back page

UTANGULIZI KWA KALAMU YA MURTADHA  HAKAMI

next page

 

بسم الله الرحمن الرحيم

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEM.

 

UTANGULIZI

 

    Umeandikwa na Ustaadh:Seyyid Murtadha Al-hakamiy.

 

     Unadhihiri ubora wa dini ya kiislam kwa kuwa kwake ni dini inayo kubaliana na maumbile na ni dini inayotegemea dalili.

Chimbuko la maarifa yake ni mtiririko wa maumbile.

     Huchukua maarifa yake kutoka kwenye maumbile, na hupata mafundisho yake kwenye chemchem ya maumbile.

Fikra zake hutokana na uchambuzi wa kimantiki na dalili, kila muislaam anapo shikamana nao, uwezo na nguvu zake za kimaumbile hukamilika, na huthibiti ndani ya nafsi yake, mazingatio na uwezo wa kidhati.

Na dini ya kiislamu humtengenezea mwanadamu dhati iliyo kamilika, na akili yenye kufahamu na moyo wenye uelevu, moyo ambao hufahamu ukweli na uhakika na humpa busara yenye kumsaidia kudiriki uongofu, na masikio yenye kudadisi na kuchukua yaliyo ya kheri, na ulimi mwema utamkao mambo ya kheri, na humtengenezea vitu vingi katika dhati yake, vitu amba-vyo huufanya utu wake ukamilike kiroho.

Na uislamu humuwekea muislamu kiongozi wa maarifa yote: Nae ni Imani ya Mwenyezi Mungu na kumuogopa, kama amba-vyo huifanya imani ya uadilifu wake kuwa ni sawa na moyo wake unao sawazisha kati ya mambo yanayo ufanya uhai ushamiri, na Imani ya ujumbe wake ni sawa na ufahamu wake upambanuao jema na baya, na hivyo Imani ya marejeo (yaani kiama) kumsisi-tizia moyoni mwake kuhisi kuwepo marejeo ya kudumu, kama ambavyo huifanya itikadi yake ya uimamu kuwa msingi wa kifikra, miongoni mwa misingi inayo ijenga  shakhsiya yake ya kiislamu katika ujenzi madhubuti, na kumtofautisha kimadhe-hebu tofauti iliyo madhubuti.

Nakila itikadi ya kiislamu huijenga shakhsiya ya mwislamu, na kila akida kati ya itikadi za kiislamu ina kuwa ni sawa na kiwiliwili kilicho hai ndani ya shakhsiya yake na athari zake huonekana katika maisha yake kifikra na kimwenendo.

Kwa hivyo basi Shekh Mohammad Hassan Aali Yassin amejitolea kufanya kazi ya kuijenga shakhsiya hii ya kiislamu na kuitengeneza ndani ya nyoyo za waislam, kwa vigezo vya ufahamu na maarifa yake katika vitabu vingi vilivyo vipana na vilivyo faulu kutokana na muelekeo wake wa kielimu udhihirishao ukweli.

       Na vilevile aliombwa na Marjiul A’ala (kiongozi wa juu wa kidini) Imam Khui kuingia katika uwanja huu wa jihadi kwani ni mwanafunzi wake alie bobea na akaharakia kuvieneza vitabu hivi vya kiislamu katika mizizi ya itikadi na misingi yake na kuzifanyia wepesi itikadi hizi ili kiwe ni chakula kitamu chenye kumuongezea muislamu ufahamu, na chenye kukidhi mahitaji yake ya kimaumbile ya kuhitajia itikadi ya dini.

       Kwa hivyo tunayatoa mafundisho haya ya kiislamu yenye kudumu kwa muundo mzuri, kwa usaidizi na uangalizi wa kiongozi wake wa dini na kiongozi wa madhehebu yake, na Allah ndie muongozaji kwenye njia iliyo sawa. 

 

                            Najaf , 13 Rajab 1392. 

                            MURTADHA AL-HAKAMIY.

 

 index