back page

SEHEMU YA KWANZA

next page

 

Sanadi (Silsila ya wapokezi wa hadithi)

Waislamu wanaafikiana kuhusu kuwepo kwa hadithi hii na maulamaa wa kiislamu wameinukuu kwenye vitabu vyao tofauti tofauti, vya hadithi, vya tafsiri (ya Qurani) na vya historia, kwa kuzitaja njia nyingi za wapokezi na sanadi zilizosahihi zenye kutegemewa.

Katika kitabu kiitwacho “Ghayatul Muram”, mwa-ndishi wake ametaja hadithi thalathini na tisa kutoka kwa njia za wapokezi wa kisunni na hadithi thamanini na mbili kutoka kwa njia za wapokezi wa kishia.([1])

Vile vile Allama Mir Haamid Husein(r.a) ameipo-kea hadithi hii kutoka kwa kikundi cha maulama wakubwa wa madhehebu yote, wanaokaribia baina ya tisini na mia, tangu karne ya pili hadi karne ya kumi na tatu.([2])

Naye seyyid Almuhaqqiq Abdul Aziz Attaba tabai (r.a) amemzidi kwa kuwataja maulama mia na ishirini na moja wa karne ya pili hadi karme ya kumi na nne.([3])

Kwa hivyo basi, idadi ya maulama wa kisunni walioinakili hadithi hii, imefikia mia tatu na kumi na moja.

Ibnu hajar katika kitabu cha Assawaiqul Muhriqa amesema kuwa “Na hadithi hii ina njia nyingi za wapokezi”.([4])

Hata hivyo hadithi hii imetajwa katika vitabu vyenye kutegemewa na vilivyo maarufu. Miongoni mwavyo ni Sahihu Muslim, Sunanut Tirmidhi, Sunanud Darami, Musnadu Ahmad, Ibnu Hanbal, Khasaisun Nasai, Mustadrakul Hakim, Usudul Ghaba, Alaqdul Farid, Tadhkiratul Khawaass, Dhakhairul uqba, Tafsiruth Tha’alabi na vinginevyo.

Hii, ni bila ya kuvitaja vitabu vyote vya kishia. Hata hivyo wameipokea hadithi hii, maswahaba wengi, wake kwa waume.

Ibnu Hajar amesema katika Assawaiqul Muhriqa kuwa “Hadithi ya tamassuk (yaani hadithuth thaqalain) ina njia nyingi za wapokezi, (zilizotufikia) kutoka kwa maswahaba zaidi ya ishirini”([5])

Kitabu cha Abaqatul Anwar kimeinukuu hii hadithi kutoka kwa vitabu vya kisunni kutoka kwa maswahaba thalathini na wanne, wake na waume.([6]) Bali idadi ya maswahaba wa kike na kiume inafikia zaidi ya hamsini ikiwa tutaongezea pia njia zote za upokezi za kisunni na za kishia zilizo tajwa katika vitabu vya Ihqaqul Haqq na Ghayatul muram na vinginevyo.

Haya ndio majina yao, kama ifwatavyo:-

1)     Amirul muumin Ali ibnu Abi Talib (a.s).

2)     Al-imam  Alhasan ibnu Ali (a.s).

3)     Salman Alfarisi.

4)     Abu Dhar Alghaffari.

5)     Ibnu Abbas.

6)     Abu Sa’id Alkhidri.

7)     Jabir Ibnu Abdillah Al-Ansari.

8)     Abul Haitham Ibnu Attaiham.

9)     Abu Rafi’I – mtumwa wa Mtume Mtukufu (s.a.w.a.)

10) Hudhaifa Ibnu Alyaman.

11) Hudhaifa Ibnu Usaid Alghaffari.

12) Khuzaima Ibnu Thabit Dhush shahadatain.

13) Zaid Ibnu Thabit.

14) Abu Huraira.

15) Abdullah Ibnu Hantab.

16) Jubair Ibnu Mut-im.

17) Albarrau Ibnu Aazib.

18) Anas ibnu Malik.

19) Talha ibnu Abdillah Attamimi.

20) Abdul Rahman Ibnu Auf.

21) Sa’ad Ibnu Abi Waqqas.

22) Amru Ibnu Al-aas.

23) Sahal Ibnu Sa’ad Al-ansari.

24) Udai Ibnu Hatam.

25) Uqba Ibnu Amir.

26) Abu Ayyub Al-Ansari.

27) Abu Shuraih Alkhuza’i.

28) Abu Qudama Al-ansari.

29) Abu Laila Al-ansari.

30) Dhamira Al-aslami.

31) Aamir Ibnu Laila.

32) Seyyidatuna Fati Matuz Zahra (a.s).

33) Ummu Salama.

34) Ummu Hani.([7])

35) Zaid Ibnu Arqam.

36) Ibnu Abi Dun-ya.

37) Hamza Al-Aslami.

38) Abdu Ibnu Hamid.

39) Muhammad Ibnu Abdur Rahman Ibnu Fulad.([8])

40) Abu Tufail Aamir Ibnu Waathila.

41) Amru Ibnu Murra.

42) Buraira.

43) Habashi Ibnu Junada.

44) Khalifa Umar Ibnu Alkhattab.

45) Malik Ibnu Alhuwairith.

46) Habib Ibnu Badlil.

47) Qais Ibnu Thabit.

48) Zaid Ibnu Sharahil Al-Ansari.

49) Aisha Binti Sa’ad.

50) Afif Ibnu Aamir.([9])

51) Abdullah Ibnu Umar.([10])

52) Ubai Ibnu Ka’ab.([11])

53) Ammar.([12])

Muhammad Mubin Allak-hanwi([13]) na waliyyullah Allakhanwi.([14])

Naye Alhaithami anaseme wazi ya kuwa wapokezi wa hadithi hii ni thiqa (waliyosifiwa kuwa wakweli katika upokezi wa hadithi) ([15]) pamaja na dalili nyingi nyinginezo zenye ushahidi juu ya usahihi wa hadithi hii na ya kuwa ni mutawatir (Yaani hadithi iliyo pokelewa na watu wengi sana, kiasi cha kutuondolea shaka kuwa huenda ikawa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) hakuwahi kusema maneno haya.)

Vile vlie kikundi kikubwa kimesema wazi kuwa ni hadithi mutawatir, miongoni mwao akiwa ni Assanani katika Kitabu chake, Mulhaqatul abhathul musaddada, aliposema, “Na riwaya zake (hadiththuth thaqalain) pa-moja na ushahidi zinazoutoa ni mutawaatir kimaana”([16]) (yaani kuwa riwaya zake zinatafautiana kamatamshi lakini zinapatana kimaana pamoja na kuwa ni nyingi sana).

Na kwa vyovyote vile, madhehebu ya kislamu yameafikiana kuhusu usahihi wa hadithi hii na wala hakuna chembe ya shaka kuwa imetoka kinywani mwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a).


 

([1]) Ghayatul muram; uk, 211.

([2]) Nafahatul Azhar Fi Khulasatil aqabatil an-war, uk: 199 – 200 Chapa ya kwanza mwaka wa 1414. H.

([3]) Nafahatul Azhar, uk 88 – 97.

([4]) Assawaiqul Muhriqa, uk 34.

([5]) Assawaiqul Muhriqa, uk: 230.

([6]) Nafahatul Azhar, uk: 227 – 236.

([7]) Hawa wote wametajwa katika Nafahatul Azhar uk: 227 – 236.

([8]) Wametajwa katika Ihqaqul haqq J: 23, uk: 161– 164”.

([9]) Wametajwa katika Ihqaqul haqq J; 23, UK: 161 – 164.

([10]) Biharul Anwar J; 37, uk: 190 – 191 kwa njia za wopokezi wa kisunni.

([11]) Biharul Anwar j: 38, uk 123.

([12]) Ghayatul Muram uk: 231 kwa njia za wapokezi wa kishia.

([13]) Nafahatul Azhar J:1, uk: 491.

([14])Nafahatul Azhar J:1, uk: 493.

([15]) Amenukuliwakutoka kwenye kitabu cha Faidhul Qadir. J:3, uk: 15.

([16]) Nafahatul Azhar j: 1, uk: 482.

    

index