back

KWAJINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA RAHEMA NA MWENYE KUREHEMU.

next page

 

Kitabu ambacho kiko mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu kilichotungwa na Mheshimiwa Ghulam Ridhaa Haidary Al-Abhary kwa lugha ya kifarsi na kimepigwa chapa na kujulikana kwa jina  ((Negahiy bar zendegani hazarat Faatimeh Maasumeh (a.s) likimaanisha jina hili mtizamo juu ya maisha ya mwenye heshima na baraka Faatima (a.s) aliyetakaswa na Mungu (s.w) na kikafasiriwa kwa lugha ya Kiarabu kwa amri mkuu  wa  idara na kitengo cha  fedha cha haram takatifu, Mheshimiwa Muhammad Hussain Fakihi Al-mirzayiy na kusambazwa kwa amri yake mwenyezi mungu amlipe kwa jitihada zake njema na ndipo kilipofasiriwa na katika lugha nyingine tofauti tofauti kama vile Kiurdu, Kiingereza, Kiswahili, Kihausa n.k.

Tunawaombeni kila atakaye kisoma kitabu hiki basi amsalie Mtume na kumuomba Mwenyezi Mungu awape ushindi na uhuru Waislamu wote kote Duniani Amin.

Fadhila za kitabu hiki zimwendee mama mpenzi na mwenyezi mungu ampe shifaa kwa fadhila na baraka za mtume wetu   Muhammad (s.a.w).

 

index