back page

SEHEMU YA TATU

next page

 

Matamshi ya hadithi kama yalivyo kuja vitabuni

1) Katika hijja ya mwisho

 ((اني اوشك ان ادعى فاجيب واني تارك فيكم الثقلين كتاب الله عزوجل حبل ممدود من السماء الى الارض وعترتي اهل بيتي وان اللطيف الخبير اخبرني انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فانظروني بما تخلفوني فيهما.))

a) “Huenda nikaitwa (na Mola wangu) nami nikajibu, nami ninaacha kati yenu viwili vizito, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aiyetukuka, ambacho ni kamba iliyonyooshwa toka binguni hadi ardhi. Na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu. Hakika Mjuzi wa (yote) yaliyofichika na yaliyodhahiri amenijulisha kuwa havitatengana kamwe mpaka vita-kaponijia huko hodhini (mwa kauthar) basi angalieni vile mtakavyovitendea baada yangu”.([1])

((اإني قد تركت فيكم ما ان اخذتم به لن تضلوا بعدي الثقلين احدهما اكبر من الآخر)).

b) “Hakika mimi ninaacha kati yenu ambavyo mki-vichukua (na kushikamana navyo) kamwe ha mtopo-tea baada yangu, navyo ni vizito viwili, kimoja kati yavyo ni kikuu kuliko kinginecho”.

Na katika hijja ya mwisho katika sehemu iitwayo Ghadir khum aliongeza maneno haya (kwa kusema):

((فانظروا كيف تخلفوني فيهما فانهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض)) ثم قال: ((ان الله عزوجل مولاي وانا مولى كل مؤمن)) ثم اخذ بيد علي فقال: ((من كنت مولاه فهذا وليّه))

c) “Basi angalieni mtakavyo vifanyia baada yangu, kwani, kamwe havitotengana hadi vitakaponija kwenye hodhi”, kisha akasema, “Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka ni Bwana wangu, nami ni bwana wa kila muumini”. Kisha akaushikia mkono wa Ali na kusema “Ambaye mimi ni bwana wake, basi huyu Ali ni bwana wake”.([2])

2) Katika Ghadir Khum

قال في غدير خم ايضاً:((اذكركم الله في اهل بيتي اذكركم الله في اهل بيتي اذكركم الله في اهل بيتي)).

“Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu katika Ahlu-baiti wangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu katika Ahlubaiti wangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu katika Ahlubaiti wangu”.([3])

3) Katika hotuba ya Mwisho siku aliyoaga dunia

Katika siku aliyoaga dunia na kurudi kwa Mola wake alisema katika hotuba yake ya mwisho:

((اني تركت فيكم امرين لن تضلوا بعدي ان تمسكتم بهما كتاب الله عزوجل وعترتي اهل بيتي فان اللطيف الخبير قد عهد الي انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض كهاتين ـ وجمع مسبّحتيه ـ ولا اقول كهاتين ـ و جمع مسبّحته والوسطى ـ فتمسكوا بهما ولا تقدموا فتضلوا)).

a) “Hakika mimi ninaacha mambo mawili kati yenu, mkishikamana nayo hamtapotea kamwe baada yangu Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu Aliyetukuka, na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu, kwani mjuzi wa yaliyoficha na yaliyodhahiri Amenijulisha kwamba (Mambo haya mawili) hayato-tengana kamwe mpaka yatakaponijia katika hodhi (ya kauthar) kama hivi viwili – (akavishikanisha vidole vyake viwili vya shahada) – na wala sisemi kama hivi viwili (akakishikanisha kidole cha shahada na kidole cha kati) basi shikamaneni nayo (mawili) na wala msiwatangulie (Ahlubaiti wangu) msije mkapotea”.([4])

((قد تركت فيكم ما ان تمسكتم به لن تضلوا بعدي كتاب الله بين ايديكم تقرؤونه صباحاً ومساءً وفيه ما تلقون وما تدّعون الاّ تنافسوا ولا تحاسدوا ولا تباغضوا وكونوا إخواناً كما امركم الله الا ثم اوصيكم بعترتي اهل بيتي)).

b) “Nimekwishaviacha kati yenu ambavyo mkishi-kamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilicho mikononi mwenu, mnakisoma asubuhi na jioni, na ndani yake kuna yale mnayokutana nayo na yale mnayodai. Kwa hivyo msishindane wala msihusudiane wala msichukiane, na kueni ndugu kama alivyokuamrisheni Mwenyezi Mungu kisha nawa usieni kizazi changu (ambao ni) Ahulbaiti wangu”.([5])

((فلا تقدموهما فتهلكوا ولا تعلموهما فانهما اعلم منكم))

c) ((Basi misivitangulie (vizito viwili) msije mka-angamia na wala msivifunze kwani vina elimu zaidi kuwaliko nyinyi)).([6])

((فلا تسبقوا اهل بيتي بالقول فتهلكوا ولا تقصروا عنهم فتذهبوا فان مثلهم فيكم كمثل سفينة نوح من ركبها نجا ومن تخلف عنها هلك ومثلهم فيكم كمثل باب حطة في بني اسرائيل من دخله غفر له الا وان اهل بيتي امان امتي فاذا ذهب اهل بيتي جاء امتي ما يوعدون. الا وان الله عصمهم من الضلالة وطهرهم من الفواحش واصطفاهم على العالمين الا وان الله اوجب محبتهم وامر بمودتهم...))

d) “Basi msiwatangulie Ahlubaiti wangu kwa kauli msije mkaangamia na wala msibaki nyuma yao msije mkapotea kwani mfano wao kati yeni ni mfano wa safina ya Nuhu (a.s) aliyeipanda aliokoka na aliye-baki nyuma (bila kungia) aliangamia. Na mfano wao kati yenu ni mfano wa mlango wa Hitta (msamaha) katika wana wa Israeli, aliyeuingia alisamehewa. Tambueni kuwa Ahlubaiti wangu ni amani kwa umma wangu, basi watakapoondoka Ahlubaiti wangu (ardhini) kitawajia umma wangu kile walichoahidiwa (yaani kiyama); Tambueni kuwa Mwenyezi Mungu Amewa-hifadhi hawa kutokana na upotofu na kuwatakasa kutokana na machafu na kuwachagua juu ya walim-wengu wote. Tambueni kuwa Mwenyezi Mungu Amewajibisha kuwapenda wao (na Ameamuru kuwa wapendwe).([7])

((اني تارك فيكم الثقلين كتاب الله عزوجل وعترتي اهل بيتي الا وهما الخليفتان من بعدي ولن يفترقا حتى يردا علي الحوض)).

e) “Hakika mimi ninaacha kati yenu Viwili vizito Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kizazi changu(ambao ni) Ahlubaiti wangu. Tambueni kuwa viwili hivi, ndivyo makhalifa wawili baada yangu na havitatengana kamwe, baada yangu mpaka vitakapo-nijia huko hodhini (mwa kauthar)”.([8])

((اني تركت فيهم خليفتين كتاب الله واهل بيتي وانهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض))

f) “Hakika mimi ninaacha kati yao makhalifa wawili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlubaiti wangu, navyo havitoachana kamwe mpake vitakapo-nijia hodhini.”([9])

((اني تارك فيكم الخليفتين: كتاب الله حبل ممدود ما بين السماء والارض وعترتي أهل بيتي وانهما لن يفترقا حتى يردا عليّ الحوض)).

g) “Hakika mimi ninaacha kati yenu makhalifa wawili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu (ambacho) ni kamba (ya Mwenyezi Mungu) iliyonyooshwa baina ya mbingu na ardhi, na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu, nao (makhalifa wawili) hawato-tengana kamwe hadi watokapo nijia hodhini (mwa kauthar).([10])

((وان اللطيف الخبير نبّأني انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فسألت ذلك لهما ربي فلا تقدموهما فتهلكوا ولا تقصروا عنهما فتهلكوا ولا تعلموهم فانهم اعلم منكم من كنت اولى به من نفسه فعلي وليه اللّهم وال من والاه وعاد من عاداه)).

h) “Kwa hakika Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyo-dhahiri amenijulisha kuwa havitatengana kamwe mpaka vitakaponijia kwenye hodhi. Basi niliviombea haya kwa Mola wangu, kwa hivyo msivitangulie msije mkaangania na wala msibaki nyuma msije mkaanga-mia, na wala msiwafunze (Ahlubait wangu) kwani wao wanajua zaidi yenu. Ambaye mimi ni bwana wake basi Ali ni bwana wake. Ewe Allah mpende ampendaye (Ali) na mfanyie uadui amfamyiae  uadui.”([11])

4) HUKO JUHFA

katika hotuba yake (s.a.w.a) huko Juhfa, Ghadir khum alisema;

((ألست اولى بكم من انفسكم قالوا بلى يا رسول الله)) قال ((فاني سائلكم عن اثنين: القرآن وعترتي))

“Je si mimi ninazitawala nafsi zenu zaidi ya mnav-yozitawala nyinyi nafsi zenu?” wakajibu “Ndiyo, ya Rasulallah” akasema “basi mimi nitawaulizeni kuhu-siana na vitu viwili (siku ya kiyama), Qurani (tukufu) na kizazi changu”.([12])


 


([1]) Musnad Ahmad J: 3, uk: 17.

([2]) Mustadrakul Haakim J: 3, uk: 109.

([3]) Maana ya meneno haya ni kwamba waislamu wasi-wapuuze Ahlubaiti wa Mtume(s.a.w.a) wala kuwetendea mabaya na kuwaadhulumu bali washikamane nao na kuwafuata (mtarjumi) – Musnad Ahmad Ibnu Hambal. J: 4, uk: 367.

([4]) Yanabul Mawadda J: 1, uk 116.

([5]) Arjahul Matalib uk: 341.

([6]) Almu’ujamul Kabir, J: 3, uk: 63, H: 2661.

([7]) Nafahatul Azhar aliyenukuu kutoka kwenye Kitabul Arbai’n Fi Fadhaili Amiril Muuminin (kilichoandikwa kwa hati ya mkono) J: 1, uk: 374.

([8]) Faraidus Simtain J: 2, uk: 144.

([9]) Majmauz zawaid uk: 162.

([10]) Ihyaul mayyit cha Suyuti uk: 64, chapa ya Darul ulum.

([11]) Almu’ujamul Kabir cha Attabrani J: 5 uk: 167 katika ufafanuzi juu ya hadithi nambari 4971.

([12]) Hilyatul Auliya j:9 uk: 64 na Ihyaul Mayyit uk: 57 – 58.