UTAMBULISHO WA TAASISI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu.

(ومن يبتغ غير الاسلام ديناً فلن يقبل منه وهو في الآخرة من الخاسرين). آل عمران، آية 85.

(Na mwenye kufuata dini nyingine tofauti na Uislaam hatokubaliwa kwake amali yoyote nae siku ya akhera (kiama) atakuwa miongoni mwa watu wenye hasara) Al-imran aya 85.

 

UTANGULIZI

Kutokana na ukweli kwamba Uislaam ndio dini ya mwisho ya Mwenyezi Mungu, na kwa kuzingatia kuwa ujumbe wa Uislaam ndio hitimisho la ujumbe wake wa mbinguni, na watakiwacho watu kukifanya ni kujiunga na dini hiyo na kushikamana nayo na kuamini na kutekeleza matendo kwa mujibu wa dini hiyo.

Na kwa kuzingatia kuwa Uislaam ndio dini itakayo bakia milele na ambayo inakwenda sambamba na zama na maendeleo, kwa hakika dini hii ilikuja ili kuwa kikomo cha mateso na taabu walizo kuwa wakizipata wanadamu, na ilikuja ili kuyaponya majeraha, maumivu na matatizo waliyo kuwa wakipambana nayo kwa muda mrefu na kuyaondoa kwa mkono wa huruma, na kuwaokoa kutokana na dhuluma na ukandamizaji pia kuwatoa kwenye viza (kiza) hadi kwenye nuru (mwanga) ya Mwenyezi Mungu yenye kuchomoza na  kuangaza, na kwa kuzingatia (kutilia maanani) kuwa ujumbe wa kiislaam ulio wa milele ndani yake una ubainifu wa kila kitu, na ni tiba ya kila gonjwa na ni jibu la kila tatizo, kwa hivyo basi ilikuwa ni haki na wajibu kwa (juu ya) watu wenye ikhlaas kati ya wafuasi wake kuieneza na kuifikisha kila upande wa dunia kwa kusimamisha na kutekeleza wajibu na majukumu na kuitekeleza amana waliyo pewa kwa kuwafikishia waja wa Mwenyezi Mungu.

Kutokana na sababu hiyo ndio maana Taasisi ya Imam Ali (a.s) ikiwa chini ya kivuli cha Marjiu muongofu (mwenye muongozo) mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa Sayyid Sistaniy (Mungu amzidishie umri) ukachukua na kujibebesha jukumu la kuutafsiri ujumbe huu mkubwa wa Mwenyezi Mungu na maarifa na fikra yoyote ulizo nazo, na itikadi pia hukumu na sira (mwenendo) na habari kwa mtazamo sahihi unao kwenda sambamba na mfumo wa Ahlul-baiti (a.s) juu yao rehma na amani katika lugha tofauti (mbalimbali) zilizo hai na zizungumzwazo ulimwenguni wakiwa mbali na madhehebu potovu na mielekeo potovu iliyo mbali na kiini cha dini hii tukufu.

Na kutokana na uzoefu na utambuzi ambao tumeupata katika muda wa miaka kumi kuanzia mwaka 1415 hijiria, kwa hakika tumeweza kuweka mpango wa muda mrefu, muda ambao unatulazimu kiupatia jamii ya kiislaam kutokana na mahitaji yake kwa hivi sasa maarifa na mafunzo ya kiislaam, ama kuhusiana na mpango wa muda mrefu ni  ule ambao unasimamia jukumu la kufanya uchunguzi na utafiti wa mahitaji na sifa maalum za kila mahala kutokana na tofauti ya mazingira na mahitajio ya sehemu na jamii hizo, na maarifa hayo kuyatafutia njia mbali mbali zinazo faa (zilizo munasibu) kuweza kutatua mahitajio yao  na kutekeleza matakwa yao kwa kuwapatia vitabu vyenye maarifa ya kiislaam vilivyo tarjumiwa na kutafsiriwa kutoka kwenye vyanzo mama vya kiislaam kwa mikono yenye uaminifu na ya watu wenye utambuzi na uzoefu na ambao wanauzoefu wa kazi hiyo na wenye ikhlas ya kazi hiyo, na vilivyo tolewa katika utoaji ulio mzuri na vikiwa kwenye vazi safi na vinavyo kwendana na muono ulio salama.

Kwa hakika amali hii ngumu na kubwa ambayo imetekelezwa na Taasisi hii tukufu katika muda huu mchache ni kazi inayo stahili kuenziwa na kutukuzwa na hasa tukifahamu ya kuwa Taasisi hii imeweza kutarjumu  (kutafsiri) vitabu mbali mbali kwenye lugha zaidi ya 30 kati ya lugha hia zinazo zungumzwa duniani, na imeweza kutarjumu zaidi ya vitabu mia sabini (170) katika maudhui na nyanja tofauti kama vile Itikadi, Adabu (kanuni za lugha) Hukumu za kisheria na habari pia maarifa mbali mbali, na tuna taraji (Twamtaraji) muumba alie takasika atukubalie huduma hii chache tuifanyayo katika kuihuisha dini yake na kulieneza jambo lake hili hakika yeye ndie msikivu na mwenye kujibu maombi ya waja.

Enyi ndugu zetu katika ubinadamu (utu) na ndugu zetu katika Itikadi njooni mjichotee maarifa kutoka kwenye chemchem hii iliyo safi imalizayo na kukata kiu ya mwenye kiu na njooni kwenye dini ya haki na Itikadi sahihi na fikra zenye kuongoza  kwenye njia iliyo nyooka na kwa hakika Mwenyezi Mungu mtukufu anasema:

(ادع الي سبيل ربك بالحكمة والموعظة الحسنة وجاد لهم بالتي هي احسن)

 (Walinganie watu kwenye njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa yaliyo mema) (suratun-nahli aya 125).

 

 

 

VITENGO VYA TAASISI YA IMAM ALI (A.S)

 

Taasisi hi inavitengo vingi, vitengo ambavyo husaidia sana katika shughuli zake na katika kutekeleza majukumu yake, na ifuatayo ni orodha ya vitengo vya Taasisi hii kama ifuatavyo:

1-Kitengo cha usaidizi wa mambo ya idara na mahesabu.

2-Kitengo cha Tarjuma (utafsiri wa vitabu).

3-Kitengo kijishughulishacho na kijana (mtoto) wa kiislaam.

4-Kitengo cha mtandao wa Internet.

5-Kitengo cha hati na uchoraji wa hati asili ya kiarabu.

6-Kitengo cha uchapishaji vitabu.

7-Hazina ya vitabu (store).

8-Maktaba.

1-Kitengo cha Usaidizi  wa mambo ya idara na mahesabu:

Kitengo hiki wadhifa wake ni kusimamia mambo yote ya Taasisi hii wakati mkuu wa Taasisi anapo kuwa safarini au nje ya Taasisi, kisha husimamia bajeti  ya mwaka mzima ya Taasisi na husimamia mahudhurio ya wafanyakazi na uangalizi wa ulipaji wa mishahara na hesabu za watarjumi.

2-Kitengo cha Tarjuma: (ufasiri)

Baada ya ofisi ya Taasisi kukamilisha uteuzi wa kitabu kinacho takiwa kufanyiwa tarjuma (kutafsiriwa) na idara ya taasisi au watu wenye uzoefu na wataalamu wa kazi hii katika taasisi hii na lugha inayo takiwa kutarjumiwa kitabu hicho, Taasisi humteua kati ya watu wenye uzoefu na wafanyao kazi hiyo na wenye ujuzi wa kufanya kazi hiyo mtu mmoja wapo ambae atachukua jukumu la kutarjumi kitabu hicho kulingana na makubaliano wayafanyayo na idara ya Taasisi hii, makubaliano ambayo ndani yake huwa na masharti (mapendekezo)  kadhaa ambayo hutakiwa kutarjumiwa kitabu kile kwa mujibu wa masharti yale, na kati ya masharti hayo ni kama yafuatayo: Usalama wa maana ya kitabu kinacho tarjumiwa.Tarjuma ifanywe kulingana na kanuni za lugha itumikayo kutarjumi na kufuata mfumo  mzuri katika tarjuma na katika kipindi ambacho makubaliano yamefanyika, na baada ya mtarjumi kukamilisha kazi yake na kukabidhi kazi yake ikiwa kamili, tarjuma ile hupewa mpitiaji na msahihishaji mwenye ujuzi na ambae huipitia tarjuma hiyo na kuangalia ni kwa kiasi gani iko sambamba na asili ya kitabu kilicho tarjuma na kuthibitisha ya kuwa tarjuma hiyo iko katika kiwango na mustawa mzuri au wa wastani kwa asilimia 80% au zaidi, kisha husahihisha makosa na kuandika maoni yake kwenye asili ya tarjuma hiyo, na baada ya hapo hupelekwa tarjuma hiyo kwenye sehemu ya uchapishaji  na kuiingiza katika  na kurekebisha  makosa yale ndani ya computer na baada ya uchapishaji kukamilika hutolewa chapa ya kwanza na kukabidhiwa mtarjumi kwa ajili ya kuangalia  usalama wake na kwamba hakuna makosa yoyote ya kifani, kiuchapishaji au ya kiuandishi, na ikiwa kutakuwa na makosa au maoni yoyote basi huandika maoni hayo ili yaweze kuingizwa kwenye computer na kutolewa chapa ya pili ili ipitiwe kwa mara ya pili, ikiwa chapa hiyo ya pili haikuwa na makosa baada ya uangalizi na kupitiwa  kwa mara ya pili basi hiyo huwa ndio chapa ya mwisho na baada ya hapo hutolewa copy kisha hutumwa wizara ya Irshad kwa ajili ya kupitishwa kwa ajili ya  kuchapisha kitabu na baada ya hapo hupelekwa kwenye uchapishaji.

3-Kitengo cha Internet:

Ni jambo lililo wazi kwa kila mmoja umuhimu wa kwenda sambamba na zama na vyombo vya kisasa na teknolojia ambayo katika zama zetu hizi limekuwa ni jambo lisilo wezekana nani vigumu kujiweka kando na kuto faidika nayo, na vimekuwa ni vyombo muhimu sana vya mawasiliano na kubadilishana fikra, habari na maalumati katika ulimwengu wetu wa leo. Kwa manti hii na kwa ajili ya kuchangia katika mwendo huu wa kueneza kusimika na kupandikiza athari za kielimu na kimatendo na kueneza maarifa ya kiislaam na mafhumu yake yaliyo simama juu ya msingi wa kifikra na mfumo (Mwenendo) wa Ahlul-baiti (a.s) kwa usulubi ulio sambamba (unao nasibiana na) mahitaji (matakwa) ya ulimwengu wetu wa hivi sasa, kwa hivyo kulikuwa na haja kubwa kwa Taasisi ya Imam Ali (a.s) kujumuisha katika kazi zake kituo cha Internet kwa ajili ya kutangaza kazi zake izizalishazo katika uwanja wa maarifa ya kiislaam, na katika kumbukumbu za siku kuu ya iddil-ghadiir mwaka 1423 hijiria sawa na 2003 A.D mpango huu kwa usaidizi wa Allah ukaingia katika utekelezaji wake ili watu wenye uwezo wa kutumia na kufaidika na Internet waweze kufaidika kwa kuingia kwenye kituo chetu na kunufaika pia kufaidika nacho kwa kujipatia maarifa ya kiislaam.

4- Kitengo kijishughulishacho na mtoto wa kiislaam:

Baada ya uongozi wa Taasisi kuhisi kuwa kuna haja kubwa ya kumpatia mtoto wa kiislaam utamaduni wa kiislaam kutokana na idadi kubwa ya waarabu kuishi katika mazingira yasiyokuwa ya kiislaam, lilianzishwa jarida la Mujtaba, jarida ambalo linajishgughulisha na watoto walio kati ya umri wa miaka 10-15 na jarida hilo lilianza kutoka (kusambazwa) miaka mitatu iliyo pita na baada ya kutoa   maudhui na visa ambavyo haikuwa kutolewa na jarida lolote la kiarabu katika ulimwengu wa kiarabu, jarida hili lilipata upokezi mkubwa na wa pekee (usio na mfano) kwani liliweza kuenea katika pembe zote za dunia bila kuwa na mawakala wa kulismbaza, na barua mbali mbali zilizo pokelewa katika ofisi ya jarida hili kutoka Amerika, Australia, Europ na katka nchi za ghuba, pia maombi mbali mbali na mengi yaitakayo Taasisi kulitarjumi katika lugha zingine ni dalili tosha juu ya upokezi huo. Katika kuitika maombi hayo Taasisi ya Imam Ali (a.s) huko Kenya ilichukua jukumu la kulitarjumi jarida hilo katika lugha ya Kiingereza na kuchapisha zaidi ya copy elfu moja (1000) kila mwezi na katika kipindi cha mwisho kitengo cha Internet cha Taasisi ya Aalul-baiti tawi la Lahor-Pakistani-likachukua jukumu la kulitarjumi jarida hilo katika lugha ya kiurdu na hadi hivi sasa zimetoka copy mbili. Na kabla ya kuanza mpango wa jarida la Mujtaba, Taasisi ilifanya makubaliano na baadhi ya waandishi wenye fani ya uandishi kwa ajili ya watoto wa kiislaam kwa kuandika visa vinavyo simulia maisha na mwenendo wa maimamu wa Ahlul-baiti (a.s) na masahaba wao watukufu, na kwa hivi sasa sisi tumeliweka kwenye saiti yetu ili watu wote waweze kufaidika nalo, huenda kwa kufanya hivyo tukapata tawfiq ya kufikisha maarifa haya yatokayo kwenye chemchem safi yenye kumeremeta na yatokanayo na fikra na mwenendo wa Ahlul-baiti wa nyumba ya Mtume (s.a.w) juu yao rehma na amani na kuwafikishia watoto wote wahamiaji ambao wamenyimwa na wanao pambana na ukosefu wa utamaduni na wapambanao na vishawishi vya kifikra katika mazingira yasiyo kuwa ya kiislaam.

5-Kitengo cha uchoraji na uandishi wa asili wa hati ya kiarabu:

Taasisi imefaulu kupata sifa ya aina yake kutokana na kuitilia kwake hima hati ya kiarabu na kukipatia kitengo hiki nafasi ya juu na ya pekee, kwa hivyo ndio maana tunaona ya kuwa ugunduzi na ufanisi na utoaji mzuri vimekuwa ni sifa za pekee zilizo dhihiri na kuonekana katika uteuzi wa (mbao) na nassi mbali mbali zilizo changanyika na utoaji mzuri wa kifani na uchoraji wenye kuvutia na unaokwenda na zama zetu hizi na unao wiana na herufi za kiarabu na rangi zenye kuingiliana ili kuondoa mfumo na utoaji ambao hutoa ujumbe wa kina katika ibara zake za fani hii ya asili ya hati za kiarabu.

6-Kitengo cha uchapishaji:

Hiki ni kitengo ambacho kina husiana tu na kazi ya uchapishaji vitabu ambavyo hulengwa kusambazwa kwa lugha tofauti kiasi kwamba kitabu katika kitengo hiki hupitia katika hatua mbili: Baada ya kitabu kuchapishwa hupewa mtarjumi kwa ajili ya masahihisho na katika hatua ya pili mchapaji huchukua chapa ile kwa ajili ya kuingiza masahihisho na maelekezo na baada ya hapo hutolewa chapa ya pili ambayo kwa mara ya pili tena hupewa mtarjumi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya hapo hutolewa chapa ya mwisho.

 

 

7- Hazina (store):

Hiki ni kitengo chenye jukumu la kuhifadhi vitabu na nassi mbali mbali zilizo kwisha chapishwa na kusambazwa, na kitengo hiki huzihifadhi nyaraka na chapa hizo kwenye mafaili ambapo hutumika tena pale yanapo takiwa kwa siku za mbeleni.

8-Maktaba:

Maktaba imegawanywa sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni ile inayo jumuisha vitabu mbali mbali vichapishwavyo kwenye taasisi mbali mbali ulimwenguni (taasisi za nchi mbali mbali) na ambavyo hupatiwa taasisi hii kama zawadi.

 

Na sehemu ya pili inajumuisha vitabu vya kiarabu ambavyo vyakadiriwa kuwa ni vitabu elfu moja katika maudhui tofauti kama vile Fiqhi na Usuul, Qur’an pamoja na vitabu vingine katika maudhui mbali mbali ambavyo hufaidika navyo wafanya kazi katika kazi zao.

 

Anwani ya Taasisi:

Jamhuri ya kiislaam ya Iran-Qum-eneo la Swafaiyyah- mtaa wa Mumtaz- nyumba namba 30.

Simu: 0098 251 7743996

Fax: 0098 251 7743199

Box 37185/ 737.

Pasword:3715616854 (ramzil-bariid)

www.alimamali.org

www.alimamali.net

www.alimamali.com

Anwani ya sait:

Barua pepe:               Info@alimamali.com

Msimamizi wa kituo:  Webmaster@alimamali.com

Jarida la Mujtaba:     Mujtaba@alimamali.com