back page

HATIMAYE MSAFARA WAINGIA MJI WA SAVEE.

next page

Hatimaye msafara uliingia katika mji wa Savee, lakini kutokana na shida na uchovu mwingi na pia kubadilika kwa hali ya hewa safari iliingia dosari pale maradhi yalipomwanza bibi maasumah (a.s), yalikuwa ni maradhi makali kiasi kwamba sasa hawakuwa na uwezo wa kuweza kuendelea na safari na sasa kutokana na maradhi yaliyo changanyika na uchovu wingi wa safari ulipelekea mwili mtukufu wa bibi maasumah kubadilika rangi. Na sasa walikuwa wakijiuliza maswali kadhaa lakini swali gumu ambalo lilikuwa juu yao ni kwamba hivi kweli bibi maasumah katika hali kama ile angeweza kutekeleza ile nia na azma aliyokuwa nayo na kuendelea na safari ili kuonana na kaka yake mpenzi huko Marw?.

Swali hili lilimuumiza hata bibi maasumah mwenyewe na kumsababishia majonzi makubwa. Hivyo basi msafara ulisimama na baada ya kushauriana waliamua ya kwamba waende katika mji wa karibu ili bibi maasumah (a.s) aweze kupata matibabu na kisha waendelee na safari yao kuelekea Marw. Kwa pamoja msafara ulikubaliana kwamba uelekee katika mji wa Qom.

Qom ni mji wa pekee ulioonekana kuwa na mashia wengi japo kuwa katika zama hizo dhehebu hilo lilikuwa ni halijaenea katika mji ya Iran, lakini kutokana na kuhama kwa mashia wengi kutoka katika miji ya Kuufe ulioko Iraq na kuja Iran ambako walikusanyika katika mji wa Qom. Mji ambao wakazi wake walikuwa wamejawa sana na mapenzi mazito juu ya Ahlulbayti wa Mtume wetu Mtukufu.

Kutokana na uadui wa wazi uliokuwa ukifanywa na watawala waliokuwa madarakani katika enzi hizo dhidi ya Ahlulbayti na hii ilisababisha mashia wengi sana kuhama kutoka katika miji mingine mingi kama vile Kufaa na kuja kuujenga mji wa Qom na hasa ndio waliouanzisha.

Na pindi zilipowafikia watu wa Qom khabari za kuwepo kwa bibi maasumah ndani ya Irani katika mji wa Savee na vilevile ni mgonjwa, walikusanyika watu wa Qom ili kupanga na kisha kuongozana hadi katika mji wa Savee ili kumlaki bibi maasumah na kuongea naye uwezekano wa yeye kuja katika mji wa Qom. Hivyo basi waliamua kumteua mjumbe wa kuwawakilisha huko nae ni bwana Mussa bin Khazraj aupeleke ujumbe wao hadi kwa maasumah na kisha amweleze ni kiasi gani watu wa Qom walivyokuwa na shauku ya ziara yake katika mji huo ujumbe ambao aliuafiki bibi maasumah na kuamuru msafara uelekee Qom. Na aliyekuwa akiuongoza msafara huo alikuwa ni bwana Mussa bin Khazraji, aliuongoza msafara huo hadi katika mji ambao wakazi wake walikuwa na mapenzi na shauku kubwa ya kumuona mjukuu huyo wa Mtume wetu mtukufu na dada yake Imamu Ridhaa (a.s) katika mji wa Qom.

index