Tunajifunza kutokana na hadithi hii tukufu mambo yafwatayo:-
1– Mtume(s.a.w.a) aliwajulisha waislamu kifo chake.
Mtume Mtukufu (s.a.w.a) aliwajulisha waislamu kuhusu kifo chake. Hadithi nyingi zinaonyesha maana hii, kama vile kauli yake tukufu aliyoisema;
((اني اوشك ان ادعى فاجيب))
“Hakika mimi huenda nikaitwa (na Mola wangu) nami nikajibu.”
Na kauli yake:
((ان الله عزوجل اوحى اني مقبوض))
“Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu na Aliyetukuka ameniteremshia wahyi (kunijulisha) kuwa mimi nitafariki”. Pamoja na kauli nyingi nyinginezo.
Hizi hadithi zinaonyesha kuwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) alipozungumza maneno hayo alikua katika hali ya kubainisha wadhifa wa umma baada ya kufa kwake, ili usibaki katika hali ya kupuuzwa, jambo lisilomstahiki Mtume(s.a.w.a) kwani mfano wake, ambaye ni mwanzilishi wa uislamu, atawezaje kuridhia kuuacha uislamu na waislanu hivi tu, bila ya mwelekeo, baada ya kupitio mateso na misiba katika kuuasisi uislamu na serikali ya kiislamu? Kamwe, hekima ya Mwenyezi Mungu pamoja na elimu ya Mtume Mtukufu (s.a.w.a) haimruhusu yeye (s.a.w.a) kufanya vivyo.
2) Kutotengana kwa Qurani na kizazi cha Mtume (s.a.w.a)
Kuviacha vitu viwili (yaani Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ) katika umma ni sawa na kuvifanya kuwa makhalifa wake. Basi Quran na kizazi chake Mtume (s.a.w.a) ni makhalifa wawili wa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) katika ummu. Vinachukua cheo cha Mtume (s.a.w.a) vinapo-dumu kuwa pamoja na kutofarikiana, na hii ndio sababu tunaona kwenye hadithi nyingi Mtume (s.a.w.a) akiviita makhalifa, kama alivyopokea Ahmad katika kitabu chake cha Musnad kutoka kwa Zaid ibnu Thabit, aliyesema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema:
((اني تارك فيكم خليفتين))
“Hakika mimi ninaacha kati yenu makhalifa wawili”.([1])
Vile vile imepokewa kutoka kwa Abu Sa’id Alkhidri ya kwamba alisema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a.) alihotubia na kusema:
((يا ايها الناس اني تركت فيكم الثقلين خليفتين))
“Enyi watu, hakika mimi nimeacha kati yenu vizito viwili, vikiwa (kama) makhalifa wawili”. ([2])
Au kwa riwaya nyingine;
((اني مخلّف فيكم الثقلين))
“Hakika mimi ninaviacha viwili vizito kuwa makh-alifa kati yenu”.([3])
Na kwenye riwaya nyingine alisema:
((قد خلفت فيكم الثقلين))
“kwa hakika nimeviacha viwili vizito kuwa makhalifa kati yenu”.([4])
Lengo la kukifanye kizazi chake (s.a.w.a) kuwa khalifa na kukiachia cheo chake si jengine ila tu, ni kukipa majukumu yake, na hii kwa njia nyingine inathibitisha uimamu na uongozi wa kizazi chake (s.a.w.a) juu ya umma wake.
Kwa hivyo basi, hadithi hii inatuthibitishia vilevile uongozi wao katika mambo ya kisiasa kama inavyo-thibitisha uongozi wao katika mambo ya kielimu na mengineo. Inatuthibitishia pia wajibu wa kuwafuata kiujumla, na wala haikushurutisha jambo lotote lile katika kuwafuata. Imetuthibitishia pia uharamu wa kuwatangulia au kubaki nyuma (yao).
Lakini, ni sikitiko kubwa kuona kuwa umma wa kiislamu uliwaacha na kuwapuuza Ahlulbait (Baada ya kuwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ametilia mkazo sana.) na wala hawakujali haki zao, kwani hawaku-unyenyekea uimamu na uongozi wao, bali walifanya yale waliyoya fanya baada ya kuwa Mtume (s.a.w.a) amemteuwa na kumuainisha Imamu katika sehemu nyingi na hasa katika siku yake ya kuaga dunia.
Zaidi ya hayo hawakuchukuo hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu na wala adabu na sunna za Mtume (s.a.w.a) walibaki bila kuziandika hadi baada ya nusu ya karne ya pili ya hijriya takriban, ali po kuja khalifa Umar ibnu Abdul Aziz na kuifuta sheria hii, kwa kuona kuwa hadithi tukufu zina potea. Ndipo maula-maa wa kisunni wakaanza kuandika hadithi za Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ziilizobaki (kama vile Malik na Ahmad ibnu Hambal na Bukhari na wengineo (kwa utaratibu huo) baada ya kuzisahao nyingi kati ya hizo au baada ya kufariki kwa kwa waliokuwa wamezihi-fadhi. Baadhi ya wachunguzi wa hadithi wamesema ya kwamba “Hadithi wanazozitegemea (ndugu zetu masunni) katika kutoa hukumu za sheria hazizidi mia tano”.
Na kwa hivyo sunna (hadithi) za Mtume Mtukufu (s.a.w.a) kwa ndugu zetu masunni zilikuwa hazijaku-sanywa wala hawakuzijua kabla ya nusu ya karne ya pili, na hali ya kuwa sunna kamili ilikuwa pamoja na Ahlul bait (a.s) tangu kuaga dunia kwa Mtume (s.a.w.a).
Kwa hivyo basi, nini sababu ya kuiacha na kuipuuza elimu ya Ahlulbait, ilhali walikuwa wakina-kili sunna ya Mtume (s.a.w.a) kama ilivyo kuwa, kwa ukamilifu.
Almuhaqqiqul wahiid (Muhakiki wa aina yake) Seyyid Burujurdi (r.a) amesema ya kwamba, “Kuna hadithi nyingi zilizopokelewa kutoka kwa Ahlul bait (a.s) zisemazo kuwa wana kitabu kilichoandikwa kwa imla([5]) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) na kwa khati za Imam Ali bin Abi Talib (a.s), ambacho ndani yake kuna Sunna zote za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) na yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kuyafikisha kwa umma wake, katika mafunzo na hukumu za kidini.”
Kisha alitaja baadhi ya riwaya hizi zenye kuon-yesha kuwepo kwa kitabu kwa imla ya Mtume (s.a.w.a) na kwa hati ya Ali (a.s) na kusema, “Inadhihiri kutokana na hadithi hizi mambo yafwatayo”.
Kwanza: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) hakuuacha umma baada yake bure, bila ya Imamu wa kuwaongoza, wala bayana ya kutosha, bali aliwacha-gulia Maimamu, watukufu, waongozao na kuihifadhi dini, kisha akawapa mafunzo yanayomhusu Mwenyezi Mungu, faradhi za kidini, sunna na adabu, halali na haramu, hekima na athari, na yote wanayoyahitajia watu hadi siku ya kiama, hata ikiwa mtu atamkwaruza mwenzake amewaelezea ni kiwango gani cha faini (dia) kinachofaa kutolewa. Wala hakumruhusu yeyote kuhukumu au katoa fatwa kwa kutumia rai na maoni yake au kwa kutumia Qiyas (kufananisha hukumu za sheria kama wafanyavyo ndugu zetu masunni) kwani hakuna maudhiu au jambo lolote lisilokuwa na hukumu thabiti itokayo kwa Mwenyezi Mungu, Aliye Mjuzi Mwenye Hekima, bali Mtume (s.a.w.a) alimju-lisha Imam Ali Ibnu Abi Talib (a.s) sheria na hukumu zote na kumuamuru kuwa aziandike na kuzihifadhi. Na kuwakabidhi Maimamu (a.s) katika kizazi chake. Basi Ali (a.s) aliandika kwa hati yake (tukufu) na kuwakabidhi waliokusudiwa (yaani Maimamu).
Pili: Mtume (s.a.w.a) alimwamuru Imam Ali Ibnu Abi Talib (a.s) peke yake kuandika na wala hakuna yeyote mwengine katika zama zake aliyejua aliyoku-wa ameandika. Kisha alimwusia kuwa kitabu hiki kiwe mikononi mwa Maimamu kumi na wawili baada yake. Basi inauwajibikia umma wote wa kiislamu kuchukua elimu inayo husu halali na haramu, na yote wanayohitajia katika dini yao kutoka kwake Ali (a.s) na Maimamu watokanao na kizazi chake, kwani wao ndio wasiri wa Mtume (s.a.w.a) na ndio hazina ya elimu yake na wahifadhio dini yake.
Tatu: Kitabu hiki kilikuwa mikononi mwao Maimamu (a.s). Imam Muhammad Baqir (a.s) na Imam Ja’afar Swadiq (a.s) waliwaonyesha baadhi ya maswahaba wao na wengineo katika wafuasi wa dhehebu la kisunni, ili kuitimiza hoja, na ili kuwaon-dolea shaka mioyoni mwao”.
Katika sehemu nyingine Seyyid Burujurdi ana-endelea kusema. “Basi inawajibika kuchukua hadithi katoka kwao, kwani zinaaminika zaidi kuliko za wengineo”.([6])
3) Wajibu wa Kushikamana na Quran na kizazi kitukufu(a.s).
Hadithi hii inatufunza ya kwamba ni wajibu kwa waislamu kushikamana na Qurani tukufu na kizazi, vyote viwiti kwa pamoja. Kwa hivyo basi kushika-mana na kimoja na kukiacha kingine ni kosa kwani maagizo ya hadithi ni kushikamana na vyoze viwili.
Basi watu wameamrishwa kushikamana na Qurani kama walivyoamwrishwa kushikamana na kizazi cha Mtume Mtukufu (s.a.w.a). Katika baadhi ya riwaya imepokewa kuwa alisema:
((وقد تركت فيكم ما ان تمسكتم به لن تضلوا بعدي كتاب الله بين ايديكم تقرؤونه صباحاً ومساءً وفيه ما تلقون وما تدّعون).
“Nimeacha kati yenu ambacho mkishikamana nacho hamtapotea kamwe baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilicho kati yenu, mnakisoma asubuhi na jioni. Ndani nwake mna yote mnayokutana nayo na yote mnayodai…”([7])
Kurejeshwa kwenye Qurani kunaonyesha kuwa inabayana na ufafanuzi wa kutosha, na hii si kutokana na jambo jengine, ila tu ni kwa kuwa, maana dhahiri ya maneno yake ni hoja, kwa hivyo maana ya dhahiri ya maneno yake na aya zake za Muhkamat (zilizo dhahiri) ni nuru na uongofu. Naam, ufafanuzi wa lazima unaachiwa Mtume (s.a.w.a) na kizazi chake kitukufu, kwani Qurani tukufu, haikutoa maelezo yote kuhusu swala, zaka, hijja na mambo mengineo.
Vile vile kufafanua daraja za mafunzo yake na mambo yanayohusiana na akhlaq na jamii na mengi-neyo yote, ni jukumu lililo mikononi mwa kizazi kitoharifu(a.s). Kwa vyovote vile, haijuzu kuacha kuirejelea Qurani kwa kudai kuwa umeshi kamana na kizazi cha Mtume (s.a.w.a), kwani kizazi chenyewe kimeifanya Quran tukufu kuwa ndio kipimio cha haki, zinapo hitilafiana riwaya na hadithi za Mtume (s.a.w.a) na pia na kime kuwa kikiirejelea Qurani katika kupambanua baina ya hadithi zilizodhaifu na zilizosahihi. Kisha kizazi kitukufu kilitilia mkazo kuwa watu wairejelee Qurani na kuitegemea, na kuwahimiza katika mambo mengi yenye uhusiano na Qurani, kama vile kuisoma Qurani na kuizingatia. Kuhusiana na haya, yatutosha kauli yake Amirul muuminin Ali (a.s) aliyosema.
((واعلموا ان هذا القرآن هو الناصح الذي لا يغش والهادي الذي لا يضل والمحدث الذي لا يكذب وما جالس هذا القرآن احد الا قام عنه بزيادة او نقصان: زيادة في هدىً ونقصان من عمىً واعلموا انه ليس لاحد بعد القرآن من فاقة ولا لأحد قبل القرآن من غنى فاستشفوه من ادوائكم واستعينوا به على لأوائكم فان فيه شفاءً من اكبر الداء وهو الكفر والنفاق والغي والضلال فاسألُوا الله به وتوجهوا اليه بحبه ولا تسألوا به خلقه انه ما توجه العبادُ الى الله تعالى بمثله)).
“Tambueni kuwa hii Qurani ni mtoaji nasaha asiye hadaa, na mwongozaji asiyepoteza, na mzungumzaji asiyedanganya. Hakuna anayeketi karibu na hii Qurani, ila tu husimama akiwa na ziyada (katika jambo) na upungufu (katika jambo). Ziada katika uongofu na upungufu katika upofu (na upotofu). Tambueni, kuwa, hakuna mwenye haja, (na ufukara) baada ya kuwa na Quran, na hakuna mwenye utajiri kabla ya kuwa na Qurani. Basi jitibuni kwayo kutokana na maradhi yenu, na itegemeeni katika shida zenu, kwani ndani yake kuna tiba ya ugonjwa mkuu zaidi, nao ni ukafiri, unafiki udanganyifu na upotofu. Basi, muombeni Mwenyezi Mungu kwayo na mumuelekee kwa kui-penda, na wala msiwaombe viumbe vyake kwayo. Hakika waja hawakumwelekea Mwenyezi Mungu kwa njia bora mfano wake (Qurani).
“Na jueni kuwa Qurani ni mtetezi atakaye kubaliwa utetezi wake (siku ye kiyama) na mzungumzaji anayesadikiwa. Na (Jueni) kuwa atakayetetewa nayo siku ya kiyama atakubaliwa (na Mwenyezi Mungu) na ambaye Qurani itashuhudia maovu yake (mbele ya Mwenyezi Mungu) siku ya kiyama itasadikiwa (na kukubaliwa)”.([8])
Vile vile yatutosha kauli yake Imam wetu Ja’afar Sadiq (a.s) aliyosema,
((ثلاثة يشكون الى الله عزوجل: مسجد خراب لا يُصلى فيه اهله وعالم بين جهّال ومصحف معلق قد وقع عليه الغبار لا يُقرأ فيه)).
“Vitu vitatu vitashitaki kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, (siku ya kiyama), msikiti ulioharibika ambao watu wake hawaswali ndani yake, na mwana chuoni katikati ya wajinga (wasiotaka kusoma) na Msahafu uliotundikwa, uliojaa mavumbi, usiosomwa”.([9])
Na kauli yake (a.s) nyingine:
((ان هذا القرآن فيه منار الهدى ومصابيح الدُجى فليَجْلُ جالٍ بَصَرَه ويفتح للضياء نظره فان التفكر حياة قلب البصير كما يمشي المستنير في الظلمات بالنور)).
))Haikika ndani mwa hii Qurani kuna nuru ya uon-gofu, na taa (zinazowaka) na kuondosha kiza, basi na atembeze mtembezaji macho yake na ayafungue ili kuupokea mwangaza (wake) kwani tafakari ndio uhai wa moyo wenye busara (na ayatembeze macho) kama yule anayetaka nuru yake atembeavyo gizani”([10])
Tambueni kuwa mwenye kutosheka tu nakuwataja Ahlul bait(a.s) bila ya kufwata maagizo na makatazo ya Qurani na mwelekezo wake, basi atakua hajachukua kutoka kwa Ahlulbait (a.s) kikamilifu, kwani wao hawaridhishwi kamwe na mtu kuiacha na kuipuuza Qurani.
Vile vile haifai kutosheka na Qurani pekee, kwani ufafanuzi kuihusu Quran kiupana pamoja na hukumu na elimu za Qurani zote ziko kwao, Ahlul bait (a.s).
Haya ni pamoja na haja iliyoko ya kuwepo kwao katika kuimarisha uadilifu, malezi bora, utakaso na kuondoa kuhitilafiana (baina ya waislamu) pamoja na mambo mengineo katika ulimwengu.
Kushikamana na Qurani bila ya kushikamana na Ahlulbait sio kushikamana kikamilifu na Qurani, kwani aya za Qurani zenyewe zinatuele keza katika kuwatawalisha juu ya mambo yetu yote na kuwatii na inatuelekeza katika wajibu wa kuwapenda, kwani kila moja wapo (Qurani na Ahlulbait) – kama ilivyo katika baadhi ya hadithi – inaifafanua nyengine na kuafikiana nayo.([11])
Kwa hivyo basi, la wajibu ni kushikamana na vyote viwili, na hili ndilo jambo lililotiliwa mkazo katika hadithuth thaqalain, isemayo:
((ما ان تمسكتم بهما لن تضلوا بعدي))
“Mkishikamana navyo (vizito viwili) hamtapotea kamwe baada yangu” pamoja na riwaya nyingi nyingi-nezo.
4) Sababu ya kuiita Qurani na kizazi vizito viwili (Thaqalain)
kuiita Qurani na Ahlul bait kuwa ni vizito viwili (Thaqalain) huenda ikawa ni kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa ni vitu vyenye thamani na utukufu sana. Hata hadithi yenyewe yaelezea binafsi kuhusu utukufu wa Quran na cheo kitukufu cha Ahlul bait (a.s).
Imenakiliwa kutoka kwenye kitabu cha Abaqatul Anwar kutoka kwa Ibnul Athir ya kwamba ameandika kwenye kitabu chake cha Annihaya kuwa “chochote kilicho hatari na chenye thamani huitwa “thaqal” (kizito). Basi ameviita vizito viwili (Thaqalain) ili kuonyesha utukufu wa cheo cha vitu hivi viwili na kwa hivyo neno kizito lafaa kusomwa kwa kutamta fatha mbili (Juu ya herufi mbili za mwanzo – yaani – ثَقَلُ (Thaqal)”.
Qurani ni tukufu zaidi ya Kitabu chochote kilichoteremshwa na Mwenyezi Mungu, nayo ni muujiza wa milele, itaendelea kuwepo madamu jua lipo. Nayo ni ufunuo (wahyi) usiopatwa na ubatilifu kabla yake wala baada yake, na ni nuru na uongofu.
Vile vile, kizazi, hakina mfano katika sifa, elimu na fadhila tukufu. Kama ilivyo makosa kuwalinganisha Mitume watukufu (a.s) na watu wa kawaida, vile vile ni makosa kuwalinganisha Ahlul bait (a.s) na watu wengineo wa kawaida, kwani wao ni mahujja([12]) wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe vyake na wao ni hazina ya elimu yake.
Amirul muuminin Ali ibnu Abi Talib (a.s) katika maneno yake mafupi, (yaliyoko kwenye kitabu cha Nahjul balagha) kuhusu Ahlul bait (a.s) kwa kusema:
((انهم موضع سره ولجأ امره وعيبة علمه وموئل حكمه وكهوف كتبه وجبال دينه بهم اقام انحناء ظهره واذهب ارتعاد فرائصه… لا يقاس بآل محمد(ص) من هذه الامة احدٌ ولا يسوّي بهم من جرت نعمتهم عليه ابداً هم اساس الدين وعماد اليقين اليهم يفيء الغالي وبهم يلحق التالي ولهم خصائص حق الولاية وفيهم الوصية والوراثة الآن اذ رجع الحق الى اهله ونقل الى منتقله)).
“Wao ni wasiri wake (Mwenyezi Mungu) na maficho (sanduku) ya mambo yake, na chemchemi ya elima yake na marejeo ya hekima zake, pango za vitabu vyake na milima ya dini yake. Kwa kupitia kwao amenyoosha kupinda kwa mgongo wa dini na kuondosha kutetemeka kwa viungo vyake (dini) …… Hakuna katika umma huu anayeweza kulinginanishwa nao, na kamwe hawezi kusawazishwa nao yule anayetawaliwa na fadhila zao. Wao ndio msingi wa dini na nguzo ya imani. Aliyewatangulia (na kupita mipaka) yampasa kuwarejelea, na aliyebaki nyuma yampasa kuwafikia. Wana sifa zote za kustahiki uwalii (uongozi) na wao ndio wenye wasia (wa Mtume (s.a.w.a) na urithi (wake). Huu ndio wakati ambao haki imemrudia mwenyewe (anayeistahiki) na kunakiliwa hadi kwenye mahala pake.”([13])
Huenda mtu akadai, kama alivyosema Zamakhshari, kuwa neno thaqalain limetumiwa kwenye hadithi kwa lengo la kuvifananisha vizito viwili na majini (yaani) kama wanavyoitwa (watu na majini) thaqalain (ndani ya Qurani) kumaanisha dunia, vile vile thaqalain (Quran na Ahlul bait) limetumika kumaanisha dini.([14])
Na huenda ikawa makusudio ya kutumia neno hili thaqalain, ni kuonyesha kuwa kutenda na kushikamana na vizito viwili na kutii na kuchunga haki zao na kuviangalia ni jambo zito. (Hii ni) kama walivyofasiri baadhi ya wajuzi wa lugha ya kiarabu, na wajuzi wa hadithi tukufu kama alivyo nukuu Alhamwini kutoka kwa Ibnul Abbas, ya kwamba, “Aliulizwa maana ya kauli ya Mtume (s.a.w.a) “Hakika mimi ninaacha
((اني تارك فيكم الثقلين)) kati yenu thaqalain (vizito viwili)?” akasema “kwa kuwa kushikamana navyo nikuzito (Thaqiil)”.([15])
Na katika riwaya nyingine vile vile kutoka kwake, amesema, “kwa kuwa kushikamana navyo na kutenda kufwatana navyo ni kuzito (thaqiil).”([16])
Maneno haya vile vile yametajwa katika kitabu cha Abaqatu; Anwar kama ilivyopokewa kutoka kwa Al-azhari kwenye kitabu cha Tahdhibul lugha na kwenye vitabu vingine pia.([17])
Kwa hivyo basi, kufuatana na kauli hii neno (ثِقْلُ) (Thiqlu) lenye kasra – lina maana ya mzigo mzito au mojawapo ya vitu vizito, lakini hii ni kinyume cha maana dhahiri ya hadithi, kwa kuwa (ikifasiriwa vivyo) itakuwa ina sifia hali ya hivi vitu viwili, na ilhali dhahiri ya hadithi inawajibisha hii kuwa sifa ya vitu vivyo (wala siyo sifa ya hali yavyo) kwa kuwa vyenyewe ni vizuri na vyenye utukufu na cheo.
5) Maana ya Al-itrah (kizazi).
“Al-itra” (kizazi) kama lilvyotajwa katika Annihaya na katika vitabu vinginevyo ni jamaa wa karibu wanaomhusu mtu.
Kwa hivyo basi neno hili haliwa kusanyi wasio kuwa jamaa wa karibu wanaomhusu mtu, mbali na wasio kuwa jamaa wa karibu, bali kinacho kusudiwa hapa kufuatana na mnasaba wa hukumu na maudhui([18]) sio yeyote yule, katika jamaa wa karibu kwani sifa zao zilizotajwa kwenye hadithi- kama kuwafanya kuwa ni sawa na Quran tukufu na mizani ya haki na uongofuhazitusaidii katika kulitumikisha neno hili kuwakusanya wote. Kwa hivyo basi wanaokusudiwa – kama ilivyo tajwa waziwazi kwenye riwaya chungu nzima – ni Ahlul bait waliotajwa katika Qurani tukufu kuwa wametoharishwa (kutokana na madhambi) nao ni Maimamu Maasumu waliowatoharifu.
Ibnu Abil Hadid amesema kuwa “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) alishabainisha kuwa ninani kizazi chake (itrah) aliposema”.
((اني تارك فيكم الثقلين))
“Hakika mimi ninaacha kati yenu thaqalain (vizito viwili)” kisha akasema;
((وعترتي اهل بيتي))
“Na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu” (yaani watu wa nyumba yangu). Kisha akabainisha katika sehemu nyingine kuwa ni nani Ahlubaiti wake, alipowakusanya chini ya shuka, ilipoteremka aya
]انما يريد الله ليذهب عنكم الرجس اهل البيت ويطهركم تطهيراً[
“Hakika Mwenyezi Mungu Anataka kakuondo-leeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakasenikabisa kabisa” na kusema;
((الّلهم هؤلاء اهل بيتي فاذهب الرجس عنهم))
“Ewe Allah, hawa ndio Ahlubait wangu, basi waondolee uchafu”.([19])
Aljurjani Ash-shafii; (Aliyefariki katika mwaka wa 365 H.) amepokea kutoka kwa Abu Said ya kwamba alisema, “Hii aya – ayatut tat-hir’ – (aya ya kutakaswa kwa Ahlulbait), iliteremshwa kuwahusu watu watano… Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s)”([20])
Adh-dhahabi katika Talkhisul mustadrak amepokea kutoka kwa Ummu Salama ya kwamba alisema,
((في بيتي نزلت ]انما يريد الله ليذهب عنكم الرجس اهل البيت ويطهركم تطهيراً[ فارسل رسول الله (ص) الى عليّ وفاطمة والحسن والحسين فقال: ((الّلهم هؤلاء اهل بيتي)) قالت ام سلمة: ((يا رسول الله ما انا من اهل البيت؟ قال: لا انك إلى خير وهولاء اهل بيتي الّلهم اهلي احق)).
“Hakika Mwenyezi Mungu Anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa”. ilitermka nyumbani kwangu. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) akawatumania Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s), na kusema, “Ewe Allah hawa ndio Ahlubaiti wangu”. Ummu Salama akamwambia (Mtume (s.a.w.a)) “Ya Rasulallah, Je, mimi si katika Ahlulbait?” akamjibu “Hakika wewe u katika kheri, na hawa ndio Ahlubaiti wangu. Ewe Allah Ahlubati wangu ndio wenye haki zaidi”.([21])
Na kuna riwaya nyingi nyinginezo zinazoonyesha kuwa Ahlul bait katika ayatut tathir wanao kusudiwa ni watu makhsusi.
Na hivyo ndivyo ilivyo pia katika riwaya zinazoifasiri “ayatul mubahala” (aya ya kuapizana kwa Mtume (s.a.w.a) na wakristo wa Najran) ambazo vile vile zinaelezea kuwa makusudio hasa ya Ahlul bait ni akina nani.
Muslim amepokea kwa isnadi yake, kwamba “ayatul mubahala([22]) ilipoteremka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s) na kusema.
((اللهم هؤلاء اهل بيتي ـ اهلي ـ))
“Ewe Allah hawa ndio Ahlu baiti wangu, Jamaa wangu (wa nyumbani)”.([23])
Na ndio sababu imetajwa kwenye kitabu cha Abaqatul Anwar kukiri kwa maulama wa dhehebu la kisunni kuwa hadithuth thaqalain inazungumza kuhusu Maimamu watokanao na Ahlulbait (wala haiwahusu watu wengine).
Miongoni mwa maulama hawa ni Alhakim Attirmidhi, aliyesema kuwa, “Basi kauli ya Mtume wa Mwenyezi, Mungu (s.a.w.a) kuwa
((لن يفترقا حتى يردا علي الحوض))
“Havitatengana kamwe mpaka vitakaponijia huko kwenye hodhi (ya kauthar)” na kauli yake kuwa
((ما ان اخذتم به لن تضلوا))
“Mkishikamana nacho hamtapotea kamwe”, inawa-husu Maimamu. Basi wao ni maseyyid (mabwana) na wala haiwahusu wengine”.([24])
Na miongoni mwao ni Sibtu Ibnil Jauzi, alipoitaja hii hadithi katika Tadhkiratul khawass, chini ya unwani ya (ذكر الائمة) “Tunayoyataja kuwahusu Maimamu”.([25])
Na miongoni mwao ni Alkanji Ash-shafii katikakifaya tut Talib (baada ya kuitaja riwaya ya Zaid Ibnu Arqam na tafsiri yake ya Ahlulbait, kuwa ni wale walioharanmishiwa kula sadaka) alisema kuwa – “Hii tafsiri ya Zaid kuwahusu Ahlul bait hairidhishi, kwani amesema “Ahlulbait ni wale ambao wameharamishiwa kula sadaka baada yake – (yaani baadaye Mtume sawa) – ilhali kuharamishiwa kwao sadaka sio tu baada ya kufariki kwa Mtume(s.a.w.a), bali hata katika uhai wake. Vile vile kuharamishwa huku hakuwahusu tu waliotajwa (katika hadithi) bali kunawahusu hata Bani Muttalib”. mpaka akafikia kusema, “Bali lililo sahihi ni kuwa Ahlul bait ni Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s) kama alivyopokea Muslim kwa isnadi yake kutoka kwa Bibi Aisha (aliyeseme).
((ان رسول الله خرج ذات غداة وعليه مرط مرَّجل من شعر اسود فجاء الحسن بن علي فادخله ثم جاء الحسين فادخله معه ثم جاءت فاطمة فادخلها ثم جاء عليّ فادخله ثم قال ]انما يريد اللهُ ليذهب عنكم الرجس اهل البيت ويطهركم تطهيراً[ )).
“Siku moja asubuhi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) alitoka akiwa amejifinika kwa shuka iliyoshonwa kwa sufi nyeusi; Hasan ibnu Ali akamjia, (Mtume) akamwingiza (ndani ya shuka). Kisha akaja Husein, akamwingiza (pia). Kisha akaja Fatima, akamwingiza (pia). Kisha akaja Ali, akamwingiza (vile vile) : Kisha akasema “Hakika Mwenyezi Mungu (Anataka) kukuon-doleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (Anataka) kukutakaseni kabisa kabisa”.
Na hii ni dalili ya kuonyesha kuwa Ahlulbait ni wale ambao Mwenyezi Mungu Aliwaita kwa kauli yake Ahlulbait ambao Mtume (s.a.w.a) aliwaingiza ndani ya shuka”.([26])
Kuna maulamaa wengine wengi waliokiri (kuwa Ahlulbait katika hadithuth thaqalain ni Maimanu Maasumin), walio tajwa, majina yao pamoja na maneno yao (yaani maulamaa) kwenye kitabu cha Abaqatul Anwar.([27])
Haya, bila ya kutaja riwaya nyingi zilizo mutawatir([28]) katika vitabu vyetu zinazohusiana na mlango huu, ambazo miongoni mwazo ni riwaya aliyoipokea Ibnu Babaweihi katika kitabu cha “Uyunu Akhbarir Ridha (a.s)” kutoka kwa Imam Ja’afar Swadiq (a.s) kutoka kwa babu zake watukufu (a.s) kutoka kwa babu yake, (ambaye ni) Imam Husein (a.s) ya kwamba alisema”,
((سُئل اميرالمؤمنين (ع) عن معنى قول رسول الله ((اني مخلف فيكم الثقلين: كتاب الله وعترتي)) مَن العترة؟ قال: انا والحسن والحسين والائمة التسعة تاسعهم مهديهم وقائمهم لا يفارقون كتاب الله ولا يفارقهم حتى يردوا على رسول الله حوضه)).
“Amirul muminin Ali (a.s) aliulizwa maana ya kauli yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) (aliyosema) “Hakika mimi ninaacha kati yenu vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na (itrah) kizazi changu”. Ni nani itrah (kizazi)? Akasema “Ni mimi, Hasan, Husein na Maimamu tisa, wa tisa kati yao ndiye Mahdi na Qaim, (kamwe) hawa tengani na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nacho hakitengani nao, hadi watakapomjia Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenye hodhi yake (ya kauthar)”.([29])
Kwa hivyo ni wazi kuwa “itrah” (kizazi) ni Ahlul bait, nao ni Maimamu watoharifu na maasumin ([30]) watukufu (a.s).
6) Quran na Ahulbait ndio kamba ya Mwenyezi Mungu
Qurani ni kamba ya Mwenyezi Mungu kama Asemavyo Mwenyezi Mungu;
]واعتصموا بحبل الله جميعاً ولا تفرقوا[
“Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote, wala msitengane”.
Kuna riwaya nying zinazoshuhudia jambo hili. Miongoni mwazo, ni riwaya aliyoipokea Abu Said Alkhidri kutoka kwa Mtume (s.a.w.a) ya kwamba alisema,
((اني اوشك ان ادعى فاجيب واني تارك فيكم الثقلين: كتاب الله وعترتي كتاب الله حبل ممدود من السماء الى الارض وعترتي اهل بيتي وان اللطيف الخبير اخبرني انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فانظروا كيف تخلّفوني فيهما)).
“Huenda nikaitwa na (Mola wangu) nami nikajibu, nami ninaacha kati yenu vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooshwa kutoka mbinguni hadi ardhini nacho Kizazi changu ni Ahlubait wangu (watu wa karibu wa nyumbani kwangu). Naye Mwingi wa huruma Aliyemjuzi wa yote amenijulisha kwamba havitotengana kamwe mpaka vitakaponijia kwenye hodhi (ya kauthar). Basi angalieni mtakavyo-vitendea baada yangu”.([31])
Vile vile kamba ya Mwenyezi Mungu inawaku-sanya Ahlulbait (a.s), kwa kuwa wamefanywa kuwa sawa na Quran katika hadithuth thaqalain, na kwa kuwa wameteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwaongoza watu. Basi kushikamana nao ni sawa na kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo inatuzuia na kupotoka na kuangamia.
Katika Tafsiru Alaur Rahman’ baada ya kuitaja aya hii,
((واعتصموا بحبل الله جميعاً…))
“Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote…”
Mwandishi amesema, “yaani jizuieni kutokana na kuanguka, kwa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu mkiwa katika hali ya umoja, na (pia) kwa kushikamana na) kile ambacho amekijaalia kuwa ni chenye kuwahifadhi (na kuwazuia) kutokana na kuanguka kwenye upotofu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) ameshatu julisha kuwa ni nani wanaoitwa kamba, ambayo mwenye kushikamana nayo hapotei, katika kauli yake kwenye hadithuth thaqalain isemeyo:
((ما ان تمسكتم بهما لن تضلوا كتاب الله وعترتبي اهل بيتي))
“Ambavyo mkishi kamana navyo hamtapotea kam-we, (navyo ni) Kitaba cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambao ni) Ahlubait wangu”. Neno kamba limetumika katika (maana) kuonyesha kuwa kutoshi-kamana nayo kutamfanya mtu kuanguka kwenye upotofu mkubwa na kuangamia.”([32])
Dalili nyingine inayo tuthibitishia kuwa neno kamba halikutumiwa makhsusi kwa Qurani, bali lime-wakusanya pia Ahlul bait, ni kuwa, Mtume(s.a.w.a) amekusanywa kwenye maana hii katika aya
]وكيف تكفرون وانتم تتلى عليكم آياته وفيكم رسوله ومن يعتصم بالله فقد هدى الى صراط مستقيم[
“Na mnakanushaje, hali nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu, na Mtume wake yuko pamoja na nyiye? Na mwenye kumshika Mwenyezi Mungu sawa sawa basi yeye amekwishaongozwa katika njia iliyonyooka”
Katika aya hizi ni dhahiri kuwa kushikamana na aya za Mwenyezi Mungu na kumfwata Mtume (s.a.w.a) ni sawa na kushikamana na kamba ya Mwe-nyezi Mungu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika aya iliyotangulia, kwamba kushikamana navyo ni kushikama na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo basi kama vile Mtume (s.a.w.a) ni mfano wa kamba ya Mwenyezi Mungu, vile vile kizazi chake kitukufu chenye kuchukua cheo chake (baada yake) ni mfano wa kamba ya Mwenyezi Mungu.
Haya pamoja na kuongezea riwaya nyingi zilizoe-lezea wazi wazi jambo hili. Miongoni mwazo ni riwaya iliyopokewa kwenye Abaqatul Anwar kutoka kwa Sheikh Suleiman Al-hanafi Alqanduzi katika tafsiri ya aya “Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote…” alisema kuwa “Ath-tha’alabi amepokea kwa sanadi yake (silsila ya wapokezi) kutoka kwa Aban Ibnu Taghlib kutoka kwa Ja’afar Swadiq (R.a.) ya kwamba alisema.
((نحن حبل الله الذي قال الله عزوجل: واعتصموا بحبل الله جميعاً ولا تفرقوا)).
“Sisi ndio kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka Amesema. “Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msiachane”.
Vile vile mwandishi wa Kitabul Manaqib ame-pokea kutoka kwa Said Ibnu Jubair (R.a) kutoka kwa Ibnul Abbas (r.a) ya kwamba alisema:
((كنا عند النبي صلى الله عليه وسلم اذ جاء اعرابي فقال يا رسول الله سمعتك تقول: واعتصموا بحبل الله فما حبل الله الذي نعتصم به؟ فضرب النبي صلى الله عليه وآله وسلم يده في يد عليّ وقال: ((تمسّكوا بهذا هو حبل الله المتين)).
“Tulikuwa pamoja na Mtume (s.a.w.a) alipokuja bedui mmoja wa kiarabu na kumwambia “Ya Rasulallah, nilikusikia ukisema “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu”. Basi ni ipi kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo tutashikamana nayo? Mtume (s.a.w.a) akaupigisha mkono wake kwenye mkono wa Ali na kusema “Shikamaneni na huyu, yeye adiye kamba ya Mwenyezi Mungu iliyoimara”.([33])
Na miongoni mwazo ni hadithi aliyoipokea Annumani kwa isnadi yake kutoka kwa Hariiz Ibnu Abdillah kutoka kwa Abu Abdillah Ja’afar Swadiq Ibnu Muhammad (a.s) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu zake (a.s) kutoka kwa Ali (a.s) ya kwamba alisema,
((خطب رسول الله في مسجد الخيف – وهي خطبة مشهورة في حجة الوداع – قال فيها: … الا واني مخلف فيكم الثقلين: الثقل الاكبر والثقل الاصغر: الثقل الاكبر القرآن والثقل الاصغر عترتي اهل بيتي هما حبل ممدود بينكم وبين الله جل وعز ان تمسكتم به لن تضلوا سبب منه بيد الله وسبب بايديكم)).
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) aliho tubia kwenye msikito wa Alkhiif – (Nayo ni hotuba mashu-huri katika hijjatul wida’a (hijja yake ya mwisho) – na kusema” …. Tambueni kuwa mimi ninaacha kati yenu vizito viwili, kizito kikubwa na kizito kidogo. Kizito kikibwa ni Quran, na kizito kidogo ni kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu. Navyo (viwili hivi) ni kamba iliyonyooshwa baina yenu na baina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na Mwenye Nguvu. Mkishikamana nayo hamtapotea kamwe. Sehemu moja yake iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na sehemu (nyingine) iko mikononi mwenu”.([34])
Na miongono mwazo ni hadithi aliyoitaja Ibnu Abil Hadid, ya kwamba Mtume (s.a.w.a) alisema,
((خلّفت فيكم الثقلين كتاب الله وعترتي اهل بيتي حبلان ممدودان من السماء الى الارض لا يفترقان حتى يردا علي الحوض)).
“Nemeacha kati yenu viwili vizito (kama) makhalifa (wawili) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (amboa ni) Ahlubait wangu, (hivi viwili) ni kamba mbili zilizonyooshwa toka binguni hadi ardhini, (na) havitatengana mpaka vitakapanijia huko hodhini (mwa kauthar). ([35])
Kwa hivyo basi, la wajibu kufanya katika kuleta umoja na kuondosha utengano na ufarikiano, ni kushikamana na vizito viwili na kuzuia utengano kabisa, kwani hivi ndivyo vinavyoleta umoja, kama ilivyo kuwa katika zama za Mtume (s.a.w.a) umoja ulipatikana kwa kushikamana na Mtume wake (s.a.w.a). Yatupasa basi, sisi waislamu, kuamka kutoka usingizini na kushikamana na sababu muhimu na ya asili ya umoja wetu. Ndipo tutakuwa tumepata umoja wa kweli tulioamrishwa kuwa nao katika aya tukufu, na umoja huu utakuwa umeondoa umoja wa juu juu, hata ingawa ni umoja unaofaa, unaostahiki kuwepo.
Kisha kuiita Qurani na kizazi kwa jina la kamba ya Mwenyezi Mungu kunaonyesha wazi uhusiano mkubwa vilivyonao na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo mwenye kushikamana navyo atakuwa kwa hakika ameshikamana na Mwenyezi Mungu. Na kunaonyesha pia kuwa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu ndio njia ya pekee ya kujihifadhi kutokana na upotovu.
7) Kutotengana kwa Qurani na kizazi kitukufu milele:
Qurani na kizazi kitukufu cha Mtume Muhammad (a.s) ni vyenye kuandamana daima kama mapacha wawili na havitotengana kamwe na vitadumu kuwepo. Hadithi nyingi za thaqalain (vizito viwili) zimesema wazi wazi jambo hili. Kwa mfano kauli yake Mtume (s.a.w.a) isemayo,
((الا وانهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض))
“Tambueni kuwa viwili hivi havitatengana kamwe hadi vitakaponijia huko hodhini (mwa kauthar)” Na mfano wa kauli yake nyingine,
((وان اللطيف الخبير اخبرني انهما لن يفترقا))
“Na hakika Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyodhahiri Amenijulisha ya kwamba havitatengana kamwe”.
Hizi zilikuwa habari za ghaibu na bishara kuhusu kubaki kwa Qurani na kizazi kitukufu hadi siku ya kiyama. Bishara ya kuonyesha kuwa Qurani tukufu na kizazi, vitadumu kuwepo na hakuna wakati ambao havitakuwepo. Kama vile Qurani ni muujiza wa milele, vile vile kizazi cha Mtume (s.a.w.a) ni muujiza wa milele na kamwe hakitakosekana ardhini (hiki kizazi).
Kuna hadithi nyingi pia zilizotamka waziwazi jambo hili, mfano wake ni ile iliyopokewa na Sheikh Suleiman Alhanafi Alqanduzi kwa isnadi yake kutoka kwa Imam Hasan (a.s) ya kwamba alisema,
((خطب جدي(ص) يوماً فقال بعد ما حمد الله واثنى عليه: معاشر الناس اني ادعى فاجيب واني تارك فيكم الثقلين كتاب الله وعترتي اهل بيتي ان تمسكتم بهما لن تضلوا وانهما لن يتفرقا حتى يردا علي الحوض فتعلّموا منهم ولا تعلموهم فانهم اعلم منكم ولا تخلو الارض منهم ولو خلت لانساخت باهلها)).
“Siku moja babu yangu (Mtume) (sawa) alihotubia. Baada ya kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, alisema” Enyi watu, hakika mimi nitaitwa (na Mola wangu) nami nitajibu, nami ninaacha kati yenu viwili vizito, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu, mkishikamana navyo hamtapotea kamwe. Navyo havitatengana kamwe hadi vitakaponijia kwenye hodhi (ya kauthar). Basi jifun-disheni kutoka kwao na wala msiwafundishe kwani wao ni wajuzi zaidi yenu, na kamwe ardhi haitobaki bila wao. Lau kama itabaki bila wao, basi itaangamia pamoja na watu wake”.([36])
Hili ni jambo linalokubaliana na akili, kwani ardhi kubaki bila Hujja wa Mwenyezi Mungu (ambaye ni Mtume (s.a.w.a) au Imamu) ni kinyume cha hekima ya Mwenyezi Mungu, hekima ya kutaka kutimiza hoja (yaani itmamul hujja) zake, (kwani Mwenyezi Mungu hawezi kuwaadhibu viumbe vyake kabla ya kuwatumia mwongozo kamili na kuwaonyesha jinsi ya kutekeleza kufwatana na mwongozo huo. wakiwa Mitume na Maimamu ndio waalimu na wafafanuzi wa mwongozo huu, ambapo watu wakiwa watakosa kuufwata watakuwa hawana hoja na dalili ya kujitetea mbele ya Mwenyezi Mungu kwani ameshatimiza na kukamilisha hoja zake kwa kuwapa mwongozo). Kuna hadithi nyingi zinazo elezea jambo hili. Miongoni mwazo ni hadithi zisemazo kuwa:
a) Ahlul bait ni amani kwa watu wa ardhini
Katika kitabu kiitwacho “Fadhailu Ali Ibni Abi Talib” cha Ahmad Ibnu Hambal amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Ali (a.s) ya kwamba alisema,
((قال رسول الله ((النجوم امان لاهل السماء اذا ذهبت النجوم ذهب اهل السماء واهل بيتي امان لاهل الارض فاذا ذهب اهل بيتي ذهب اهل الأرض)).
“Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, “Nyota ni amani kwa watu wa mbinguni, zitakapoondoka nyota (basi) watu wa mbinguni wataondoka (na kuangamia). Nao Ahlu baiti wangu ni amani kwa watu wa ardhini, watakapoondoka Ahlu baiti wangu (basi) watu wa ardhini wataondoka (na kuangamia)”.([37])
Na katika “Aamal” cha Sheikh Attusi kwa Isnadi yake kutoka kwa Ibnu Abbas, ya kwamba alisema,
((قال رسول الله(ص): ((النجوم امان لاهل السماء واهل بيتي امان لامتي فاذا ذهب النجوم ذهب اهل السماء واذا ذهب اهل بيتي ذهب اهل الارض)).
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) amesema, “Nyota ni amani kwa watu wa mbinguni, na Ahlubaiti wangu ni amani kwa umma wangu, zitakapoondoka nyota, (basi) watu wa mbinguni wataondoka na wata-kapoondoka Ahlubaiti wangu (basi) watu wa ardhini wataondoka (na kuangamia)”.
Alhamwani amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Abdullah Ibnul Abbas ya kwamba alisema:
((قال رسول الله: ان خلفائي واوصيائي وحجج الله على الخلق بعدي لاثنا عشر اولهم اخي وآخرهم ولدي. قيل يا رسول الله ومن اخوك؟ قال: علي بن ابي طالب. قيل: فمن ولدك؟ قال: المهدي الذي يملأ الارض قسطاً وعدلاً كما مُلئت جوراً وظلماً والذي بعثني بالحق بشيراً لو لم يبق من الدنيا الا يوم واحد لطوّل الله ذلك اليوم حتى يخرج فيه ولدي المهدي فينزل روح الله عيسى بن مريم فيصلي خلفه وتشرق الارض بنور ربها ويبلغ سلطانه المشرق والمغرب)).
“Kwa hakika Makhalifa wangu na Mawasii wangu na Mahujja wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe baada yangu (watakuwa) kumi na wawili wa mwanzo wao ni ndugu yangu na wa mwisho wao ni mwanangu”. Akaulizwa “Ya Rasulallah, na ni nani ndugu yako?” Akasema, “Ali Ibnu Abi Talib” akaulizwa, “Na ninani mwanao?” Akajibu, “Almahdi ambaye ataijaza ardhi kwa usawa na uadilifu baada ya kujazwa kwa ujeuri na dhulma. Naapa kwa yule Aliyeniteuwa kwa haki kuwa mbashiri, lau kama ardhi itakuwa haijabakisha ila siku moja, Mwenyezi Mungu Atairefusha hiyo siku ili Amdhihirishe mwanangu Almahdi. Basi (siku hiyo) Atamshusha Isa Ibnu Maryam (kutoka mbinguni) naye ataswali nyuma yake (Almahdi) na hapo ardhi itanawiri kwa nuru ya Mola wake, na utawala wake (Almahdi) utafika mashariki na magharibi.”([38])
Almuwaffaq Ibnu Ahmad (mmoja katika maulama wakubwa wa kisunni) amenukuu hadithi kutoka kwa Salman Almuhammadi([39]) ya kwamba alisema”.
دخلت على النبي(ص) واذا الحسين على فخذه وهو يقبل عينيه ويلثم فاه وهو يقول: ((أنت سيد بن سيد واخو سيد وابو السادة انت امام بن امام اخو امام وابو الائمة، انت حجة بن حجة اخو حجة ابو حجج تسعة من صلبك تاسعهم قائمهم)).
“Nilimtembelea Mtume (s.a.w.a) nikampata Husein akiwa (ameketi) mapajani mwake, huku (Mume) (s.a.w.a) anayabusu macho yake na mdomo wake na kumwambia, “wewe ni bwana, mwana wa bwana (seyyid), ndugu wa bwana, na baba wa mabwana. Wewe ni Imamu, mwana wa Imamu, ndugu wa Imamu, na baba wa Maimamu. Wewe ni Hujja mwana wa Hujja ndugu wa Hujja baba ya mahujjah tisa watokanao na kizazi chako, wa tisa wao akiwa ndiye Alqain (Almahdi).”([40])
Muslim katika kitabu chake “Sahihu Muslim” amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Jabir Ibnu Samura ya kwamba alisema”.
سمعت النبي(ص) يقول: ((لا يزال امر الناس ماضياً ما وليهم اثنا عشر رجلاً)) ثم تكلم النبي (ص) بكلمة خفيت علي فسألت ابي: ماذا قال رسول الله (ص) فقال: قال: ((كلهم من قريش)).
“Nilimsikia Mtume (s.a.w.a) akisema, “Mambo ya watu yataendelea kutangamana madamu watu kumi na wawili wanawatawala”, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu alitamka neno ambalo sikulipata, basi nilimu-uliza baba yangu “Je, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) amesema nini?” akasema “Amesema, “wote watatokana na Qureish”.([41])
Alhamwini amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Nafii ya kwamba alisema”,
سمعت رسول الله(ص) يقول: ((لا يزال الدين قائماً حتى تقوم الساعة ويكون عليكم اثنا عشر خليفة كلهم من قريش)).
“Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) akisema “Dini itaendelea kuwepo hadi siku ya kiama, na wataendelea kuwatawala Makhalifa kumi na wawili wote wanaotokana na Qureish.”([42])
Pamoja na riwaya nyingi nyinginezo.
Na hii ndiyo sababu tunamuona Samhudi ananakiliwa kwenye kitabu cha “Jawahirul Aqdain” kutoka kwenye kitabu cha “Tanbihatuth thaqalain” akisema kuwa “Hii inaonyesha kuwepo kwa watu wanaostahiki kushikamanwa nao, miongoni mwa Ahlul bait na kizazi kitoharifu, katika kila zama wanapokuwepo hadi siku ya kiyama. Na ndio sababu hadithi zikasisitiza katila kushikamana nao, kama zilivyosisitiza kuhusu Quran tukufu. Na hiyo ndiyo sababu, kama tutakavyoelezea baadaye, wakawa ni amani kwa watu wa ardhini, ambapo wa kiondoka nayo ardhi itaondoka”.([43])
Vile vile Ibnu Hajar katika kitabu chake “Assawaiqul Muhriqa”, na katika hadithi zinazosisitiza katika kushikamana na Ahlul bait, kuna ishara kuwa wata-endelea kushikamanwa nao hadi siku ya kiyama, kama Qurani tukufu ilivyo, na ndiyo sababu wakawa ni amani kwa watu wa ardhini”.([44])
Kwa hivyo basi hadithi hii tukufu ni katika dalili za kuonyesha ulazima wa kuwepo Imamu katika kila zama, na hili ni jambo lililowazi kwa watu wenye busara.
8) Hadithuth thaqalain inaonyesha kuwa Ahlul bait (a.s) ni maasumu.
Hii hadithi tukufu inaonyesha kuwa Qurani na Ahlul bait ni maasumu kwani imemdhaminia mwenye kuvifwata (hivi viwili) kwamba hatopotea wala kuangamia, bila ya kumwekea sharti lolote. Ni wazi kuwa haingetoa dhamana hii lau kama havingekuwa maasumu.([45])
Kuna hadithi nyingi za thaqalain zilizotamka waziwazi kwa maneno haya, kwa ibara tofauti tofauti.
a) Miongoni mwazo ni,
((ايها الناس اني تارك فيكم ما إن اخذتم به لن تضلوا: كتاب الله وعترتي اهل بيتي)).
“Enyi watu hakika mimi ninaacha kati yenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambacho ni) Ahlubaiti wangu”.([46])
b) Na Miongoni mwazo ni;
((ما ان تمسكتم به لن تضلوا: كتاب الله عزوجل وعترتي اهل بيتي)).
“Ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, pamoja na kizazi changu Ahlu baiti wangu”.([47])
c) Na Miongoni mwazo ni zile zilizotamka wazi wazi,
((هذا علي مع القرآن والقرآن مع عليّ لا يفترقان حتى يردا علي الحوض)).
“Huyu Ali yuko pamoja na Qurani, nayo Qurani iko pamoja na Ali, hawatatengana hadi watakaponijia huko hodhini (mwa kauthar)”.([48])
d) Na miongoni mwazo ni dua ya Mtume Mtukufu (s.a.w.a) aliyomsomea Ali (a.s) kwa kusema”.
(الّلهم ادر الحق معه حيث كان)).
“Ewe Allah, ipitishe haki pamoja naye popote alipo”.([49])
Hizi ni pamoja na dalili nyinginezo, kama vile ayatut tathir inayoonyesha na kuthibitisha umaasum wa Ahlul bait, pamoja na hadithi mutawatir zinazoon-yesha kuwa hao ni maasumu.
e) Na Miongoni mwazo ni hadithi aliyoipokea Alhaakim kwa isnadi yake kutoka kwa Abu Dhar ya kwamba alisema:
قال رسول الله(ص) : ((انما مثل اهل بيتي فيكم مثل سفينة نوح من ركبها نجا ومن تخلف عنها غرق)).
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) amesema “Hakika mfano wa Ahlubaiti wangu kati yenu ni mfano wa jahazi ya Nuhu, aliyeipanda aliokoka na aliyebaki nyuma (bila kuipanda) alighariki.”([50])
f) Na miongoni mwazo ni aliyoipokea Attabarani kutoka kwa Abu Said, aliyesema kwamba,
قال رسول الله(ص): ((وانما مثل اهل بيتي فيكم مثل باب حطة في بني اسرائيل من دخله غفر له))
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) amesema, “kwa hakika mfano wa Ahlubaiti wangu ni mfano wa mlango wa “hittah” kwa wana wa sraeli, aliyeingia (ndani yake) alisame- hewa (madhambi yake).”(s)
Seyyid Sharafudin (r.a) amesema kwamba, “sababu hasa ya kufananishwa kwa Ahlulbait na mlango wa hitta ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Aliufanya mlango huo kuwa ni dhihirisho mojawapo la unyenyekevu mbele ya utukufu wake na utiifu mbele ya hukumu yake na kwa hivyo, hii ikawa ndio sababu ya kupata maghfira (msamaha), Vile vile (Mwenyezi Mungu) Amejaalia pia utiifu wa umma huu kwa Ahlulbait wa Mtume wake (s.a.w.a) na kuwafwata Maimamu hao kukuwa ni dhihirisho mojawapo la unyenyekevu mbele yake na utiifu mbele ya hukumu. Na kwa hivyo hii ikawa ndio sababu ya kupata maghfira. Hii ndio sababu ya wao kufananishwa na mlango huo.
Hata hivyo baadhi ya maulama wa kisunni wamekiri jambo hili, miongoni mwao akiwa Razi, Ibn Hajar Alhaitami, Aljalalus suyuti, Assanad na wengineo.([52])
Ibnu Abil Hadid amemnukuu Abu Muhammad Ibnu Muttawaih kutoka kwenye kitabu cha “Alkifaya” akisema, “Hakika Ali (a.s) ni maasumu hata ingawa sio kwa isma (umaasumu) ya wajibu, na wala isma sio sharti kwa Imamu lakini dalili za kisheria (Quran na hadithi) zimethibitisha ya kwamba yeye ni maasumu na mwenye yakini, na ya kwamba hili ni jambo linalomhusu yeye pekee, wala maswahaba wengine hawakupewa. Tofauti katika maneno yetu iko wazi tunaposema “Zaid ni maasumu” na tunaposema “Zaid ni maasumu kiwajibu, kwa kuwa yeye ni Imamu na katika masharti ya Imamu ni kwamba awe ni maasu-mu”. Kauli ya kwanza inaambatana na dhehebu letu la (kisunni) na kauli ya pili inaambatana na dhehebu la Imamiya (mashia)”.([53])
Jua ya kwamba, Qurani imekuwa maasumu kwa kuwa imetoka kwa Mwenyezi Mungu Ambaye hapa-twi na kosa katika vitendo vyake na wala katika kuiteremsha Qurani, au katika kuwateremshia Mitume (a.s) wahyi wake na katika kuwafikishia watu, kwani lengo la kuwaongoza watu ni kuwafikisha kwenye maslahi yao halisi na ya hakika. Basi, ikiwa Mwenyezi Mungu atafanya kinyume cha hayo atakuwa amefanya kinyume cha hekima yake tukufu.
Vivyo hivyo umaasumu (isma) wa Maimamu ni kwa kuwa elimu yao imetokana na Mtume (s.a.w.a) na Mwenyezi Mungu na kwa hivyo elimu zao haziwezi kupatwa na makosa wala kasoro, kwani wao wame-teuliwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu na kuwatakasa, na kama tujuavyo makosa na upotofu hayasaidii katika kulifikia lengo hili tukufu na wala hayanasibiani na hekima ya Mwenyezi Mugu.
Kwa hivyo basi Qurani na kizazi kutukufu cha Mtume (s.a.w.a) ni maasumu, na vyote viwili vimehi-fadhiwa kutokana na makosa, na kuvifwata kunamhi-fadhi mtu katokana na kuangamia. Hii ikiwa ni fadhila ya kipekee, na iliyomakhsusi kwa hivi viwili tu.
9) Uhusiano wa kizazi kitukufu na Mwenyezi Mungu
a) Kauli yake Mtume (s.a.w.a) isemayo:
((هما حبل ممدود من السماء بينكم وبين الله عزوجل))
“Viwili hivi ni kamba iliyonyooshwa toka binguni iliyoko baina yenu na Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka.”
b) Na kauli yake (s.a.w.a)
((سبب منه بيد الله وسبب بايديكم))
“Upande mmoja wake (kamba hii) uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na upande mwengine uko mikononi mwenu.”
c) Na kuali yake (s.a.w.a)
((انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض))
Hakika hivi viwili havitatengana kamwe hadi vita-kaponijia huko hodhini (mwa kauthar)”.
d) Na kauli yake (s.a.w.a)
((ما ان تمسكتم بهما لن تضلوا))
“Mkishikamana navyo hamtapotea kamwe”
e) Na kauli yake (s.a.w.a)
((هذا علي مع القرآن والقرآن مع علي لا يفترقان)).
“Huyu Ali yuko pamoja na Qurani, nayo Qurani iko pamoja na Ali (Hivi viwili) havite-ngani.”
f) Au kauli yake (s.a.w.a)
((فلا تقدموهما فتهلكوا ولا تقصروا عنهم فتذهبوا))
((Basi msiwatangulie msije mkahiliki na wala msibaki nyuma yao msije mkaangamia”.
g) Vlie vile kule kuwafananisha na jahazi ya Nuhu (a.s.) au kuwafananisha na nyota, pamoja na kauli yake isemayo.
((انهما خليفتي رسول الله (ص) ))
“Hakika” hivi viwili ni makhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a).
Hizi pamoja na nyinginezo nyingi ni dalili zionye-shazo wazi ukaribu wa kizazi kitukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, na ya kuwa walikuwa wakiongo-zwa na Mwenyezi Mungu.
Huu uhusiano nao na Mwenyezi Mungu na ukaribifu wao mbele yake ndio uliowafanya kuwa tofauti na watu wengine. Na ndio sababu twasema kuwa Uimamu wao haukuwa sawa na Ukhalifa wa makhalifa wa ndugu zetu masunni, kwa sababu ya tofauti ya kiasili iliyoko baina ya Uimamu huu na Ukhalifa huo.
Uimamu kwetu una asili moja na Utume, bali tofauti iliyoko baina yao ni wahyi uliyomakhsusi kwa Mitume. Ama Mwongozo wa Mwenyezi Mungu wa kighaibu (kwa njia isiyokuwa ya wahyi) ungali unaendelea, nao Maimamu waongofu wamechukua majukumu yote ya Mtume (s.a.w.a) aliyotwikwa na Mwenyezi Mungu.
Hii ni kinyume cha Uimamu (Ukhalifa) kwa ndugu zetu masunni. Kwani wao wanauchukulia kuwa utawala na uongozi wa dhahiri, bila ya kulazimisha umaasumu na uadilifu katika Imamu (Khalifa).
Hata hivyo hadithuth thaqalain imetuthibitishia kuwa Uimamu una maana ile ile iliyotajwa katika kizazi kitukufu cha Mtume(s.a.w.a).Basi wao Maimamu wamechukua vyeo vile vya Mtume (s.a.w.a) kama vile uongozi wa kidini na uongozi wa kisiasa, ila tu tofauti iliyoko baina yao na Mtume (s.a.w.a) ni kwamba wao wanachukua sheria za uislamu kutoka kwa Mtume (s.a.w.a) na wanamfuata yeye (s.a.w.a) katika mambo yote na wanaongozwa kwa nuru yake na ni Makhalifa wake katika umma wake. Basi wanachukua majukumu yake yote ikiwa miongoni mwayo, ni utawala wa hukuma (serikali).
Kwa hivyo basi, maana halisi ya Uimamu kwetu ina tofautiana na maana halisi ya Uimamu kwa ndugu zetu masunni. Hadithi inatusaidia pamoja na dalili za kiakili zinazo kubaliwa na wenye akili wote, kuthibitisha jambo hili, na ndio sababu mashia ithnaasharia wakatofautiana na waislamu wengineo katika kuitakidi kudumu na kuendelea kuwepo uhusiano wa kighaibu na mwongozo wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuendelea kuwepo kizazi kitoharifu cha Mtume (s.a.w.a).
Imamu wetu wa nane, Imam Ali Ridha (a.s) amasema.”
((ان العبد اذا اختاره الله عزوجل لامور عباده شرح صدره لذلك واودع قلبه ينابيع الحكمة وألهمه العلم إلهاماً فلم يعي بعده بجواب ولا يُحيّر فيه عن الصواب)).
“Mja anapoteuliwa na Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu na Aliyetukuka ili kuyasimamia mambo ya waja wake, humpanulia kifua chake kwa ajili yake (kazi hii) na huweka moyoni mwake chemchemu za hekima, na humfunulia elimu sawa sawa (kwa njia ya) ilhamu (kiasi cha kuwa) hashindwi katika kutoa jawabu, na wala hapatwi na shaka na jawabu iliyo ya haki”.([54])
10) Wajibu wa kuwafuata Ahlulbait ni sawa na wajibu wa kukifuato Kitabu cha Mwenyezi Mungu
Lililo la wajibu ni kuwafuata Ahlulbait kama ilivyowajibu kukifuata Kitabu Kitukufu (Quran). Hili ndilo linalo kusudiwa na hadithuth thaqalain. Basi haitoshi kuwaheshimu tu na kudhihirisha mapenzi na mahaba bila ya kuwafwata. Dalili ya haya tusemayo, ni kule kufanywa Ahlul bait kuwa kizito cha pili pamoja na Quran, pamoja na kauli yake Mtume (s.a.w.a).
((فلا تقدموهما ولا تقصروا عنهما)).
“Basi msiwatangulie na wala msibaki nyuma yao” na kauli yake,
((ما ان تمسكتم بهما لن تضلوا))
“Mkishikama navyo hamtapotea”.
Na ni wazi kuwa kushikamana na kizazi ni kutenda kufuatana na kauli zao na maagizo na makatazo yao na kuufuata mwenenda wao Mtukufu.
Hii ndio sababu tunamuona Taftazani ananukuliwa akisema baada ya kuitaja hadithi hii, “Je huoni kuwa (Mtume(s.a.w.a)) aliwataja pamoja na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka (kwa kusema) kuwa kushikamana navyo viwili kunamuokoa mtu kutokana na kupotoka. Kushikamana na kitabu hakumaanishi ila tu kuchukua katika elimu na mwongozo wake na (hiyo ndiyo maana ya kushikamana na) kizazi vile vile!!([55])
Imepokewa kuwa Ibnu Hajar amesema kuwa, Mtume (s.a.w.a) aliwahimiza watu kuwafuata, kushi-kamana nao na kuchukua elimu kutoka kwao.([56])
Na hii inamaana kuwa maamrisho na makatazo yatokanayo na kizazi kitukufu ni lazima yafuatwe kama ilivyo wajibu kuyafuata maamrisho na makatazo ya Qurani tukufu.
Ikidaiwa kuwa maamrisho na makatazo yao ni hayo hayo maamrisho na makatazo ya Qurani tukufu, sisi tutajibu kwa kusema, maamrisho na makatazo yao ni mapana zaidi, kwani huenda wakati mwengine yakatoka kwa unwani kuwa wao ni Mawalii(viongozi) juu ya mambo yote ya umma, nayo nikufuatana na hadithi iliyotuamrisha sisi kufuata maamrisho yao na kuacha makatazo yao bila ya kupunguza wala kuongeza chochote, na hiyo ndiyo maana ya “wilaya mutlaqa” yaani uongozi usio kuwa na mipaka.
Mwandishi wa Abaqatul Anwar amefaidisha na kufanya wema aliposema: “Hakika hadithi (hii) inamaaniisha kuwa ni wajibu kuwafuata Ahlul bait katika maneno yao, vitendo, hukumu na itikadi zote. Na ni dhahiri kuwa cheo hiki na cha namna hii hakiwezi kupatikana ila tu kwa yule ambaye amefikia daraja ya Uimamu na Uongozi mkuu (wa cheo cha juu kabisa) baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a).([57])
Naye Seyyid Sharafu Din amesema “Zimepokewa hadithi nyingi zilizo mutawatiri na sahihi zinazoonye-sha na kuelezea wajibu wa kukifuata kizazi cha Mtume (s.a.w.a) .
Na hasa hadithi zilizopokelewa kwa njia za upokezi za kizazi kitoharifu, (yaani kwanye vitabi vya hadithi vya kishia).([58])
Kwa hivyo basi kuifasiri hadithi hiyo eti kuwa inauusia umma kukipenda na kukiheshimu kizazi hicho kitoharifu na wala sio (kwamba kuna uwajibu wa) kuwafuata, kunapingana na yaliyomo kwenye hadithi hiyo kama vile kukitaja kwenye hukumu moja na Quran na kukiweka sawa nayo na kuwazuia watu kukitangulia au kubaki nyuma ya kizazi hicho, kuam-risha kushikamana nacho, na kuchukua kutokana nacho hakumpi mtu nafasi ya kuifasiri hadithi hii kama walivyoifasiri. Hii nipamoja na dalili nyingi-nezo, zinazomzuia mtu kuifasiri vivyo.
Kwa hivyo basi sababu hasa ya kusema kuwa Quran na kizazi kitoharifu, vimejaaliwa kuwa Maima-mu katika kuwaongoza watu imefahamika. Hili ni jambo lililowazi katika hadithuth thaqalain, kama alivyosema Imam Ja’afar Swadiq (a.s.),
((وقد امر رسول الله (ص) ان يقتدى بالقرآن وآل محمد وذلك حيث قال في آخر خطبة: اني تارك فيكم الثقلين الثقل الاكبر والثقل الاصغر اما الاكبر فكتاب ربي واما الاصغر فعترتي اهل بيتي فاحفظوني فيهما فلن تضلوا ما ان تمسكتم بمهما)).
“Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.a) alishaamuru kuwa ifuatwe Qurani (pamoja) na Aali Muhammad (kizazi chake) pale aliposema katika hotuba yake ya mwisho (kabla ya kufarikiana na dunia)” Hakika mimi ninaacha kati yenu viwili vizito, kizito kikubwa na kizito kidogo. Ama kikubwa ni Kitabu cha Mola wangu na ama kidogo ni kizazi changu (ambacho ni) Ahlubaiti wangu. Basi nihifadhini katika (kuviangalia) vitu hivyo viwili, kwani hamtapotea kamwe mtakapo-kuwa mmeshikamana navyo.”
11) Kutopingana kwa hadithuth thaqalain na ile iliyopokewa katika Majmauz Zawaid
Jua ya kwamba hadithi iliyopokelewa kwenye kitaba cha Majmauz Zawaid kutoka kwa Abu Huraira ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) alisema;
اني خلفت فيكم اثنين لن تضلوا بعدهما ابداًً: كتاب الله ونسبي ولن يفترقا حتى يردا علي الحوض)).
“Hakika mimi ninaacha kati yenu vitu viwili, (ambavyo) baada yavyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na nasaba yangu. Na havita-tengana kamwe hadi vitakaponijia Kwenye hodhi (ya kauthar)”. Hadithi hiyo haipingani kamwe na hadithi zilizomutawatir (nyingi) zinazoonyesha kuwa Mtume (s.a.w.a) aliacha Kitabu na kizazi, kwani umekw-ishajua Kuwa kizazi (Al-itra) ni Jamaa wa karibu wa Mtume, kwa hivyo basi kutumia neno nasaba (katika hadithi ya Abu Huraira) kunachukuliwa kuwa kusudio lake ni wale wa karibu. Na kusudio hili la wale jamaa wa karibu linajulikana kuto kana na kanuni iitwayo “Munasabatul hukmi wal maudhu”, (Mnasaba wa hukumu na maudhui – yaani, kuangalia hukumu imetolewa kwa mnasaba gani ili kufahamu maudhui ya hukumu na hukumu yenyewa) kusudio lake sio kuwafuata jamaa wote wa karibu ambako kutamfanya mtu aongoke, bali kusudio lake ni jamaa maalum ambao ni maasum, kama zionyeshavyo hadithi nyingi ambazo tulizoashiria na kuzitaja baadhi yake hapo awali.
Vile vile baadhi ya hadithi zinazosisitiza kushi-kamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume (s.a.w.a) hazipingani na hadithi mutawatir zinazosisitiza juu ya kushikamana na Kitabu na kizazi, kwani sunna ya hakika na iliyosahihi haipatikani ila tu kutokana na kizazi kiongofu. Kwa hivyo, hakuna mgongano wala mpingano kati ya hadithi hizo ikiwa hadithi hii itakuwa imethibiti kuwa imetoka kwa Mtume (s.a.w.a) Ama hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) ya kwamba alisema,
((مهما اوتيتم من كتاب الله فالعمل به لا عذر لاحد في تركه فان لم يكن في كتاب الله فبسنة مني ماضية فان لم يكن مني سنة ماضية فما قال اصحابي إن اصحابي بمنزلة النجوم في السماء فايهما اخذتم به اهتديتم)).
“Kwa kiasi chochote kile mlichopewa (kili choko) katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu basi yeyote yule hana udhuru wa kutokitenda. Na ikiwa hakipo ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu. basi (kitapatikana) katika Sunna yangu na ikiwa hakikupatikana katika Sunna yangu basi(kitapatikana) katika yale wasemayo maswahaba wangu. Hakika maswahaba wangu ni mfano wa nyota zilizo binguni, yeyote (kati yao) mtakayemfuata, mtaongoka.”([59]) Hiyo hadithi haikuba-liki kwa sababa nyingi. Nazo ni kama zifuatazo:
Kwanza Maulamaa wakubwa wa kisunni wameta-mka wazi wazi kuwa hadithi hii ni dhaifu. Mwandishi wa kitabu cha “Abaqatul Anwar” amewataja baadhi yao katika utangulizi wa kitabu chake. Miongoni mwao (aliowataja) wakiwemo Ahmad Ibnu Hambal, Albazzaz, Addaru Qutni Ibnu Hazm, Albaihaqi, -hata ingawa yeye mwenyewa anainakili hadithi hiina Ibnu Asakir, Ibnul Jauzi, Ibnu Duhya, Abu Hayyan, Adh-dhahabi, Ibnul Haitham, Ibnu Hajar Al-asqalani na wengineo katika wale waliosema waziwazi kuwa hadithi hio sio sahihi au kuwa ni dhaifu au kuwa Mtume (s.a.w.a) alizuliwa (hadithi hii).([60])
Kwa hivyo basi hadithi hii dhaifu haina nguvu na uwezo wa kuipinga hadithuth thaqalain iliyomutawatir na isiyo kuwa na shaka ndani yake kuwa imetoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a).
Pili:
Pamoja na kuwa hadithi hiyo ni dhaifu pia inapingana na ijmai (makubaliano na maafikiano ya maulama wote) na akili pia, kama anavyosema Allama Mir Husein “Hakika hadithun nujum (hadithi ya nyota) inaonyesha kuwa maswahaba wote wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) walikuwa wema, ambapo, kufuatana na ijmai sivyo hivyo kamwe. Vile vile inaonyesha kuwa wote ni wenye kuungoza umma (katika njia iliyonyooka) ambapo sivyo pia, kwani kikundi kikubwa kati yao kiliwapoteza watu wengi. Vile vile inaonyesha kuwa maswahaba wote wanastahiki kufuatwa na umma na hilo pia ni jambo lisiloweza kuwa sahihi kamwe kwani wengi wao walikuwa ni watu wenye kasoro ambazo ziliwafanya wasistahiki hilo”.
Hadi kufikia kusema, “Zimeteremka aya katika Kitabu cha Mweneyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, zinazoelezea wazi wazi hali za kikundi kikubwa cha maswahaba, na hasa aya zilizoko katika sura ya Anfal Bara-ah, Ahzabi Jum-ah na ya Munafi-quun. Basi je Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) anaweza akawateuwa maswahaba wote wake kuwa viongozi wa umma na hali kama hii?”.
Mpaka kufikia kasema, “zimepokewa hadithi nyingi kutoka kwa Mtume (s.a.w.a) zenye kuwalaumu na kuwashusha daraja baadhi ya maswahaba, utakazozi-pata kwenye Sihahu na Masanid([61]) zenye kutegemewa. Miongoni mwazo ni “hadithul haudh.” (Hadithi ya hodhi) “hadithul irtidad” (hadithi ya kuritadi kwa maswahab) na hadithi isemayo “msirudi baada yangu makafiri”, hadithi isemayo kuwa “ushirikina ndani yenu umejificha zaidi ya kutambaa kwa sisimizi”, hadithi isemayo “sijui mtakayoyafanya baada yangu”, hadithi isemayo, “mtaufuata mwenendo wa mayahudi na manaswara”, na “hadithut tanaafus” (Hadithi ya kushindana), hadithi isemayo, “katika maswahaba kuna ambaye hatoniona (huko peponi) nami pia sito-mwona”, hadithi isemayo “katika maswahaba wangu kuna wanafiki”, hadithi isemayo, “wenye kunizulia uwongo wamezidi”, na nyingi nyinginezo ambazo zinawalaumu baadhi ya maswahaba. “Na zipo hadithi katika vitabu vya ndugu zetu masunni zinazoonyesha waziwazi kuwa Mtume (s.a.w.a) alikataza na kuzuia kufuatwa maswahaba kama hao. Katika baadhi yazo, ame sema.
((ان من اقتداهم في النار))
“Hakika mwenye kuwafwata hao ataingia motoni.”
Hadi kufikia kusema.
((وقال الحنفي: تكون بين اصحابي فتنة يغفر الله لهم لسابقتهم ان اقتدى بهم قوم من بعدهم كبهم الله تعالى الى نار جهنم.))
“Naye Alhanafi amesema (amepokea), “kutatokea fitna baina ya maswahaba wangu, Mwenyezi Mungu atawasamehe kwa yale waliyo yatanguliza. Watu watakao kuja baada yao wakiwafuata Mwenyezi Mungu awatumbukize katika moto wa Jahanam.”([62])
Tatu: lau kama tutakubali kuwa hadithi hii ni sahihi, lakini tunapata kuwa haipingani na hadithuth thaqalain kwani inaingia na kuambatana na yale yote yaliyo tajwa kwenye hadithi ya thaqalain, kwa kuwa imewaamuru (waislamu) kutenda, kufuatana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kusema kuwa mwenye kupuuza kutenda hayo hana udhuru (wa kutoa). Kisha ikiwa ufafanuzi kuhusu kitu haupatikani katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi (hadithi), imeamuru kuwa ifuatwe sunna ya Mtume (s.a.w.a.). Na ikiwa sunna haipatikani (hadithi) ikaturejesha kwa maswahaba. Na ni wazi kuwa sunna sahihi na ya hakika wako nayo Ahlul bait wa Mtume (s.a.w.a) na kuwafuata hao ni wajibu wa daraja ya mbele. Basi Ahlul bait wanapo-kuwepo hakuna nafasi ya kuwafuata maswahaba.
Nne: Hakuna awezaye kukanusha tofauti iliyo-kuwepo baina ya maswahaba katika kuzinukuu huku-mu za Mwenyezi Mungu na mambo mengineyo kuto-kana na kutojua kwa wengi wao. Hata wao wenyewe walikiri kuwa hawakuwa na elimu. Hivyo basi itawezekanaje kwa Mtume(s.a.w.a) kuwafanya kuwa marejeo ya umma katika maongozo ya kidini pamoja na kuthibiti ujahili wao na kuhitilafiana baina yao.
Haya, tukiongeza pia vitendo vya haramu walivyo-tenda baadhi yao, kama vile kuuza pombe, kuchukua riba katika biashara, na vinginevyo, vilivyotajwa katika Kitabu cha “Abaqatul Anwar”.([63]) Audhubillah!! kutokana na kumnasibishia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.a) mambo kama hayo, (Mtume) aliye-teuliwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu.
Mtume(s.a.w.a) ametukuka na ametakasika kutokana na kunasibishiwa mambo kama hayo. Hii ni kufuatana na hukumu ya akili na hadithi zilizomutawatir, ikiwa miongoni mwazo ni hadithuth thaqalain, ambayo kama ujuavyo, iliubainishia umma njia iliyonyooka isiyo kuwa na upotofu. Basi mwenye kuipuuza hiyo njia kwa madai hayo, kwa hakika atakuwa ameiacha njia iliyonyooka na kujiingiza kwenye upotofu, husuda, chuki na ushindani, hayo yote ni miongo ni mwa mambo ambayo yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.a), naye akatilia mkazo kwa kusema,
((اني سائلكم عن اثنين: القرآن وعترتي))
“Hakika mimi nitawaulizeni kuhusu vitu viwili, Qurani na kizazi changu”.([64])
12) Hadithuth thaqalain inathibitisha kuwa Uimamu ni wa kizazi pekee
Hadithuth thaqalain inaonyesha kuwa kizazi cha Mtume (s.a.w.a) kilipata Uimamu baada tu ya Mtume (s.a.w.a) kuaga dunia bila ya kupita muda na kwa hivyo hilo ndilo linalofaa kufuatwa kama tuonavyo katika hadithi zilizomutawatir zinazoonyesha kuwa Mtume (s.a.w.a) alimfanya Imam Ali (a.s) kuwa wasii khalifa na walii (kiongozi) baada yake.
Na hii ndio sababu Seyyid Murtadha (r.a) katika Kitabu cha Shafii ananukuliwa akisema “Hadithi hii inaonyesha kuwa Amirul Muumini Ali (a.s.) alikuwa ndiye Imamu baada ya Mtume (s.a.w.a) pasipo kupita muda”.([65])
13) Mwenye kushikamana na Qurani na kizazi kitukufu, huyo ndiye mwenye kuongoka
Mwenye kushikamana na Qurani na kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.a) huyo ndiye aliyeongoka kufuatana na kauli ya Mtume (s.a.w.a) aliye mkweli na mwaminifu, katika hadithuth thaqalain iliyomu-tawatir. Na wala haifai kumwita mpotofu au raafidhi (mkataa haki) mwenye kushikamana navyo, kwani Mtume (s.a.w.a) hakosei katika kauli yake. Kuna hadithi nyingi zionyeshazo kuwa mashia, wafuasi wa Ahlul bait (a.s) ndio watakaofuzu siku ya kiama. Basi (ndugu yangu) usighafilike.
Kwa kumalizia ninamuomba Mwenyezi Mungu awajaalie ndugu zetu waislamu kutafakari katika hadithuth thaqalain, iliyomutawatir na inayokubaliwa na maulama wa madhehebu yote ya kiislamu.
Kwani hadithi hiyo ni nuru ambayo Mtukufu Mtume(s.a.w.a) aliwaangazia waislamu ili wasije wa-kapotea wala kufarikiana, baada ya kuondoka kwake.
Ewe Allah, tujaalie sisi na waislamu wote ulimwe-nguni, kushikamana na Kitabu Kitukufu na Kizazi Kitoharifu, Amina ya rabbal alamina.
Seyyid Muhsin
Alkharrazi
Mji wa Qum Almusharrafa
Tarehe 21 Ramadhen 1416 H.
([1]) Musnad Ahmad Ibnu Hambal J: 5, uk: 182 na uk: 189.
([2]) Nafahatul Azhar J: 1, uk: 459 kutoka kwenye Tafsiru Anwari iliyoandikwa kwa hati ya mkono.
([3]) Samtun Nujum Al-a’wali, j: 2, uk: 509 na Nafahatul Azhar j: 2, uk: 38.
([4]) Yanabiul Mawadda j: 1, uk: 38.
([5]) Imla ya Mtume (s.a.w.a) inamanisha kuwa alikuwa akimwambia Imam Ali huku Imam akiandika yote aliyaamriwa kuandika (Dictation).
([6]) Jaami’ul Ahadith J: 1 uk: 7 – 12.
([7]) Arjahul Matalib uk; 341 chapa ya lahore kama ilivyonakiliwa katika Ihqaqul haqq j: 9, uk: 367.
([8]) Nahjul Balagha hotuba ya 176.
([9]) Alkafi, J: 2, uk: 449, H: 3.
([10]) Alkafi; J: 2, uk: 438, H: 5.
([11]) Ghayatul Muram uk: 226.
([12]) Hujja wa Mwenyezi Mungu ni mtu aliye mkamilifu kama vile Mitume na Maimamu ambaye Mwenyezi Mungu atamtumia kutoa hoja juu yetu siku ya kiama kutuambia mbona hamkutenda na ilhali huyu alitenda naye ni binadamu kama nyinyi.
([13]) Nahjul Balagha – hotuba ya pili.
([14]) Alfaiqu cha Zama khshari J: 1, uk: 179.
([15]) Faraidus Simtain j: 2, uk: 140.
([16])Tah-dhibul lugha J: 9, uk: 78.
([17]) Nafahatul Azhar J: 2, uk: 201.
([18]) Hii ni kanuni mojawapo katika elimu ya Usulul Fiq-hi.
([19]) Sharhu Nahjil Balagha – cha Ibnu Abil Hadid j: 6, uk: 375.
([20]) Al kamil Fir Rijal J: 6, uk: 2087 chapa ya Beirut kama ilivyo nakiliwa kwenye Ihqaqul Haqqi.
([21]) Ihqaqul Haqq, J: 2, uk: 519 kutoka kwa talkhisul Mustadrak kilichochapisha baada ya Almustadrak na kuunganishwa nacho – (yaani Mustadrak) J: 3, uk: 416 chapa ya Haidar Abad.
([22]) Sura ya Aali Imran aya: 61.
([23]) Sahihu Muslim J: 4, uk: 1871.
([24]) Nawadirul Usul uk: 69.
([25]) Tadhkiratul Khawass, uk: 290.
([26]) Kifayatul Talib, uk: 54.
([27]) Nafahatul Azhar j: 2, uk: 341 – 347.
([28]) Tawatur ni sifa inayopewa hadithi (riwaya) iliyopo-kelewa na wapokezi wengi wa hadithi kiasi cha kuondoa shaka kuwa huenda waliafikiana kumzulia Mtume (s.a.w.a.) maneno haya.
([29]) Uyunu Akhbarur Ridha (a.s) J: 1, uk: 25 – 57.
([30]) Maasumu ni mtu asiyetenda dhambi wala kosa wala kusahau kwani ametakaswa na Mwenyezi Mungu.
([31]) Attabaqaatul Kubra j: 2, Uk: 194.
([32]) Alaur Rahman, uk: 322. (kwa tofauti kidogo)
([33]) Nafahatul Azhar j:2 uk: 254 na Yanabiul Mawadda J:1, uk: 118.
([34]) Ghaibatun Nu’umani uk’ 42 – 43.
([35]) Sharhu Nahjil Balagha cha Ibnu Abil Hadid J: 9, uk: 133.
([36]) Yanabiul Mawadd J: 1, uk: 20 chapa ya Istambul.
([37]) Fadhailu Ahmad uk: 179 na: 267.
([38]) Faraidus Simtain J: 2, uk: 312 na 562.
([39]) Ndiye Salman Alfarisi.
([40]) Maqtalul Husein, uk: 147.
([41]) Sahihu Muslim J: 3, uk: 1452.
([42]) Faraidus Simtain J: 2, uk: 150.
([43]) Nafahatul Azhar J: 262, kutoka kwa Jawahirul Aqdain, kilichoandikwa kwa khati ya mkono cha Faidhul Qadir, J: 3, uk: 15.
([44]) Assawaiqul Muhriqa uk: 232.
([45]) Maasumu ni yule aliyehifadhiwa kutokana na makosa na madhambi aina yote.
([46]) Sahihu Tirmidhi J: 5, uk: 662, H: 2786.
([47]) Ihyaul Mayyit, ,: 30 – 32.
([48]) Mustadrakul Hakim J: 3, uk: 124 Faraidus Simtain uk: 176 na 138.
([49]) Mustadrakul Haakim, J: 3, uk: 124 Nafahatul Azhar J: 2, uk: 267.
([50]) Mustadrakul Haakim j: 3, uk: 151.
([51]) Almu’ujus Saghir j: 2, uk: 22.
([52]) Nafahatul Azhar j: 2, uk: 268 – 269.
([53]) Sharhu Nahjul Balagha ya Ibnu Abil Hadid j: 6, uk: 376.
([54]) Alkafi J; 1, uk: 157.
([55]) Sharhul Maqaswid J: 2, uk: 222 iliyonuukuliwa kutoka kwa Nafahatul Azhar J: 2, uk: 248.
([56]) Assawaiqul Muhriqa, uk: 231.
([57]) Nafahatul Azhar j: 2, uk: 247.
([58]) Almuraja’at uk: 25 .
([59]) Nafahatul Azhar uk: 115 – 156 j: 3.
([60]) Nafahatul Azhar j: 3, uk: 115 – 156.
([61]) Moja ya sihahu ni sahihu na moja ya masanid ni musnad navyo ni vitabu vya hadith.
([62]) Nafahatul Azhar J: 3, uk: 168 – 171 Kanzul Ummal J: 11; uk: 174.
([63]) Nafahatul Azhar j: 2, uk; 178 – 218.
([64]) Hilyatul Auliya J: 9, uk: 63.
([65]) Ash-shafi’I Fil Imama J: 3, uk, 122.