back page

MAREJEO  YA  KIAMA

 

 

 

 

) ǡ (

Suratu At-taghaabun. Wale ambao wamekufuru walidai kuwa hawatafufuliwa, sema ndio, ninaapa kwa (haki ya) Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa kisha mtapewa habari za yale mliyo yafanya, na jambo hilo ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu.

       ( )Suratul- Jaathiya

 Mwenyezi Mungu anakuhuisheni kisha atakufisheni kisha atakukusanyeni siku ya kiama, hakuna shaka kuhusu (suala) hilo.

( )

                  Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu.

 

 

 

UTANGULIZI

 

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.

Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe, na rehma na amani ziwe juu ya mbora wa viumbe vyake Muhammad na jamaa zake walio wema na walio twahirika.

Uislamu huu mtukufu na yote uliyo kuja nayo kwa viumbe mingoni mwa hukumu na amri, na kwa yote uliyo yakusanya kwenye pande zake kama kuwataka kutekeleza vitendo fulani au kuviacha vingine, na kwa yote uliyo yakusudia na kuyalenga kama kuyajenga maisha juu ya misingi madhubuti kati ya mahu-siano yote kwa ujumla, mahusiano ya mtu na jamii yake, na mahusiano ya jamii na watu wake na mahusiano ya wote hao na serikali au dola, na mahusiano ya dola na watu wake, kisha juu ya mahusiano hayo, akaweka uhusiano wa mtu na Mola wake,na mfumo au mwenendo wake kwenye ibada na kwenye kujikari-bisha kwa Mwenyezi Mungu.

Uislamu huu wenye kubakia milele na yote uliyo nayo kati ya hukumu hizo na mambo yaliyo amrishwa kufanywa, na nidhamu au mpangilio wa mambo, na mafunzo mbalimbali, je umemuachia muislamu  nafasi ya kufanya matendo na kufanya amali zake juu ya msingi wa uhuru na uteuzi, na kutekeleza amri hizo akitaka mwenyewe na kutofanya akitaka vilevile?

Au umemuwekea hali ya lazima ambayo haifai kujighafilisha nayo na kuzembea kwenye hali hiyo, na ili kudhamini kuwa ataji-lazimisha na kutekeleza, ukamuekea mwenye kukhalifu amri zile au mambo yale ya lazima adhabu na athari zingine zimfanyazo muislamu awe ni mwenye kutii moja kwa moja na kuyatekeleza yote kiukamilifu bila kughafilika?

Na ikiwa hukumu hizo amelazimishwa Muislamu kuzite-keleza bila kukhalifu hata kidogo, je adhabu ina husika tu na kule kwenda kinyume ambako habari zake huifikia serikali na serikali kumpitishia aliefanya matendo haya au alie khalifu amri hizo hukumu iliyo wekwa na kanuni ya maovu kwenye hali kama hii, kisha suala hilo linaishia au kukomea kwenye  mipaka hiyo tu?

Na upi msimamo kuhusu maovu na ukiukaji au kukhalifu ambako hufanywa siri na habari zake kutojulikana na kupotea njia zake na asitokee yeyote kuyafahamu wala kanuni kutekele-zwa?

Na ni upi msimamo wa ukiukaji ule ambao haumhusu yeyote kati ya watu ili aweze kusimama dhidi ya ukiukaji huo  mwenye kutoa habari za kufanyika kwake na kutoa dalili juu ya kuonyesha kuwa amefanya makosa alie kiuka na kufanya mambo yake, bali kila kilichopo katika ukiukaji huo ni kuwa ni uasi wa amri moja wapo kati ya amri za Mwenyezi Mungu katika kitendo kimojawapo kati ya vitendo vya sala au hukumu moja wapo kati ya hukumu za funga kwa mfano?

Na hata ukiukaji ule ambao hutekelezwa hukumu yake (kuadhibiwa kama kupigwa viboko au mawe) kwa Mwenye kutenda au kuchukuliwa fidia kutoka kwa mtendaji. Je ukiukaji huo hufuatia juu yake haki ya Mwenyezi Mungu (nayo ni ile iitwayo kuwa ni haki ya jumla kwenye istilahi ya kanuni zilizo wekwa) au ni kwamba kutekelezwa hukumu au kutoa fidia kunatosha kumtoa mfanyaji wa ukiukaji ule kwenye dhima ya haki nyingine yeyote?

Na muislamu huyu ambae anaitakasa nia yake kwenye utiifu na kuizuia nafsi yake na vitu vingi vyenye ladha na kujiziwia na matamanio yake na matakwa yake na vitu mbalimbali vipendwa-vyo na nafsi, kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujikaribisha kwake, kama vile mwenye kufunga ambae kiu na njaa humtaabisha na akaendelea kubakia kwenye hali hiyo na kutovijali vitu hivyo, au kama muuzaji ambaye anaweza kupu-nguza kipimo au kughushi (kudanganya) kwenye bei ya bidhaa lakini asifanye hivyo, na mfano wa hao watu ambao wanauwezo wa kufanya matendo ya haramu lakini wakajizuwia nayo na kujiepusha nayo.

Muislamu huyu ambae anajiwekea kwenye nafsi yake vitu kama hivi na kujinyima huku kuliko kukubwa, je matokeo ya kujinyima kule yanakuwa ni kuonyesha kuwa amemtii mola wake jinsi inavyo takiwa na hakuna kitu kingine nyuma ya utiifu huu, au kuna maana kuwa kuna malipo badala ya kujinyima kule anayo yahisi mwanadamu atakayo pewa badala ya kuwa amejinyima na kwamba matamanio ya kimaisha ya dunia yaliyo mpita haikuwa na hasara kwa maana ya kawaida ya hasara, bali ilikuwa ni aina fulani ya kujiwekea akiba na hazina, kiasi kwa-mba atayapata siku fulani yale malimbikizo yake ambayo ni mengi na matokeo yake ya manufaa na faida, na akahisi wakati huo raha na utulivu na kupata msukumo zaidi wa kuweka hazina na kujilimbikizia kwa hamasa kubwa na ikhlasi?

Na mbadala huu tulio uashiria ikiwa utasihi basi ni lini utafanyika? Na itakuwa vipi, yaani utatekelezwa vipi?

Ni lazima ufanyike mbadala huo baada ya kuwa mwanadamu ameukamilisha umri wake wote na siku zingine za uhai wake ili ionekane wazi ni kwa kiasi gani anastahili malipo haya katika hali ya kumrudia Mola wake na kufanya utiifu, au kustahili kupata mateso na adhabu, katika hali ya kuvuka mipaka na kufanya maasi.

Kwa hivyo ni lazima kuwe na hali ya kurejea baada ya kifo kwenye hesabu na kuhukumiwa ili kumpa kila  mtu anayo stahili kupewa kati ya wema au ubaya yakiwa ni malipo ya matendo aliyo yatanguliza na kazi alizozifanya. Lakini je linawezekana hilo? Na dalili yake ni ipi? Na je mwanadamu mwenye akili na busara anaweza kuamini kuwa kuna uwezekano wa kurejea baada ya kufa, kwa ajili ya kufanywa hesabu na kumuangalia au kumuainisha anaestahili kupata thawabu au adhabu.

Hayo ndio yatakayo elezewa kwenye kijitabu hiki kwa kuya-bainisha na kuyafafanua, na kukiwa na matarajio ya kuyaweka wazi masala hayo na kuyadhihirisha kwa msomaji mwenye kutaka kuelewa, tukilazimika katika kufanya hivyo kutumia ibara zilizo salama, na fikra zilizo wazi, na kurahisisha kwa haya tuyazungumziayo, na kujiepusha na istilahi za kifalsafa na mambo mengine yaliyomo kwenye falsafa hizo kama kutumia maneno magumu na yasiyo eleweka.

Na matarajio yangu yote ni kuwa kurasa hizi zimekusanya mambo na malengo yaliyo kusudiwa, na zenye kufikia na kuyathi-bitisha makusudio, na kuyaelezea kama inavyo stahili kwenye ufafanuzi wa masala haya, na kuyabainisha kiukweli wake wa asili ulio safi.

Na jambo linalopaswa kusemwa ni kuwa:

Huenda msomaji akawa na matarajio kutoka kwangu, nami nikizungumzia msingi huu muhimu kati ya misingi ya uislaam kuwa bahthi yangu ni bahthi ya kiakili tu iliyo wazi kwa kuzichukua rai na kuzijibu, kama vile ambavyo hufanya bahthi kwenye masala ya kifalsafa na kutoa msimamo kutoka kwenye bahthi hiyo kwa uhuru kamili wa kupinga na kukubali.

Lakini, uhakika wa mambo hapo unatulazimu kufuata mfumo mwingine unaotofautiana na huo unaotarajiwa kwa tofauti kidogo.

Tunafanya hivyo kwa sababu sisi tunaishi katika hali ya kuamini marejeo kwa ujumla wake na tukiwa ndani ya uzio wa itikadi na hukumu za sheria, na ni lazima kwetu, kutokana na hali hii, tuzitegemee dalili na ushahidi wa Mwenyezi Mungu  (ushahidi wa Quran) kifikra, kimfumo na kidalili na kurudi kwenye Quran kila tunapo taka kuchagua kilicho bora au kinacho faa kati ya vitu vinavyo dhaniwa kuwa vinafaa, vitolewavyo kwa ajili ya kufanyiwa utafiti na kujadiliwa, na kwamba tusivuke na kutoka kwenye mambo hayo kwa ujumla, kwenye duara hilo lililothabiti na lenye mipaka maalumu ambayo haifai kuivuka kwa hali yoyote ile.

Na kulazimika kufanya hivyo hakuna aibu yoyote au jambo la kushangaza au upingaji wa hukumu ya kiakili, bali huenda ikawa ndio natija ya kimantiki pekee ambayo haina shaka yoyote kuisema na kuifuata miongozo yake, maadamu inawekwa na hali ya kwenda hatua kwa hatua kwenye Imani ya misingi ya itikadi, na kuifanya kuwa ni mfumo kwa maana kamili ya neno hilo, na wenye kuwiana wenyewe kwa kiwango cha juu kabisa.

Hakika tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Muumba na Muwekaji wa vitu vyote, na hatukuwa na dalili juu ya Imani hiyo isipokuwa  akili pekee.[1]

Na tukaamini, kutokana na hayo na kwa kukubali na kuwa chini ya hukumu ya dalili, uadilifu wake ulio takaswa na matama-nio na uongo na dhulma na makusudio mabaya.[2]

Kisha tukaamini, kutokana na hayo vilevile, na kwa kukubali kuwa chini ya hukumu ya dalili, utume na ujumla wa mitume wote, na utume wa mwisho ( wa Mtume Muhammad) (s.a.w) pamoja na yote yaliyomo ndani yake kama vile wahyi na kuwe-kwa kwa sheria.[3]

Na kwa kuamini kwetu sehemu hizi tatu zenye kufuatana moja baada ya nyingine, bahthi ya kiitikadi kuhusu maaadi ina kuwa ni sehemu ifuatayo sehemu zilizo tangulia, kwa sababu sehemu hii inategemea kwanza msingi wa Imani juu ya Mwenyezi Mungu Muumba, Muadilifu, na pili Imani ya Mtume aliye Mkweli na mwenye kuswadikishwa, na tatu kukiamini kitabu cha Mwenyezi Mungu kilicho teremshwa.

Baada ya hayo hakutabakia jambo la kushangaza ikiwa tutafanya kuwa ni lazima mazungumzo yahusianayo na itikadi yasitoke, kufuatana na hali inavyo lazimu kwenye mipaka ya Kitabu hiki (Quran) na sheria zake maalumu, kwa kuzingatia kuwa kitabu hiki ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake (s.a.w).

Pamoja na yote hayo hakika sisi kwenye mwendo wetu ndani ya maudhui haya hatuta jiepusha na akili na dalili au ushahidi wake, bali tutaielekea kwa heshima ya kiwango cha juu, ili tuiulize ni kiwango gani imekinaika na masala ya marejeo (kiama) na kwamba ni jambo ambalo ni muhali kuwa au linawezekana? Na kwamba je ni katika vitu ambavyo akili ina uwezo wa kuwaza kutokea kwake au haiwezi kuliwaza na kulifikiria? Na je jambo hili linawiana na akida au haliwiani?

Na kwa kufanya hivyo, yote hayo kwa muhtasari wake yanakuwa ni mchanganyiko mzuri wa kufuata dalili (Quran) na kutokiuka kamwe, na kufuata muongozo wa akili, bila kupunguza haki au kupitukia kwenye haki ya upande wowote kati ya pande mbili (Qurani na akili).

Na Mwenyezi Mungu amesema kweli pale aliposema:

( ) Mwenyezi Mungu hakuna Mungu isipokuwa yeye, atakukusa-nyeni katika siku ya kiama hakuna shaka kwa hilo, na ni nani mkweli zaidi kwenye mazungumzo kuliko Mwenyezi Mungu?

)                                                                                     .(

Na wanasema:Ahadi hiyo ni lini (itakuwa), ikiwa nyinyi ni wakweli? Sema:Mnayo miadi (marejeo) siku ambayo hamtache-leweshwa hata saa moja wala kutanguliziwa.

                      ( )

Siku ambayo kila nafsi itayakuta mambo yote ya kheri iliyo yatenda yakiwa yameletwa mbele yake na maovu aliyoyatenda.

    )   ( ɡ ɡ ɡ  

 Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye na mama yake na baba yake, na mkewe na watoto wake. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na jambo lenye kumshughulisha. Nyuso siku hiyo zitakuwa ni zenye kumeremeta zikicheka na zenye bishara  na furaha, na nyuso zingine siku hiyo zitakuwa na mavumbi juu yake zikiwa zimefunikwa na giza na weusi.

Na mwisho wa maombi yetu ni kuwa tunamhimidi Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe.

Al-Kaadhimiya-Iraq.

 

MUHAMMAD  HASSAN AALU-YAASIN.

 

 

 

***

 

 

MAREJEO  NI  LAZIMA

 

Hakuna budi kwa mwenye kufanya utafiti wa kimaudhui, kwenye masala ya  Al-maaad (marejeo) kwanza kabisa asimame katika mwendo wa utafiti wake kwenye fikra ya Al-maaad akiwa hana rai yoyote ihusianayo na maudhui haya kama maelezo na ufafanuzi juu ya masuala haya, ili uweze kuthibiti ukubwa na ulazima wa kuwepo marejeo na kuwa ni lazima yatokee kwenye ulimwengu wa itikadi na aweze kufahamu sababu zifanyazo kuwa ni lazima marejeo yatokee na ulazima wake na dalili zake za kidini.

Na mwenye kufanya utafiti akiweza kusimamisha dalili juu ya jambo hili la lazima, hapo atakuwa na uwezekano wa kuhamia kwenye hatua ya utafiti mwingine na kutoa au kuendelea kutoa maelezo kuhusu maudhui hayo, na kufanya hivyo ni kwa sababu ya kuwa, kuikubali hatuwa hii inakuwekea msingi mzuri na madhubuti au ina kuandalia njia ya kuyakubali mambo yanayo-tokana na kukiri huku ambayo ni kama matawi ya jambo hili la asili.

Na hatutoweza kufikia kwenye natija itakiwayo isipokuwa kwa kwenda taratibu hatua kwa hatua kuelekea kwenye natija hiyo kwa kupitia hatua ambazo zote zina ungana na kila ifuatayo ikiwa imeungana na iliyotangulia kwa kiunganishi madhubuti ambacho kitatuondolea pazia na ukweli kuonekana:

 

01: Je mwenyezi mungu aliamuru na kukataza?

 

Sidhani ya kuwa kuna watu wenye kuelewa na wenye akili timamu wasio elewa -kwa maana halisi ya kuelewa- ya kwamba Mwenyezi Mungu ameamrisha na kukataza na kwamba sheria ya kiislamu ni mkusanyiko mkubwa wa amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu.

Na usomaji wa haraka kwenye Qurani tukufu unatupa dalili isiyo na shaka juu ya hilo, amesema Mwenezi Mungu Mtukufu:

( ) Simamisheni Swala na mtoe zaka

( )Imefaradhishwa juu yenu funga kama ilivyo faradhishwa juu ya wale ambao walikuwa kabla yenu.( ) Na amefaradhisha Mwenyezi Mungu juu ya watu kuhiji kwenye nyumba (Tukufu).

( ) Na fahamuni ya kwamba kitu chochote mtakacho kipata kama ghanima (faida) hakika khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu.

( ) Piganeni kwenye njia ya Mwenyezi Mungu ki kweli kweli.

( ) Mwenyezi Mungu amehalalisha biasha-ra na ameharamisha riba.

( )

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na ihsani (wema) na kuwapa haki watu wa karibu, na anakataza machafu na maovu na uzinifu.

( ) Na baadhi yenu wasiwasengenye baadhi  (wengine)

( ) Msichunguzane.

( ) Hakika huzua uongo wale ambao hawaziamini aya za Mwenyezi Mungu.

( ) Jiepusheni sana na dhana.

( ) Ole wao wenye kupunguza vipimo.

Na aya tukufu nyingine zilizo mfano wa hizi zilizo jaa amri na makatazo mbali mbali ya Mwenyezi Mungu.

Kwa hivyo basi, hakuna shaka hata kidogo kuwa Mwenyezi Mungu ame amuru na kukataza.

 

02: Je amri hizi na makatazo hayo yalikuwa ni mambo ya lazima au ni muongozo?

Hakika elimu ya Usulul-fiqhi imemaliza kuyafanyia utafiti masala haya kwa upana zaidi, na muhtasari wa utafiti huo kuhusu maana ya amri ulikuwa ni kwamba: Amri ni dalili ya uwajibu (wa jambo) na iko dhahiri katika uwajibu pale ambapo amri hiyo itakuwa haina alama ijulishayo kuwa ni jambo la mustahabu (lisilo lazima bali linapendeza). Na kwamba Uwajibu unatokana na hukumu ya akili kwamba ni lazima kutii amri ya mola (bwana) na kwamba ni wajibu kutekeleza amri yake kwa ajili ya kutekeleza haki ya utawaliwa na kuwa mja. Kama ambavyo muhtasari wa Nahyi (Katazo) ni kuwa neno la kukataza ni Kama neno la amri katika kujulisha kwake (ni dalili) juu ya ulazima (wa kuacha kitendo) kiakili na katazo liko dhahiri katika kujulisha kuwa jambo lililo katazwa  ni haramu. Na kwamba swigha ya kukataza ikitoka kwa mtu ambae anawajibika kutiiwa, itakuwa natija na matokeo ya ulazima wa kumtii mtawala huyo na uharamu wa kumuasi, kwa hukumu ya akili, kwa kutekeleza haki ya utumwa na utawaliwa, ni kutofaa kuacha kitendo ambacho amekikataza.[4]

Na vipi amri isiwe hivyo wakati Mwenyezi  Mungu amesema:

( ) Alicho kupeni Mtume kichukueni na alicho kukatazeni kiacheni.

Na anasema Mwenyezi Mungu:

( )

Na wajihadhari wale ambao huenda kinyume na amri zake kupatwa na mitihani au kupatwa na adhabu iumizayo.

Kwa hivyo basi, hapana budi kusema kuwa amri na maka-tazo ya Mwenyezi Mungu ni mambo ya lazima kwa maana kamili ya neno hilo, na hakuna nafasi ya kuchagua (khiyari) na kutoa ruhusa.

 

03: Ni nini matokeo ya kukhalifu amri na makatazo?

Na ikiwa Mwenyezi Mungu ameamuru na kukataza, na amri zake na makatazo yake yakawa ni mambo ya lazima, haifai kuyakiuka na kwenda kinyume nayo, basi je matokeo ya ukiukaji huu ni mateso na adhabu, kwa maana ya kimadi, au masuala haya hayavuki athari za kiadabu na kimaanawiya ya ukiukaji tu.

Na inatosha kujibu swali hili kuonyesha aya za Qurani zifuatazo ili tuweze kuelewa matokeo ya ukiukaji wa amri za Mwenyezi Mungu na matokeo yake.

Anasema:

( )Na mwenye kwenda ki-nyume miongoni mwao na amri zetu tutamuonjesha adhabu ya moto.

( ) Hakika mimi nina ogopa, ikiwa nitamuasi Mwenyezi Mungu, adhabu ya siku kubwa.

)                                                                                                       .( 

Na ni kijiji gani kilicho kwenda kinyume na amri za mola wake na Mtume wake tukakipa hesabu iliyo kali na tukakiadhibu kwa adhabu iumizayo.

( ) Ni kitu gani kilicho kuingi-zeni motoni? Wakasema hatukuwa ni miongoni mwa wenye kusali.

( )Ole wao wale ambao walidhu-lumu kutokana na adhabu ya siku iumizayo (kali). Kwa hivyo basi, hapana budi kusema kuwa kutakuwa na adhabu za kimwili juu ya kila mwenye kukiuka amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu ambazo kwa ujumla wake huunda kitu tukiitacho kwa jina la Sheria za kiislamu.

 

04: JE AHADI ZA THAWABU NA ADHABU ZA MWENYEZI MUNGU NI VITU VYA KWELI AU ZINA MALENGO YA KUWAHIMIZA WATU KUFANYA  TWAAA?

 

Zimenifikia habari ya kuwa kuna watu wasemao kwamba: Hakika Quran kurudia mara kwa mara kutaja marejeo baada ya kufa, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu aliwaahidi malipo mema watiifu na akaahidi kuwaadhibu waasi, hakika kufanya hivyo ni katika njia ya kuhimiza na kuwatisha tu ili watu waweze kuwa na msukumo wa kufanya utiifu na kujitenga na maasi, bila kuwepo lengo la kweli la maana ya kimaddi la kufikia kwenye neema au adhabu, kana kwamba msemaji huyu katika maneno yake haya ameyasema kutokana na itikadi yake isemayo kuwa kiwiliwili hupotea na kupukutika, na kwa kufa haiwezekani kukirudisha baada ya kupukutika kutokana na kuwa ni muhali kukirudisha kwenye hali yake ya mwanzo kitu ambacho kimetoweka, na wakati huo hakubakii nafasi ya kuwepo neema na adhabu kwa maana yake ya kimaddi, kwa Hivyo waadi (kuahidi) na waidi (kutishiwa) vina kuwa ni vitisho tu visivyo na maana yoyote kati ya maana za kutekeleza.

Na ukweli ni kuwa sisi tunapo soma Quran tukufu, na Mwenyezi Mungu aliiteremsha kwa lugha ya kiarabu iliyo wazi, na sisi ni wana lugha yake na wenye kufahamu zaidi sehemu za kutumia maneno yake na maana yake na matamshi yake, hatuoni sababu yoyote  itupayo ruhusa ya kulitafsiri tamko tofauti na dhahiri yake na maana yake kwa sababu limekuja tamko hilo likiwa halina alama ijulishayo kukusudiwa maana iliyo tofauti na dhaahiri ya maneno yake.

Na ikiwa matamshi yatumikayo kwenye sehemu ambazo Qurani inawahutubia watu yametumika bila kuwa na alama inayo ruhusu kufanya taawili, ina lazimika basi kuyachukulia matamshi hayo kwenye maana yake halisi na ya asili, na haifai kwetu kwa hali yoyote kuyachukulia kwenye maana ya majazi (yasiyo ya hakika) au mubalagha (kusisitiza) au vitisho au ahadi za uongo ziwatiazo watu hamasa ya kufanya kitu fulani.

Na tutatoa, katika sehemu ifuatayo, baadhi ya aya tukufu ambazo zinakusudia kutaja ufufuo na marejeo na zikisisitiza kutokea kwa mambo haya kwa masisitizo kamili, ili tuweze kufahamu kwa uwazi wake usio na kipingamizi na usio na taawili, na ubainifu wake ulio safi ambao haukubali maana yoyote kati ya maana za kufunga na za mzunguko.

( )Kama tulivyo anza kumuumba kiumbe wa mwanzo tutamrudisha, ni ahadi iliyo juu yetu hakika sisi ni wenye kufanya hivyo.

( )Amewawekea muda maalumu usio na shaka kutokea kwake.

( )Na tumewafufua hatukumuacha yeyote miongoni   mwao.

   ȡ ) (               Na kitawekwa kitabu, na utawaona watu waovu wakiyaogopa yaliyomo ndani ya kitabu hicho na wakisema, ole wetu kina nini kitabu  hiki hakiliachi jambo dogo wala kubwa isipokuwa tu kimetoa hesabu yake na watakuta waliyo yafanya yamewahu-dhuria (mbele yao) na Mola wako hatamdhulumu yeyote.

( )Kisha nyinyi baada yake mtakufa kisha hakika nyinyi siku ya kiama mtafufuliwa.

( ) Je mnadhania ya kuwa tumekuumbeni kwa mchezo na kwamba nyinyi hamtarejea kwetu?

      ( ) Ewe Mola wetu hakika wewe ni mwenye kuwakusanya watu siku ambayo haina shaka ndani yake (juu ya kuwepo kwake). Hakika Mwenyezi Mungu haendi kinyume na ahadi zake.

     )                            (               ǿ         Enyi majini na watu je hawakukujieni Mitume watokanao nanyi, wakikusomeeni na kukusimulieni aya (dalili) zangu na wa-kikuonyeni  kuhusu kukutana na siku yenu hii? Wakasema: Tunashuhudia juu ya nafsi zetu, na maisha yao ya dunia yakawa-hadaa.

( ) Hakika siku ya kutolewa hukumu ni yenye kupangwa na kuahidiwa kwa wakati maalumu.

( ) Hiyo ni siku ya haki basi mwenye kutaka ashike njia na aende kwa Mola wake.

 ( ) Na kila nafsi ikapewa malipo ya matendo iliyo yafanya, na yeye Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi wa mambo wayafanyayo.

  ȡ )     )                      Na wakasema wale ambao walikufuru, hakitatujia kiama. Sema ndio na ninaapa kwa haki ya Mola wangu hakika kitakujieni hicho kiama, (Mwenyezi Mungu ni) Mjuzi wa mambo ya ghaibu, hakuna kijifichacho kwake hata kama ni kiasi cha tembe ndogo iliyoko mbinguni na wala ardhini, na hata kilicho kidogo zaidi ya hicho wala kikubwa isipo kuwa kimo kwenye kitabu kilicho wazi, ili awalipe wale ambao walio amini na wakafanya matendo mema. Hao wana msamaha na riziki iliyo bora.

 (    (            Na wakaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa viapo vyao vya nguvu kwamba Mwenyezi Mungu hatowafufua walio kufa. Kwa nini (asiwafufue)?  Ni ahadi iliyo lazimika kwake (kuwafufua na kuwalipa) lakini watu wengi hawajui. Ili awabainishie yale ambayo walikuwa wakitofautia ndani yake na ili wale walio kufuru waelewe ya kuwa wao walikuwa ni waongo.

    )                                                                                     (       Na ni kipi kikujulishacho ni ipi siku hiyo ya mwisho? Kisha ni kipi kikujulishacho ni ipi hiyo siku ya mwisho? Siku ambayo nafsi haitamiliki kwa ajili ya nafsi nyingine kitu chochote na amri siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivo natija ni ipi?

Ikiwa Mwenyezi Mungu ameamrisha na kukataza, na amri zake na makatazo yake yakawa ni ya lazima kutekelezwa.

Na ikiwa kukiuka amri hizi na makatazo haya humlazimu mtu kupata adhabu.

Na adhabu hiyo ikawa ni adhabu ya kimada kwa maana yake maalumu na sio kwa ajili ya kuogopesha watu na ya uongo.

Basi kwa hivyo ni lazima tuseme ya kwamba: Marejeo ni jambo la lazima na hakuna makimbilio kwa muislamu, ila kusema hivyo na kuamini ulazima wake na kwamba bila shaka yatatokea.

Na haya ndio ambayo tumefahamishwa na aya tukufu tulizo zitaja, kwa kusema wazi kuwa marejeo ni jambo lisilo na shaka kutokea kwake nayo ni siku ya haki ambayo haitacheleweshwa kwa muda wa saa moja wala kutangulizwa saa moja, na kwamba lengo la kuwekwa siku hiyo ni kuwahesabia watu na kuwahu-kumu, ambapo hupewa kila nafsi malipo yake iliyo yatenda, kufuatia kitabu kisicho acha jambo dogo wala kubwa isipokuwa hutoa hesabu yake, kwani ndani ya kitabu hicho kila nafsi itakuta mambo ya kheri iliyo yatenda yakiwa yamehudhuria mbele yake, na mambo mabaya iliyo yatenda, na wakati huo waovu watakuwa wakiogopa yaliyomo ndani yake.

Na kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kurejea ni ahadi iliyo ya haki juu yake na ni nani mkweli zaidi kuliko Mwenyezi Mungu katika uzungumzaji, na kwamba wale ambao walidai ya kuwa hawatofufuliwa na kwamba hakitawajia kiama ni makafiri na waongo, na adhabu kali siku hiyo itakuwa kwa wakadhibi-shaji, wale ambao wanaikadhibisha siku ya mwisho, na haika-dhibishi siku hiyo isipokuwa kila mwenye kukiuka na mwenye dhambi. Amesema kweli Mwenyezi Mungu mtukufu.

Na tunapofikia kwenye natija hii kutokana na mtiririko wa mazungumzo, inakuwa ni lazima, ili bahthi hii ienee pande zake zote, tusimame sehemu hii kwa muda ili tuchunguze kwa yakini ni kitu gani hasa kitakacho rejea?

Je roho pekee kama walivyo dai wasemao kuwa ni muhali kurejea kiwiliwili? Au mwili pekee, kama Jubai alivyosema na wafuasi wake kuwa roho na mwili vile vile? Au ni roho na mwili kama waaminivyo wana fikra wengi wa kiislamu?!

Hakika lifahamikalo haraka akilini, na kwenye ufahamu kutokana na mfumo wa aya za Quran zinazo husu maudhui haya, ni kuwa marejeo yatakuwa ni ya mwili ulio hai wenye kuhisi na kufahamu ladha ya neema na machungu ya adhabu, yaani mwili wenye roho ukiwa una sehemu zake zote uzitumiazo na kufaidika nazo na sifa zake na tofauti zake.

Na kwamba aya hizo kutokana na maana yake kuwa wazi na makusudio na maana kuwa bayana na lafdhi, zinakataa aina yoyote ya kutafutwa maana kwa ujanja au kufanyiwa taawili ambayo pengine wanaweza kuitegemea watafutao maana kwa ujanja na wafanyao taawili. Basi huenda ikawa ina uwazi wa hali ya juu katika maana na madhumuni, uwazi ambao unazuwia kusiwezekane kuificha na kuifunika funika na kuzungusha huku na kule kwa aina yoyote ile.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

) ɡ . (.

 

Suratu-fuswilat:18-22 Na (wakumbushe) siku maadui wa Mwenyezi Mungu watakapo kusanywa katika moto wakawa manatengwa makundi makundi, hata watakapo ujia (moto huo), macho yao na masikio yao na ngozi zao vitatoa ushahidi juu ya yale waliyokuwa wakiyatenda. Na wataziambia ngozi zao: Kwa-nini mnatushuhudilia? Zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambae alie kitamkisha kila kitu na ndie alie kuumbeni kwa mara ya mwanzo, na kwake mnarudishwa. Na hamkuwa ni wenye kujifichia yasiweze kutoa ushahidi juu yenu macho yenu wala masikio yenu wala ngozi zenu, lakini mlidhani kuwa Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika yale yote mnayo yafanya.

) (                                                                                           Surat-Yassin:56     Hivi leo tunaweka vizibo juu ya midomo yao, na mikono yao itazungumza nasi, na miguu yao itashuhudia waliyo kuwa wakiya-chuma.                                                                                                 

) ǡ (

Suratu Annisaa:56.Hakika wale ambao walikufuru aya zetu tutawaingiza motoni, kila zitakapo iva ngozi zao tunawabadili-shia ngozi zingine, ili waonje adhabu.     

) (

                                                              .Suratul-Kiyama 3-4

Je mwanadamu anadhani ya kuwa hatutaikusanya mifupa yake? Kwa nini! Sisi ni wenye uwezo wa kukusanya misitari ya ncha za vidole vyake.

Hakika usomaji wa uchunguzi makini wa aya hizi, unatuju-lisha kwa dalili iliyo wazi na kwa ubainifu ulio mkubwa juu ya kuwa, marejeo yatakuwa  ni mwili na roho kwa hali yake ya kawaida, ukiwa na masikio, macho, ngozi, midomo, mikono, miguu na mifupa, kuhisi maumivu na adhabu. Na maneno haya hayawezi kudhaniwa kwa aina yoyote ya dhana na shaka na taawili .

Na hapa ni lazima tusiache na kusimama angalau kidogo kwenye aya mbili za mwisho ili tusimame kwenye nukta zile za kielimu ambazo zimeashiriwa na kuelezwa na aya mbili zilizo-tajwa, na kwenye uhakika ule ambao aya hizo mbili zimetunaba-hisha juu yake kabla hazijagunduliwa na elimu ya kisasa kwa muda wa karne na karne, mambo ambayo tunaweza kuyachu-kulia kuwa ni miongoni mwa dalili kubwa kabisa zilizo wazi za kuonjesha umuujiza wa kitabu hiki cha muujiza na cha milele.

Hakika sababu ya kufanya hivyo ni mambo yaelezwayo na tiba ya kisasa kwamba mishipa ya maumivu iko kwenye tabaka la ngozi, ama viungo vya ndani na mishipa yenye nyama na viungo vilivyomo ndani hisia zake ni dhaifu, kutokana na hali hiyo daktari huelewa kwamba kuungua kidogo ambako hakuvuki kwenye ngozi huwa na maumivu makali sana tofauti na kuungua sana ambako huvuka kwenye ngozi hadi kufika kwenye viungo vya ndani, kwa sababu pamoja na kuungua sana nakuwepo kwa hatari, hakutoi maumivu makali, na Mwenyezi Mungu ana-tuambia: Hakika moto kila unapo ila ngozi ile yenye mishipa ya maumivu tunaibadilisha na kuweka ngozi mpya ili maumivu yaendelee bila kukatika, na ili waonje adhabu iumizayo.

Na hapa inadhihiri na kuonekana hekima ya Mwenyezi Mungu kabla mwanadamu hajafahamu, na Mwenyezi Mungu ni Mtukufu na mwenye hekima.[5]

Ama aya ya pili ndio aya ambayo inawapinga wasio amini marejeo kwa kutoamini kwao marejeo, kisha inasisitiza juu ya marejeo: Kwa nini! tunaweza kuiweka sawasawa mistari ya ncha za vidole vyake (au viganja vyake). Basi ni zipi sifa hizi za mistari hii?

Elimu ya kisasa inasema:

Hakika Banaan ni mpangilio wa kitaalamu ulio mzuri na wa ajabu uliopo kwenye mistari ya ncha za vidole Michoro ya misitari ya vidole vya mwanadam, na kwamba kila mwanadamu ana michoro na miundo ya kitaalamu yenye kutofautiana kiuka-milifu na miundo ya mtu wa pili vyovyote watakavyo kuwa karibu kwenye damu au kizazi au nasabu (ukoo), na hakuna kwenye jamii ya wanadamu wa ulimwengu huu watu wawili wenye kufanana misitari ya vidole vyao.

Na katika uchunguzi wa ncha za vidole vya mwanadamu uliofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1884 A.D, uchunguzi ulio kuwa makini baada ya kugunduliwa vyombo vya kukuza vitu, elimu iliweza kuthibitisha kuwa kila mwanadamu ana ramani yenye umbo maalumu na yenye sehemu madhubuti na makini za mistari iliyo pangika ambayo zimechukua umbo maalumu zuri na lenye kupendeza kwenye ngozi ya vidole vyake, vikionyesha hali yake ya siri ambayo imewekwa na uwezo wa Mwenyezi Mungu wa hali ya juu kwenye vidole vyake.

Hakika mistari hii huwa ni yenye kuonekana wazi na yenye ncha iliyo pinda na iliyo  chimbika na yenye umbile jembamba sana, kiasi kwamba huonekana sehemu zake zote zilizo nyembamba na michoro yake na miundo yake juu ya karatasi pindi unapo pakazwa juu ya karatasi wino na  kukandamiza juu ya karatasi.

Vilevile huonekana na kubakia mistari hii ikiwa thabiti juu ya madini yaliyo mororo na kioo na ubao ulio safi kutokana na ngozi ya ncha za vidole kuwa na tezi zitoazo jasho na mafuta.

Na sensa ya ulimwengu wa leo iliyofanywa kwa ajili ya kufanya utafiti wa elimu ya mistari ya vidole imeeleza kwamba katika kila watu milioni mianne, hupatikana alama moja inayo ashiria kufanana kiukamilifu kwa mistari yote kati ya watu wawili, isipokuwa ni kwamba kufanana huko hakuwi na kufikia kiwango cha kuwa sawa na kufanana kiukamilifu.

Na hivi leo vimefunguliwa vituo maalum vya kielimu  pembe zote za dunia ya leo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa elimu ya mistari ya vidole, ili kuwajua na kuwatambua  watu kwenye miamala na matendo yao na kwenye matukio ya uovu na wizi, kiasi kwamba hugundua kuwa kwa kugusa tu kioo au kuishika silaha au chombo chochote huacha juu yake alama  na athari zikiwa zimethibiti, na kisha alama na athari hizi huchapishwa kwenye karatasi kwa njia maalumu ili kuzihifadhi na kuzifanyia uchunguzi na kuzifanya kubwa kwa ajili ya kuzilinganisha na mistari ya vidole vya watuhumiwa na washukiwa.

Na miongoni mwa mambo ya ajabu sana ni kuwa maumbo haya ya kitaalamu yaliyo jipanga vizuri kwenye ramani ya ncha za vidole vya mwanadamu, yanabaki yakiwa thabiti tangu saa ya mwanzo ya kuzaliwa na muda wote wa uhai, kiasi kwamba misingi yake haiathiriki kwa kukua kwa mwili bali huwa vikubwa na kupanuka pembe zake bila mabadiliko yoyote, kana kwamba yamewekwa chini ya chombo cha kuzikuza wakati wa kuzili-nganisha kati ya ramani mbili katika siku za utotoni na wakati anapo kuwa mkubwa na utaziona kuwa ni nuskha (kopi) iliyo sawasawa na asili yake kabisa bila kubadilika.

Na miongoni mwa mambo yashangazayo kweli kweli ni kuwa ramani ya mistari ya vidole inapopatwa na uharibifu au kasoro kutokana na kusagana au kusagika wakati wa kazi au pindi inapo jeruhiwa na kuungua kwa kiasi kikubwa, na kuungua juu juu, viungo vya mwanadamu hukua ili kuirudisha ramani ile ile ya asili  na sehemu zake zote zikiwa zimepangika kwa umakini wake wa kiwango cha juu sana na sifa zake za hali ya juu za kitaalamu na muungano wake wenye kupendeza kama kwamba kuna mkono uliojificha unaoziamrisha chembe zake zikue kwa muelekeo maalumu na kuweka picha iliyo sawa na ile ya asili ya msitari iliyo haribika bila kukosea au kutofautiana.

Na hakika elimu na utafiti wa mistari ya vidole zimethibitisha kuwa umbo na ramanai zake za kitaalamu na mistari yake yenye kupambwa hurejea kwenye maungio manne ya msingi:

01- Kiungio cha mistari iliyo pinda kama upinde.

02- Kiungio cha mistari iliyo nyooka.

03- Kiungio cha mistari ya kudumu au kuendelea, yenye mzunguko ulio unganika kwenye sehemu kuu au kituo kikuu na iliyo ingiliana na mingine na ambayo hukua umbo lake taratibu ikianzia ndani hadi kutokezea nje, nayo hushirikiana kwenye kituo kimoja kikuu katikati ya kiganja.

04- Kiungio cha mistari iliyo pandana, nayo ni mchanganyiko wa mistari ya viungio vitatu. Kiungio cha mistari iliyo pinda kama upinde, na ilio nyooka, na ya kudumu au ya kuendelea, kiasi kwamba vinakuwa vimeungana na vingine kwenye umbo gumu na la kustaajabisha.

Hakika michoro ya vidole hivi leo inacheza dauru kubwa na la hatari, kwenye ulimwengu wa maovu na wizi na kuwatambua watu pande zote za ulimwengu.

Fadhila yote ya kuyatambua maelfu ya matukio na wasababi-shi wake inarudia siri hii ya Mwenyezi Mungu ambayo ni ya ajabu ambayo aliiumba na kuiweka kwenye ngozi ya vidole katika mwili wa mwanadam.

Uislamu wetu mtukufu hufahamika kuwa ndie mgunduzi wa mwanzo wa siri hii ya ajabu na ngeni katika miili ya wanadamu na ambayo ni ngumu, pale Quran ilipo ashiria kuhusu suala hilo ikizitanabahisha akili kuhusu umuhimu wa maumbile haya yaliyo pangiliwa kwa makini kwenye ncha za vidole vya mwanadamu, na kuhusu kila mwanadamu kuwa na ramani yake maalumu ya utaalamu maalumu.[6]

 

***

 

 

 

UWEZEKANO  WA  KUWEPO  MAREJEO  NA 

 

DALILI  ZAKE.

 

 

Tumetaja kwenye utangulizi wa kijitabu hiki ya kuwa sisi tunaishi na suala la marejeo kwa ukamilifu wake ndani ya jengo la itikadi na ndani ya maeneo yake maalumu.

Na tumeashiria sehemu hiyo ya kuwa Imani ya marejeo ni hatua itokanayo na Imani ya ule msingi mkubwa, na tunakusudia Imani ya Mwenyezi Mungu mtukufu muumba wa ulimwengu na muanzilishi wa kuwepo kwa ulimwengu na  walimwengu na ni sababu ya juu kabisa ambayo sababu zote hurejea kwake, pasina kuwepo sababu ya kuwepo kwake au sababu ya kusaidizana nae katika kuanzisha kuwepo kwa ulimwngu.

Na inapothibiti Imani kama hii iliyo thabiti na madhubuti ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kwamba yeye ndiye chanzo cha viumbe na chanzo cha ulimwengu na kwamba  madda ni moja kati ya viumbe vyake hata kama watadhania na kuamini kuwa ni ya tangu na tangu kama wasemavyo baadhi ya wanafikra wa kimadda (materialists)[7], hakutakuwa na kizuwizi mbele ya mwanadamu kitakacho mzuwia kuamini kuwepo kwa marejeo na ufufuo na kukubali uwezekano wa kutokea na kuwa si muhali kutokea kwake.

Hakika akili kumuamini mfanyaji wa kwanza inajifungulia njia ya kuamini uwezo wa mfanyaji huyo wa kuweza kufanya kitendo chake kwa mara ya pili na kwa mara elfu kadha, na kwamba jambo hilo ni miongoni mwa mambo ya badaha , yaani ya wazi kwenye akili yasiyo hitaji ufafanuzi wala dalili na ushahidi zaidi, na inatosha kutoa mfano juu ya jambo hilo kwa kumuangalia mtu alie weza kuunda kitu fulani, kwa mfano mashine itumiayo nguvu za umeme yenye uwezo mkubwa, hakika uwezo wa mtu huyo wa kuweza kutengenza tena kitu kile halitakuwa ni jambo la kusitasita au kulitilia shaka, madamu tumekinaika kuwa yeye ndie muundaji wa kitu kile kwa mara ya kwanza.

Hakika muundaji wa gari lau kama atasambaratisha gari lile na kuliweka kwenye vipande tofauti vidogo vidogo maelfu kwa maelfu, kisha akasema kuwa anaweza kuliunda na kulirudisha gari lile ikiwa limeungwa kama ilivyo kuwa, hakuna mtu yeyote ulimwenguni atakae jitokeza na kumtaka atoe dalili juu ya uwezo huo, na haitafanyika hivyo isipokuwa ni kwa sababu mfanyaji wa kitu kwa mara ya mwanzo ana uwezo wa kukifanya kwa mara ya pili na ya tatu na kwa mara mia kadha na kwa mara milioni na kwa njia hii ya utoaji ushahidi juu ya uwezekano wa kurejea na kwa mujibu wa utaratibu huu wa kupanda kwenye ngazi ya akida, Qurani tukufu imetoa dalili juu ya ubadaha (uwazi wa akilini) wa marejeo baada ya kifo (yaani ni suala lisilo hitaji dalili).

Na hebu tutoe baadhi ya aya hizo tukufu ambazo zilihusika na kuweka wazi ukweli huu na kufafanua uwezekano wake kwa kila mwenye akili na ufahamu na uelevu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

) . ǡ (.

Na wakasema, tutakapo kuwa mifupa na mapande yaliyo sagikasagika, je sisi tutafufuliwa kwa maumbile mapya? Sema kuweni mawe au chuma au kiumbe kingine ambacho kinaone-kana kikubwa au kigumu kwenye nyoyo (fikra) zenu. Hapo watasema, ni nani atakae turudisha (kwenye hali yetu ya mwzanzo)? Sema ambae alikuumbeni kwa mara ya mwanzo. Suratu-Israai:49-51.

) (.

Na mwanadamu anasema:Ikiwa nitakufa je nitatolewa tena nikiwa hai? Je mwanadamu hakumbuki ya kuwa sisi tumemu-umba hapo kabla na hakuwa ni chochote.Suratu Maryam:66.

) (.

Siku ambayo tutaikunja mbingu kama ukunjaji wa kurasa (karatasi) zilizo andikwa, kama tulivyo kianzisha kiumbe cha kwanza tutakirudisha (hivyo). Ni ahadi juu yetu hakika sisi ni wenye kufanya hivyo.Suratul-ambiyaa 104.

( ) Mwenyezi Mungu huwaanzi-sha viumbe kisha atawarudisha kisha mtarudishwa kwake. Suratu-Al-ruum:11.

) (.

Na watasema:Tutakapo kuwa mifupa na mapande yaliyo sagika sagika je sisi tutafufuliwa kwa maumbile mapya? Je hawa-kuona ya kuwa Mwenyezi Mungu alieumba mbingu na ardhi ni Mwenye uwezo wa kuumba mfano wao.Suratul-Israai: 49-51.

) ɡ ɡ ǡ (.

Hakika tulimuumba mwanadamu kutokana na chembe chembe za udongo, kisha tukamfanya kuwa ni mbengu za uzazi kwenye mahali madhubuti, kisha tukaumba kutokana na mbengu za uzazi pande la damu, na tukalifanya pande la damu kuwa pande la nyama, na pande la nyama tukaliumbia mifupa, na mifupa tukaivisha nyama kisha tukakiumba kiumbe kingine, ametakasika (Mwenyezi Mungu) mbora wa uumbaji, baadae hakika nyinyi mtafishwa, kisha  nyinyi siku ya kiama mtafufuli-wa. Suratul-muuminuuna :12-16.

) (.

Sisi tumekuumbeni, basi kwa nini hamsadiki? Je mmeyaona maji ya uzazi myatoayo? Je nyinyi ndio myaumbayo au sisi ndio wenye kuyaumba? Sisi tumekikadiria kifo kati yenu, nasi si wenye kushindwa kuleta viumbe mfano wenu na kukuumbeni kwenye umbo msilolijua, na hakika mnajua umbo la kwanza (kuumbwa kwenu) kwanini hamkumbuki? Suratul-Waaqia:57-62.

Je anadhani mwanadamu ya kuwa ataachwa hivi hivi? Je hakuwa ni mbegu ya uzazi ya manii yatokayo kwa kuchupa, kisha akawa pande la damu na (Mwenyezi Mungu) akamuumba na kumuweka kwenye umbo la sawa, na akamfanya namna mbili mwanamume na mwanamke. Je (alie kufanya hivyo) hakuwa ni muweza wa kuwahuisha na kuwarudisha kwenye uhai walio kufa? Suratul-qiyama:36-40.

Je hawakuona ya kuwa Mwenyezi Mungu ambae ameumba mbingu na ardhi na hakuchoshwa na kuwaumba kwao ni Mwenye uwezo wa kuwahuisha walio kufa ? Naam hakika yeye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu Suratu-Ahqaafi:33.

Je hatukukuumbeni kutokana na maji yaliyo dhalili na tukayaweka mahali pa utulivu hadi muda maalumu na tukakadi-riya (wakati wa kutoka mtoto). Na si ni  wazuri kabisa wa kukadiria. Ole wao siku hiyo wanaokadhibisha! Suratul-mursalat:20 24.

Je mwanadamu hakuona ya kuwa sisi tumemuumba kutokana na maji ya uzazi, na ghafla ana kuwa ni adui wa wazi, na akatupigia mfano na kasahau kuumbwa kwake akasema: Nani ataihuisha mifupa ikiwa imeharibika na kusambaa? Sema ataihuisha yule amabae aliiumba kwa mara ya mwanzo, nae ni mjuzi wa kila kitu.Suratul Yaasin 77-79.

Je alie umba mbingu na ardhi si mwenye uwezo wa kuumba viumbe mfano wao? Naam, na yeye ndie Mwingi wa kuumba na Mjuzi.Suratu-Yaasin 81.

Je tulichoka kwa kuumba kwa mara ya kwanza? (Hata tushindwe kuumba umbo la pili). Basi wao wako kwenye shaka juu ya umbo jipya. Suratu-Qaf:15.

Hakika kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi (na kugumu) kuliko kuwaumba watu, lakini watu wengi hawajui.

Enyi watu ikiwa mko kwenye shaka kuhusu ufufuo, hakika sisi tumekuumbeni kutokana na udongo kisha mbegu za uzazi kisha pande la damu kisha pande la nyama lenye umbile (kamili), na lisilo na umbile (kamili), ili tukubainishieni. Nasi tunavithibi-tisha kwenye mifuko ya uzazi tuvitakavyo hadi muda uliowekwa kisha tunakutoweni mkiwa watoto, kisha tunakuleeni ilimfikie kuwa wakubwa, na kuna wanao kufa na kuna warudishwao kwenye umri dhalili, ili asijue chochote baada yu kuwa alikuwa  akijua mambo.

Na unaiona ardhi ikiwa imetulia kimya na tunaposhusha juu yake maji inataharuki na kukuwa na kuotesha kila aina ya mimea iliyo mizuri. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ndie haki na kwamba yeye anawahuisha wafu na kwamba yeye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu, na kwamba kiama kitakuja hapana shaka ndani yake, na hakika Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini. Suratul-Hajji:5-7.

Hakika mmetujia kama tulivyo waumba kwa mara ya mwanzo bali mlidhani ya kuwa hatukukuwekeeni miadi hii. Suratul-kahfu:48.

Kwa hivyo inatudhihirikia wazi kuwa hakika Mwenyezi Mungu ambae ameumba mbingu na ardhi ni mwenye uwezo wa kuumba viumbe mfano wa hivyo kama alivyo kiumba kiumbe cha mwanzo atakirudisha hivyo hivyo. Na kwamba uumbaji wa pili hautatofautiana na uumbaji wa mwanzo tunao ufahamu kwa kuushuhudia kwa macho yetu. Na kuwa alieipa mbegu ya uzazi uwezekano na nguvu ya kukua hadi kufikia kuwa pande la damukisha kuwa pande la nyama kisha kuwa mtoto na kuwa kijana hadi kuwa mzee, ni Mwenye uwezo wa kuifanya tena kazi ya uumbaji na kuvifufua na kuvihuisha na kuvirudisha kama vilivyo kuwa.

Kwa hivyo ataihuisha mifupa nayo ikiwa imebadilika na kuwa mchanga kama alivyo iumba hapo kabla na haikuwa ni chochote. Na hilo si la ajabu maadamu yeye Mwenyezi Mungu ndiye ambae aliviumba vitu kwa mara ya mwanzo, nae ndie ambae ameiumba mbingu na ardhi na  hakuchoshwa na kuviu-mba na ni mwingi wa kuumba na  mjuzi.

Ametakasika yule ambae ufalme wa kila kitu umo kwenye miliki yake Ametakasika mola wa walimwengu. Na hii ndio mantiki ya akili na maumbile na dhamiri, vikiwa vime epukana na aina yoyote ya shaka na dhana.

Ama mwenye shaka na kujitatiza kwenye ukweli huu ulio wazi hatumzingatii kuwa ni mwenye shaka kuhusu marejeo ili tuweze kuingia kwenye mazungumzo yenye kumuhusu, bali shaka yake hii inajulisha kutokuwa mkweli kwenye madai yake ya kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndie Muumbaji wa mwanzo, na wakati huo hatastahili kutaka zitolewe dalili kuhusu suala la marejeo au kudai kulipinga suala hilo au kutokinaika na suala hilo, bali inampasa atafute dalili za kuamini kwa uumbaji wa mwanzo, na muumbaji wa mwanzo, kwa kuzingatia kuwa marejeo -kama tulivyo tangulia kusema- ni kurudia kufanya kitu ambacho hapo kabla kilikwisha tengenezwa na kutokea, na Imani ya hayo yaliyo tangulia inapothibiti kwa kukinai na kwa yakini kutakuwa hakuna shaka kamwe katika kuthibiti marejeo.

Huenda kukawa na mwenye kutoa pingamizi kuhusiana na haya yaliyo tangulia na akasema: Hakika kupinga kwetu suala la marejeo sio kupinga kuumba kwa Mwenyezi Mungu na kuviweka kwake viumbe, bali ni kusalimu amri juu ya hukumu ya akili katika  hukumu yake kuwa ni  muhali kurejea, baada ya mwanadamu kutokana na kifo chake kuwa ni kitu kilicho potea na kutoweka, na nijambo lililo wazi kuwa  kilicho kwisha potea na kutoweka ni muhali kukirudisha, na sijambo la kiakili mtu mwenye akili kuamrishwa kuamini mambo yasiyo wezekana (yaliyo muhali).!

Huu ndio muhtasari na ufupi wa shubha ambayo wenye kuikubali ni wengi na waisemayo ni wenye kuhesabika, baada ya jambo hilo kuwatatiza na kuchanganya kati ya hili na lile au wakaghafilika  kunako maana ya kweli ya kifo na marejeo.

Lau kama wenye shubha (shaka inayofanana na haki) hiyo wangetaka kuzama na kuliangalia kwa ndani, kidogo wangeweza kuelewa uwazi wa jambo hilo, kwani ingemuwia wazi ya kuwa kifo kilivyo, si kutoweka viungo vya mwanadamu, bali ni kuvitenganisha na kuvisambaza viungo vile, na baadhi ya watu walidhani ya kuwa mwili baada ya kuachana na kusambaa vinapotea na kutoweka haviwi tena, lakini ukweli ni kuwa viungo hivyo vipo vikiwa vimetawanyika na chembe zake kusambaa, na Mwenyezi Mungu anapotaka kuvirudisha atavikusanya kwa uwezo wake viungo hivi vilivyo sambaa na kuviunganisha na kuviweka kwenye hali yake ya mwanzo ukiwa ni mwili na roho na sifa zake, na hayo ndio marejeo (kiama).

Na tunaelekezwa na kuongozwa mwongozo bora kwenye maana hii na maneno yaliyo zungumzwa kwenye Quran tukufu kutokana na suali la Ibrahimul-Khalil (a.s) alipo muuliza Mola wake kwa kusema: Nionyeshe vipi unawahuisha wafu?

Na jawabu la Mwenyezi Mungu aliyetakasika kwa Ibrahim lilikuwa ni kauli yake Chukua ndege wanne wakatekate yaani Ibrahim awakatekate vipande vidogo vidogo na avichanganye vyote uchanganyaji ambao hauwezi kutofautisha wala kutengani-sha kati ya ndege wale,Kisha weka juu ya kila mlima kati ya vipande hivyo kipande kimoja yaani kipande kimoja kati ya vile alivyo vichanganya, kisha waite, watakujia wakitembea kwani Mwenyezi Mungu atapambanua viungo vya kila ndege kuvito-fautisha na ndege mwingine, na kukusanya kila kipande kuki-weka na chenzake vikijitenga na vinginevyo, na kuviwekea uhai wakati ndege anapo kamilika kwenye umbo lake maalumu.

Na mfano huu wa Qurani ulio makini na ulio wazi ya kuwa kifo ni sawa na kuvitenganisha viungo na sio kutoweka kama wadhaniavyo baadhi ya wapingaji.

Kwa hivyo basi, kwenye jambo hili hakuna maana yoyote kati ya maana za kutowezekana na kuwa muhali wala shubha yoyote kati ya shubha zipingazo kwa kusema ni jambo lisilowezekana kiakili kama wanavyodai baadhi ya watu hao.

Kutokana na kuwa marejeo, kama tulivyo tangulia kusema, yana maana ya kurudi kwa watu wote, baada ya kufa kwa malengo ya kufanyiwa hesabu na kuhukumiwa, kisha kupewa thawabu (yaani malipo mema) na kuadhibiwa kutokana na matokeo ya hukumu ile Na tutawafufua na hatutamuacha miongoni mwao yeyote Siku ambayo kila nafsi itayakuta iliyo yatenda kati ya mazuri yakiwa yameletwa mbele yake, na maovu aliyo yatenda.

Hakika marejeo haya ni lazima yatanguliwe na kumalizika kwa ulimwengu na vyote vilivyomo, vitu na wanadamu kiasi kwamba uhai utasimama kufanya kazi na vyote vilivyo hai kufariki siku ambayo tutaikunja ardhi kama ukunjaji wa kurasa zenye maandishi siku ambayo ardhi itabadilishwa tofauti na ardhi hii, na mbingu (vile-vile).

Je hilo linawezekana kiakili? Na je elimu ya kisasa inaweza kutuongezea na kutuelekeza kwenye uwezekano huu kutokana na kufungukiwa na nyanja mbali mbali na sehemu nyingi za ugunduzi wa vitu au habari zisizo julikana na kutoa habari za mambo yatakayo tokea siku za usoni?

Profesa Frank Allen anasema:

Hakika kanuni za mwendo wa joto (dynamic law), zinajuli-sha kwamba vitu vitoavyo nguvu kwenye ulimwengu huu vinapotelewa na kuondokewa na joto lake taratibu, na kwamba vitu hivyo vinaelekea kwenye siku ambayo vitakuwa vyote kwenye siku hiyo, chini ya kiwango cha joto cha chini kabisa ambacho ni sifuri, na siku hiyo nguvu yote itakosekana na itakuwa ni muhali kuwepo uhai. Hakuna budi kutokea kwa hali hii ya kutoweka kwa nishati zote (energy) wakati kiwango cha joto cha vitu kitakapo-fikia chini ya sifuri kwa kupita kwa muda.

Naye Profesa Edward Luther Keel anasema:

Kuna uhamaji wa joto wenye kuendelea kutoka kwenye vitu vya joto na kuhamia kwenye vitu vya baridi, na haiwezekani kutokea kinyume kwa nguvu za kidhati (ya kibinafsi) kiasi kwamba joto likarudi (lenyewe binafsi) na kuhama kutoka kwenye vitu baridi kwenda kwenye vitu vyenye joto. Na maana ya hayo ni kwamba ulimwengu unaelekea kwenye kiwango cha joto ambacho vitu vyote vitakuwa na kiwango cha joto kilicho sawa na ndani yake nguvu ya usaidizi. Na siku hiyo hakutakuwa na kazi ya kemia au maumbile, na hakutakuwa na athari ya uhai wenyewe kwenye ulimwengu huu.

Naye Profesa Claud M.Nathaway anasema:

Sir (bwana) Isack Newton alikuja kufahamu ya kuwa nidhamu ya ulimwengu huu inaelekea kwenye kusimama (kuisha) na kuwa inakaribia kwenye hatua ya kiwango cha joto cha vitu vingine (vitoavyo nguvu) kuwa sawana utafiti wa joto umeunga mkono rai hizi na umetusaidia kupambanua kati ya nishatiweza (energy potential) na isiyoweza, na imegundulika kwamba kunapo tokea mabadiliko yoyote ya joto hakika sehemu fulani ya nishatiweza, na kwamba hakuna uwezekano mwingine ila kuwa na mabadiliko haya kwenye maumbile kwa njia ya kinyume.

Naye Boltsman alitilia umuhimu uchunguzi wa kutaka kufahamu hali hii, na katika uchunguzi wake akatumia uwezo wake wote wa kugundua na vipimo vyake vya mahesabu, hadi akathibitisha kuwa kukosekana kwa nishati weza (energy potential) ambayo ina ashiriwa na kanuni ya pili ya mwendo joto ya joto (dynamic law of heat), si jambo lingine isipokuwa ni hali mahsusi katika matukio mengi ya jumla inayo ashiria kuwa mabadiliko yoyote au mgeuko wa kimaumbile hufuatiwa na hali ya kuzorota au kuwepo upungufu kwenye nidhamu ya ulimwe-ngu. Na katika hali ya joto kubadilika kwa nishati kutoka kwenye nishati weza na kuwa nishati isiyo weza, huchukuliwa kuwa ni ukosefu au upungufu wa nidhamu katika kiungo fulani au kwa ibara nyingine, ni kuzorota na kuharibika kwa jengo.

Naye Dr Muhammad Jamalud- din Afandi:

Wataalamu wa sayari wote wanasisitiza ya kuwa jua, kama sayari nyingine yoyote ni lazima ipatwe na hali ya kuzidi kwa ghafla kwenye joto lake na ukubwa wake na miaka yake kwa kiwango ambacho akili haiwezi kukikubali, na wakati huo anga lake la nje litapanuka pamoja na vilivyomo ndani ya anga lake, navyo ni moto na moshi hadi kuufikia mwezi na kusababisha kasoro kwenye uwiano (nidhamu) wa jamii ya sayari zote. Na kila jua kwenye anga (mbinguni) ni lazima lipitie kwenye hali kama hizi kabla halijafikia kwenye uwiano wake wa daima, na jua letu kwa dhati yake halijapitia mzunguko huu bado.[8]

Amesema mwenyezi Mungu mtukufu:

Basi ingoje siku ambapo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri Suratud- dukhan:10 (itakuwa siku hiyo) wakati litakapo parama jicho, na mwezi utakapo patwa, na jua na mwezi kukusanywa, siku hiyo mtu atasema makimbilio yako wapi? Suratul-Qiyamah:7-10.

Na ardhi na majabali yatabebwa na kupigwa pigo moja Suratul-Haaqqah:14. Kwa hivyo basi, siku ya marejeo na dalili zake na kila litufahamishalo kuhusu siku hiyo, kama vile kumali-zika kwa ulimwengu na kutoweka kwa uhai, ni siku ambayo inawezekana kutokea kwa hali yoyote, bali ni jambo la lazima na lisilo na shaka kwenye ufahamu wa kielimu ya kisasa.

 

 

***

 

Na elimu ya kisasa ikiwa imezidi kutupa matumaini ya ukweli huu basi hakika baadhi ya wanafalsafa wa zamani ambao elimu haikuwasaidia kwenye zama zao kuweza kufahamu ukweli, walishikilia na kuchukua kauli zisemazo kuwa ulimwengu utabakia kwenye hali yake ya hivi sasa bila kumalizika wala kuondoka, kwa kutoa ushahidi  wa jua juu ya hayo, ambalo pamoja na kuwa lina umri mrefu sana, halijatokewa na mabadi-liko yoyote yanayoashiria kupungua au kuyayuka kwake na haya yana maana kwamba litabakia milele na milele, kwani lau kama lingekuwa limepangiwa kumalizika kungedhihiri kwenye jua hilo vitu vijulishavyo  kumalizika huko kama upungufu au kubadilika au kuyayuka.

Ubatilifu wa madai haya unakuwa wazi kutokana na kufaha-mu uhakika ufuatao:

01- Hakika kanuni ya diynamic ya joto imetufahamisha ya kuwa joto halitadumu milele, na kwamba siku ya kumalizika kwake ambako kutapelekea kumalizika kwa ulimwengu bila shaka yoyote itakuja na kutokea kama tulivyo elezea kwa upana.

02- Hakika wachunguzi wametoa habari za kutokea kwa milipuko mingi juu ya anga la jua kwa kiwango cha masafa makubwa sana na mapengo yamedhihiri katika sehemu zilizoto-kea milipuko hiyo ambayo haiwezi kufasiri isipokuwa kwa kusema kuwa ni kulika (kuisha) kwa sayari ya jua

03- Wataalamu wa sayari kusisitiza kwa hali ya kupanuka anga la nje la jua hadi kufikia kwenye mwezi, kiasi kwamba uwiano wa sayari zote unaingiwa na kasoro, kama tulivyo tangu-lia kusema.

Na maana ya yote hayo ni kuwa kumalizika kwa ulimwengu ni jambo la lazima, hakuna makimbilio, na kwamba kauli ya kubakia milele kwa jua ni kauli isiyo kuwa na dalili yoyote.

Ama dalili ya wale wasemao ya kuwa hakuna marejeo kwa kutumia kanuni ya kuwa Madda haimaliziki ili kuyafanya sahihi madai yao, ni dalili yenye kupingwa kwa hali yoyote ile kwa sababu kauli isemayo kutomalizika kwa madda, imekuwa ni miongoni mwa kauli za zamani, ambazo elimu imezivuka na kusema kuwa itamalizika. Na sawa mada imemalizika au haikumalizika, kwani masala haya hayana mahusiano yoyote na maudhui ya bahthi yetu, kwa sababu marejeo ni mabadiliko kwenye sura ya madda na sio kumalizika kwake.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu Siku itakayo badili-shwa ardhi isiwe ardhi hii na mbingu hii na ni tofauti kubwa iliyopo kati ya kubadilika na kumalizika.

Na muhtasari wa kauli ni kuwa:

Hakika kiama kitakuja, hakuna shaka ndanyi yake, na Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini.

Na hakika wale ambao hutia shaka kuhusu kiama wako kwenye upotevu wa mbali na siku kitakapo simama kiama siku hiyo watapata hasara wenye kubatilisha ( kuwepo kwa kiyama).

Na kiyama hicho kitakuja pindi ardhi itakapofikia kileleni mwa utamaduni wake na mwanadamu kufikia mwisho wa maendeleo yake, na ardhi kuchukua mapambo yake, na mwana-damu kudhania ya kuwa anakihukumu kila kitu na akawa ni mwenye uwezo wa kufanya kila kitu, basi yeye akawa ana hukumu na kutawala suala la mvua, na kupandikiza au kulima kwenye ardhi yenye changalawe, na kwenye jangwa na kuhami-sha nyoyo na macho kutoka kwa wafu na kuwawekea watu walio hai, na akawa anasafiri kwenye sayari na anapasua chembe chembe za atom, na anahamisha majabali. Hakika Mwenyezi Mungu anatuahidi kwa kutuonya.

Hadi ardhi itakapo pambwa na kuwa vitu vya kuvutia na watu wake kudhania kuwa ni wenye uwezo juu yake, itawajia amri yetu usiku na mchana na tutawafanya kuwa kama mavuno kana kwamba hayakuwa ni mimea siku ya jana.

Na katika aya hii kuna uzuri (jamala) na siri (fumbo). Mwenyezi Mungu anasema, hakika kiama kitakuja usiku au mchana, na hakuna tafsiri ya maneno hayo isipokuwa ardhi iwe kama tufe la duara, nusu yake ni usiku na nusu nyingine ni mchana, basi kitakapo kuja kiama, nacho kitakuja ghafla,na hakikuwa kiyama isipokuwa ni kama kupepesua jicho au karibu zaidi ya hivyo, nusu ya wakazi wake watakuwa kwenye usiku na nusu ya pili watakuwa kwenye mchana.

Kisha Qurani inatufikisha kwenye alama ya mwisho kati ya alama za kiama nayo ni kupulizwa kwa balagumu na kusimama kwa kiama.

Na matukio ya kiama yanayo simuliwa na Quran ni ya kutisha, kwa kuyasikia damu huganda kwenye mishipakwamba jua litapatwa na mwezi kushikwa na majabali yatangoka na nyota zitatawanyika, na mabahari yatapasuka, na ardhi itatete-meka na viumbe hai vyote ardhini na mbinguni vitapiga kelele.

Yatatokea haya wakati wa kupulizwa parapanda la mwanzo. Na likipulizwa kwa mara ya pili watafufuka wote na kuanza hesabu.[9]

Na kitabu kitawekwa, na utawaona waovu wakiyaogopa yaliyomo ndani yake, na wakisema:Ole wetu kina nini kitabu hiki hakiachi jambo dogo wala kubwa isipokuwa hulihesabu. Na watayakuta mambo waliyo yatenda yakiwemo, na Mola wako hamdhulumu yeyote. (Suratul-kahfu :49).

 

 

Na kitabu kitawekwa na wataletwa manabii na mashahidi na itatolewa hukumu kati yao kwa haki, na wao hawatadhulumi-wa. Na itapewa kila nafsi malipo ya matendo iliyo yatenda, na yeye ni Mjuzi zaidi wa mambo wayafanyayo. Surat-uz-zumar: 69-70.

 

AMESEMA KWELI MWENYEZI MUNGU ALIE TUKUKA NA ALIE ADHIM.

 

***

 

 


[1] Rejea Kitabu Allah-bainal-fitrat wad-dalil chapa ya Baghdaad 1389 H=1967 A.D, na Bairut 1392 H=1972 A.D.

[2].Rejea Kitabu chetu Al-adlul-ilahi bainal jabri wal-ikhtiyaar, Baghdaad 1389 H=1970 A.D, Bairut 1392=1972 A.D.

3.Rejea Kitabu chetu An-nubuwatBaghdaad 1392 H=1972A.D, Bairut 1392=1972 A.D.

 [4] Usulul-fiqhi cha mudhwaffar, 1/55-59-89-90.

[5] Al-Islam wat-Twibul-hadith:66.

[6] Dr Ibrahim Ar-rawiy-Majallatu Al-adlu Annajafiya toleo la 1 ukurasa  1/6-2-6

[7] Rejea kwenye bahthi ya kuwa madda si ya tangu na tangu na majadiliano na wasemao ya kua ni  ya tangu na tangu kwenye kitabu (Hawaamishu ala kitabi. Naqdi fikrid-dini) Chapa ya Bairut/1391h-1971 A.D.

[8] Rejea kwenye kitabu Allah yatajalla fi-asril ilm Ukurasa:8-29-92-167.

[9] Al-Qurani, cha Mustafa Mahmud:207-209.