MATAWI YA TAASISI  HII DUNIANI

 

1-Taasisi ya Imam Ali (a.s) Londan.

Baada ya mwaka mmoja tangu kuasisiwa taasisi ya Imam Ali (a.s) katika mji mtukufu wa Qum ilionekana kuwa kuna haja kubwa ya kufungua tawi lake katika mji wa Londan na ilifanya hivyo kwa sababu zifuatazo:

1-     Kutokana na nafasi ya mji huo katika nchi za Europ.

2-     Kutokana na wingi wa familia za kiislaam na za kiarabu na wairaq waishio kwenye mji huo.

3-     Kutokana na ulazima na mahitaji ya kuwasiliana na Marjiu mtukufu katika mji wa Najaf.

Kutokana na sababu hizi na kwa ajili ya kufaidika na sababu hizi lika anzishwa tawi hili tukufu mwaka 1416 Hijiria, na tawi hili hufanya kazi ileile ambayo hufanywa na makao makuu ya Qum na hubadilishana nashati na uzoefu wa kazi mbali mbali, kwani tawi lililo tajwa limechukua jukumu la kutarjumi vitabu muhimu kama vile Al-fatawal-muyassarh sehemu ya Ibada na Muamala na ibadaya hijja na mas’ala mbali mbali ya kifiqhi (Al-masailul-fiqhiyyah limuslimii-gharbi na vitabu vingine vya kielimu na maarifa, na vyote hivyo ni vya mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa Sayyid Sistaniy (Mungu amzidishie umri), na tawi hili liko chini ya usimamizi wa Fadhilatul-hujjah Sayyid Murtadha Al-kashmiriy.

Anwani: Uingereza- Londan

Simu: 0044 02084598164

Fax: 0044 02084511072

Anwani ya Saiti: www.najaf.org

Barua pepe: post@najaf.org

 

2-Taasisi ya Imam Ali (a.s) tawi la Bairut.

Kutokana na kushika kasi kwa kazi katika taasisi ya Imam Ali (a.s) katika mji wa Qum na kudhihiri kwa natija na matunda ya kazi ya taasisi na kupata upokezi mkubwa wa vitabu na jarida la taasisi hii katika lugha tofauti zilizo hai na kwa ajili ya kupanua wigo wa kazi za taasisi lilianzishwa tawi jipya la taasisi ya Imam Ali (a.s) katika mji wa Bairut mwaka 1417 Hijiria ili kufaidika na anga la Lebanoni lililo wazi na huru katika kuchapisha vitabu vinavyo tumwa huko kutoka makao makuu ya Qum ili viweze kutumwa na kufikishwa kwenye nchi tofauti za kiarabu na zinginezo duniani, pia kufaidika na watu wenye maandalizi na hadhi ya kufanya tarjumi na kuweza kufaidika na vipaji hivyo walivyo navyo watu hao walioko Lebanoni, na tawi hili limeweza kutoa vitabu vingi na kudhihiri masokoni, na kati ya hivyo ni hivi vifuatavyo:

1-Aslush-shia wa usuuliha-kwa kifaransa. (Asili ya ushia na misingi yake)

2-Ad-dalilul-islaamiy lil-atfaal- kwa kifaransa

3-Duau kumail kwa kifaransa.

4-Haki za mwanamke katika Uislaam kwa kiarabu.

5-Duau kumail kwa kiingereza.

6-Maarifatullah kwa kinorwey.

Na kutokana na kupokelewa na kupendwa sana Jarida la Mujtaba ambalo hutolewa na taasisi ya Imam Ali (a.s) makao makuu ya mji mtukufu wa  Qum imeamuliwa kuwa tawi la taasisi la Bairut lichukue jukumu la kuchapisha Jarida hilo na kuliingiza kwenye soko la nchi za kiarabu na Ghuba.

Pia katika mji wa bairut kimeanzishwa kitengo cha tarjuma kwa lugha ya kihispania, na kitengo hicho kinaendeshwa na Fadhilatush-shekh Mualimiy Zaadah ambae ndie mwenye kutarjumi vitabu vya kiislaam katika lugha ya kihispanyora na kati ya vitabu ambavyo visha toka kwa lugha hii ni kama vifuatavyo:

1-Aimmatul-hudaa (Maimamu wa uongofu).

2-Issa bin Maryam wal-qur’an

3-Risalatul-huquuq

4-Swahifatus-sajjadiyyah.

5-Aqaidul-imamiyyah

6-Duau kumail wa Duaus-swabah.

7-Al-masaailul-mustahdatha juzu 1-2 kati ya fatwa za mheshimiwa Sayyid Sistaniy (Mungu amzidishie umri).

8-Utoaji wa Jarida la Nurul-hikmah.

Anwani: Lebanon- Bairut.

Simu: 009611541431

Fax: 009611541431

  

3-Taassi ya Imam Ali (a.s) Kenya.

 Baada ya kushauriana na mheshimiwa Al-hujjah Sayyid Murtadha Al-murtadha lilianzishwa tawi la Taasisi ya Imam Ali (a.s) katika mji wa Nairobi nchini Kenya ili liweze kuchukua majukumu ya kutarjumi Jarida la kizazi kipya cha kiislaam katika lugha ya Kiingereza na kulisambaza katika nchi zizungumzazo lugha hiyo na hadi hivi sasa kazi hiyo isha kamilika  na toleo la kwanza lisha toka na Jarida hilo lilipata upokeaji wa hali ya juu na mkubwa katika sehemu tofauti kama Europ Amerika na Afrika, na hadi hivi sasa idadi ambayo imekwisha toka ya Jarida hilo ni hadi namba 18, na toleo la mwisho lilikuwa ni toleo la mwezi wa Safar mwaka 1424 Hijiria.

 Kama ambavyo taasisi imefanya kazi ya kutarjumu baadhi ya visa vya Shahidah bintil-hudaa katika lugha ya kiingereza.

 

 Na kuna matawi mengi mengine ya taasisi ya Imam Ali (a.s) sehemu tofauti za dunia kati ya hayo ni haya yafuatayo:

 4-Tawi la taasisi ya Imam Ali (a.s) katika mji wa Montralia- Kanada.

5-Tawi la taasisi ya Imam Ali (a.s) Bankok-Tailand.

6-Tawi la taasisi ya Imam Ali (a.s) katika mji wa Amsadam-Holand.

7-Tawi la taasisi ya Imam Ali (a.s) Paris-Ufaransa.

 

Na matawi haya yanafanya kazi ya kutarjumi vitabu vya kiislaam na kuvisambaza sehemu mbali mbali ambazo matawi hayo hufanya kazi yake.