhui haya - navyo ni vingi  na vinapatikana- Na lengo letu hapa ni kuonyesha baadhi ya mifano na ushahidi kwa kupita haraka kwenye mazungumzo na ili kukamilisha mfumo wa bahthi yetu.

Miongoni mwa ishara hizo za kielimu ni maelezo yaliyo kuja kwenye kauli yake tukufu :( ) Anakifanya kifua chake kuwa finyu (kutokana na kudhikika) kana kwamba anapanda juu mawinguni.

Kwani imethibitika kutokana na majaribio na baada ya mwanadamu kuvuka na kupaa kwenda  juu kwenye umbali tofauti kuwa kuruka angani na kuvuka matabaka ya juu angani, hukifanya kifua cha mtu kudhikika na kubana hadi kufikia kiwango cha kukosa pumzi katika umbali ambao Oxigen hupungua na kuwa chache.[10]

Na miongoni mwa ishara hizo za kielimu ni kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo: ( )Na tulizituma pepo zenye kuchavusha (kuhamisha mbegu za mimea)Na elimu ya kisasa inasema kuwa :Hakika kazi ya uchavushaji (Pollination) ni ya aina mbili: Ni ile ya kibinafsi ya mmea kujichavusha wenyewe. Na ya mchanganyiko kwa kupitia uhamishaji mbegu za uzazi (Chavuo) za mmea (Pollen) kutoka kwenye mmea hadi kwenye vijiyai vya mmea mwingine, na ni lazima kuwepo nyenzo zihamishazo mbegu za uzazi, na huenda ukawa uhamishaji huo ni wa sehemu ya mbali sana, na nyenzo muhimu kati ya hizo ni upepo. Bali kuna aina fulani ya mimea ambayo hazikutani mbegu hizo za uzazi bila kutumia nyenzo ya upepo.[11]

Na miongoni mwa ishara hizo ni yale yatiwayo mkazo na wanajimu (Astronomers) ya kwamba jua kama nyota nyingine yeyote, ni lazima ipatwe na hali ya kuzidi kwa ghafla kwa joto lake na ukubwa wake na miali yake kwa kiwango ambacho akili haikubaliani nacho, na wakati huo anga lake la nje linapanuka kutokana na kubeba moto na moshi hadi kuufikia mwezi, na hapo mfumo wa jua (Solar system) wote huingiwa na kasoro katika uwiano wake.

Na kila jua katika mawingu ni lazima lipitie kwenye hali kama hii kabla halijafikia kwenye kiwango chake cha daima, na jua letu lenyewe bado halijafikia mzunguko, na kutokana na haya inatuwia wazi kwamba maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu katika kuelezea ni lini itakuwa siku ya kiama na kuisha kwa ulimwengu:

 

 

 )

 (  [12]

Na pindi macho yatakaposhikwa na mshangao, na mwezi kushikwa, na kukusanywa jua na mwezi, siku hiyo mwanadamu atasema:Makimbilio yako wapi?

Na miongoni mwa mambo ya kweli ya kielimu yaliyotajwa na Qurani tukufu ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

( )Na mola wako alimfunulia (na kumfahamisha) nyuki kwamba jitengenezeeni majumba kwenye majabali na kwenye miti na katika vitu wavitandikavyo (na kuezekea dari ya nyumba zao).

Vituo vya kielimu vijihusishavyo na maudhui haya, vimetue-leza kwamba nyuki kwa mara ya kwanza alipo jitengenezea makazi, alitengeneza kwenye majabali, walikuwa wakiishi kwenye mapango na kuzaliana humo, kisha kukatokea maendeleo kadhaa kwa kuzingatia mazingira na sababu za kianga wakalazimika kuhama kutoka kwenye makazi ya majabalini na kuhamia mitini, na zilikuwa zikichagua miti yenye matunda na mashimo ili ziifanye ni nyumba na sehemu ya kuishi.

Na mwanadamu alipotaka kuwafuga kama alivyofanya kwa wanyama wengi akawatengenezea makazi yenye kufanana na makazi aliyo waona wakiishi ndani yake, na makazi hayo yalikuwa yametengenezwa kutokana na udongo, kisha akaendelea kuyafanyia marekebisho kwa muda wote na kutengeza makazi kwa kutumia vijiti vikavu na mbao, kisha akaendelea hadi kufikia kwenye makazi waliyo yaunda kwenye zama za leo.

Kwa hivyo basi kuteremka kwa nyuki au kuendelea kwake katika makazi kutoka kwenye majabali hadi kwenye nyumba yoyote iundwayo na mwanadamu, ndio mambo ambayo iyasema-yo Quran.[13]

Na miongoni mwa ukweli huo wa kielimu ulio  elezwa na Quran tukufu ni kuhusu ardhi, mambo ambayo yalikuwa hayajulikani, wanazuoni hawakuyafahamu isipokuwa kwenye miaka ya hivi karibuni iliyopitia, ya kwamba ardhi vyovyote itakavyo tofautiana katika aina zake, ina njia au mianya ambamo hewa hupita, bali kutofautiana kwa ukubwa wa njia au nyufa hizo na idadi yake, ndio sababu ya msingi ya kutofautiana aina ya ardhi, udongo au mchanga.

Na haikujulikana isipokuwa hivi mwishoni kwamba nyufa hizo zina hewa, na kwamba kuteremka kwa maji ardhini huipa msukumo  hewa kusogea mbele na kukaa sehemu yake maalumu, na kwa kukua elimu ya kemia na maumbile imefahamika kuwa udongo unapo ingiwa na maji hutanuka (expend) na kunywea (contract) pale unapokauka, na kwamba wakati njia au nyufa hizo za ardhini zinapo jawa na maji, chembe za udongo huanza kutembea kwa nguvu ya msukumo wa maji kwenye nyufa hizo kana kwamba ardhi ikipata maji hutaharuki na ukubwa wake kuongezeka, na imewezekana kupima kutaharuki kwa ardhi, pindi inapopata maji kama ambavyo imewezekana kufahamu kuzidi kwa ukubwa wake (kiwango chake).

Na uhakika huu ulithibiti, ambao huzingatiwa kuwa ni mato-keo ya maendeleo ya kielimu ya zama hizi, Qurani ilikuwa imeshatuelezea  katika kauli ya  Mwenyezi Mungu isemayo:

( )            Na utaiona ardhi ikiwa imetulia kimya lakini pindi tukitere-msha maji juu yake hutikisika (hutaharaki) na kukua na kuotesha mimea ya kila aina yenye kupendeza. Na mtikisiko ni ile harakati ya ardhi, na neno (rabat) ni kuongezeka kwa umbo lake. Na uhakika huu umepambanuliwa na kuelezwa kwa uwazi kutokana na hali ionekanayo kwenye baadhi ya majengo ya kisasa yenye kuanguka na kuporomoka au nyufa baada ya kunyesha mvua au jengo hilo kutokwa maji[14].

Na miongoni mwa uhakika  huo vilevile, ni yale yaliyo gundu-liwa na elimu ya kisasa kwamba: Minyeso (secretion) kwenye kiwiliwili cha mwanadamu ni ya aina mbili: Aina moja ina faida kwenye mwili wa mtu kama vile minyeso ya kuminginya chakula (digestive secretion). Na ya njia ya uzazi na baadhi ya minyeso ya ndani ambayo huwekea nidhamu vyombo au viungo vya mwili na aina zake. Aina hii ni ya lazima kwa ajili ya maisha na haina madhara yoyote.

Na aina nyingine haina faida kamwe, bali ni kinyume chake, inalazimika kuitoa kwenye kiwiliwili na kuitupa nje, kwa sababu imeundwa kwa chembe zenye sumu na ikibakia kwenye mwili itaudhuru, nayo ni kama mkojo na haja kubwa na jasho na damu ya hedhi.

Mwenyezi Mungu anaposema kwenye kitabu chake kitukufu:

) (.

Na wanakuuliza kuhusu wakati wa damu ya hedhi, sema wakati wa hedhi ni udhia, jitengeni na wanawake wakati wa damu ya hedhi. Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kutufundisha kabla ya elimu ya wanadamu haijafikia kiwango cha kuelewa kitu chochote kuhusu minyeso  kwamba damu ya hedhi ni maudhi, na kwamba haina faida yoyote kwenye mwili, kisha akawaamrisha wanadamu kutowakaribia wana wake wakati wa kutoa damu hiyo ya hedhi kwa sababu viungo vya uzazi vya mwanamke vinakuwa katika hali ya kusongamana kwa damu, na mishipa iko kwenye hali ya msukosuko, kwa sababu ya minyeso itolewayo na tezi za ndani (internal glands)

maingiliano ya kijinsia wakati huo yanakuwa na madhara, bali kufanya hivyo huenda kukazuwia kutoka kwa damu ya hedhi na kusababisha matatizo na misukosuko kwenye mishipa, na pengine inaweza kuwa ni sababu ya kuwashwa kwenye viungo vya uzazi.[15]

Na miongoni mwa uhakika huo vilevile ni kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo. ( . ) Nina- apa kwa vituo vya nyota, na hakika hicho ni kiapo kikubwa lau mngekuwa mnafahamu. Wanazuoni wa mambo ya Sayari (Wanajimu) wanatueleza ya kwamba umbali uliopo kati ya nyota na nyota unafikia kiasi cha kutatanisha au kuitatiza akili, na zinastahiki kwa Muumba kuapa kwa vituo vyake kwa sababu mfumo wa nyota ambao ni mfumo wa anga ambao uko karibu sana na sisi, uko mbali nasi kwa kiasi cha miaka elfu mia saba (700 elfu) ya mwanga, na mwaka wa mwanga ni sawa na kilometa milioni kumi.[16] Na uhakika  mwingine ulio ashiriwa na Quran ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

( ) Na tuliotesha kwenye (ardhi) hiyo kila aina ya mmea wenye kipimo maalum. Kiasi kwamba aya hii imetujulisha kuwa kila mmea una kipimo au uzito maalum, na hivi karibuni imegunduliwa kwamba kila aina moja kati ya aina za mimea, umetengenezwa kwa chembe maalumu na kwa kipimo mahsusi chenye mpaka, kiasi kwamba ikiwa kitazidishwa kiwango cha chembe zile au kupungua mmea ungeweza kugeuka kutoka kwenye hali yake ya kawaida, na kwamba kiwango cha baadhi ya chembe hizi jinsi kilivyo makini, kiwango ambacho ili kuelewa vilivyo kinahitaji kuwe na vipimo vilivyo madhubuti zaidi walivyo weza kuvigundua wanadamu.[17]

Na hivi ndivyo upande wa kielimu wa Qurani unavyo kuwa ni dalili ya kukamilisha upande wa kibalagha na ufasaha katika kutoa dalili wazi na yenye kukata ushauri kwamba Qurani ni kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho hakina shaka ndani yake, na ni muujiza wa dini hii itakayo bakia kwa muda wote ambao  mbingu na ardhi zita kuwepo.

) (

Hakika Quran hii inawaongoza (watu) kwenye njia iliyo nyooka kabisa na inawapa bishara njema waumini ambao wanafanya matendo mema ya kwamba wao wana malipo makubwa.

) (.

Ni utengenezaji wa Mwenyezi Mungu ambae kila kitu ame-kitengeneza katika hali ya umakini (na kukikamilisha). Hakika yeye ni mwenye habari za yale myafanyayo.

 

SHUBHA NA UTATUZI WAKE

 

Hapo mwanzo tuliwatanabahisha kwenye utangulizi wa kitabu hiki kwamba sisi hatukuielezea historia ya Mtume (s.a.w) iliyo nzuri na kuiandika sera yake yenye kumeremeta, bali tumewarejesha kwenye kitabu chetu kikubwa tulicho kiandaa na kukiita (Fiirihaabirrasul), na tuna taraji kuwa tutawafikishwa kukimalizia sehemu ya mwisho kwa muda mfupi ujao Inshaa-llah.

Lakini -pamoja na hayo- hatuwezi kumaliza mazungumzo yetu kuhusiana na utume kiujumla yaani wa mitume wote na hasa ujumbe au utume wa Mtume wetu (s.a.w), bila kuelezea nukta mbili muhimu ambazo haifai kwa mwenye kufanya utafiti na mwenye kuzama na kudadisi katika maudhui ya utume kuacha kuyaelezea na kutoondoa ugumu au shubha zilizo yazunguka masala haya, na hasa ukizingatia kuwa yameungana moja kwa moja na cheo cha utume na utukufu wa ujumbe wa mbinguni na kuepukana kwake kutokana na matamanio na ladha, na kutokana na ulimwengu wa mizigo ya maovu na madhambi makubwa.

Nayo ni masala kuhusu Kuoa wake wengi na Ismah yaani kuhifadhika na kutokufanya makosa.

Na msomaji yeyote hatapingana na mimi kwa dhana kubwa kuwa pande hizi mbili zinagusa cheo cha ujumbe wa mbinguni ulio takasika kuliko yanavyo gusa au kuhusika na sera (historia) ya Mtume Mtukufu. Na tutaandika kwenye kurasa zifuatazo muhtasari wa maudhui haya mawili kwa namna ambayo ina wiana na mtiririko wa utafiti huu, na kuwiana na njia na mfumo tulio uchagua wa kufupisha na kutilia mkazo kwenye nukta  muhimu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye mtoaji wa tawfiq.

 

KUOA WAKE WENGI

 

Miongoni mwa masala yenye umuhimu mkubwa katika maisha ya Mtume (s.a.w) ni masala ya kuoa wake wengi au kuwa na wake wengi, hadi kufikia kiwango ambacho maadui wa kiislamu, wakiongozwa na mustashrikina kupata upenyo mkubwa katika madai ya kuitia kasoro na kuharibu sura ya dini hii na Mtume wake muaminifu.

Na kabla ya kuingia kwenye maudhui yenyewe, ni vizuri kua-shiria kwamba mtu mwenye cheo au mtu mkubwa na mtukufu ikiwa kama atampenda mwanamke na akatamani kuwa na uhusiano nae, hilo si jambo la aibu, bali ni hukumu ya maumbile na mantiki ya maisha ya viumbe, na Mtume ni mwanadamu kwa hisia zake na tabia zake (anakula chakula na anatembea masokoni)[18] Sema: Mola wangu ametakasika, je sikuwa mimi isipo kuwa ni mwanadamu nilie tumwa (na Mwenyezi Mungu)[19].

   Hakika aibu iliyo kubwa ni kuvuka mipaka kwa mapenzi hayo hadi kumfanya mtu aache mambo yake mengine ya wajibu, na kumtoa kwenye hali yake ya usawa, na kumchukulia wakati wake wote na uchangamfu wake wa kazi.

Je adui yeyote kati ya maadui wa Mtume Muhammad (s.a.w)- mustashrikina na wengineo, anaweza kusema ya kwamba Muhammad (s.a.w) alishughulishwa na mwanamke fulami hadi kufikia kuacha kazi zake zote za wajibu hata kama kazi hiyo ni ndogo? Au kazi fulani yenye umuhimu mdogo, bali tukifanya utafiti hatutapata kwamba Muhammad (s.a.w) alifanya hivyo isipokuwa tutakuta kuwa aliupa utume haki yake na mwanamke alimpa haki yake pia, na hiyo ni dalili moja wapo ya utukufu wa mtu huyo adhimu.

Na kama kweli shahawa na matamanio yangekuwa yameuta-wala moyo wa Mtume, asingejulikana katika mji wa Makka kwa sifa ya kujistiri na mambo ya kijinsia na kuwa na haya tangu utotoni mwake, na angeweza kuoa tangu mwanzoni mwa ujana wake wanawake na mabinti wa kabila lake walio kuwa mabikra ambao walikuwa ni mashuhuri kwa uzuri ulio pita kiasi, na angeweza kujizuwia kuoa wanawake wengi hawa walio kuwa wamekwisha olewa, na wakiwemo miongoni mwao wenye umri mkubwa sana au walio kuwa wamekaribia kwenye uzee.

Hakika Mtume katika kuoa kwake alikusudia -katika baadhi ya nyakati- kuwa mkwe wa watu ambao watamuongezea nguvu katika kufikisha ujumbe wake na kumfanya awe imara zaidi, na wakati mwingine alikusudia kuwaonyesha baadhi ya wajane upole wake na huruma yake na kuwahifadhi wajane hao walio kuwa wamepatwa na misiba ya kufiwa na waume zao kwa sababu ya uislamu na vita vyeke.

Na kutokana na sababu hii au ile orodha ya wanawake walio olewa na Mtume ikawa kubwa, orodha ambayo maadui wa Uisla-mu waliiona kuwa ni dalili ya kuvuka mipaka kwa Mtume katika matamanio ya kijinsia na kusalimu amri mbele ya matamanio ya nafsi na tabia zake.

Na katika sehemu ifuatayo tutatoa  orodha ya wakeze mtume (s.a.w) ambao aliwaoa na kukutana nao kijinsia, na tutaelezea kwa ufupi kuhusu maisha yao, ili ibainike wazi na uonekane ukweli wa yale tuliyo yasema yakidhihiri wazi.

Wa kwanza: Khadija binti Khuwailid:

 

Mtume (s.a.w) alimfanyia biashara kiasi kwamba Khadija akamfahamu Mtume na Mtume nae akamfahamu Khadija, na akachukua uamuzi wa kumuoa akiwa tiyari amekwisha olewa mara mbili.

Na mtume alipo muoa Khadija alikuwa na umri wa miaka 25 na Khadija alikua na umri wa miaka 40, na mwana mke pekee kati ya wakeze Mtume kuishi na Muhammad (s.a.w) kama mumewe kabla hajapewa utume na Mwenyezi Mungu na akiwa mbali na mwanga wa utume na utakasifu wake.

Na inatosha kuwa ni jambo la kujifakharisha kwa Khadija kuwa yeye ndie aliekuwa mtu wa kwanza kuamini ujumbe huu na kutoa kila alicho kimiliki kwa ajili ya kuwalingania watu kwenye dini ya Mwenyezi Mungu.

Na baadhi ya maadui wa Uislamu walimzulia na kudai  kuwa sababu iliyompa msukumo Muhammad kumuoa Khadija akiwa amemzidi kwa umri wa zaidi ya miaka 15, ni tamaa yake aliyo kuwa nayo ya kutamani utajiri wa Khadija kwani yeye alikuwa ni masikini wa kupindukia, na kitu kinacho weka wazi ubatili wa madai hayo ni ile hali tuionayo ya Mtume (s.a.w) kumpenda Khadija na kumthamini kwa muda wote wa maisha yake bali Mtume alibakia akiwa na mapenzi makubwa kwa Khadija pamoja na kuwa tiyari kisha kufa na akimuheshimu, heshima na mapenzi ambayo wakati mwingine yalikuwa yakiamsha wivu kwa baadhi ya wakeze wengine.[20]

Je mapenzi haya na uaminifu kama huu unawiana na uoaji wa tamaa na kutaka maslahi? Hakika muumin huyu wa mwanzo alijipatia nafasi ya pekee kwenye Uislamu tofauti na akina mama wengine wa waumini kwa kuwa Mwenyezi Mungu alimpa utuku-fu wa aina ya pekee wa kukihifadhi na kukilinda kizazi cha mtume kiwe ni chenye kuendelea kupitia kwa Khadija na kwa kupitia binti yake kipenzi wa Muhammad[21](s.a.w).

Wa pili: Saudah binti Zumua:

Alikuwa mjane mwishoni mwa ujana wake. Mumewe ambae alikuwa ni muislam alifariki wakati Mtume alipokuwa Makka kabla ya kuhama. Na akaishi katika hali ya tabu za upweke na ujane, Mtume akamuoa ili kumuondolea taabu hizo mbili na kumpa utulivu wa moyo katika maisha yake ya uzeeni, na mume alikuwa ni Mtume Muhammad (s.a.w) , sio Muhammad mwe-nye kutafuta ladha na starehe.

 

Wa tatu:Aisha binti Abi bakar:

Binti na msichana mwenye umri mdogo. Nae ndie mwanamke pekee kati ya wake zake Mtume aliekuwa bikira. Mtume alimuo-lea Madina baada ya kuhama

Wa nne: Hafswa binti Omar binil-Khatab:

Mumewe alifariki kutokana na athari ya jeraha alilo lipata kwenye vita vya badri na Hafswa alikuwa tasa, Omar alikutana na Othumani na kumwambia amuoe binti yake, Othumani akasema: Sihitajii mwanamke, kisha akakutana na Abubakar akamtaka amuoe binti yake, Abubakar hakusema lolote, Omar akamkasirikia Abubakar, ghafla Mtume (s.a.w) akamposa na kumuoa[22] ni kana kwamba Mtume (s.a.w) alitaka kuwa badala ya mumewe aliekufa kwa sababu ya vita vya kiislamu, na kumuo-ndolea upweke wa ujane ambao baba yake alikuwa akimtafutia mume ili kumuokoa na upweke huo.

Wa tano:Zainab binti Khuzaimah:

Kabla ya kuolewa na Mtume alikuwa amekwisha olewa mara mbili. Na mumewe wa pili alikufa shahidi siku ya Badri, Mtume akamhurumia na kumuoa kwa ajili ya kumkirimu yeye na mumewe aliefariki hali ya kuwa hakukaa kwenye nyumba ya Mtume isipokuwa miezi minane kisha akafikiwa na kifo

Wa sita: Ummu Salamah:

Mumewe alijeruhiwa kwenye vita vya uhud, na jeraha lile likapoa hadi likakaribia kupona. Kisha akatoka na kikundi cha jeshi moja wapo kati ya vikundi vya jeshi alivyo kuwa Mtume akivituma, jeraha lile likajiachia na hali yake ikawa mbaya kutokana na jeraha lile hadi akafariki.

Na akamuacha Ummu Salamah akiwa na watoto wake. Mtume alimuoa kwa kumuonea huruma na kwa ajili ya kuwalea watoto wake, na hasa akizingatia kuwa mumewe alikuwa ni mtoto wa shangazi yake Mtume. Na Ummu Salamah alimuomba msamaha Mtume kwa kutokubali kwake kuolewa na Mtume kutokana na umri wake kuwa mkubwa na kuwa na watoto wengi. Mtume hakukubaliana na uombaji msamaha huo kwa sababu  lengo lake  la kumuoa ni kumlea kwenye utu uzima huo na kuwalea watoto wake.

Wa saba: Zainab binti Juhsha:

Ni binti wa shangazi yake Mtume (s.a.w) kwa mara ya kwanza aliolewa na zaidu bin Haritha aliekuwa mtumwa wa Khadija binti Khuwailid na akamtoa zawadi na kumpa Mtume (s.a.w) Mtume akamuachia huru na kumuita kuwa ni mtoto wake wa kulea na akafahamika kwa watu kwa jina la Zaidu bin Muhammad na akabakia akieleweka kwa jina hilo hadi ilipo teremka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

( ) Waiteni kwa nasaba za baba zao, na hapo ukabati-lishwa ubini wake na kutumiwa ubini wa baba yake wa kweli ambae alikuwa ni Haaritha.

Na Zaidu kumuoa Zainab kulitokana na utashi wa Mtume na ikafanyika hivyo, kama vile kwa kufanya hivyo alitaka kuweka au kusimamisha dalili ya kivitendo ya kuondoa tofauti na utabaka kwenye jamii ya kiislamu, kwa sababu hiyo akamlazimisha binti wa shangazi yake kumridhia Zaidu kama mumewe.Yule binti pamoja na kaka yake wakapinga suala hilo na kukataa. Na ilipoteremka aya isemayo:

) (

Muumini wa kiume na wa kike hawakuwa wenye hiyari Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo hukumu jambo lolote.

Wakalazimika kukubali kufanyika ndoa hiyo kwa lazima bila kutaka. Na ndoa ikafanyika kutokana na amri hiyo. Lakini ilifanyika kwa hukumu ya kulazimishwa, na haikuwa ni ndoa njema iliyo simama kwenye msingi wa mapenzi au kuelewana, bali Zainab mara zote akionyesha kuchukizwa na kutoridhia kwake ndoa hiyo na akimuonyesha mumewe Kiburi na majivuno kuwa Zaidu asili yake ni ya watu duni na kuwa yeye ana asili tukufu. Basi Zaidu hakuweza kuendelea kuishi pamoja nae na akaazimia kumtaliki ili kuepukana na matatizo hayo na mambo hayo yamtiayo unyonge.

Lakini alikuwa hawezi kumpa talaka bila kumtaka ushauri Mtume, na akamtaka ushauri Mtume, Mtume akamzuwia kufa-nya hivyo na akamwambia kama Qurani ilivyo tueleza:

( )Kaa na mkeo na muogope (mche) Mwenyezi Mungu. Kwani hata Mtume akielewa kuwa ndoa hiyo haitadumu hadi mwisho hata kama ataweza kuisimamisha na kuizuwia talaka kwa muda, na akaazimia kumuoa Zainab ikiwa Zaidu atamtaliki na kumuacha ili kuwa ni badala ya ndoa iliyo shindwa na yenye maisha ya chuki aliyo isababisha yeye mwe-nyewe.

Lakini yeye Mtume alikuwa akiogopa kufanya hivyo kutoka-na na maneno ya watu kuhusu suala hilo, kwa sababu waarabu wa zama hizo za ujahili walikuwa wakichukizwa na suala la mtu kumuoa mke wa mwanae wa kulea. Na mwishowe, Zaidu akateke-leza azma yake aliyo ikusudia na kumtaliki Zaina. Na hapo Mwenyezi Mungu akamuamuru Mtume wake kumuoa binti huyo ili kwa kufanya hivyo iwe ni kufuta au kuondoa ufahamu wa kimakosa ulio kuwa umeenea wa kuonekana kuwa ni vibaya mtu kumuoa mke alie pewa talaka na mwanae wa kulea, asie mwanae wa kweli. Na kuhusu suala hilo Mwenyezi Mungu amesema:

) (.

 Na pindi Zaidu alipo maliza haja zake kutoka kwake tukakuozesha binti huyo ili kusiwe na dhiki juu ya waumini kwa kuoa wake walio talikiwa na watoto wao wa kulea.

Na kutokana na hayo inaonekana kuwa ndoa ilifanyika kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika njia ya kudhihirisha hukumu ya sheria ambayo ilikuwa ni lazima kudhihirishwa, na ilikuwa ni utekelezaji wa kivitendo wa hukumu hiyo kwa kiwango cha juu.

Na baadhi ya maadui wa kislamu walijaribu na hasa wale mustashrikina kutengeneza visa au hekaya kuhusu suala hili, na wakadai kuwa Muhammad alikuwa amekwenda nyumbani kwa Zaidu akamuona mkewe Zaidi akavutiwa nae na akamhimiza Zaidi ampe talaka ili aweze kumuoa yeye.

Na madai haya ubatilifu wake uko wazi kwa yeyote mwenye kufanya mazingatio kwa sababu Zainab ni binti wa Shangazi yake Mtume na Mtume alikwisha muona na kumfahamu hata kabla Zaidu hajamuona. Na Lau kama angekuwa na mapenzi nae au kumtamani, angemuoa yeye mwenyewe na asingemlazimisha kukubali kuolewa na Zaidu.

Wa nane:Juwairiyah binti Haarith:

Alikuwa ni binti wa Sayyid na kiongozi wa bani mustalaq na mke wa mmoja wapo kati ya watu wa kabila lake. Kisha akashi-kwa mateka na kuletwa hadi madina na akawa ni sehemu ya fungu la mmoja kati ya waislamu akakubaliana na mtu yule ili ajikomboe kwa kumpatia kiasi fulani cha pesa, mwanamke huyu akaja kwa Mtume akimdhihirishia heshima (cheo) yake na kizazi chake na sifa zake alizokuwa nazo na hali aliyokuwanayo kwa hivi sasa, na akamtaka amsaidie kulipa kiwango kile cha pesa, na Mtume akataka kumfanyia huruma kutokana na hali yake na kumzidishia utukufu wake na kwa kufanya hivyo ili aweze kuwavuta watu wa kabila lake waingie kwenye uislamu, akamfa-hamisha kuwa atatoa kiasi hicho cha pesa ili kumkomboa na kumuonyesha kuwa yuko tayari kumuoa, akafurahi kwa kusikia hivyo furaha isiyo na kifani.

Na athari za tabia au tendo alilo lifanya Mtume, tendo lionyeshalo hekima ya utume, ilikuwa ni waislamu kufanya hara-ka kumuachia huru kila mateka au mtumwa walie kuwa nae, atokae kwenye kabila la mama huyu, mateka wote wakawa huru. Kwa kuzingatiya kuwa wamekuwa wakwe zake Mtume (s.a.w).

Wa tisa: Swafiyah binti Hayyi:

Aliolewa mara mbili na watu wa kabila lake la kiyahudi, na akashikwa mateka kwenye vita vya Khaibar, Mtume akamuoa ili kutoa mfano mzuri katika kuwa enzi mateka na kuwalinda au kuwahifadhi.

Wa kumi:Ummu Habibah binti Abi Sufyan:

Alikuwa ameolewa. Alihama pamoja na mumewe kwenda uhabeshi pamoja na waislamu wengine walio hama, na huko mumewe akaritadi nae hakumfuata wala kumtii mumewe katika utashi wake, bali alibakia pamoja na kuwa alikuwa ugenini- akiihifadhi dini yake na imani yake, na siku hizo akiishi uhabeshini katika hali ya machungu na maumivu, akiwa hana mume mwenye kumlea, wala mwenye uwezo wa kurudi Makka, wakati ambapo baba yake na ndugu zake na vijana wote au watoto wote wa familia yake walikuwa ni miongoni mwa maadui wakubwa wa uislamu na waislamu.

Na Mtume alipo elewa hali yake kwa uwazi akamtuma mtu kwenda uhabeshi atakae ongea nae kuhusu kuolewa na Mtume, nae akakubaliana na hilo, na akarudi Madina pamoja na Jaafar Bin Abi Twalib ili awe ni mmoja wapo kati ya wakeze Mtume na mama wa waumini, kwa kumkirimu kutokana na uvumilivu wake na kutotetereka kwake na kuvumilia maumivu katika njia ya kubakia kwenye Uislamu.

Wa kumi na moja:Maymunah binti Haritha:

Ni mjane mwenye umri wa miaka (49), alijitoa Zawadi kwa Mtume akimtaka amjalie awe mmoja wapo kati ya wakeze kama Quran ilivyo eleza wazi:

( )Na mwanamke muumini akiji-toa nafsi yake awe ni zawadi kwa ajili ya Mtume Nae Mtume akaitikia ombi lake akamuingiza kwenye idadi ya wakeze na Mama wa waumini.

Na baada ya hayo yote:

Je katika orodha hii kuna vitu au sababu za msukumo wa kutaka ladha ao shahwa, au kuna kitu kinacho toa msukumo wa matamanio ya nafsi na kijinsia katika kuoa wake wengi? Je mtu mwenye kuoa wanawake wengi wenye idadi kama hii kubwa wakiwemo wajane na wazee ni mtu mwenye kuitikia matamanio yake ya kijinsia?

Bali haiwezekani mtu kama huyu kuwa ni mtu wa kawaida bali atakuwa ni mtu alietumwa au kupewa ujumbe wa Mwenyezi Mungu, alie epukana na kila aina ya starehe za kimwili kwa kiwango cha juu, na mwenye kuhisi majukumu na upole na huruma na mapenzi ya kiutu yaliyo makubwa?!

 

***

 

 

ISMAH

(KUHIFADHIKA KUTOKANA NA KUTENDA MADHAMBI NA MAKOSA)

 

 

Hakika miongoni mwa mambo ya badaha (yaliyo wazi katika akili) ni kuwa Mtume hawi ni Mtume mwenye kupokea habari za mbinguni na kuzisimulia kwa watu na dini ambayo ni lazima kuitii, kuinyenyekea na kuikubali isipokuwa tu atakapo kuwa ni mwenye kuhifadhiwa pande zote hasa katika ukweli wa mazu-ngumzo, na asiwe ni mwenye kusahau na awe ni mwenye kujiepu-sha na maovu, na kujizuwia kufanya maasi ya aina yoyote, na kujifunga kwenye utiifu (utiifu wa aina zote zile) ili habari zake ziwe na zifikie kwenye kiwango cha kukubaliwa bila shaka yoyote na ziwe ni zenye kutoa yakini, ziepukane na mambo yaletayo shaka kwenye kauli zake na matendo yake na kazi zake mbali mbali zingine azifanyazo.

Na haya ndiyo yaliyo itwa na wanazuoni wa elimu ya akida kwa jina la Al-ismah. Na kwa msingi huu ismah ina kuwa na maana ya nguvu na uwezo wa ndani ya nafsi ya mtume inayo mlinda na kumzuwia na aina yoyote ya kuacha kutii amri za Mwenyezi Mungu au kufanya maasi au mambo mabaya au kusema kauli mbaya au matendo yake kuwa ni yenye kupingana.

Na pamoja na kufahamu nafsi ya mtume na kazi yake kwenye maisha yote kwa ujumla, inakuwa ni lazima kukubali na kukiri kuwa Mtume ni lazima awe maasumu (amehifadhika kutokana na kufanya madhambi na makosa) na kuamini hivyo au kusema hivyo ni kitu cha lazima kisicho na uwezekano wa kukiepuka, na kwa msingi huo fikra za shia imamiya zimekuwa zikitilia mkazo ulazima wa kuwepo Ismah na kuwa ni jambo ambalo halina mjadala kwani ni lazima liwepo.

Na shia akiwa yuko pekee kwenye kauli hii kati ya fikra zingine za (madhehebu) ya kiislamu ambazo hazikuona ulazima wa kuwatakasa mitume kwa aina hii ya utakaso, wakiwemo muutazila, watu watumiao akili, ambao pamoja na masisitizo yao juu ya Ismah (kuhifadhika) ya mitume kutokana na kufanya madhambi makubwa tu, wamesema kuwa inajuzu wakafanya madhambi madogo ambayo hayana athari yoyote isipokuwa katika kupunguza thawabu bila kuchukiwa au kuchukiza.[23]

Na kutokana na ukweli kuwa tuko kwenye kuelezea maudhui ya utume kwa mapana yake na kuweka tathmini ya nafasi yake ya kidini kwa kipimo sahihi, ilikuwa ni lazima kuzionyesha aya hizo zitoazo hisia au zipelekeazo kuyahisi hayo tuliyo yaelezea na kufafanua makusudio yake, ili jambo hili liwe wazi kwa kila alie changanywa na kuto  kulielewa jambo hilo, na kukata au kuzuwia uwezekano wa kuingia mazungumzo yenye shaka au shubha kwa kutumia hoja za kweli na yakini, na zenye ufahamu ulio sahihi.

Aya ya kwanza:

( )

Ili Mwenezi Mungu akusamehe madhambi yako yaliyo tangulia na yaliyo fuatia kwani wenye madai walidai kuwa kuhusishwa mtume na madhambi katika aya hii kume elezwa wazi bila uficho.

Hakika wafasiri wa Quran wametaja mielekeo mingi katika kubainisha makusudio ya tamko  dhambi, na muelekeo bora kati ya hiyo ni ule alio uchagua Sharifu Murtadhwa[24](rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu hake) na bwana huyu  ni mwenye nafasi ya kipekee katika elimu ya lugha na kanuni zake, yeye alisema kuwa makusudio ya neno dhambuka yaani madhambi ya kaumu yako kwako, kwa sababu neno Ad-dhambu ni masdari (chimbuko la maneno). Na masdari mara nyingine hudhifiwa (kuongezwa) kwa mtendaji (Faailu) kama tusema-vyo:Shairi lako limenifurahisha au adabu (ujuzi wa lugha) yako au utenzi wako, ambapo masdari imedhifiwa kwa mtendaji wake, na pengine hudhifiwa kwa mtendewa kama tusemavyo: Siku-pendezwa na kufungwa kwako au ugonjwa wako umenichukiza. Kwani masdari imedhifiwa kwa yule aliefungwa au alie ugua nae ni mtendewa.

Na neno dhambika katika aya limedhifiwa kwa mtendewa, na inakusudiwa dhambi aliyo tendewa Mtume Muhammad (s.a.w) kutoka kwa kaumu yake kwa kumshutumu na kumdharau na kumkadhibisha na kumpiga vita na maudhi mengine aliyo fanyiwa. Bali mtiririko wa aya hauwiani isipokuwa tukiitafsiri aya hiyo kama hivyo tulivyo sema. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

) (

Hakika sisi tumekupa ukombozi (wa mji wa makka) ulio wazi ili Mwenyezi Mungu akusamehe madhambi yako yaliyo tangulia na yaliyo fuatia na azitimize  neema zake kwako.

Hakika msamaha katika aya umekuja baada ya ukombozi, na ambapo  hakukuwa na ukombozi siku ya kushuka kwa aya kwani aya zilitelemka baada ya suluhu ya hudaibiya. Naye Mwenyezi Mungu aliita hii suluhu kuwa ni ukombozi kwa sababu ilikuwa ni njia ya kuelekea kwenye ukombozi wa makka na ilikuwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye ukombozi.Kwa  hivyo basi maana kamili ya aya hizi tukitaka kuzifafanua inakuwa kama ifuatavyo:

Hakika sisi tulikufungulia (tulikupa) wewe ukombozi ulio wazi ili Mwenyezi Mungu kwa ajili yako ayasamehe madhambi ya kaumu yako waliyo kufanyia na watakayo yafanya baada ya suluhu hii na mpaka utakapo timia ukombozi, na ili Mwenyezi Mungu azitimize neema zake kwako kwa ukombozi na ushindi mkubwa.

Na ikiwa Ad-dhambu ni madhambi yale aliyo yafanya Mtume (s.a.w) yeye mwenyewe kama ionekanavyo kwa watu wasio fanya mazingatio, basi je kuna uhusiano gani kati ya kusamehe madhambi na kuja kwa ukombozi? Na kwa nini msamaha uje baada ya ukombozi? Hatupati maana kwenye kufuatana huku kwa matukio haya isipokuwa ikiwa ukombozi unauhusiano na msamaha wa madhambi ya wale walio mkosea Mtume ambao mji wao utakombolewa kwa jeshi la Mtume na utawala wao na nguvu yao kuporomoka na hadhi yao ya kijahili kushuka.

Aya ya pili:

 

) . . (

Na kumbuka pindi ulipo kuwa ukimwambia yule ambae alineemeshwa ulipo mwambia: Shikamana na mkeo (kaa na mkeo) na umche Mwenyezi Mungu na ukiyaficha katika nafsi yako yale ambayo Mwenyezi Mungu ni mwenye (kutaka) kuya-dhihirisha (ya kwamba umuowe mke wa Zaidu bin Haritha) na ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndie mwenye haki ya kumchelea (Zaidi), na pindi alipo maliza haja zake kwake, tuka-kuozesha wewe.

Kwani watu fulani walidai kwamba katika  aya hii kunakemeo na lawama zimuelekeazo Mtume kwa yale aliyo kuwa akiyaficha  kwenye nafsi yake na ambayo alikuwa akichelea watu kuyaelewa.

Na aya hii kama waelewavyo wasomaji inahusiana na kisa cha Zaidu bin Haritha na mkewe Zainab bin Juhsha. Na tume-eleza kuhusu maudhui haya kwa upana zaidi kwenye kurasa zilizo tangulia. Na msomaji akifanya utafiti na mazingatio kwenye maudhui tuliyo yaelezea kuhusiana na suala hili, ataelewa maku-sudio ya aya hii na ataelewa mtiririko wa sentensi ya kuwa zinajulisha kitu gani, bila kupata ndani yake maana ya kulaumi-wa au kekemewa.

Aya ya tatu:

)        (

 Mwenyezi Mungu amekusamehe kwa kuwa umewapa wao idhini (ruhusa) hadi ikubainikie wale ambao ni wakweli na uweze kuwajua waongo, kwani baadhi walidai kuwa Mtume kuzungu-mziwa kwa kutumia sentensi isemayo Mwenyezi Mungu amekusamehe ni dalili ya kufanya dhambi (makosa) kwa kuzingatia kuwa msamaha haufanyiki isipokuwa ni kwa yule mwenye makosa.

Na ukweli ni kuwa maana ya aya hii haiwezi kuwa wazi kwa msomaji kabla hajasoma aya zilizo kabla ya aya hii au zilizofuatia na zilizo itangulia aya hii ambazo ndizo zikamilishazo maana yake na kuweka wazi makusudio yake, Mwenyezi Mungu amesema:

     )    ..   .. (

Laukama mali za vitani zingekuwa ni rahisi kupatikana, yaani zinapatikana kwa wepesi na ukaribu, na safari ingekuwa ya wastani (si ya mbali sana wala karibu sana) na haina taabu yoyote wangekufuata lakini mwendo umekuwa mrefu na wa mbali sana na wataapia kwa jina la Mwenyezi Mungu wakisema:Laukama tungeweza kupata silaha mali na ngao tungetoka pamoja na wewe, wanaziangamiza nafsi zao na Mwenyezi Mungu anafahamu yakuwa wao ni waongo, Mwenyezi Mungu amekusamehe kwa kuwapa ruhusa, yaani ilikuwa haipaswi kuwapa ruhusa hadi uweze kuwafahamu wale ambao wanasema kweli na uweze kuwafahamu waongo.

Hawakuombi ruhusa wale ambao wanamuanini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho kupigania njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi sana wa wachamungu. Hakika wakuombao ruhusa ni wale ambao hawa-muamini Mwenyeze Mungu wala siku ya mwisho na nyoyo zao ni zenye shaka, na wao wako kwenye shaka zao wakitahayari na kubabaika, lau kama wangetaka kutoka wangefanya maandalizi na kujiweka tayari kwa safari hiyo

Na kwa kufanya mazingatio kwenye aya hii tunakuta kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo Mwenyezi Mungu amekusamehe, haikuwa ni dhambi kwa maana ya kisheria yaani dhambi ya kukhalifu au kwenda kinyume na hukumu moja wapo kati ya hukumu za Mwenyezi Mungu, bali lengo la aya hii ni kumuongoza na kumueleza Mtume mfumo au njia ambayo angeitumia kuwaelewa wasemao kweli na waongo kati ya maswahaba zake (wafuasi wake ) ambao walitoa nyudhuru na sababu za kutoshiriki kwenye vita (jihadi).

Lau kama asingewaruhusu na kuchelewesha kufanya hivyo angewafahamu wale ambao walisema kweli na angewaelewa waongo, lakini kuwaruhusu kwake watu hao ambao walidai kuwa hawana uwezo wa kushiriki na kutoka kwenda vitani kulificha uhakika wa mkweli na muongo, kwani pande zote mbili zilitoa nyudhuru, kwa hivyo haikuwezekana kuwapambanua.

Aya ya nne:

( )Na alikukuta ukiwa umepotea akakuongo-za. Na upotevu ni kinyume na Ismah (kutotenda madhambi) bila ya shaka yoyote.

Na ukweli ni kuwa neno dhwalaal katika lugha lina maana ya kwenda na kuondoka na mtume alikuwa kama tunavyo fahamu hajui jinsi gani au vipi atamuabudu Mwenyezi Mungu, na vipi ataweza kutekeleza majukumu yake ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo alikuwa ameacha kufanya ibada kwa maana yake kamili hadi Mwenyezi Mungu alipo muongoza na kumjulisha jinsi ya kufanya hivyo kwa kumteremshia ujumbe wa kiislamu.

Na aya hii ni sehemu moja wapo kati ya silsila ya aya zenye kutaja idadi ya neema za Mwenyezi Mungu juu ya Mtume na malezi kamili aliyomfanyia.

) (.

Akakulea, na akakukuta ukiwa umepotea hujui jinsi ya kumuabudu mola wako akakuongoza,na akakukuta ukiwa fakiri akakutajirisha, ambapo aya hizi zinajulisha makusudio yake kwa uwazi kabisa, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuwekea Muhammad aliekuwa yatima mbadala wa kumuangalia na kumlea, na akiwa fakiri alimuandalia mtu atakae mpa na kumto-sheleza (kumtajirisha), kisha akamuongoza kwenye uislamu na jinsi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu baada ya kuwa alikuwa ameacha kufanya hivyo na hali ya kuwa alikuwa ni mwenye kubabaika hajui na akiwa hana muongozo wa namna ya kuabudu.

Aya ya tano:

( ) Na tukakuondolea mzigo wako. Neno wizri kama lifahamikavyo kwa watu wa kawaida lina maana ya dhambi. Na ukweli ni kuwa neno wizri katika lugha ni mzigo mzito au kitu kizito, na hivyo madhambi yameitwa kuwa ni awzaar kwa sababu humlemea na kumuwia mazito mbebaji wake na kumfanya  atoe juhudi zaidi.

Na (kwa kuyazingatia hayo) inakuwa kila kitu kinachomtia mwanadamu uzito na kumtia hima na kumfanya afanye juhudi ni wizri kwa kufananishwa na kitu kizito kikweli kweli kama ilivyo fananishwa dhambi na kitu kizito na kuitwa  kwa jina hilo la wizri vile vile.

Na kitu kilicho kuwa kikimlemea Mtume na kumtia uzito na kumfanya atoe juhudi na kumletea huzuni, ni yale mambo waliyo kuwa wakiyafanya kaumu yake, kama ushirikina na upotovu na kujiepusha na wito wa uislamu na kutokubali ujumbe wa Allah na kuwa dhidi ya dini aliyo tumwa nayo, ukiongezea kuwa alifa-nywa kuwa mnyonge mbele yao akiwa hana maandalizi wala watu wa kumsaidia na kuzuwia maudhi ya washirikina na shari zao. Na hii ndio wizri yaani huzuni nzito ambayo ilikuwa ikiulemea mgongo wa Mtume kwa maumivu na ghamu na kuathirika na hali hiyo.

Na huenda ushahidi wa wazi kabisa uonyeshao kuwa maana hii ndio iliyo kusudiwa kwenye aya, ni kufuatia baada ya aya hiyo, kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo:

( ߡ ǡ )                                     Na tukakuinulia utajo wako, hakika pamoja na uzito kuna wepesi. Kwani kuinuliwa utajo na kubainishwa kuwa kuna wepesi baada ya uzito, haviwiani isipokuwa itakapo kuwa makusudio ya wizri ni ile ghamu (huzuni) nzito aliyo kuwa akiibeba Mtume ikiwa ni matokeo ya kaumu yake kujiepusha na uongofu na wito wa uislamu na baada ya hayo yote.

Huu ndio utume kwa maana yake ya ujumla,ujumbe wenye mwangaza na uongofu uongozao na wenye nidhamu yenye kupendeza na nzuri kwa ajili ya maisha. Na huyu ndie Mtume wa mwisho alie tumwa kwa watu akiwa ni shahidi, mtoa bishara, muonyaji, mlinganiaji kwenye njia ya Mwenyezi Mungu kwa idhini yake na  taa iangazayo, na ambae hatamki kwa matamanio yake, bali ayatamkayo ni wahyi ushushwao kwake.

Na hatuna kitu kingine cha kuyamalizia mazungumzo haya isipokuwa tunasema: Ewe Mola wetu tumeyaamini uliyo yatere-msha na tumefuata Mtume basi tuandike pamoja na wenye kushuhudia.

Sifa zote anazistahiki Mwenyezi Mungu alietuongoza kwenye haya na hatukuwa ni wenye kuongoka kama si Mwenyezi Mungu kutuongoza.

 


 

[1] Rejea kwenye maudhui ya (kumfahamu Mwenyezi Mungu kupitia maumbile na dalili) Chapa ya Baghadad 1389 H -1969 na kitabu chetu (Hawaamishi ala kitaabi naqdul fikri ddiiniy) chapa ya bairuti 1391 H - 1971.

[2] Rejea kwenye maudhui ya kitabu chetu hiki (Uadilifu wa Mwenyezi Mungu kati ya kutenzwa nguvu na uteuzi (Utashi) 1390 H 1970 AD.

[3] Amewataja pamoja na kauli yao hii Imam Ghazali katika kitabu chake Al-mankhuli:13.

Na rejea kwenye kitabu: Madhaahibul-Islaamiyyin cha Dr Abdur-rahmaani badawi:Juzu 10/746.

[4] Majmaul-bahrain cha Tureihi,Juzu (1/405) Chapa ya Najaf 1378 H.

[5] Al-mankul cha ghazali 282-289

[6] Mutawatiri: Ni hadithi inayopokelewa na kunakiliwa na watu wengi sana kiasi kwamba wingi wao unazuwia shaka kuwa walikubaliana kudanganya.      

[7] Rejea kwenye kitabu-Al-bayaan fi-tafsiril-Quran Juzuu 1/76-79.

[8] Al-muujizatul-khalidah:21

[9] Al-Ihtijaaj:205

[10] Allahu yatajalla fi asril-ilm.Ukurasa 166

[11] Al-Quranul-kariim wal-ulumul-hadithah 81-85

[12] Allahu yatajallah fi-asril-ilmi-167.

[13] Al-Quranul-Kariim wal-ulumul-haditha 19-21.

[14] Al-Quran wal-ilmul-hadith 82-82

[15] Al-Islaam wattwibbul-hadith -40

[16] Allahu-yatajalla fi-Asril-ilm

[17] Al-bayaan Juzuu 1/54

[18] Aya za Qurani tukufu

[19] Aya za Qurani tukufu

[20] Imepokelewa kutoka kwa mwana Aisha mama wa waumini (Mungu amuwie radhi) ya kuwa amesema:Sikumfanyia wivu mwanamke yeyote kama nilivyo mfanyia wivu Khadija, na wala sikuwa nimewahi kukutana nae, lakini ilikuwa ni kutokana na Mtume kumtaja sana khadija, na wakati mwingine alikuwa akichinja mbuzi na kuwagawia marafiki zake Khadija kama zawadi.

Pia imepokelewa kutoka kwake (Mungu amuwie radhi):

Mtume (s.a.w) alikuwa hatoki nyumbani hadi amtaje Khadija na kumsifu kwa sifa nzuri, siku moja akamtaja nikashikwa na wivu na nikase-ma:Khadija hakuwa isipo kuwa bibi kizee na Mwenyezi Mungu amekubadili-shia na kukupa alie bora zaidi yake?! Mtume akakasirika hadi nywele zake za mbele zikawa zikitikisika kutokana na ghadhabu, kisha akasema:Hapana, nina apa kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, hajanibadilishia bora zaidi yake. Aliniamini watu walipokufuru, na kuniswadikisha (kuniku-bali) watu walipo nikadhibisha, na aliniliwaza kwa mali  yake pindi watu walipo ninyima, na Mwenyezi Mungu aliniruzuku watoto kutoka kwake pindi aliponinyima watoto kwa wana wake wengine.Akasema Aisha:Nikasema moyoni mwangu sintamtaja tena Khadija kwa ubaya kamwe. Rejea Kitabu Nihayatul-irab Juzuu la 17 Ukurasa 172.

 [21] Kauli iliyo mashuhuri kati ya wana historia ni kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa na mabinti wanne: Zainab, Rukayya, Ummu Kulthum na Fatima. Lakini utafiti wa historia haukubaliani na kauli hii mashuhuri, bali tukifanya uchambuzi wa kutaka kufahamu kuwa ni yupi binti wa Mtume, hatutampata mwingine isipokuwa Fatima na tutakata shauri kuwa ndie binti yake wa pekee. Na tunatoa hapa chini ishara fupi ya shaka hizo kwani nafasi haituruhusu kueleza zaidi:

A:ZAINAB.

Baadhi ya wanahistoria wanasema kuwa Zainab alizaliwa Mtume akiwa na umri wa miaka thalathini (Al-Istiiaab.Juzuu 4/292 na usudul-ghaba.Juzuu 5/467 pia Nihayatul-irab juzuu 18/211.Na aliolewa na Abul-aasi bin rabiibin Abdul-uza bin Abdis shamsi -nae ni mtoto wa shangazi yake- kabla baba yake hajapewa utume. Na akamzalia mtoto aitwae Ali (nae alifariki akiwa mdogo) na huyu mama, alisilimu pindi mama yake alipo silimu mwanzoni mwa utume,na uislamu ukamtenganisha kati yake na mumewe, isipokuwa ni kwamba Mtume alikuwa hawezi kutekeleza kwa matendo, amri ya kuwatenga-nisha, akabakia kwenye nyumba ya mumewe hali ya kuwa ni muislam, nae akiwa mshirikina.(Ili kuyapata yote hayo rejea Taarikh Attwabari, Juzuu ya 2/467-468 pia Twabaqat Ibnu Saad Juzuu 8/24, na Usudul-ghaba Juzuu 5/467 na Nihayatul-irab juzuu 18/211).

Ninasema: Hakika muhtasari wa tunayo fahamishwa na riwaya hizi ni kuwa, Zainab wakati wa baba yake kupewa utume, alikuwa na umri wa miaka kumi, je inawezekana binti huyu mwenye miaka kumi kuolewa na kuzaa watoto wawili? Akiwa na miaka saba kwa mfano? Au miaka nane? Kwa hivyo basi ni lazima Zainab awe ni binti wa Abu Haala mumewe Khadija wa mwanzo. Rejea Nihayatul-irab 18/171.

 

B: RUQAYYA:

 

C: UMMU KULTHUM:

Baadhi ya wana historia wamesema kuwa Ruqayya alizaliwa  Mtume akiwa na umri wa miaka 33 na dada yake Ummukulthum ni mdogo wake. (Al-Istiiab 4/292. Nihayatul-irab:18/212) Na wana historia wameku-baliana  kuwa mabinti hawa wawili waliolewa na Utba na Utaiba watoto wa Abi Lahab bin Abdul Mutwalib kabla ya kupewa utume, na wanasema kuwa walisilimu pindi mama yao alipo silimu katika siku ya kwanza ya utume. (Twabakat Ibnu Saad Juzuu 8/24-25). Na pindi Mtume alipo tangaza wazi wito wake wa uislamu Abu Lahab akawaamrisha watoto wake kuwataliki mabinti hao wawili, na akawataliki, Othumani akamuoa Rukayya na akahama nae kwenda uhabeshi pamoja na muhajirina wa mwanzo walio kimbia mateso ya washirikina. (Taarikh Attwabari Juzuu 2/330-331-340 na Nihayatul-irab 18/212 pia Al-iswab 4/297).

Ninasema : Je! yawezekana Rukayya kuolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka saba na kupewa talaka katika umri huu? Na je! Inawezekana kwa dada yake Ummukulthum kuolewa na kuachika nae akiwa hajavuka miaka sita kwa makadirio yaliyo makubwa?

 

[22]Twabakaat Ibnu Saad Juzuu 8/56-57.

[23] Madhhabul-Islamiyyin cha Dr Abdurrahman Badawi juzuu 1/478.Na pia rejea kitabu Al-mankuul cha Imamu Alghazaly:223-225.Kwani mtunzi amesema kwenye kitabu hicho kuwa Ismah ya mitume si wajibu, na akaongeza na kusema Hakika sisi tunasema kuwa inafaa kwa Mwenyezi Mungu kumpa utume kafiri na kumzatiti kwa kumpa miujizana muhakiki wa kitabu hicho akaongeza maelezo yake chini ya ukurasa huo na kusema: (Na marawafidhi wakapinga: (yaani Shia Imamiyya) wao wakasema kuwa haiwezekani pamoja na kuwa masala haya hayahitaji kurefushwa utafiti wake na kuzipambanua dalili zake, kutokana na tulivyo yataja kuwa ni masala yenye ubadaha (yaliyo wazi), na kwamba wujdani zetu (ufahamu wa nafsini) (Inner consciousness) zinashuhudia kwamba mtume ambae ana uwezekano wa kusahau na kuteleza au kufanya makosa, au maasi na mambo mengine mabaya haiwezekani kukubaliwa na kufuatwa kauli zake na haiwezekani kutiiwa amri zake na kujiepusha na makatazo yake.

Ninasema : Pamoja na hayo hakika maudhui haya yamechukua nafasi kubwa na kuandikwa kwenye vitabu vyote vya akida vyenye kujihusisha na masala haya, na sababu muhimu zaidi ya kuyadhihirisha na kuyatilia mkazo na umuhimu kwa kiwango hicho, ilikuwa ni kuwepo kwa baadhi ya aya za Qurani tukufu ambazo dhahiri ya aya hizo au ukiziangalia kwa juu huenda zikampatia mtu hisia ya kuwa Mtume (s.a.w) alifanya dhambi na kuasi. (kufanya maasi). Na muutazila wakasema, isipokuwa yale madogo (hawezi kufanya maasi makubwa).

[24] Tanzihul-Ambiyaa 117