back page

MAHDI  MTARAJIWA KATI  YA  TASWAWWUR  NA  TASDIQ

next page

 

 

(KUMFAHAMU  NA  KUMSADIKI)

 

Suratu-Zukhruf:61 ( )

 

Na hakika yeye ni alama ya Kiama.Muqaatil bin Sulaiman amesema na mufasirina wengine walio mfuata, hakika aya hii imeteremka kumhusu Almahdi.

Ibn Hajar Al-haitami As-shaafii: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:Surat Aswaf:9  ( )

Ili aidhihirishe juu ya dini zote, hata kama washirikina watachukia.Said bin Jubair amesema : Ni Mahdi atokanae na kizazi cha Fatima (a.s).

            Al-haafidh Al-Kanjiy As-shaafii.

 

***

 

 

UTANGULIZI

 

         Kwa jinala Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema

                                  Mwenye kurehemu.

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu kwa neema alizotoa na kutupa ilhaam. Na rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad na Ali zake wema.

Zilitolewa na kuzalishwa shubha na shaka kuhusu maudhui ya Mahdi mtarajiwa na kutawaliwa na majibizano, kati ya viku-ndi vya waislamu, hata baadhi ya waandishi na watunzi wa vitabu kufikia hatua ya kusema na kuona kuwa kumuamini Mahdi au fikra ya Mahdi ni sawa na kuamini mambo yaliyo pandikizwa yasiyo na ukweli au kuamini visa vya watu wa kale.

Kwa hivyo ilikuwa ni lazima kwa watafiti walio jihusisha na masomo ya kiislam, kutokana na hali hii, kuyaelekea na kuyafanyia utafiti maudhui haya, kwa kiwango kikubwa na kuyapa umuhimu mkubwa, na kuziandaa kalamu zao kwa ajili ya utafiti kuhusu masuala haya kwa uhuru kamili na uwazi, ili waweze kuondoa shubha zenye kutokea, na kuzibatilisha shaka zitokanazo na dhana, na kuyabatilisha madai yaliyo zuiliwa, na kuondoa pazia kwenye ukweli ulio wazi ili uweze kuonekana mbele ya watu wote kwa uhakika wake wa Uislamu au kama yalivyo kiuhakika wake ndani ya  Uislamu wenye kumeremeta na kutoa mwanga.

Na huenda kati ya watu kuna wanao dhania kwamba kuyazungumziya maudhui haya na mengine mfano wake ni miongoni mwa masala ambayo yanaweka kizuwizi cha kuleta ukaribu na kuelewana kati ya waislamu na kuchochea moto wa tofauti kati yao uzidi kuwaka na kulindima, na kwamba kuweka na kubakiza sitara au pazia kwenye mambo haya ni vizuri na ni jambo lenye manufaa zaidi, lakini kufikiria hivyo, kama ninavyo amini, ni dhana zisizo kuwa na ukweli na zisizo ufikia ukweli kwa aina yoyote, kwa sababu kuficha jambo haijawahi kuwa ni utatuzi wa matatizo kama haya, bali kufanya hivyo hakutatoa athari yoyote isipokuwa ni kuandaa mazingira mapana ya kupatikana dhana mbaya na kubobea hali ya kutofautiana na kuyachanganya mambo tofauti, kwa sababu hii kufanya utafiti wa makusudi kabisa kwa uwazi na ukweli ni jambo lenye athari ya upeo wa juu na lenye faida nyingi, kwani ukweli utadhihiri (uliokua haufaha-miki) na uongo wa kuunda na ulio zuliwa utakuwa wazi, na madirisha au nafasi za kutia shaka na kutoamini zitajifunga.

Na kutokana na haya, matarajio yangu kwenye kurasa hizi yalikuwa ni kwamba hizi kurasa ziwe hatua tuzifanyazo kwenye njia hii kuelekea kwenye lengo kubwa na ziweze kuwa juhudi zenye nia safi katika kujaribu kuleta  mtazamo ulio salama na mafundisho yaliyo wazi na kuziba nyufa.

Na katika kijitabu hiki sintakuwa na nafasi kubwa -kwani kinaandikwa kwa msukumo huu mtukufu na kutaka kulithibi-tisha lengo hilo la juu kabisa- isipokuwa ni kuyadhihirisha kwa ukweli na kutoa hukumu iliyo salama, na kufanya utafiti ulio epukana na matamanio na mapenzi ya upande fulani.

Na matarajio yangu yote ni kuwa msomaji mtukufu apate ndani yake dalili zitakazo ondoa wingu jeusi ambalo limetanda juu ya maudhui haya kwa karne zote zilizo pita na apate dalili zinazo weka wazi msimamo wa Shia Imamiyya kuhusu masala ya Mahdi na (kuhusu) fikira ya Mahdi.

Na himidi zote ni za Mwenyezi Mungu ambae alituongoza kwa hili, na hatukuwa ni wenye kuongoka lau kama si Mwenyezi Mungu kutuongoza.

Iraq-Al-Kaadhimiyya

 

MUHAMMAD HASSAN AALU-YAASIN.

 

***

 

Muhtasari wa maudhui tuliyo yamaliza kwenye utafiti wa Uimamu[1] ni kuwa Uimamu kwa hukumu ya Hadithi, Quran na Akili ni sehemu ikamilishayo ujumbe, na ni sehemu iufanyayo ujumbe wa kiislamu uendelee kuwepo, na kwamba dalili zote zilizo julisha ulazima wa kuwepo utume na uwajibu wake zinafaa kuzinukulu na kuzitumia kutolea dalili juu ya ulazima wa kuwepo uimamu, kwa sababu kuwepo kwa utume bila ya uimamu ni kuwepo kuliko  katika kusiko endelea, na hali hiyo inapingana na jengo la Uislamu lililo simama juu ya msingi wa kuendelea ujumbe hadi siku ya mwisho.

Kwa hivyo basi utume ni mwanzo wa uhai, na uimamu ni kuendelea kwa uhai ule na lau kama ingefaa kwetu kusema na kukubali utume bila uimamu, ingefaa kusema kuwa ujumbe wa Mtume una mtazamo finyu na wenye mipaka maalumu, hauku-weza wenyewe kujikadiria umri wa kuendelea kuwepo baada ya uhai wa Mtume wake, na haukuweka akiba kwa ajili ya kuyathi-bitisha malengo yake kwa kumteua Wasii ili aendeleze kazi na kuwepo kwa ujumbe wake.

Na ukweli ni kwamba, lau kama usia usingethibiti kutoka kwa Mtume (s.a.w) kwa njia ya riwaya na habari zilizo nukuliwa, hakika akili pekee ni yenye kuhukumu ulazima wa kuwepo usia na kuwa ulifanyika, na kwamba mtu yeyote miongoni mwetu haridhii kughibu na kuacha mali zake ziwezazo kutoweka au kufa na kuacha vitu mbali mbali hata kama ni vichache, bila kuzikabidhi mali hizi au zile kwa mtu alie muusia na muaminifu aziendeshe na kuzipangilia na kuzilinda.

Basi je ina juzu kwa Mtume wa Uislamu kuuacha urithi wake mkubwa, urithi ambao ni wa watu au wanadamu kwa zama zote, bila kumuweka wasii atakae uchunga na kuulinda urithi huu na kuuangalia kama inavyo stahili?!

Hakika mazingira yote yaliyo uzunguka Uislamu siku au wakati alipo fariki Mtume (s.a.w) yanatuita na kutulingania kuamini kuwa Mtume aliusia, na kwamba hakuliacha pandikizo lake lenye baraka jangwani, lipigwe na upepo mkali au joto kali lenye kuunguza au tukio lenye kulitokea, na kulifanya litoweke. Na hivyohivyo ina dhihiri wazi kuwa Shia Imamiyya hawakutoa maneno yahusianayo na kupinga kwao uchaguzi kutokana na hisia ya chuki kwa mtu fulani, au kutokana na rai yao  ya kisiasa kwa maana ifahamikayo na yenye kuenea ya siasa, bali waliona kwenye Quran na Hadith dhamana sahihi ya maisha na nyenzo ya ujenzi iliyo salama, na basi wakawa wamevutiwa katika kuunga mkono rai hii kwa roho ya imani juu ya Uislamu na ikhlasi kwa ajili ya malengo na kuhisi maslahi ya Uislamu.

Ali bin Abi Twalib (a.s) alikuwa ni Imamu wa kwanza alie thibitishwa kwa dalili kwani riwaya za Mtume (s.a.w) ni nyingi sana nani mutawaatiri kumhusu yeye, baadhi zikimuelezea wazi na zingine zikimuashiria. Na riwaya zote hizo pamoja na kutofautiana matukio yake na minasaba yake na mifumo yake zinalenga, kama tulivyo tangulia kusema, kwenye kitu kimoja nacho ni kumteua mwenye cheo cha uimamu na ukhalifa baada ya kufa kwake Mtume (s.a.w).

Na imamu wa pili alikuwa ni Hassan bin Ali . Na watatu ni Hussen bin Ali. Na wa nne ni Ali bin Hussen Assajad. Na wa tano Muhammad bin Ali Albaaqir. Na wa sita ni Jaafar bin Muhammad Asswadiq. Na wa saba Mussa bin Jaafar Al-kaadhim. Na wa nane Ali bin Mussa Al-ridhaa. Na wa tisa Muhammad bin Ali Al-jawaad. Na wa kumi ni Ali bin Muhammad Alhaadi. Na wa kumi na moja ni Al-Hassani bin Ali Al-askari. Kisha alikuwa Muhammad binil-Hassan al mahdi ndie Imamu wa kumi na mbili[2], na alighibu kwenye macho ya watu hadi Mwenyezi Mungu atakapo toa idhini ya kudhihiri kwake na kuujaza ulimwengu kutokana na yeye, uadilifu na usawa kama ulivyo jawa na dhuluma na ujeuri[3].

Na mishale ya kutuhumu na kupinga ikamuelekea Almahdy kwa nguvu zote na kwa kutia mkazo na kusisitiza, na maneno yakawa mengi kwenye maudhui haya ya ghaiba (kufichika na kutoonekana) hadi kufunikwa na mawingu mazito ambayo hayakuwezeshi kuona na kufahamu na kukupa uwezo wa kudadisi na kupambanua lililo sahihi, na watafiti wengi ambao ni wenye ikhlasi wakajiweka kando na maudhui haya kwa kuyakimbia matatizo yake na ugunu wake, na sauti za wapingaji zikaja juu na kusikika kwa kudhalilisha na kufanya istihizaa nazo zikidhania kuwa silaha yake iliyo simama kwenye msingi wa kufanya maskhara na kutoa hila kuwa ni silaha kali yenye kukata isiyo katwa na wala haishindwi.

Na hivyo ndivyo utafiti wa Almahdi na fikra ya kuwepo Almahdi ulivyo jitenga na kuwa mbali na mfumo wa kielimu ulio salama. Na ukawa si utafiti wa kimaudhui wenye amani na ikhlasi, na ukawa chini ya msukumo wa mapenzi ya nafsi yaliyo mbali na akili na mantiki.

Na kutokana na hayo ilikuwa mfumo wetu kwenye kijitabu hiki ni lazima ufuate upande na mfumo usiofuata mapenzi na uwe ni mfumo wa kimaudhui, ili tujiepushe na tofauti ambazo wengi walizitumbukia. Na mfumo huu utasimama juu ya msingi wa kuyagawa mazungumzo hayo sehemu tatu .

Sehemu ya kwanza inakusudia kuitoa fikra yenyewe ya (Mahdi) na jinsi mahusiano yake na Uislamu yalivyo, na sehemu ya pili inaelekea kumuonyesha na kumuainisha (Mahdi) kwenye dalili zilizo pokelewa za Mtume, na sehemu ya tatu inazungumzia maudhui ya uwezekano wa kughibu na kutoonekana, na dalili zake.

Na mwendo huu ulioandaliwa na ufanyao uchunguzi, kama ninavyo itakidi, utachukuwa dhamana ya kutoa ufafanuzi na kuweka wazi kiukamilifu mambo yatakavyo gundulika na kupatikana kwenye mwendo huu na matokeo yake, na kutoa ufahamu makini wa matatizo yake kwa uhakika wake na ukweli wake wa asili ulio mbali na mapenzi na matamanio na malengo mengine.

 

 

SEHEMU   YA  KWANZA

 

FIKRA  YA  KUWEPO  KWA  MAHDI

 

Lau kama tutavitupia jicho la haraka vyanzo vya historia, na hasa historia ya dini mbali mbali, tungeweza kuelewa na kuona kwa uwazi kuwa kumuamini au Imani ya  Mahdi sio jambo lihusikanalo na shia Imamiyya tu na sio katika mambo ambayo haya kuwepo kwenye dini na wao wakalizuwa, kama wasemavyo baadhi ya waandishi, bali jambo hilo sijambo lihusikanalo na waislamu peke yao na kutowahusu watu wengine wafuatao dini mbalimbali za mbinguni. Bali ukweli ni kuwa mayahudi na wakristo wana itakidi kuwepo kwa msuluhishi mwenye kutara-jiwa kuja katika zama za mwisho nae ni Eliya kwa mayahudi na Issa (Yesu) mwana wa Maryam kwa wa Kristo.

Kama ambavyo waislamu kwa ujumla, pamoja na madhehe-bu yao na vikundi vyao tofauti tofauti wanaamini hivyo kwani Shia Imamiyya (Ithina asharia) na kiisaniyya na Ismailiyya, wao wana amini kuwepo kwa Mahdi na wanasema wazi kuwa hilo ni katika mambo ya lazima ya madhehebu yao. Nao masunni wameamini vivyo hivyo (kuwepo kwa Mahdi) kwa kushikamana na rai hiyo kupitia maimamu wa madhehebu zao na wapokezi wao wa hadithi na baadhi yao wakadai kuwa wao ni akina Mahdi kama ilivyotokea Morocco, Libya na Sudan.

Na hivi ndivyo dini tatu za mbinguni (Uislamu,Ukristu na uyahudi) zinavyo kutana katika kuamini fikra hii ya Mahdi.

Na hivyohivyo mashia wanakutana na ndugu zao waislamu kwenye suala hili. Na wanaitakidi kuhusu Mahdi, mambo aliyo yasimulia Dr. Ahmad Amiin katika rai za masuni  kuhusu huyo Mahdi kuwa Yeye ni katika alama za kiama, na kwamba ni lazima adhihiri kwenye zama za mwisho mtu atokanae na kizazi cha Mtume, atakae iendeleza dini na kudhihirisha uadilifu na waislamu watamfuata na atayatawala madola ya kiislamu, na anaitwa Al-mahdi.[4]

Na kwamba rai yao kuhusu suala hilo ni kama rai ya Sheikh Abdul-Azizi bin Baaz, raisi wa chuo kikuu cha Kiislamu cha Madina pindi alipo sema:Hakika suala la Mahdi ni suala lenye kueleweka na hadithi kuhusu suala hilo ni mustafiidha (zimepo-kewa na wapokezi watatu kwenye kila tabaka) bali ni mutawaatir (wapokezi wake ni wengi sana) na zenye kuungana,  nazo kwa ukweli kabisa zina thibitisha kuwa kuja kwa  mtu huyu alie ahidiwa, ni jambo lililo thibiti na kutokea kwake ni jambo la Haki.[5]

Na kutokana na haya hakika fikra hii (fikra ya kuja kwa Mahdi) yenyewe ni sahihi kama asemavyo muandishi wa Misri wa zama hizi aitwae Abdul-Hasiib Twaha  Hamud.[6]

Lakini la kustajabisha na kuchekesha kuhusu suala hili, ni kuwa Abdul-Hasiib huyu hakugundua pale alipo isahihisha fikra hii kama ilivyo tangulia, ya kwamba alijipinga yeye mwenyewe, na alisahau kuwa alishawahi kutoa kauli ya kuwa:Fikra ya Mahdi ni mojawapo kati ya matunda ya itikadi za (dini ya) Sabaiyyah[7], nae kwa kusema hivyo anakusudia kuwa fikra hii imechukuliwa kutoka kwenye itikadi za mayahudi na haina mahusiano yoyote na Uislamu, hata ingawa hakusudii kwenye ibara yake hii isipokuwa kuwatuhumu Mashia ya kuwa wamechu-kua itikadi zao kutoka kwa mayahudi na kuwa hazina mahusiano yoyote na dini ya Kiislamu lakini kwa hakika amewatuhumu waislamu wote bila ya kutambua, kwa tuhuma mfano huo, na akazizingatia na kuzihesabu fikra alizoziita kuwa ni fikra sahihi hapo mwanzo kuwa ni moja wapo kati ya matunda ya itikadi za sabaiyyah, na huku ni kupingana kimaneno na kutetereka. Na ikiwa yatatujulisha juu ya jambo lolote maneno hayo, hapana shaka yanatujulisha nia mbaya na maradhi ya nafsi aliyo nayo, na hasa ukizingatia kuwa utafiti wa kihistoria wa zama zetu hizi umethibitisha kuwa hakuna mtu alieitwa Abdullah bin Sabai na kwamba huyu ni mtu alietengenezwa katika akili na kuundwa na akapambwa na kupewa sifa za kuwa ni mtu muhimu, na ana fikra fulani na ndie muwekaji wa itikadi na rai kadha, na huenda wale watu ambao walikuwa wakilirudia mara kwa mara jina la Abdullah bin Sabai mwanzoni mwa Uislamu walikuwa wakiku-sudia swahaba mtukufu Ammar bin Yaasir, kama wasemavyo baadhi ya watafiti.[8]

Na vyovyote iwavyo hakika natija ipatikanayo kutokana na utafiti wa kina na ulio safi usio na uchafu ni kuwa, Shia hawaku-zua fikra ya Mahdi, na wala hawakufuata itikadi ya dini ya Sabaiyyah au dini nyingine isiyo kuwa ya Sabaiyya, bali ni kwamba fikra ya kuwepo Mahdi ni fikra iliyo bashiriwa na dini tatu za mbinguni (Uyahudi, Ukristo na Uislamu), na kwamba Uislamu ulipotilia mkazo juu ya ukweli wa kielimu wa fikra  ya Mahdy waislamu walifanya haraka kuikubali na kuinukulu na kusalim amri mbele ya fikra hiyo kwa kukubali kikamilifu.

Na haiwezekani yote haya yawe ni kunyenyekea kwa kitu kiitwacho kwa jina la upotovu wa Shia na bidaa zao, bali ni kukubali na kunyenyekea kuliko sahihi kwenye ukweli utokanao na itikadi za Kiislamu na hadithi za Mtume (s.a.w).

Na mwanazuoni mtukufu wa kisuni wa Iraq, alitoa muhtasari wa ukweli huu aitwae Sheikh Swafau ddin Aalu-Shaykh Al-halkah na akasema: Ama Mahdi mtarajiwa, hadithi zilizopoke-lewa kumhusu zimefikia kiwango kikubwa na ni zenye kutuachia matumaini kwamba huyu atakuwapo zama za mwisho, na ataurudishia Uislamu usalama wake na imani, atairudishia nguvu yake, na dini atairudishia uzuri wake, nazo ni hadithi muta-waatir bila shaka yoyote wala shubha, bali inasihi kutumia sifa ya mutawaatir kwa zinginezo zilizoduni yake, kufuatana na istilahi zote zilizo andikwa kwenye elimu ya Usuul.

Ama athari tuzipatazo kutoka kwa maswahaba, zisemazo wazi kuwepo kwa Mahdi, ni nyingi sana zina hukumu ya Rafu (kuinuliwa hadithi bila kutaja baadhi ya wapokezi).

Hakika hadithi alizo zitaja Al-barzanji kwenye kitabu cha Al-ishaah Liasharaatisaaa, na Aalusi kwenye Tafsiri yake, na Tirmidhy na Abu Dawud na Ibnu maaja na Alhakim na Abu yaali na Tabaraan na Abdur-rrazaaq na Ibn Hanbali, na Muslim, Abu Naiim, na Ibn Asakir, na Bayhaqiy, na Al-khatiib kwenye historia yake na Daruqutniy na Rady aany, na Naiim bin Hamad katika kitabu Alfitan na Ibnu Abu Sheiba na Abu Naiim Al-kuufiy, na Al-bazzaz, na Dailamiy na Abdul-Jabbar Al-khulaniy kwenye Kitabu chake cha historia, na Aljuwainiy na Ibnu Habban na Abu Amru Addamiy kwenye sunani zake,  katika yote hayo kuna dalili za kutosha.

Kwa hivyo kuamini kutokea kwa Mahdi ni waajibu, na kuitakidi kudhihiri kwake ni kuzikubali na kuziswadikisha hadithi za Mtume (s.a.w).[9] Na wanazuoni wengi wa kiislamu walifanya haraka kukubali na kukiri fikra ya Mahdi na kuzisahihisha habari zake kwa kutunga vitabu na vijitabu vya kutoa fatwa na kufutu masala katika maudhui hayo ili vizazi  vijavyo viweze kufahamu suala hili na ukweli wake kama ilivyo pokelewa kwenye sheria kupitia kwa Mtume Mtukufu (s.a.w) na miongoni mwa waandishi hao wa maudhui haya, tukitaja baadhi kwa mfano, walikuwa ni:

1- Ubad bin Yaaqub al-rawajiniy alie kufa mwaka 250H. Ana kitabu kiitwacho Akhbaarul-Mahdi.

2- Abu naiim Al-Isbihaaniy alie fariki mwaka 430h. Ana kitabu kiitwacho Ar-baina hadithan fi amril-Mahdi[10] na kitabu Manaaqibul Mahdi[11] na kitabu Naatul  Mahdi.

3- Mohammad bin Yuusuf Al-Kanjy Ashaafiiy aliefariki mwaka 658 H, ana kitabu kiitwacho al-bayaan fi akhbari Swahib zzamaan, kimechapishwa.

4- Yuusuf bin yahya Assalmy Ashaafiiy alie fariki mwaka 685 H. Ana kitabu kiitwacho Uqad-Addurar fi Akh-baaril Mahdiyil Muntadhar.[12]

5- Ibnu Qayyim Al-jauziya aliefariki mwaka 751 H, ana kitabu kiitwacho Al-Mahdiy.

6- Ibnu hajar Al-haitamy Ashaafii alie fariki mwaka 852 H, ana kitabu kiitwacho Al-qaulul-mukhtasar fi alaamatil Mahdiy-Almuntadhar.[13]

7-Jalaalu ddin Asuyutwiy alie fariki mwaka 911 H, ana kitabu

Al-urful-wirdiy fi akhabaril-Mahdy kimechapishwa na kitabu Alamaatul-Mahdi

8- Ibnu Kamaal basha Al-hanafi aliefariki mwaka 940 H, ana kitabu Tal-khisul bayan fi alaamat Mahdiyyi Aakhiriz -zamaan.[14]

9- Mohammad bin tuuluun Ad-damash-qi alie fariki mwaka 952 H, ana Kitabu Al-muhdi ila ma-warada fil Mahdi.[15]

10- Aly bin Hussaamud-din Al-mutaqiy Al-hindiy alie fariki mwaka 975H, ana kitabu al-burhaan fi alaamati mahdiy Aakhiriz-zaman na kitabu Talkhiisul-Bayaan fi akhbari Mahdiy Aakhiriz-zaman.[16]

11- Ali Al-qaariy Al-hanafiy aliefariki mwaka 1014 H, ana kitabu Arrad alaa man hakama wa qadha annal Mahdy jaaa wa madhwa.

Na kitabu Al-mashrabul-wirdiy fi akh-baril Mahdy.[17]

12- Mar-ii bin Yusuf Al-Karamiy Al-hanbaliy alie fariki mwaka 1031 H, ana kitabu Faraidu-fawaidul-fikri fil Imamil-Mahdiyil-Muntadhwar.[18]

13- Al-Qaadhi Muhammad bin Ali Ash-shaukani alie fariki mwaka 1250 H, ana kitabu Ataudhihu fi tawaturi majaaa fil Mahdiy Almuntadhar wad-dajaali wal-masiih.[19]

14- Rashid Arrashid Atadhafiy Al-halabiy wa zama hizi ana kitabu Tanwiir Ar-rijaal fi dhuhuril-Mahdy wa dajjal kime chapishwa.

Hivyo hivyo washairi walikuwa pamoja na fikra ya mahdi na Mahdi mwenyewe, kwani kaswida zao zilikuwa na madhumuni na maana yaelezayo fikra hiyo na ambao ni wengi, na kaswida zao ni zenye kuelezea kutarajiwa kutokea siku yake, na kukiri kuja kwake kusiko na shaka na miongoni mwa washairi hao kwa mfano na kama ushahidi na sio kuwataja wote ni:

1- Al-Kumeit bin Zaid Al-asadi, aliefariki mwaka 126 H, na kuhusu suala hilo anasema:Ni wakati gani itasimama haki kwenu na wakati gani atasimama Mahdy wenu wa pili.[20]

2- Ismaail bin Muhammad Al-himyari alie fariki mwaka 173H, nae anasema kuhusu hiloNi kwamba Bwana wa utawala na mwenye kusimama (na kuleta mabadiliko) ambae nafsi yangu inamuelekea kwa kuimba, anayo ghaiba, ni lazima aghibu. Basi Mwenyezi Mungu amrehemu mwenye kughibu, atakaa kipindi fulani kisha atadhihiri kipindi kingine, na kuujaza uadilifu mashariki yote na magharibi.[21]

3- Daabal a-Khuzaiy aliefariki mwaka 246 H, anasema kuhusu hilo:Kutoka kwa Imamu hakuna shaka atatoka. Atasi-mama juu ya jina la Mwenyezi Mungu na baraka zake, na atatu-pambanulia haki na batili na atatoa malipo kwa neema na adhabu.[22]

4- Mihyaar-Ad-daylamy aliefariki mwaka 428 H, anasema kuhusu hilo:Huenda zama za kesho zikaiponya mioyo ya wenye ghadhabu kutokana na wenye kukufanyia uadui.

Huenda ushindi wa haki ukawa juu ya jambo lisilo wezekana, huenda upungufu ukashindwa na utukufu na ubora kwa kusikia kwangu wito wa huyo mtu wenu atakae simama akiitikiwa na kila mwenye kuomba msaada.

5- Ibnu Muniir Attaraabilsiy aliefariki mwaka 548 H, amese-ma kuhusu hilo kwa njia ya mzaha na utani Nimewatawalisha watu wa kizazi cha umayya walio safi watukufu na walio barikiwa na ninamkadhibisha mpokezi na ninatia ila kwenye kudhihiri kwa Mahadi.[23]

6- Muhammad bin Twalha Ashaafiy aliefariki mwaka 652 H, anasema:Na alisema Mtume (s.a.w) kauli tuliyo ipokea. Akaendelea hadi kusema Na hakika alimdhihirisha kwa kueleza nasaba yake na sifa zake na kumuita jina lake, na inatosha kauli yake kuwa anatokana na mimi kudhihiri uhai na maisha yake na katika pande la nyama yake ni Zahra ndio mahala pake na sharafu yake watakao sema ni Mahdi hawa kukosea kwa hilo walilo litamka.[24]

7- Ibnu Abil-hadiid Al-Muutazilii alie fariki mwaka 656 H, amesema kuhusu hilo: Hakika nimefahamu ya kuwa ni lazima aje Mahdi wenu, na siku ya kuja kwake ninaitarajia. Atahudu-miwa na vikosi vya jeshi la Mwenyezi Mungu, kama mtu mwenye maumivu amekuja akiwa ni mwenye ushindi na kikisonga mbele kizazi cha Abil-hadidi wa kiwa mashujaa na walio mashuhuri na mikuki iliyo inuliwa juu.[25]

8- Shamsud-din Muhammad bin Tuulun Al-Hanafy Ad-damsh-qiy aliefariki mwaka 953H, anasema kwenye kasida yake akiyataja majina ya Maimamu kumi na wawili:Na Askari Hassan alietwahirika Muhammadul-Mahdi atadhihiri.[26]

9- Abdullah bin Alawi Al-hadaad Attarimy Ashaafii, alie fariki mwaka 1132 H, na kuhusiana na hayo amesema: Muhammad Al-mahdi ni khalifa wa Mola wetu, Imam wa uongofu na dola lake linasimama kwa uadilifu kana kwamba namuona (siku hizo) akiwa baina ya maqaam na nguzo yake (yaani kati ya nguzo ya kaaba  na maqam ya Ibrahim) wakimpa baiya kila upande wenye kumpongeza. Na anasema katika sehemu nyingine: Na kwetu kuna Imam umefika wakati wa kutoka kwake, atasimama kwa amri ya Mwenyezi Mungu kama ipasavyo, na kuujaza ulimwengu kwa haki na uadilifu na uongofu, kama ulivyo jazwa jeuri kwa dhulma ya watu waovu.[27]

 

 

SEHEMU   YA  PILI

 

MAHDI  NI  NANI ?

 

Hakika Uislamu uliipinga rai ya mayahudi ya kuwa Elia ndie msuluhishaji mwenye kusubiriwa na pia rai ya wakristo isemayo kuwa yeye ni Issa mwana wa Maryam.Vilevile hali ya wazi ya matokeo ya nje imeipinga rai ya madhehebu ya kiisaaniya ya kuwa huyo mwenye kusubiriwa ni Muhammadi bin Alhanafiya na madhehebu ya Ismaailiyya, ya kuwa huyo ni Ismaail bin Jaafar kwani imethibiti kufariki kwa Muhammad na Ismaili na kubatilika fikra ya kubakia kwao. Basi imebaki tofauti na hitilafu kati ya Ahli sunna na Shia Imamiya katika kumuainisha Mahdi ni nani.

Na muhtasari wa itikadi za Ahli sunna ni kuwa Mahdi atadhihiri zama za mwisho na atasimama kwa upanga na kwamba Habari zake zimekuwa mutawaatiri (nyingi sana na zingine mustafidhi, kwenye kila tabaka kuna wapokezi wawili au watatu kwa wingi wa wapokezi wake kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuhusu kutokea kwake na kwamba yeye anatokana na kizazi chake Mtume, na kwamba atamiliki au kutawala kwa muda wa miaka saba.

Na kwamba ataijaza ardhi na ulimwengu kwa uadilifu, na kwamba atatoka pamoja na Issa (a.s) na kuwa yeye atawaongoza kwenye sala umma huu na Issa atasali nyuma yake.[28]

Na muhtasari wa itikadi ya Shia Imamiyya ni kuwa atadhi-hiri katika zama za mwisho Mahdi atokanae na nasaba ya Ali na atasimama kwa upanga, na kwamba ataujaza ulimwengu uadilifu na usawa na atatengeneza mazingira yawezeshayo kuutekeleza Uislamu kiukamilifu katika ardhi yote.

Kwa hivyo ni sehemu ipi yenye tofauti kati ya kauli mbili hizi?

Hakika kati yao imefungika kwa upande wa masunni kwenye kauli au kwenye itikadi yao ya kuwa, Mahdi huyu atazaliwa katika zama za mwisho, na hivi sasa hayupo, na haijulikani ni wakati gani atakao zaliwa na baba yake ni nani? Kwa msingi huu aliweza  Sunuusiy huko Libia na Abdul-Rahmaan wa huko Sudan na wengineo kudai kuwa wao ni akina Mahdi na kusimama kwa upanga (Silaha).

Ama Shia Imamiyya, wao rai yao ni kuwa Mahdi ni Muhammad bin Hassan bin Ali bin Muhammad bin Ali bin Mussa bin Jaafar bin Muhammad bin Ali bin Hussen bin Ali bin Abi twaalib (a.s) na kwamba yupo kwenye dunia hii lakini watu hawamtambui. Na hii ndio nukta yenye tofauti kati ya pande hizi mbili.

Kutokana na ukweli kuwa mwenye kutoa madai ndio huiti-shwa dalili ya madai yake, kama ilivyo katika fiqhi (sharia) ya kiislamu, basi sisi tutatoa ushahidi ambao wana utegemea Mashia kwenye kuthibitisha yale wanayo yaitakidi, na tutaonyesha usha-hidi mwingine walio utumia kuzibatilisha rai za wapingao fikra hii, ili jambo hili liweze kuonekana na kujulikana wazi kwa kila mwenye macho mawili. Na kutokana na ukweli kuwa mashia kama tulivyo eleza mwanzoni mwa maudhui haya kuwa wana amini kuwa uimamu ni cheo cha kupewa na Mwenyezi Mungu na kina hitajia dalili na uteuzi, wame amini kuwa uimamu wa Mahdi, Muhammad bin Hassan kufuatana na dalili zilizopo na kwa kuzitii dalili hizo, na kufuatana na matamshi yake yaliyo wazi kabisa.

Huenda kukawa na mwenye kuuliza, dalili hizo ni zipi na lafdhi zake ni zipi na ni nani alie zisimulia na kuzipokea?

Ili kulifafanua jawabu la swali hilo ni lazima kuashiria kuwa dalili hizo zimhusuzo Mahdi haikuwa ni habari ( hadithi) moja au mbili, bali ni habari nyingi zilizotoka kwa Mtume (s.a.w) na zilizo mutawaatir zilizovuka mamia, na zilipokewa na idadi kubwa ya maswahaba, na zikatolewa na idadi kubwa nyingine ya mahuffa-dhi na wapokezi, na kwa wingi wa istifadha    (wapokezi watatu kwenye kila tabaka) tawaatur (wapokezi wengi sana) haikuwa tena ni sahihi kufanya mjadala kuhusu usahihi wa hadithi hizi na kuhusu yakini zinazo tuletea katika kuthibitisha swala hilo. Na kwa ajili ya udadisi zaidi na utafiti wa kimaudhui tunasema:

Hakika hadithi hizi kwa sanadi yake na dalili yake zimegawa-nyika kwenye makundi matatu:

Kundi la kwanza: 

Zenye sanadi sahihi na dalili yake ni ya dhahiri zisizo na shaka yoyote, na maimamu wa hadithi na mahufadhi wakubwa walithibitisha juu ya usahihi wake au kuwa ni hassan[29](nzuri) na kuwa baadhi yake ni sahihi kufuatana na masharti ya mashekh wawili, Bukhari na Muslim.

Na hakuna shaka katika uwajibu wa kuzichukuwa hadithi za kundi hili na kuzifanyia kazi na kuyaamini mambo yanayo zungumziwa na kujulishwa na hadithi hizo.

 

Kundi la pili:

Ni hadithi zisizo sahihi katika sanadi yake hata kama dalili yake (yaani maneno yake) iko dhahiri. Kanuni zilizo kubaliwa kwenye elimu ya hadithi zinatulazimisha kuzichukua hadithi hizo vilevile, kwa kuungana kwake na kusahihishwa kwake na kundi la kwanza na kwa kuwa mashuhuri ya kuwa wanazuoni wame-zikubali, bali wanazuoni wote wamefanya ijmai kuafikiana juu ya madhumuni yake.

 

Na kundi la tatu:

Limekusanya sahihi na dhaifu, lakini hadithi hizo zinapi-ngana na hadithi zingine zote ambazo ni mustafidhi na zilizo mutawaatir. Basi kitu cha lazima ni kuziacha, na kujiepusha nazo, ikiwa haikuwezekana kuzifanyia taawili, kwa mfano zilizosema kuwa jina la Mahdi ni Ahmad au zilizo sema kuwa jina la baba yake linafanana na jina la baba yake mtume (s.a.w) au zisemazo kuwa yeye anatokana na watoto wa Abi Muhammad Hassan Az-Zakiy, kwani habari hizi ni habari chache na nadra ambazo wanazuoni mashuhuri wamejiepusha nazo.[30]

Hadithi za makundi mawili la kwanza na la pili hizo ndizo ambazo tumebainisha kuwa ni wajibu kuzichukuwa zilikuwa zikielekeza kwenye lengo kwa ibara tofauti tofauti na zikikusudia kumtambulisha na kumuainisha kwa matamshi tofauti tofauti na tunaweza kuufupisha muhtasari wake kama ifuatavyo:

Baadhi ya hadithi hizo zimethibitisha kuwa Mahdi anatokana na kabila la kikuraishi. Ametoa Ahmad na Al-manwardi ya kuwa Mtume (s.a.w) amesema:

) ԡ (

Pateni bishara ya Mahdi, ni mtu atokae kwenye kabila la kuraishi, atokae kwenye kizazi changu. Atatoka watu watakapo hitilafiana na kuwepo mtetemeko, na kuijaza ardhi kwa uadilifu na usawa kama ilivyo  jazwa dhuluma na ujeuri.[31]

Na zingine zimethibitisha, kuwa Mahdi ni katika watoto wa Abdul-Mutwalib.

Ametoa Ibn Maaja kwa sanadi yake kutoka kwa Anas bin Maalik, amesema: Nilimsikia Mtume (s.a.w) akisema:

: )                                                                                                  (   

Sisi  watoto wa Abdul-Mutwalib ni mabwana wa watu wa peponi, Mimi na Hamza na Ali na Jaafar na Hassan na Hussen na Mahdi.[32]

Na zingine zimethibitisha kuwa yeye ni katika Aalu Muhammad (Kizazi cha Mtume,(s.a.w). Amesema Mtume (s.a.w):

)                                                             (              Atatoka katika Zama za mwisho mtu atokanae na kizazi changu, jina lake ni kama jina langu, na kuniya yake ni kama yangu (jina la ubaba kwa mfano baba ya fulani) ataijaza ardhi kwa uadilifu kama ilivyo jazwa ujeuri, na huyo ndie Mahdi. Na hii ni hadithi mashuhuri.[33]

Na zingine zimethibitisha kuwa ni katika kizazi chake. Ametoa Abu Daud kwa Sanadi yake kutoka kwa Ummu Salama (Mungu amuwie radhi) amesema:Nilimsikia Mtume (s.a.w) akisema:           

(     ) Madhi anatoka katika kizazi changu.[34]

Na zingine zimethibitisha kuwa yeye ni katika Ahlul bayti. Amesema Mtume (s.a.w):

( )

 Lau kama isingebakia isipokuwa siku moja Mwenyezi Mungu angetuma mtu atokanae na Ahlul-bayti wangu aujaze ulimwengu uadilifu kama ulivyo jazwa ujeuri.[35]

Na zingine zimethibitisha kuwa, anatokana na watoto wa Ali (a.s), kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas (Mungu awawie radhi) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu:

) (.

Hakika Ali (a.s) ni wasii wangu na katika kizazi chake atatoka huyo mwenye kusimama (dhidi ya dhulma) na mwenye kusubiriwa (almuntadhar), ambae ni Mahdi atakae ijaza ardhi  usawa na uadilifu kama ulvyo jazwa ujeuri na dhulma.[36]

Na zingine zimethibitisha kuwa ni katika watoto wa Fatima.

Ametoa Muslim na Abu daud na Nasai na Ibnu Maaja na Bayhaqiy na wengine:

( ) Mahdi ni katika kizazi changu ni katika watoto wa Fatuma.[37]

Na wengine wamethibitisha kuwa ni katika watoto wa Hussen, Amesema Mtume (s.a.w):

) (

Haitaondoka dunia mpaka ausimamie umma wangu mtu atokanae na kizazi cha Hussen, aijaze ardhi kwa uadilifu kama ilivyo jazwa dhulma.[38]

Na zingine zimethibitisha kuwa ni wa tisa katika kizazi cha Hussen. Kutoka kwa Salmani Al-faarisi (Mungu amuwie radhi) amesema:Niliingia nyumbani kwa Mtume (s.a.w) mara nika-muona Hussen akiwa mapajani mwake akilibusu shavu lake na kuulamba mdomo wake na akisema:

) ϡ (.

Wewe ni Sayyid mtoto wa Sayyid, nduguye Sayyid, na wewe ni Imam Mtoto wa Imam na ndugu wa Imamu, na wewe ni Hujja mtoto wa Hujja ndugu wa Hujja baba wa Mahujja tisa, wa tisa wao ni yule atakae simama (dhidi ya dhulma) ambae ni Mahdi.[39]

Na zingine zilithibitisha kuwa yeye ni wasii wa kumi na mbili. Na Imamu wa kumi na mbili na khalifa wa kumi na mbili.

) : (.

Hakika wasii wangu ni Ali bin Abi twalib na baada yake ni wajukuu wangu wawili Hassan na Hussen watafuatiwa na maimamu tisa watokao kwenye uti wa mgongo wa Hussen (a.s), akasema:Ewe Muhammad nitajie majina yao. !Akasema:Aki-ondoka Hussen ni mwanae Ali akiondoka Ali ni mwanae Muhammad, akiondoka Muhammad ni mwanae Jaafar, akiondo-ka Jaafar ni mwanae Mussa, akiondoka Mussa ni mwanae Ali, akiondoka Ali ni mwanae Muhammad, akiondoka Muhammad ni mwanae Ali akiondoka Ali ni mwanae Hassan, akiondoka Hassan ni mwanae Alhujja Muhammad Al-mahdi hawa ndio maimamu kumi na mbili.

Yahya binil Hassan ametaja kwenye kitabu Al-umda kupitia njia ishirini za upokezi ya kwamba makhalifa baada ya Mtume (s.a.w) ni kumi na mbili na wote wanatokana na kabila la kikuraishi, katika Bukhari kupitia njia tatu za wapokezi, na katika Muslim kupitia njia tisa na kwa Abi Daud kupitia njia tatu, na katika Tirmidhi kupitia njia moja na katika Al-hamiidi kupitia njia tatu.[40]

Na zingine zimethibitisha kuwa ni mtoto wa Hassan Al-askari.

Katika manaaqib kutoka kwa Jaabir bin Abdillahi al-answary kutoka kwa Mtume (s.a.w):

)... ɡ ̡ .(

Basi baada yake ni mwanae Hassan aitwae Al-askari, na baada yake ni mwanae Muhammad aitwae Mahdi na mwenye kusimama kwa haki (Al-Qaaim) na Al-hujja, atatoweka na kutoonekana kisha atatokea, na atakapotokea ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama ulivyo jazwa ujeuri na dhuluma.[41]

Na hivyo hivyo tunakuta kuwa hadithi hizi kwa wingi huu na tofauti zake zimemuelezea Mahdi wa umma huu, na kusema kuwa ni mtoto wa Hassan Al-askari, nayo ni matokeo au natija thabiti ambayo haina kasoro ndani yake.

Na msomaji ili awe na ujuzi zaidi wa jambo hili tunatoa katika sehemu ifuatayo majina ya wapokezi wa hadithi za Mahdi zilizotajwa hapo kabla na hasa majina ya maswahaba, kwani utafiti wetu huu wa haraka hauna nafasi kubwa ya kuweza kuandika majina ya wapokezi wote kutoka kwenye matabaka mengine:

01- Abu Amama al-baahily

02- Abu Ayyub

03- Abu Said Al khudri.

04- Abu Sulaiman-mchungaji mifugo wa Mtume (s.a.w)

05- Abu tufail.

06- Abu Huraira.

07- Ummu Habiba mama wa waumini.

08- Ummu Salama mama wa waumini

09- Anas bin Maaliki.

10- Thubaan-mtumwa wa Mtume (s.a.w).

11- Jaabir bin Samrah.

12- Jaabir bin Abdillahi al-Answari.

13- Hudhaifa binil Yamaan.

14- Salman Al-faarisi.

15- Shahr bin Hawhab.

16- Twalha bin Ubaidullah.

17- Aisha mama wa waumini.

18- Abdur-rahmaan bin Auf

19- Abdallah bin Haarith bin Hamzah.

20- Abdallah bin Abbas.

21- Abdallah bin Omar.

22- Abdallah bin Amrubinil Asi.

23- Abdallah bin Masoud.

24- Othmani bin Affan.

25- Ali bin Abitwalib.

26- Ali Alhilaali.

27- Ammar bin Yaasir.

28- Umraan bin Haswiin.

29- Auf bin Maalik.

30- Qurrat bin Iyaas.

31- Mujmau bin Jariyah Al-answari.[42]

 

Ama ambao walitoa hadithi kuhusu Mahdi kati ya mahufadhi wa hadithi na wenye vitabu vya sahihi na sunanu, ni shekh Abdul-Muhsin Alubad aliwahesabu na kufikia 38 ambao ni mashuhuri na walio wema[43], na miongoni mwao ni:

 

01- Abu Daud katika Sunani yake.

02- At-tirmidhi kwenye kitabu chake kiitwacho Jamiu.

03- Ibnu Maaja kwenye Sunani yake.

04- An-nasai kwenye kitabu chake Alkubra.

05- Ahmad kwenye Musnadi wake.

06- Ibnu Habban kwenye Swahihi yake.

07- Al-haakim kwenye Mustadrak.

08- Abubakar bin Abi Shaiba kwenye Al-munswif.

09- Naim bin Hamad kwenye Kitabu Al-fitani.

10- Abu Naiim kwenye kitabu Al-Mahdi wal-hilyah.

11- At-twabaraniy kwenye kitabu Al-kabiir wal-awsat wa As-swaghiir.

12- Ad-daru-qutni kwenye kitabu Al-ifrad.

13- Al-baarudy kwenye kitabu Maarifat As-swahaba.

14-Abu Yaala al-muuswiliy kwenye Musnad yake.

15- Al-bazzar kwenye Musnad yake.

16- Al-haarith bin Abi Usamah kwenye Musnad yake.

17- Al-khatib kwenye kitabu chakeAt-talkhisul-mutashabih na katika Almut- tafaq wal-muftaraq.

18- Ibnu Asakir kwenye kitabu cha historia.

19- Ibnu Mundih kwenye kitabu chake cha historia Taarikh Isbahan.

20- Abul-hassan Al-harbiy kwenye kitabu chake Al-awwal minal-harbiyaati.

21- Tamam Ar-raziy kwenye Fawaid.

22- Ibnu Jariri kwenye Tahdhibul-Athar.

23- Abubakari bin Al-muqri kwenye Muujam wake.

24- Abu Amru Addani kwenye Sunani yake.

25- Abu Gharam Al-kuufiy kwenye kitabu chake Al-fitani.

26- Ad-daylamiy kwenye kitabu chake Musnadul-fir dausi.

27- Abu Bakar Al-Iskaf kwenye Fawaidul Akhbaar.

28- Abul-Hussen binil Munawiy kwenye kitabu chake Al-  malaahim.

29- Albaihaqi kwenye Dalailu An-nubuwah.

30- Abu-Amru Al-muqri, kwenye Sunani yake.

31- Ibnul Jawzi kwenye kitabu chake cha Historia.

32-Yahya Al-hamaniy kwenye Musnad wake.

33- Ar-ruyaaniy kwenye musnad wake.

34- Ibnu Saad kwenye Twabaqaat.

Imam (Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alizaliwa kwenye mji wa Samarra wakati wa Al-fajiri tarehe kumi na tano ya mwezi wa Shaaban mwaka 255H.[44] na baba yake akamuita Muhammad, na huo ulikuwa ni uthibitisho wa hadithi ya Mtume (s.a.w) iliyo maarufu isemayo Jina lake ni sawa na jina langu[45] na Kuniyah yake (Jina lake la ubaba) akumuita Abul-Qaasim.[46]

Na wapokezi wa riwaya wa Shia Imamiyya walisalim amri juu ya ukweli huu na wengine wengi wa makundi mengine ya kiislamu. Lakini baadhi ya waislamu pamoja na kuikubali kwao fikra ya kuja mahdi walimkataa Mahdi kwa hoja ya kuwa hakuna mtoto wa Askari, na wakatoa dalili nne kuthibitisha hoja hiyo, na tutazielezea kwa ufupi, kama ifuatavyo:

1- Walisema kuwa Askari alipo karibia kufa alimuweka mama yake (Umul-Hassan) kuwa ndie muusiwa wake wa kuya-angalia yote aliyo kuwa akiyasimamia kama  vitu vya wakfu na sadaka na mambo mbali mbali mengine, kama angekuwa na mtoto asingemuacha kumuusia na kumuusia mtu mwingine.

2- Ni kuwa Jaafar bin Ali ami yake Mahdi alipinga kuwepo mtoto wa kaka yake, na ushahidi wa baba mdogo kwenye jambo kama hili ni wenye umuhimu mkubwa.

3- Hakika mashia wanadai kuwa Askari alificha suala la mwanae kwa watu wasio maalumu na wasio wa karibu, kwa nini alifanya hivyo pamoja na kuwa maswahaba wake walikuwa ni wengi katika siku hizo huku wakiwa na nguvu, mali na uwezo wakati ambapo maimamu walio tangulia kwenye zama za utawala wa bani umaya na bani Abbas walikuwa kwenye hali ngumu zaidi na wali banwa zaidi, pamoja na hayo hawakuficha suala la watoto wao kama ufichaji huu.

4- Hakika vitabu vya historia havikumfahamu na kumuelezea mtoto wa Hassan Al-Askari wala havikusimulia habari yake yoyote. Na kwa dalili hizi nne wakapinga wapingaji kuzaliwa kwa Imam Muhammad binil-Hassan.

Tutatowa sehemu ifuatayo kwa ufupi jawabu la dalili hizi ili jambo hili liweze kuwa wazi na iweze haki kudhihiri, na kwa hivyo tunasema:

Ama jawabu la dalili ya kwanza ni kuwa:

Hakika kumuusia mama haifai kuwa ni dalili ya kupinga kuwepo kwa mtoto, na lengo la Imam kutoa usia huo ni kuwafa-nya watu wasimuelekee na kutaka kujua habari za mwanawe na watu kutojishughulisha nae na mazingira  kugubikwa na suala lake na kuwajulisha maadui zake kutokuwepo mwanae, bali aliwazidishia dhana hiyo kwa kuwafanya kuwa mashahidi wa Usia huo watu wengi katika wakubwa wa serikali ya wakati huo juu ya usia huu.[47]

Na Imam alikuwa kwenye matendo yake hayo akifuata mfumo wa babu yake Jaafar bin Muhammad As-swadiq (a.s) pale alipojiwekea wausiwa watano baada ya kufariki kwake nao ni Al-mansuril Abbasi na Arrabiu na Kadhi wa madina ukiongezea mkewe Hamidah, na mwanae Mussa bin Jaafar (a.s) na lengo lake kwa kufanya hivyo ni kuyaweka mbali macho ya watawala na maadui yasimuelekee mwanae Mussa[48], kwa sababu lau kama angemuusia yeye peke yake, bani Abbasi wangeweza kufanya jambo lolote lingine tangu siku ya kufariki baba yake, na Mansur alipofikiwa na habari za kufariki Imamu Swadiq (a.s) alimuandi-kia gavana wake wa Madina, akimuamuru azidi kumbana wasii wa Jaafar bin Muhammad, yule gavana akamuandikia Mansuur, baada ya kufanya uchunguzi, akimfahamisha kuwa walio usiwa ni watu watano na kuwa wa mwanzo wao na ambae ni muhimu ni khalifa mwenyewe. Na kwa kufanya hivyo ilikuwa ni kumuepu-shia Imamu Mussa bina Jaafar (a.s) maudhi.

Ama jawabu la dalili ya pili ni kuwa:

Hakika Jaafar ni katika watu wa kawaida, na inawezekana kwake kufanya mambo kama wafanyavyo watu wengine wa kawaida kama kukosea na kuasi na kutoa madai ya batili, na inatosha akawa kama mfano wa Kaabiil, pindi alipomuua ndugu-ye au mfano wa watoto wa Yaakub walipomtumbukiza ndugu yao kwenye kisima na wakamuudhi baba yao na kuapa viapo vya uongo ya kuwa ndugu yao ameliwa na mbwa mwitu.

Na Jaafar alidhania, nae akifahamu kufichwa suala la mtoto wa kaka yake kwa watu wasio maalumu kati ya maswahaba wa baba yake, ya kuwa atakuwa Imamu kwa kupinga kule, na kwa-mba mali za kisheria zitakusanywa kwake kutoka kila pembe na kila upande, lakini Irada ya Mwenyezi Mungu ndio yenye kushi-nda, kwani ni haraka sana ulidhihiri uongo na ubaya wa suala lake, kisha akajuta kwa yale aliyoyafanya na akatubia kutokana na uovu alio ufanya hadi kuwa mashuhuri kwa jina la Jaafar Attawaab. (Mwenye kutubia)

Na si jambo la ajabu baba mdogo kusimama kidete dhidi ya mtoto wa nduguye. Hapo zamani Abu Lahab na Abbas walikuwa ni viongozi wa kikundi cha maadui dhidi ya mtoto wa ndugu yao, Muhammad (s.a.w) kwani walipinga utume wake na kumuhusisha na uchawi na wendawazimu na kuyaongoza majeshi kumpiga vita na wakaweka mipango na mikakati ya kumua.

Ama jawabu la dalili ya tatu ni kuwa:

Hakika jambo lililo mfanya Imamu Askari kuficha suala la mwanae ni kutokana na kufahamika na kuwa mashuhuri ya kuwa Imam atasimama kwa upanga ili kuondoa dola la batili na kusi-mamisha dola la haki, kwa hivyo watawala walikuwa wakimu-ogopa mwana mapinduzi huyo na wakijiandaa na kuandaa mipango ya kumuua kwa aina yoyote ile, lau wangefahamu suala lake na kujua habari zake. Kutokana na hali hii akalazimika Imam Askari kuficha na kutozisema habari za mwanae na kuzihi-fadhi habari zake kwa siri kwa maswahaba wake maalumu. Na jambo linaloweka wazi na kuyaunga mkono maneno haya  ni kuwa serikali tawala za wakati huo waliharakisha kuwatuma wapelelezi wao wakati wa kufariki Imam Askari kwenye nyumba yake ili wamkamate mtoto yoyote atakae kuwa ndani ya nyumba hiyo.[49] Lau kama si utashi wa Mwenyezi Mungu ambao ulimfanyia wepesi Muhammad bin Hassan kukimbia na kujificha, wange-muua.

Na Imamu Askari katika ufichaji huu alikuwa na kigezo cha mama yake Mussa bin Imran alipo shushiwa wahyi kuwa ni lazima kumficha na kufanya siri kuhusu suala la Nabii Mussa kwa kumkhofia Firauni wa zama zake kama Quran tukufu ilivyoelezea kuhusu swala hilo.

Ama maimamu walio tangulia ilikuwa si lazima kwao kusimama kwa upanga, bali suala hilo liliachiwa kulingana na mazingira na mambo ya zama hizo na kufanya kulingana na mahitajio ya kila zama na mazingira yake kwa kujua ni hukumu gani au taklifu ipi inatakiwa, kwa hivyo walikuwa na amani kiasi na uhuru kwa kiwango fulani, hata kama haikuwa ni amani na uhuru kwa maana yake sahihi.

Ama jawabu la dalili ya nne ni kuwa:

Hakika kujulikana utoto au mtoto huyu kuwa ni wa huyu huthibitika katika sheria, kwa kauli ya mkunga au wanawake ambao huwepo kwenye uzazi ule (yaani mama yule anapo jifungua) na kwa kukubali mwenye kitanda (baba mzazi) na kushuhudia wanaume wawili walio waislam juu ya kukiri na kumkubali baba mtoto wake. Na pande hizi tatu zilithibitika na kupatikana kwenye uzazi ule.

Kwa mfano, Sayyida Hakimah binti wa Imam Jawaad (a.s) ndie ambae alisimamia jambo hilo la uzazi na akashuhudia uzazi huo. Na Imam Askari ndie baba na alikubali kuzaliwa kwa mtoto huyo mbele ya maswahaba wake maalumu.[50] 

Na waislamu wa zama  hadi zama zinginezo zilizo fuatia, wanasimulia habari hizo na wanashuhudia juu ya usahihi wake. Na miongoni mwa waliopokea na kusimulia uzazi huu, ukiongezea juu ya kukubaliana mashia Imamiyya wote juu ya suala hili kati ya wanazuoni wa kiislamu, kuna idadi isiyo chache ya wana historia na waandishi, kwa mfano kuna hawa wafuatao:

01-Muhammad bin Twalha Ashaafii,aliefariki mwaka 652 H.[51]

02- Sibti ibn Jawziy, aliefariki mwaka 554 H.[52]

03- Al-kanji Ashaafii , aliefariki mwaka 658 H.[53]

04- Ibnu Khalakaan Ashafii, aliefariki mwaka 681 H.[54]

05- Swalahud-dini As-swafadi aliefariki mwaka 764 H.[55]

       06- Ibnu Hajar Al-haytami Ashaafii aliefariki mwaka 852 H.[56]

07- Ibnu Swabbagh Al-maaliki, aliefariki mwaka 855 H.[57]

08- Ibnu Tuuluum Ad-damashqi, aliefariki mwaka 953[58]

09- Al-Hussen bin Abdallah Assamar qandi, aliefariki mwaka           1043.[59]

10-Mohammad As-swaban Ashaafii, aliefariki mwaka    1206.[60]

11- Sulaimani Al-kanduziii, Al-hanafiy aliefariki mwaka 129  H.[61]

12- Mohammad Amin As-suwaydi aliefariki mwaka 1246 H.[62]

13- Muumin Ashablanji Ashaafii, aliefariki katika karne ya 14 H.[63]

 

***

 

 

 

 

SEHEMU  YA  TATU

 

UWEZEKANO  WA  KUGHIBU  NA  DALILI  ZAKE

 

Imetuthibitikia kutokana na yote yaliyo tangulia kuwa fikra ya (kuja kwa) Mahdi, ni fikra iliyochimbuka kwenye sheria halisi ya kiislamu, na Mtume (s.a.w) alitoa bishara ya fikra hiyo katika hadithi zilizo kuja kutoka kwake, na wanazuoni wa hadithi tabaka kwa tabaka wakarithishana na kupeana riwaya hizo kama ilivyo thibiti vilevile ya kuwa Mahdi aliezungumziwa kwenye hadithi ni Muhammad bin Hassan Al-askari, na kwamba alizali-wa kwenye mji wa Sammarraa na habari za kuzaliwa kwake kujulikana kwa siku ile aliyo zaliwa kwa watu maalumu katika maswahaba wa baba yake, kisha akawa mashuhuri baada ya kuzaliwa kwake kwenye vitabu vya historia.

Na ni lazima kwetu baada ya kuthibitika sehemu mbili za mwanzo tuhamie kwenye maudhui ya sehemu ya tatu na ya mwisho inayo husiana na hatua ifuatiayo baada ya kuzaliwa Muhammad bin Hassan na kuthibiti  kuwa yeye ndie Mahdi.

Na huenda ikawa bora zaidi ili kufuata mfumo maalumu na ili kuweka wazi jambo hilo, twende hatua kwa hatua kwenye mazungumzo yetu kufuatia mtiririko ufuatao:

01: Je Mahdi alighibu (alifichika na kutoonekana)?

02: Tukijaalia kuwa kuna uwezekano wa kughibu, je mtu anaweza kubakia akiwa hai kwa muda wa karne zote hizo?

Na ni vizuri kwetu, na huku tukiwa tumefikia sehemu nyeti na ya muhimu zaidi katika utafiti huu, tutangulize utangulizi ufuatao kabla ya kuingia kwenye kina cha maudhui yenyewe, ili utusaidie kufikia natija zilizo safi na malengo kuwa wazi.

Hakika Uislamu uliifanya akili kuwa ndio chimbuko la itikadi na msingi wa Imani, na ukakataa kufanya taklidi (kuwa-fuata watu ufuataji usio na dalili) na ufuataji wa kiupofu, na lengo la kufanya hivyo ni kuwa misingi ya itikadi na mizizi yake ijitege-meze kwenye akili na kuitegemea akili, na misingi hiyo ipate nguvu yake na kujizatiti kutokana na akili pekee, bila kushiriki kitu kingine chochote kwenye suala hilo kama matamanio ya nafsi na kutawaliwa na hisia za ndani na kufuata watu wengine.

Na hivyo ndivyo akili ilivyo kuwa ni dalili ya kumtambulisha Mwenyezi Mungu, nayo ndiyo iongozayo kwenye Imani. Katika kuwepo Mwenyezi Mungu na Umoja wake na katika ulazima wa kuwepo kwake, kisha akili vilevile ili kuwa ni dalili ya kuthibiti-sha ulazima wa kuwepo utume na uimamu na kuwepo marejeo ya kiama yakiwa ni matawi ya Imani ya Mwenyezi Mungu alie tukuka.

Ama maneno mengine ya hukumu za sheria na dalili za kidini hazihitajii dalili ya kiakili, na si lazima kwa mambo yao kusima-misha dalili kama hii, bali inatosha kulazimika kuyakubali kwa kutolewa tu dalili yenyewe ya aya au riwaya, juu ya suala hilo kwa njia za kisheria zilizo thibitisha ulazima wa kuzitii na kuzi-fuata dalili za kidini (aya na riwaya).

Kutokana na haya waislamu wakaamini kwa ukweli na kwa yakini, masala ya kuwepo malaika kwa mfano, au kuamini kuwa Issa alizungumza akiwa mtoto mchanga au habari za mawe kumsabihi Mwenyezi Mungu yakiwa mikononi mwa Mtume (s.a.w), kwa ajili ya kuzungumziwa mambo haya kwenye Quran tukufu na sunna sahihi.

Na sisi tunapofanya utafiti kuhusu maudhui ya Mahdi na kughibu kwake tunayafanyia utafiti pamoja na waislamu wenye kukubali misingi ya uislamu na misingi ya sheria, bila ya kuwahusisha wengine wapingao kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au ambao bado hawajawa waislamu, na kufanya hivyo ni kwa sababu masala yenyewe yalivyo, yanategemea kutolewa dalili na ushahidi wa Quran tukufu na Sunna tukufu, kwa hivyo haifai kuyazungumzia masala haya pamoja na mtu asie kiamini kitabu na sunna.

Kwa ibara nyingine, hakika sisi tunayafanyia utafiti maudhui haya juu ya msingi wa itikadi ya dini yenye kujitegemeza kwenye dalili za kisheria ambazo waislamu wote wamekubaliana na kuafikiana ya kuwa ni wajibu kuvifuata na kuvifanyisha kazi na si kwa kufuata msingi mwingine wala masala haya kwa hali yoyote hayajawahi kuwa kama kazi ya kimahesabu ya kawaida kama jibu la 22 au kama kanuni ya kifalsafa ambayo haiwe-zekani kuzungumziwa na kujadiliwa kama kubatilika kwa dauru (mzunguko usio na mwisho) au tasalsulu (silsila ya vitu vyenye uhusiano isiyo kuwa na kikomo).

Kwa hivyo basi, na awe msomaji mtukufu ni mwenye kufaha-mu ya kuwa sisi tutayazungumzia na kuyafanyia utafiti masala haya au tatizo hili kwa pande zake zote kwa kufuata msingi wa kitabu na sunna kwa sababu vitu hivi viwili ndio chimbuko la sheria na mlango wa maarifa na elimu kwa waislamu, na kwamba kuvipinga na kutoka kwenye msingi wa kuvifuata ni sawa na kuupinga Uislamu na kutoka dhidi ya hukumu zake na amri zake.[64]

Ukiwa wazi utangulizi huu, tunasema:

Hakika hadithi tukufu za Mtume ambazo zimepokelewa na mahufadh wa hadithi, na wakiwemo kati yao wale ambao waislamu wamekubaliana juu ya usahihi wa hadithi zao, zimekariri mara kadha neno la kughibu. [65]

Na kati ya hadithi zingine zinasema Ataghibu, kutakuwa na hali ya watu  kutapatapa na kutahayari, na kaumu zitapotea kwenye hali hiyo.[66]

Na katika riwaya nyingine:

) (

Na katika riwaya nyingine Ataghibu na kuto onekana kwa wapenzi wake, kuto onekana ambako hatabakia kwenye Imani na kauli ya Uimamu wake isipokuwa yule ambae Mwenyezi Mungu amempa mtihani moyo wake kwa Imani.[67]

Na katika hadithi ya Ibnu Abbas:

( ӡ :) Atatumwa Mahdi baada ya kukata tamaa, na mpaka watu waseme:Hakuna Mahdi.[68]

Neno ghaib kama hadithi tulizo zitaja zilivyo,haina maana ya kumuhuisha Mahdi baada ya kufa kwake, na kumrejesha duniani baada ya kufa kwake bali hadithi hizo zina angalia kwenye ile hali ya kuto onekana kwake na kufichika kwake na watu kutomuona na kumshuhudia, na haya ndio yafahamikayo kwa haraka kwa kila msomaji pindi anapo soma hadithi hii na kulipima neno (ghaiba) lililo kaririwa kwenye hadithi hizo.

Na hadithi tukufu ambazo waislamu wamekubaliana juu ya riwaya yake.

( )Mwenye kufa na haku-mjua Imamu wa zama zake amekufa kifo cha kijahili. Hadithi hii iko wazi katika kuonyesha ulazima wa kuwepo Imamu katika kila zama na kila wakati.

Na baada ya kuthibiti kuzaliwa kwa Muhammad bin Hassan kwa dalili zisizo na shaka, neno ghaiba na ulazima wa kuwepo Imamu katika kila zama na kuwa ni dalili mbili za wazi zithibitishazo kuendelea kuwa hai kwa Mahdi kwa muda wa karne zote hizi na zinakuwa dalili za kupinga maneno mengine  yasemayo kuhusu maudhui haya, maneno yenye kutilia shaka na kutowezekana kufanyika kitu kama hicho.

Na kauli ya kuwa Mahdi amekufa, pamoja na kuwa inapi-ngana na hadithi za ghaiba na hadithi za kuendelea kuwa hai kwa uimamu, hakuna mwana historia yeyote alieitolea ushahidi, na haikutajwa kwenye kitabu chochote ikiwa miongoni mwake vitabu vya wapingao suala hili Amekufa lini? Na katika siku ipi na mwezi gani na mwaka gani na wakati gani, alipelekwa kuzikwa na ni akina nani walio hudhuria mazishi yake na amezikwa wapi na katika nchi gani??

Hakika yote haya yanatilia mkazo kuwa Mahdi, yuhai hakufa na kwamba yeye alighibu na kufichika mbali ya macho ya maadui zake, ili kuyahifadhi maisha yake na kuiokoa nafsi yake na kufichika kwake kulikuwa ni kwa aina mbili.

 

Aina ya kwanza:

Kutoonekana kwa watu pale jeshi la khalifa walipo ivamia nyumba ya Imamu Askari baada ya kufariki kwake. Na katika kipindi hiki alikuwa akiwasiliana na mawakili wake na kuwapatia majibu juu ya maswali na matatizo ambayo mashia wakiyaele-keza kwake.

Aina ya pili:

Ni kutoonekana kwake kiukamilifu kwenye macho ya watu kiasi kwamba alikuwa hawasiliani na yeyote.[69]

Hakika suali la muhimu linalojitokeza kwenye akili, baada ya kuthibitika kuwepo kwa Mahdi na kufichika kwake na maisha yake kuendelea hadi leo, ni hili: Je anaweza kubakia hai kwa muda wa miaka yote hiyo? Na je, akili ina kubaliana na hilo?

Kabla ya kujibu swali hilo tunapenda kumkumbusha mso-maji yaliyo tangulia kusemwa kuwa, mambo ya kweli ya kisheria yakithibitika kwa habari za kunukuliwa zilizo sahihi, basi sisi kwa kuzingatia kuwa ni Waislam, ni lazima kwetu kufuata na kutii habari hizo na kuikubali hata kama akili zetu hazikupata njia na muongozo wa kufahamu falsafa yake na kujua siri zake.

Kwa hakika kutofahamu hekima ya hukumu hii au sababu yake, haiwi ni dalili ya kuipinga na kuikataa, bali ni lazima kusalimu amri na kutekeleza kwa hali yoyote, na haifai katika Uislamu, Muislamu kupinga hukumu moja wapo kati ya hukumu zake au kuitoa na kutolikubali suala lolote lililo elezewa kwa hoja ya kutofahamu siri au kutokinaika na sababu iliyotolewa.

Ama umri kuwa mrefu na maisha kuendelea kuwepo kwa muda wote huo kwa mamia ya miaka sio katika mambo yaliyo muhali, na kutowezekana kama wanavyo dhania baadhi ya watu bali imepokelewa riwaya na wana historia na kusimulia juu ya kutokea hilo kwa wingi, kwenye historia ya wanadamu ambayo ni ndefu. Kwa mfano Adam (a.s) alipewa umri na kuishi kwa muda wa miaka elfu moja. Na Lukman mwenyewe alipewa umri wa miaka elfu tatu na miatano (3500). Na Salman Al-faarsi (Mungu amuwie radhi) aliishi muda mrefu hapa aridhini, na baadhi ya wana historia wanadai kuwa aliishi zama za Masihi Issa (a.s) na kuudiriki Uislamu na akafariki kwenye zama za Khalifu Omar binil Khattab.

Na wengine wengi waliopewa umri wa mamia ya miaka na habari zao kusimuliwa na wanahistoria na hasa Assajastani alie kusanya habari zao kwenye kitabu alicho kiita Al-muammarun (waliopewa umri mrefu) kilicho chapishwa kwa mara ya kwanza Misri mwaka 1323 H, 1905 AD. Huu ni uthibitisho kwa upande wa kihistoria.

Ama Qurani tukufu ndio kauli iliyo ya kweli zaidi na hoja yenye nguvu zaidi kuliko mwana historia yeyote na riwaya yeyote.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu na kauli yake ni ya kweli: Hakika Nabii Nuhu (a.s.) alikaa katika kaumu yake akiwalingania kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu kwa muda wa miaka 950 na Mwenyezi Mungu ndie ajuae ni muda gani alio ishi kabla ya kuanza wito na baada ya tuufani.

Na kwamba Mtume Yunusu (a.s) alibakia kwenye tumbo la nyangumi kwa muda mrefu na lau kama si fadhila za Mwenyezi Mungu wake angebaki kwenye tumbo lake hadi siku ya kiama.

( )Basi isengelikuwa ya kwamba yeye alikuwa ni miongoni mwa wenye kumsabihi Mwenyezi Mungu bila shaka angekaa kwenye tumbo lake hadi siku ya kufufuliwa.

Na maana ya kukaa huku ni kubakia kwake akiwa hai hadi siku ya kiama na nyangumi nae kubakia hai pamoja nae kwa muda wote huo ulio mrefu. Na kwamba watu wa pango (kahfu):

(   )                                            Walikaa kwenye pango lao miaka mia tatu na wakazidisha tisa wala hatufahamu ni kwa muda gani waliishi kabla ya kuingia pangoni na baada ya kutoka kwao.

Na kwamba:

) : ǡ ʡ (.

Au kama yule ambae alipita kwenye kijiji (akakikuta) kikiwa kimeharibika na majumba yake kubomoka akasema:Vipi Mwenyezi Mungu anaweza kuvihuisha vitu hivi baada ya kufa kwake? Mwenyezi Mungu akamfisha kwa muda wa miaka mia moja, kisha akamfufua akasema, umekaa hapa kwa muda gani? Akasema: Nimekaa kwa muda wa siku moja au nusu siku. Akasema: Bali umekaa  kwa muda wa miaka mia moja, basi kiangalie chakula chako na kinywaji chako hakikugeuka wala kuharibika, na muangalie punda wako.

Huwenda kubakia chakula na kinywaji (maziwa) kwa muda wa miaka mia moja bila kuharibika au kugeuka, ni jambo la ajabu zaidi kuliko umri mrefu wa mwanadamu na lengo lenye kustaajabisha zaidi.[70] Yote haya kwa kuongezea na mambo mengine waliyo yaandika waandishi wa historia na wana hadithi na wakayapokea kwa kuyakubali na kuhusu uhai wa Khidhiri ambae alikuwepo kabla ya zama za Mussa (a.s) na ataendelea kuwepo hadi zama za mwisho.

Je tuyaamini na kuyakubali yote hayo yaliyo zungumzwa na Quran na kupokelewa kwa wingi kwenye suna au la? Na je ina swihi kwetu kuyapinga na kuyakataa ilimradi tu akili ya mwanadamu kwa kiwango chake ilicho nacho haijaweza kufaha-mu siri ya mambo haya na bado haijaweza kufichua na kugundua mambo mengine yaliyo fichika na yasiyo julikana?

Maudhui ya kughibu kwa Mahdi mfano wake ni kama haya kiukamilifu, na ni lazima kwetu kukiri kuwa maisha na uhai wake ni wenye kuendelea kufuatia ushahidi na dalili hizo na kumswadikisha mtume (s.a.w) ambae hatamki kwa matamanio yake bali ayasemayo ni wahyi ulio teremshwa na kutekeleza amri yake Mwenyezi Mungu.

( ) Aliyo waleteeni Mtume yachukueni, na imani yetu kwa vitu hivyo haitakuwa ni ajabu au jambo geni, au kuliamini jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye Uislamu, bali kufanya hivyo ni sawa na kuamini umri mrefu wa Nabii Nuhu na kukaa kwa Yunusu kwenye tumbo la nyangumi, na kubakia kwa chakula na kinywaji (maziwa) kwa muda wa miaka mia moja bila kuharibika na bila kugeuka au kupatwa na uharibifu.

Na ikiwa dalili ya Quran na hadithi tukufu zimejulisha uwezekano wa mwanadamu kubakia hai zaidi ya miaka elfu moja na kutufahamisha kutokea hilo kwenye kaumu zilizo tangulia, basi hiyo haimaanishi kuwa jambo hilo liko juu ya uwezo wa kielimu na juu ya uwezo wa kiakili, na hii ni elimu ya kisasa inatueleza wazi ya kuwa mwanadamu anauwezo wa kubakia kwa maelfu ya miaka ikiwa ataweza kutayarishiwa nyenzo za kuzihifa-dhi nguvu za kimwili ambazo ndizo zimsaidiazo kubakia hai.

Hakika maulamaa wenye kutegemewa kwa elimu zao wanasema: Hakika chembe chembe za msingi kwenye kiwiliwili cha wanyama, zinakubali kubakia kwa muda mrefu usio na mwisho, na kuwa kuna uwezekano wa mwanadamu kubakia hai kwa maelfu kadha ya miaka ikiwa hakutokewa na vitu au vikwazo viwezavyo kukata kamba ya uhai wake, na kauli yao hii si dhana tu bali ni natija na matokeo ya majaribio (au kazi iliyo fanyiwa majaribio.

hakika mwanadamu hafi kwa sababu kuwa ameishi kwa muda wa miaka kadhaa, sabini au thamanini au mia moja au zaidi, bali kuna vitu vinavyo ingia kwenye baadhi ya viungo vyake na kuviharibu na kuto kuwepo mawasiliano kati ya viungu vyake vyenyewe na vyote vinakufa, na elimu ikiwa itaweza kuondoa vipingamizi vitokeavyo kwenye mwili au kuzuwia ufanyaji kazi wake au kuathirika kwake, hakutabakia kizuwizi kizuwiacho kuendelea kuishi mamia ya miaka.[71]

Naye John Roston anaitakidi kutokana na ugunduzi na majaribio ya kielimu kuwa kufuata njia ya kumhifadhi mwana-damu, halijabakia kuonekana kuwa ni jambo muhali lisilo weze-kana[72], kwani ugunduzi ulio thibitishwa na kuandikwa na wana-zuoni na wataalamu mashuhuri tangu karne moja takriban unatupa na kutuachia matumaini ya uwezekano wa kufikia kufahamu na kugundua chembe zenye uwiano na chembe za mwilini zitakazo saidiana kuongeza kuishi kwa miaka mingi, kwa kutegemea majaribio ya kielimu aliyo yaandika Brown Sickward, Alexy Carl, Voronor, na Minsha bonkov na Bogau Molites,Vilator na wengineo.

Ama Robert Itinger, ambae aliweka mwishoni kitabu kizuri na makini kwa anwani Je mwanadamu anaweza kubakia milele akiwa hai, hakika alileta matarajio mapya pale alipo sema: Hakika mwanadamu ambae anaishi na kupumua kwa hivi sasa anamiliki uwezo wa kubakia kwa upande wa kifizikia.[73]

Haya yote ukiongezea na maneno mengine mengi yaliyo semwa wazi yaelezeayo uwezekano wa kuyahifadhi maisha ya mwanadamu kwa maelfu ya miaka ikiwa mwanadamu atagandi-shwa kwa kipindi hiki, kwa kuzingatia kuwa kugandishwa kunazihifadhi seli (chembe) zote za uhai, na wakati wowote inapotakiwa kumrudishia mwanadamu aliegandishwa ufanyaji kazi wa mwili wake hupewa au huwekewa kiwango fulani cha joto kilicho lazima kwenye mwili na kumfanya kurudi kwenye hali yake, kama alivyo kuwa mwenye nishati kwa harakati na mwenye uhai mwingi ndani yake.

Na vyovyote iwavyo, hakika maneno ya wazi ya wataalamu wa zama hizo yanasisitiza uwezekano wa umri wa mwanadamu kuwa mrefu, na kwamba uwezekano huo ndio kitu kikubwa kiwapacho msukumo juu ya kuendelea na kufanya juhudi za kutaka kuelewa nyenzo za vitu vinavyo weza kulifanya jambo hilo lifanikiwe.

Na ikiwa inafaa mwanadamu kuweza kurefuka umri wake kutokana na maandalizi na maumbile aliyo nayo, itakuwa ni jambo linalo wezekana umri wa Mahdi (a.s) kuwa mrefu kwa karne zote hizi kutokana na hali ya kimaumbile na utashi wa Mwenyezi Mungu.

 

Na baada ya hayo:

Hakika wanadamu ambao wanaishi kwenye zama hizi ni wenye mazingira magumu sana ya kifikra na ambao ni wakati hatari sana wa utamaduni na wenye kuhitajia sana msuluhishaji huyu mwenye kutarajiwa na kusubiriwa, ambae ni lazima atoke siku fulani ili aweze kurudisha mwendo wa wanadamu kwenye njia au mfumo wake sahihi, na kumpitisha kwenye njia iliyo nyooka.

Bila shaka akili ya wanadamu, muislamu na asie muislamu, ikipata habari za mtu au msuluhishaji mfano wa huyo mwenye kungojewa, inakubali na kukiri kuwa ni lazima aje na ni lazima awepo, hata kama kusinge kuwa na dalili ya Qurani au hadithi juu ya mtu huyo au ishara juu ya mtu huyo. Bali hata mwana-falsafa wa Uingereza alie mashuhuri Bernard Show, alitoa bishara ya msuluhishaji huyo kwa msukumo wa fikra zake halisi na akaandika kitabu kuhusiana na hilo  alicho kiita kwa jina la Al-Insaan wa superman na amesema kuwa msuluhishaji huyu mwenye kungojewa ni mwanadamu alie hai mwenye ujenzi wa kiwiliwili ulio sahihi na uwezo wa kiakili wa kiwango cha juu sana kisicho cha kawaida, ni mtu wa kiwango cha juu sana na mtu huyu wa chini (yaani wa hali ya kawaida) atamfikia baada ya juhudi za muda mrefu na kwamba yeye umri wake utakuwa mrefu hata kuzidi miaka mia tatu, na anaweza kunufaika na vitu alivyo vikusanya kwenye zama zote hizo na alivyo vikusanya kwenye muda wote wa uhai wake ulio mrefu.[74]

Na Abbas Mahmud al-aqqad amesema akiongezea maelezo yake juu ya hilo: Inatudhihirikia kuwa Superman show si jambo la muhali kuwepo na kwamba wito wake kwake haukosi ukweli ulio thabiti.[75]

Na hatuwezi kupata kheri mwishoni mwa mazungumzo hayo zaidi ya kumuelekea Mwenyezi Mungu na kumuomba kwa kuse-ma:Ewe Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunashitakia kwako kumkosa nabii wetu, na kughibu kwa mtawala wetu, na kuzidi kwa maadui wetu, na idadi yetu kuwa chache, na fitina (mitihani) kwetu kuwa mikali na zama kutugeuka na kushinda. Basi mrehemu Muhammad na (Aali) jamaa zake, na utusaidie juu ya hayo kwa ushindi wa haraka utokao kwako, na kwa kuondoa taabu na madhara na kwa ushindi uutukuzao, na utawala wa haki uudhihirishao

Ewe Mwenyezi Mungu mnusuru kwa nusra iliyotukufu, na umpe ushindi ulio mwepesi na utujalie tuwe ni katika wafuasi wake na wasaidizi wake, hakika wewe ni msikivu na mwenye kujibu maombi.

Na mwisho wa maombi yetu ni kuwa tunamshukuru Mwenyezi Mungu mola wa viumbe wote.

 

 

***

 

 

NYONGEZA

 

Baada ya kutoka chapa ya kwanza ya kitabu hiki nilipokea barua kutoka kwa mheshimiwa Ustadh Muhammad Ridhwaan Al-Kasam kutoka Damaskas akipinga baadhi ya mambo yaliyo kuwemo kwenye bahthi yetu (utafiti).

Na ninafurahi sana kuelezea au kutoa shukurani zangu za dhati kwa Sheikh Al-kasam, kwa kutoa mwishoni mwa chapa hii baruwa yenyewe na jibu langu juu ya barua hiyo, huenda mso-maji mtukufu akapata ndani yake manufaa na faida fulani.

 

Na Mwenyezi Mungu ndie atoae tawfiqi.

 

***

 

 

BARUA  YA  SHEKH  AL-KASAM.

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.

Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe na rehma na amani ziwe juu ya Mtume wa mwisho.

Mheshimiwa Sayyid Muhammad Hassan Aalu Yaasin, Assalam alaykum wa rahmatullahi wa barakatuhu. Ama baada ya hayo.

Hakika nimesoma kitabu chako kiitwacho Al-Mahdil-Muntadhar baina At-taswawuri wa At-tasdiiq na uliyo yataja ndani ya kitabu hicho na kutokana na kauli yako kwamba ni utoaji wa habari ulio wa kweli na ni utoaji hukumu wenye amana na ni utafiti ulio safi ulio epukana na matamanio na mapenzi. Hakika jambo zuri lililo nistaajabisha kwenye kitabu hicho ni kauli yako kwenye ukurasa wa 50:

Hakika Uislamu umeifanya akili kuwa ni chanzo cha itikadi na msingi wa Imani na ukakataza kufanya taklidi (kuwafuata watu fulani) ufuataji wa kiupofu usio na ushahidi wala dalili.

Nina sema ewe Sayyid mtukufu hakika kutokana na haya, ilikuwa haiwezekani kwangu isipokuwa kukutolea mambo ambayo ni lazima kuelezwa kati ya mambo niliyo yafahamu kutokana na masomo yangu, kwa kuzingatia kuwa ni mmoja wapo wa wafanyao kazi kwenye uwanja huo wa kiislamu ili kubainisha ninayo yaona ni sawa, na maelezo yangu ndio haya:

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ametukataza moja kwa moja katika aya nyingi kuitakidi itikadi yoyote isiyo na yakini ndani yake na akasema Sema je mna ujuzi wowote kuhusu hili mkatutolea, na akasema tena Kwa nini hawawaletei ushahidi ulio wazi, basi ni nani dhalimu zaidi kuliko aliemzulia Mwenyezi Mungu uongo, na akasema tena Hawana ujuzi wowote kuhusu suala hilo isipokuwa ni kufata dhana.

Kwa hivyo yeye Mwenyezi Mungu anatutaka tuwe na ujuzi na maarifa na ushahidi na anatukataza kuwa na dhana na makatazo yake hayo anayaunganisha na ahadi na vitisho. Kutoka-na na hayo tunaweza kusema kuwa itikadi hazichukuliwi isipo-kuwa kutokana na yakini.

Na baada ya kukisoma kwa uchambuzi Kitabu chako na kuandika maoni yangu kukihusu, nimeona kuwa wewe umetaja kuwa fikra ya Mahdi imesimama juu ya msingi wa yakini na elimu au ujuzi ulio mutawatir na ukasema kwenye ukurasa wa 14: Kutokana na dalili za Mtume kuwa mutawatir katika haki ya Mahdi, mara kwa kueleza wazi na mara nyingine kwa kuashiria na ukamalizia pembezoni mwa kitabu kuwa mtu anaweza kurejea kwenye kitabu murajaati cha Sheikh Sayyid Abdul-Hussen Sharafud dini na kitabu Al-ghadiir juzuu ya kwanza cha Al-Amiini.

Na kwa kurejea kwenye vitabu viwili hivyo hapakuwa ndani ya vitabu hivyo chochote kinacho faa kuwa ni dalili na ushahidi wa fikra hii, isipokuwa hadithi ambazo sanadi yake ni Auhaad (zisizofikia kiwango cha mutawatir) na si hadithi zilizo mutawa-tiri. Je hadithi sahihi zina kupatieni yakini katika nadharia yenu?

Hakika suala hili ni la kushangaza.

Kisha kuna jambo lingine ni vizuri kulitilia umuhimu nalo ni pale ulipo taja kwenye ukurasa 14 kama ifuatavyo: Na ni-lazima ili kujiepusha na maovu haya awepo Imamu alie chaguliwa na mwenye sifa zote za ukamilifu, alie epukana na kutakasika na mambo yote yachukizayo, na alie mbali na kila aina ya uovu katika matendo na kutoka kwenye kanuni za sheria na hali hiyo ndiyo tuiitayo kwa jina la Isma na kuendelea.

Ndugu yangu mpenzi, hiyo ni Ismah gani?

Je kuna mwanadamu yeyote mwenye Ismah basi utasemaje kuhusu kauli ya Mtume (s.a.w) isemayo Kila mwanadamu ni mwenye kufanya makosa na watu bora (kati ya wafanyao makosa) ni wale wafanyao tauba (yaani waombao msamaha).

Je Mtume aliposema kila mwanadamu ni mwenye kukosea alimtoa kwenye hukumu hiyo mtu yeyote? Basi hoja na dalili ya Ismah iko wapi? Ukiongozea pamoja na haya kuwa wewe umetoa ushahidi wa hadithi sahihi ukurasa 53 Mwenye kufa hali ya kuwa hakumfahamu Imamu wa zama zake amekufa kifo cha kijahili, na ukafahamu kutokana na hadithi hiyo kuendelea kwa Uimamu wa Muhammad bin Hassan.

Ni mtu gani anae kubali kauli hii. Hakika sisi tunasema ya kuwa, hakika hadithi kwa matamshi yake na mafuhumu yake inasema kuwa ni juu ya kila muislamu kumfahamu Imamu wa zama zake, na ampe baia juu ya kukitekeleza au kukifuata kitabu na suna na haijulishi juu ya Imamu fulani maalumu.

Sasa kumuaminisha na kuufunga uimamu kwa maimamu kumi na mbili kumetoka wapi? Je si umeyasema hayo bila dalili?

Ikiwa tunamtaka Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, ni juu yetu kufuata dalili ya kidini, itakayo kuwa ni madhubuti tunachu-kua itikadi kutoka humo na hukumu, na itakayo kuwa ni yenye kutoa dhana tutachukua humo hukumu pekee, na haifai kwa muisilamu alie na ufahamu kamili abakie akiitakidi mambo yenye kudhaniwa na kuyaweka kwenye kiwango cha mambo ya itikadi bila kuwa na dalili na kusema kuwa Mahdi atakuja, na akaamini hivyo wakati ambapo hana dalili yoyote kati ya dalili za wahyi atakazo zitolea ushahidi juu ya kauli yake.

Na mimi ninatarajia kwa ndugu Ustadh na wafuasi wake watukufu kuwa maneno hayo niliyosema, yatulie na kukaa kwenye nafsi zao zilizo tulia ili kupata thawabu za Mwenyezi Mungu na radhi zake.

Wassalamu alykum warahmatullahi wabarakatuhu.

Damaskas, 15/Rabiiul-thani/89.  (29/07/69).

MUHAMMAD RIDHWANI Al-KASAM.

JAWABU  LA  BARUA

 

Assalamu alaykum warahmatullahi wa  barakatuhu.

 

Ama baada ya salamu,

 

01: Bado nina sisitiza kauli yangu ya kuwa Uislamu umeifa-nya akili kuwa ni chimbuko la itikadi na msingi wa Imani, na mimi niko pamoja nanyi katika kusema kuwa Itikadi hazichuku-liwi isipokuwa ni kutokana na yakini, na sitorudi nyuma kuhu-siana na haya hata kidogo, sawa natija au matokeo ya hadithi hii yawe ni yangu au yawe juu yangu.

02: Hakika hadithi za Mtume kuwa mutawatiri kwa kuelezea wazi na kuashiria (tuliko kuashiria kwenye ukurasa wa 14 kwenye chapa ya kwanza) zina mhusu Ali (a.s) na kuwa yeye ndio Imamu wa kisheria baada ya kufariki Mtume (s.a.w). Na tumekusudia kwa neno mutawatiri, tawaturi ya kimaana na sio ya kimatamshi, na tunasema hivyo kwa sababu hadithi zote zilizo zungumzia suala hilo pamoja na kusisitiza kwake, zinaelekea kwenye suala la uimamu wa mtu huyu kidhati na kumuainisha, na lau kama hadithi ambazo sanadi yake inakuwa ni ya Aahaad[76], (kufuatana na ibara uliyotumia) zingeelekea kulielezea jambo moja pekee hakika bila shaka yoyote, jambo hilo litakuwa mutawaatir.

03: Tulifanya bahthi ya Ismah kwa upana kwenye kitabu chetu Al-Imamah na ninatarajia utakisoma na kunipa rai yako kwenye maudhui hayo.

04: Ama kauli yako isemayo uteuzi na uainishaji na kulifu-nga jambo hilo kwenye idadi ya kumi na mbili, umetokea wapi? Na umekuja kutoka wapi? Je haya si umeyatowa bila dalili? Utapata jibu lako kwenye kitabu Al-Imamah kilicho ashiriwa vile vile.

05: Ama uliyo yataja mwishoni mwa barua yako kuwa Mahdi ni miongoni mwa masuala yanayo dhaniwa ambayo haifai kuyapa daraja ya kuwa ni jambo la kiitikadi, hakika maneno haya ni dalili ya kuwa hukukisoma kitabu hicho kwa mazingatio, na lau kama ungerudia kukisoma ungeona majina ya maswahaba ambao wamepokea na kusimulia hadithi za Mahdi kutoka kwa Mtume (s.a.w) na majina ya wanazuoni ambao wametunga vitabu kuhusu Mahdi, na majina ya mahufadhi walio mashuhuri ambao wamezi-thibitisha hadithi hizi kwenye vitabu vyao, na ushahidi wa wahe-shimiwa wengi juu ya kuwa hadithi za Mahdi ni mutawaatir na kukata shauri juu ya usahihi wake.

Basi ni vipi yakini isithibiti na  kukata shauri kwa yakini juu ya suala hili na kuwa na yakini kwa kuyashuhudia yote haya?

Na amani iwe juu ya mwenye kufuata uongofu na mwisho wa maombi yetu ni kuwa tuna mshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu.

 

***


 

[1] Rejea kwenye kitabu chetu Al-Imamachapa ya Beirut mwaka 1392 H (1972 AD)

[2] Rejea sehemu yetu ya uimamu.

[3] Hii ni hadithi yenyewe ya mtume, ameitoa Ibnu Hajar Al-haitamiy katika Swawaiqul-Muhriqa   ukurasa 99.

 [4] Almahdi wal-mahdawiya cha Dr Ahmad Amin Ukurasa 110.

[5] Jarida la chuo kikuu cha kiislam Toleo la 3 ukurasa 161-162.

[6] Adabu Shiia ukurasa 101 na anayaunga mkono Dr Abdul-haliim Annajaar kwenye utangulizi wake wa kitabu Al Mahdiyyi fil-Islam. Hakika maulamaa wa hadithi wanasimulia kuwa fikra ya mahdy imefikia daraja ya kuwa mutawaatir kwa maana (yaani hadithi nyingi zimekuja kwa maana hii hata ingawa matamshi yametofautiana).

[7] Adaabu Shia:16.

[8] Wuaadhu ssalaatwiin cha Dr Ali Al-wardu.

[9] Jarida la Atarbiyatul-Islamiyah/mwaka 14 toleo la 7/ukurasa:30.

[10] Alisimulia na kupokea kutoka kwake Ibnu Swabbagh Al Maaliky katika Alfusulul-Muhimma:275

[11] Amepokea kutoka kwake Al-haafidh Al-kanjii Asshaafii kwenye kitabu     chake (Al-bayaan).

[12] Na kuna Nuskha (kopi) iliyo chapwa na taasisi ya Maahadul makhtutwatil- arabiya ya Kairo.

[13] Zimepokewa hadithi kutoka kwenye kitabu hicho katika As-afu-rraghiin:139, na kuna kopi zake zillizo andikwa kwa mkono katika mji wa Halab na Istambuli. Na ninayo kopi iliyo tolewa na kusomwa kwa mtunzi na iliyo hifadhiwa huko halab.

[14] Kuna kopi iliyo andikwa kwa mkono huko Istambuli.

[15] Mtunzi amekitaja kwenye kitabu chake Al-aimatul-Itha ahar ,Uk:118.

[16]Kati ya vitabu hivyo viwili kopi iliandikwa kwa mkono iko Istambuli na ninayo kopi iliyochukuliwa kutoka kwenye asili ya kitabu cha

[17] alburhani kilichoandikwa kwa mkono na kilicho hifadhiwa huko Makka Mukarramah kwenye maktaba ya Haramul Makki.

5.Kitabu cha kwanza kopi ilio andikwa kwa mkono iko India na kopi ya Kitabu cha pili kiko Istambul.  

[18] Kuna kopi yake iliyo andikwa kwa mkono Istambuli.

[19] Majalatul-jaamia Al-Islamiyah: Toleo 3/ukurasa 131.

[20] Al-ghadir 2/184 chapa ya najaf 1365 H.

[21] Al-ghadiir 2/223.

[22] Diiwaanu, Daabul:42.

[23] Al-ghadiir 4/279.

[24] Matwaalibu ssaul 2/79.

[25] Sharhul-qawaid Assabul Alawiyat,  Uk:70.

[26] Al-aimatul Ithna-ashar :118.

[27] Diiwan Abdallah bin alawiy iitwayo Ad-duruhl-mandhum Uk:18 na      146.

[28] Swawaiqul-muhriq:99. Na irejee Al-Mahdi wal-mahdawiya.

[29] Hassan ni sifa ya hadithi kutokana na wapokezi wake.

[30] Rejea kitabu Al-mahdi:9.

[31] Aswawaiqul-muhriqa:99 na Is-aafu-raaghibiin:243 na Al-hawiy 2/124.

[32] Sunanu Ibnu maja:2/1368 rejea Al-fusulul-Muhimma:276 na Yanabiul-mawaddah:435 na Al-hawiy:2/124

[33] Tadhkiratul-khawaas: 377. Na rejea Sunani Abi Daud: 2/422 na Swawaiqul muhriqa:98 na Nurul-Abswar: 156-157 na Al-hawiy :2/129-137

[34]Sunanu Abi Daud:2/422, na Aswawaaiqul-muhriqa:97 na Is-aafur-raghi-biin:131 na Al-hawiy:2/124

[35] Sunanu Abi Daud:2/422 na Aswawaiqul-muhariqa:97,na Nurul-abswar:157 na Al-hawiy:2/124-126 na katika Musnad Ahmad bin Hanbali 1/376 na 377-430-448 Haitaondoka dunia au haitamalizika dunia mpaka awatawale waarabu mtu kutoka kwenye Ahlul-bait wangu,jina lake linafanana na jina langu. Na mfano wa hadithi hii iko kwenye Sunan At-tirmidhi:4/505 na Tadh-kiratul-hufadh:2/488 na rejea Sunanu Ibnu Maaja:2/1366.

[36] Yanabiul-mawaddah:448 na Al-hawiy:2/190.

[37] Sunanu Abi-daud:2/422na Al-bayaan:64 na Swawaiqul-Muhriqa:97 na Is-aafur-raaghibiin:131, na Sunanu Ibnu Maaja:2/1368 na Al-hawiy:2/124 na 137.

[38] Yanabiul-Mawadda:455, na katika Al-bayaan:82 na miongoni mwa hadithi ya Mtume ambayo ni ndefu, Kisha akapiga kwenye bega la Hussen na kusema Atatokana na huyu mahdi wa umma huu.

[39] Yanabiiul-mawaddat:445.

[40] Yanabiul mawadda:441/445.

[41] Yanabiul mawadda:443 na Is-aaf Ar-raaghibiin:139-140.

[42] Kuhusu orodha hii rejea, kwa kuongezea vyanzo tulivyo vitaja hapo nyuma-bahthi ya Shekh Abdul Muhsin Al-abal kwenye  majallatul-jaamiatul Islamyiyya toleo:3/128, nayo ina anuwani ya Aqidatu ahlisunna wal-athar fil-mahdiy Al-muntadhar.

[43] Majallatul jaamiatil-Islamiyyah Toleo:3/129.

[44] Al-Irhaad: 372 na Yanabiul-mawadda 451-452.

[45] Swahihu al-tirmidh :2/270 na Aswawaiqul-Muhriqa:97.

[46] Tadhkiratul-khawas:377 na matwalibus-saul:2/79 na Swawaiqul- Muhriqa :124 na Nurul Abswar:154.

[47] Alfusuulul-Ashara cha Shekhe Mufiid :13-14-.

[48] Alfusuulul-Ashara cha Shekhe Mufiid : 14

[49] Al-Irshaad:372.

[50] Al-Irshaad:372.

[51] Matwaalib As-sauli:2/79.

[52] Tadhkiratu-Khawaasi:377.

[53] Al-bayaan:102-112

[54] Wafiyatul-Aayan:3/316.

[55] Al-wafiy bil-wafiyaat:2/336

[56] Aswawaiqul-muhriqa:124

[57] Al-fusulul muhimmah:274

[58] Al-aimatul-Ithna ashar:117

[59] Tuhfat Al-twalib :17/A (imeandikwa kwa mkono na iko kwenye maktaba ya Haram ya Makka katika namba 33/historia/Dahlawi).

[60] Is-aafur-Raghibiin:140.

[61] Yanabiul-mawaddah:450-451.

[62] Sabaik Adhahab : 78.

[63] Nurul-Abswar: 154.

[64] Na mambo ya ajabu sana aliyo yasimulia Dr Ahmad Amini kwenye kitabu chake Al-Mahdi wal-mahdawiyat, Uk:108 kuhusu masala haya alipo sema ya kuwa Madhehebu ya Ibnu khaladuni ni kukubali (Alkhabarul Wahid) habari moja (hadithi) ikiungwa mkono na hukumu ya akili, na kuzikataa hadithi nyingi ikiwa akili haikuziunga mkono na kwamba yeye alipinga kuwepo kwa Mahdi na fikra ya Mahdi kwa sababu fikra hiyo inapingana na hukumu ya akili yake!!

[65] Rejea Kitabu Al-bayan cha Al-haafidh Al-kanji Ashaafii:102-113.Na sheikh Kanduzi Al-hanafii kwenye yanabiul-Mawadda ametoa hadithi ukurasa:448 kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas (radhi za Allah ziwe juu yao) wamesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): Hakika Ali ni wasii wangu na katika kizazi chake atatoka mwenye kusimama (juu ya haki) na mwenye kungojewa ambae ni Mahdi, ambae ataijaza ardhi kwa usawa na uadilifu kama ilivyo jazwa dhuluma na ujeuri. Nina apa kwa yule ambae amenituma kwa haki nikiwa mtoabishara na muonyaji, hakika wenye kusimama madhubuti juu ya kauli ya uimamu wake zama za kughibu kwake ni wachache zaidi kuliko baruti. Akasimama Jaabir bin Abdullah akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je huyo mwenye kusimama kutoka kwenye kizazi chako atakuwa na ghaiba (atatoweka na kuto onekana)?? Akasema Mtume: Ndio, ninaapa kwa jina la Mola wangu, Mwenyezi Mungu atawachekecha wale ambao wameamini na atawaangamiza makafiri. Kisha akasema: Ewe Jaabir hakika hili ni jambo kati ya mambo ya Mwenyezi Mungu na siri kati ya siri zake Mwenyezi Mungu, jiepushe kuwa na shaka kwani kutia shaka kwenye jambo la Mwenyezi Mungu ni kufuru.

[66] Yanaabiul-mawadda:488.

[67] yanaabiul- mawadda:495.

[68] Al-hawiy :2/152.

[69] Dr Ahmad Amin anawanasibishia mashia kuwa wao wana itakidi kuhusu Mahdi ya kuwa pamoja na kuwa yuko mafichoni huwatia hamasa wafuasi wake ili waondoe dhuluma na kwamba yeye anaishi mafichoni na huwaelekeza akiwa nyuma ya pazia kwa kuamuru na kukataza. Kitabu Al-mahdy wal-mahdawiya Uk:109na119 na vitabu vyote vya Shia vinasema wazi kuwa ameghibu na hawasiliani na yeyote, sasa ziko wapi kauli za kweli na iko wapi amana katika kunukuu habari?

[70] Pamoja na dalili zote hizi za Qurani zilizo wazi,hakika Dr Ahmad Amiin anaonelea kuwa mwanadamu hawezi kufichika na akabaki mafichoni kwa mamia ya miaka bila Mwenyezi Mungu kumpitishia hukumu ya kifo.Na akasema kuwa hilo haliwezekani isipokuwa kwa wajinga ambao wameondo-kewa na akili zao. Al-mahdy wal-mahdawiya:96.

Je Dr Ahmad anaonelea kuwa kusadikisha suala la kutohukumiwa kwa kifo kwa Nuhu na Yunusu na Nyangumi na watu wa Kahfu (pango) ni dalili ya ukosefu wa akili?

[71] Majallatul-Muqtatwaf,mwaka wa 59/juzuu ya tatu.

[72]Kutumia neno muhali si sawa, na sawa ni kuwa haionekani kuwa ni jambo lililo mbali kufanyika.

[73]Jaridatul-ambaa Aljarida Albaghdaadiya, toleo namba:40/mwaka wa kwanza/27  march/mwaka:-1965 A.D. 1.Bernardshow, cha Abbas Mahmud Al-aqqad/Silsila ya Iqrau/Tolea                

[74] 89/Ukurasa 124-125.

[75] Kwenye kitabu hicho Berardshow.

[76] Aahaad ni hadithi ambayo sio mutawatir iwe imepokewa na mpokezi mmoja au zaidi.

 

index